Home
Unlabelled
madentidit
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Vitabuu, watu wanalalamika njaa nyie mnataka vitabu.
ReplyDeleteLondo
madenti kweli hawa,,, mbona midomo miyeusiiii,, sijui sigara kwa bangi?
ReplyDeleteHili lilikuwa tukio gani Michuzi?
ReplyDeleteHoja nyingine zinatia kichefuche!!! Ina maana LONDA hujui umuhimu wa madai ya hawa wanafunzi??Hapo wameomba vitendea kazi ambavyo nadhani itakua ngao muhimu kupambana na umaskini katika nchi yetu na njaa ikiwepo.
ReplyDeleteJe wangeomba waongezewa posho ungesema nini???
Asante michuzi kwa pica hii kwani inazidi kufunua macho ya wengi juu ya madai ya msingi ya wananchi wengi ambayo hayapewi uziti unaostahili
Fikrathabiti,
ReplyDeleteUsije ukafikiri au kudhani kuwa ni wewe tu unayefahamu umuhimu wa elimu....., Hivi serikali ikisema leo kuwa, bilioni kadhaa tulizoagizia chakula zilitengwa kwa ajili ya kununulia vitabu utasemaje? usije ukasahau pia pesa wanazopata wanafunzi bongo ni zaidi ya mshahara wa mfanyakazi wa kima cha chizi, samahani kima cha chini.
Bado sipingi umuhimu wa kununua vitabu, lakini nachotaka kuzungumza, kuna mengine mengi pia ambayo yana umuhimu wake.
Londo
Londo, usiwatetee sana. si zile alizochikichia Prof. Mahalu (bilioni 2) zingenunua vitabu kadhaa kwa miaka hata kadhaa ijayo? je na hizo zinazopotelea mahotelini kwa ajili ya mawaziri? umesahau za kuchapisha t shirt ambazo teyari zimeishachanika? umesahau US 3.5 Million alizokula Mahita???? umesahau???? Tanzania hujengwa na wenye moyo huliwa na wenye choyo!!
ReplyDeleteHawa wakina Londo ndio wale wanaoangalia leo, wakiangalia mbali sana basi ni kesho asubuhi. Anafikiria njaa ya leo lakini amesahau hao vijana wakisoma vema ndio watakao kuwa wahandisi wa kilimo cha umwagiliaji ili kuzuia njaa za mwaka 2015 na kuendelea.
ReplyDeleteHujawahi, kusikia njaa wewe....sikieni tu lakini msiombee kuiona.
ReplyDeleteLondo
Hivi mwanafunzi asiye na vitabu kwanini aitwe mwanafunzi? Ziko wapi rekodi zinazoonyesha kuwa fedha ambazo zilipaswa kununua vitabu zimetumika kuokoa maisha ya watu wasife na njaa? Mimi naona suala la serikali kunuua chakula na kununua vitabu yote ni muhimu na yote yanapaswa kufanyika. Sio moja lisubiri jingine. Yote ni muhimu. Lakini wakati ambapo tunasikia mamilioni yakichezewa na "watalii" wanaoitwa mawaziri wanaokaa hotelini na maprofesa wengine wakiiba mabilioni kupitia ubalozi, huwezi kutetea serikali wanafunzi wanapodai haki ya kuwa na vitabu. Toka lini tukaona kuwa elimu ni suala la mzaha? Ushindani mkubwa wa dunia ijayo hauko kwenye maguvu ya kijeshi, fedha nyingi, viwanda vingi, n.k. bali maarifa.
ReplyDeleteKimsingi hakuna mtu aliyesema kuwa vitabu havina umuhimu, na kama yupo basi huyo atakuwa "mwendawazimu" kilichozungumziwa ni kuwa katika kipindi hiki wakati kuna wengine wanalalamika kuwa vitabu hakuna, wengine wanalalamikia au kufa na njaa (FULL STOOOP). Umuhimu wa nini kianze kwanza kununuliwa halikuwa suala.
ReplyDeleteLondo
Londo hauna hoja. Kaa kimya unakuja kwa staili ya kujisafishasafisha. Tumeshakuelewa ulighafilika tu.
ReplyDeletehuyu Londo nina wasiwasi ni mchokoza mada msaidizi...labda kwa staili ile ile ya Michuzi kuwaita watu fulani kuwa muhimu wakati ndio wanatumaliza. Londo, namna hii kwa kweli hatutafika! wakati sisi tunapambana na vitabu inakuwaje wenzetu wanapambana kuwa ikibidi hata watoto wa shule za msingi ikibidi wasome kwenye internet? vitabu vyenyewe vinavyoongelewa hapo utakuta ni vya mwaka 45 vinavyompa mtu basics ambazo pia bado havimtoshi mtu kupata ajira kwenye soko la utandawazi...sasa hivi akija mtu ana kampuni ya ujenzi hata uhasibu anataka kuajiri mtu ambaye anazijua software zilizotoka jana kama sio juzi za kuchora ramani!! hao vijana inabidi wakose kazi tu kwa msingi huo hadi wapenye penye wakajifunze..vijana wa nje wataitwa wataajiriwa na haa watalalamika hadi kunakucha!!vyuo vya wenzetu huhakikisha kuwa makampuni yanayotengeneza software yanafanya kazi kwa ukaribu na vyuo...
ReplyDeletenaomba nikukumbushe kuwa magap ya uchumi duniani sasa hivi hutengenezwa na maarifa, sio kulima mahindi na choroko!!! fikiria mbadilishano wa bei ya tani za kahawa na kompyuta moja! au gunia la mahindi na eyatime ya dola kumi - sijui umenipata?
katika waliotuizidi wensetu ni kuwa wakati sie katika familia kuna watu 9 ni mmoja tu anayeajirika na kuhusika kujenga uchumi, kwa wenzetu familia ina watu wanne, na wote wanaajirika na wanajenga uchumi, hapo pia nadhani umanipata! najua unajua dunia ya sasa inataka nini IT, electronics, Medicine, engineers, n.k...
Rwanda baada ya muda mfupi itakuwa mbele sana kwa IT katika region yetu! huita watalamu sehemu mbali mbali ili kujenga mfumo wao wa ufundishaji na ukuzaji wa IT...sie tubaki kulima mahindi wakati kwenye soko la dunia yanauzwa kwa bei chini kuliko kitu chochote...
siyo kwamba Tanzania haina uwezo, ni allocations ya resources tu, na priorities. kwa Tanzania priorities ni SIASA! na kutunza vizuri maslahi ya WAZEE! hivi hujiulizi ni kwanini mfanyakazi wa Tz ndio ana maslahi madogo kuliko yoyote katika region yetu? CHA JUU KINAKWENDA WAPI? MBONA WENZETU WANAWEZA NA WANAPIGA BAO VILE VILE?
kitu cha kujiuliza ni kwamba iweje wanasiasa wetu ndio watu wanaishi kama wenye makampuni makubwa sana ya kimataifa wakati biashara wanayofanya hatuioni??
labda kwa hili nitarejea hoja ya madaktari, je watanzania tunataka nini? ni vyema uende hospitali ya serekali ukute daktari aliye na furaha na kazi yake, akuhudumie kikamilifu baaada ya hapo uende moja kwa moja myumbani kwako,? au uende hospitali ya serekali, ukute daktari aliyechanganyikiwa kwa maslahi mabovu, akutibu nusu nusu, baadae uende hospitali ya binafsi umalizie matibabu huko?
Tanzania hujengwa na wenye moyo / vibogoyo na huliwa na wenye choyo/ wenye meno
"siyo kwamba Tanzania haina uwezo, ni allocations ya resources tu, na priorities".
ReplyDeleteHili kimsingi ndio nilikuwa nataka tulijadili. Nashukuru kwa kulileta.
Swala la NJAA,MAGONJWA na UJINGA ni vitu ambavyo tunapaswa kuvitengenezea mkakati thabiti wa kupambana navyo.
Na sio kitu kimoja ni muhimu kuliko kingine. Tunaweza kutofautiana nini kianze.... Lakini hatuwezi kutofautiana katika lipi ni muhimu....
Siku njema.
Londo
kama mkulima hana jembe basi huyo si mkulima, je mwanafunzi bila kitabu sijui tutamwita nani? kibaka, mzururaji,tapeli,,,
ReplyDeleteelimu ni haki ya kila mtu, ni moja ya haki za binadamu(UN), kwahiyo hii ni dhuluma kwa wanyonge.
watoto wa wakuu hawasomi kwenye public skuli, hii inaonyesha jinsi wanavyojua kwamba huko hakufai, wanasakizia kina sisi, hii inatakiwa ipigwa vita sana.
tunataka watoto wao nao wasome na sisi,na sio kina yakheee private skuli."they need 2 practise wath they preach"
jamjuah
Binafsi namuunga mkono ndugu Londo. Kwani katika siku za karibuni tumeona kuna mambo mengi yanayofanyika katika kuwalaghai wananchi wasizungumzie tatizo la njaa linalotukabili.
ReplyDeleteNazungumzia suala ambalo, nalifahamu kwa undani mnoo. Suala la kuvunjiwa vibanda "Wamachinga" na suala la kuondolewa "Wapiga debe" vituoni, na madai ya posho na vitabu kwa wanafunzi, ni moja ya mikakati ya kubadilisha vichwa vya habari vya magazeti yetu, ili watu wabadili mazungumzo.
Ni ukweli usio kificho kuwa vitabu ni suala la msingi na Elimu ni suala lisilopingika, tatizo linakuja pale "wanafunzi" na "Taasisi" nyingine wanapotumiwa kuibua mambo ambayo ni tatizo la siku zote, ili tu wale wanaowatuma, wakwepe kero za kujibu maafa yanayolikabili Taifa.
Ndugu zangu, habari hizi ni za ndani sana, na siwezi kwenda zaidi ya hapo. Naomba sana mliangalie Taifa lenu kwa jicho la "Tatu", kuna mengi yanafanyika, lakini ni jukumu lenu, kufahamu nini ni kiini macho na kipi sicho.
Mzalendo
Nadhani kuna watu wengine wamekuja kwenye uwanja huu wa mawazo kama MAMLUKI!!!Narudia tena,KUNA MTU ASIYETAMBUA UMUHIMU WA MADAI YA HAWA WATU?????
ReplyDeleteMakene naomba nawe utoe msimamao wako wa kimawazo katika hili.
Fikra Thabiti, sina makubwa zaidi ya ndugu zangu makini walivyochambua huko. Picha ya Michuzi inajisoma, haihitaji maoni kabisa. Hakuna ugali bora zaidi Afrika kama vitabu. Kama unaona nadanganya kamsome Bwana MSA katika "Mzimu wa Watu wa Kale" ili akueleze kama unataka kuona faida ya mwanga iungie gizani na kama unataka kujua faida ya chakula..shinda njaa. Hao vijana wanazungumzia ugali wa kudumu na sio chakula cha muda. Hawa ni sawa na wale wanaolilia haki ya kuzaliwa...haki ya kutambua...haki ya kujipangia. Nimepewa elimu ambayo sasa yanipa nguvu ya kuamua maamuzi ambayo FIKRATHABITI kama Mola atapenda naweza kuishi popote na kufanikisha matarajio yangu, ya wanaonizunguka, ninaowajali na kuwathamini sana na bado nikaweza kuwavumilia adui zangu. Hii ni sifa ya elimu, uvumilivu kwa akina ANONIMASI wanaotukana kama wametumwa huku, nawatazama wakinichapa shavu la kushoto na mimi kuwageuzia la kulia. Hawa vijana wanataka vitabu waweze kufikia hapa tulipo. Hatujaenda mbali lakini katika Tanzania na Afrika tumefikia hadhi ya vyeo fulani ninavyoitwa hapa UTPA Profesa wa Kiswahili. Naachia hapa Materu Monday kwangu siku mbaya sana ya shule.
ReplyDeletejamani mbona hivyo, vitabu vina nafasi yake na njaa pia ina nafasi yake,suala la vitabu limekuwa tatizo la muda mrefu mpaka hakielimu walipokuwa wakitoa matangazo yao kuhusu mfumo wa elimu hapa nchin wakaonekana wabaya na hata matangazo yao kufungiwa, lakini ukweli unabaki pale pale, kuwa elimu ni tatizo kwa nchi hii, acha njaa itatuliwe kwanza, maana ukiwa na njaa hata hivyo vitabu itakuwa ngumu kuvisoma jamani au mnasemaje By Michuzi Jr
ReplyDeleteSASA HAWA HAWANA VITABU NA TENA WANANJAA, VYOTE VYOTE. SIJUI WAMEMKOSEA NINI MUNGU.
ReplyDeleteni kweli vitendea kazi yaani instuments ni muhimu.'haki haiombwi bali inachukuliwa'
ReplyDelete