
Kwa taarifa yako tu ni kwamba huko ughaibuni kuna mtanzania aitwaye rumadha fundi ambaye ni kinara wa sanaa ya kujilinda kwa mikono mitupu (karate) aishiye mji wa Houston, texaz. Hivi karibuni alifanya mtihani na kuvuka toka daraja la tatu (3rd dan) hadi la nne (4th dan) ambalo ni kubwa kuliko mtanzania yeyote duniani kwa mtindo wa goju ryu karate. Hii picha za semina wakati wa mtihani aliofanya rumadha wa kupata dan ya nne, chini ya Sensei Master Masuda (6 dan), ambaye ni secretary general wa Okinawa Goju ryu na anaishi Okinawa chini ya Master Ihan (10 dan). Pia kulikuwako na Master Muramatsu 8 dan, aambaye aliwahi ku-train na Sensei Nantambu Camara Bomani (mwalimu wa dojo la Zanaki Tanzania) katika Dojo ya Okinawa chini ya Sensei Master Eiichi Miyazo 10dan , mapema miaka ya 70.
Kwa mlio huko si vibaya mkamtembelea. Mie naye tulicheza pamoja pale zanaki miaka ya 80, kabla yeye hajaende ughaibuni na kujiendeleza hadi kufikia ngazi hiyo. Mie nina kamkanda ka kahawaia na viel rumadha sasa ana leseni ya kufundisha popote duniani, ana mpango wa kufunguo dojo bongo nami nategemea kufanya mtihani wa mkanda mweusi.
Pichani ni Sensei Rumadha na Sensei Masuda. (Picha kwa hisani ya Houston dojo)
Ps: nakaribisha picha na habari kama hizi za wabongo mlioko ughaibuni kama utapenda nizitie bloguni tupate kufahamu mazuri mengi wabongo myafanyayo huko, hata kama ni harusi, mahafali, hafla za wabongo nk. bei dezo....


Dah Michuzi unajua siku zote nilikuwa nastaajabu sana jinsi unavyoandika habari za Karate kwa ufasaha kiasi hicho na sikujua kama karateka kwani najua waandishi wengi huwa hawawezi kuandika kwa ufasaha kama hivyo
ReplyDeleteMichuzi,
ReplyDeletehivi Bomani ni daraja gani?
asante kwa anony no. 1 na kwa anony no. 2 ni kwamba nadhani sensei nantambu camara bomani sasa ni dani 6, ngoja nicheki na jamaa nipate uhakika.
ReplyDeleteKina Sensei Magoma, Mabruki na wale wengine wa kwanza kupata Black Belt wako wapi kwa sasa?
ReplyDeleteJe unaweza picha zao zilizopigwa wakati walipofuzu?
Nakumbuka enzi za dojo likiwa bado lipo Diamond Jubilee, that is way back to 1974.
Sijui kwa nini kila nikimkumbuka Sensei Bomani nakumbuka kile kiambaza cha Empress Cinema.
Till next,
F MtiMkubwa Tungaraza
senpai (sio sensei) magoma yupo dar, mabruki (wote wawili) sina data zake, senpai marunga yupo relwe nadhani morogoro, senpai gamanya karudi kwao zimbabwe zamani. dojo lilianzia ymca ambako bomani aliwakuta kina gamanya wanacheza shotokan. wakahamia diamond kisha zanaki sekondari. hivi sasa dojo lipo zanaki shule ya msingi, mlemle ndani. kiongozi mkuu ni senpai murudka akisaidiwa na senpai almasi.
ReplyDeleteukuta wa empress palibandikwaga picha ya bruce lee kwenye enter the dragon. siku hizi hakuna hata jumba moja la sinema. yote wameua. hilo la empress sasa ni duka la samani, empire imevunjwa, wanataku kujenga nini sijui. odeon ndiyo kituo cha dtv, cameo pana ghorofa la makazi na duka. new chox imefungwa, hivi karibuni mganga mmoja wa kienyeji alikodisha ofisi za nyuma. avalon pia ni duka la samani la kampuni ya tunakopesha. drive inn ni ubalozi wa marekani.
sema pale mwenge pana jumba moja la senema la kisasa ambalo ndilo tunaponea. nasikia katika mlimani city project karibu na chuo kikuu zitajengwa zingine
Sensei Ramadha anapatikana Houston kipande gani ili tukamtembelee
ReplyDelete