nitajie sifa kumi za kula biriani ama pilau shughulini (makene, mtimkubwa, jeff, msaki mpo???)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 10, 2006

    Kwa kuangalia haraka haraka hawa jamaa watakuwa wapo hai tebo, maana kwanza kila mtu na sahani yake na wamepewa soda na maji kwa wakati mmoja.
    Nilipokaa mimi kuna ule mkanda wa karatasi na jamaa mwenye masinia anapita akiwachukia hatua zinakuwa kubwa akifika karibu na marafiki zake anapunguza hatua kidogo ..
    Inabidi uwe umepiga goti moja
    na uwe na macho mazuri ya kuona nyama zilipo wakati sinia linashuka
    likifika tu chini wali unapekuliwa na nyama zote hutoweka katika sekunde zisizozidi mbili
    nyama inashikwa mkono wa kushoto halafu unafinyanga tonge la wali na kumega kipande cha nyama mkono wa kushoto
    hapo ndo mazungumzo yanaanza .. ukifanya kosa ukanogewa na mazungumzo ujue utashangaa sinia jeupe
    Lakini kubwa kuliko yote hakikisha umekaa mahali pazuri kuna wasi wasi unaweza kunawa mara mbili bila kula

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 10, 2006

    Anony juu umesahau kwamba kila mtu anakuja na ndizi yake

    ReplyDelete
  3. Kaka weee! Mbona ukanizidisha mipigo ya njaa adhuhuri hii bwana,lol!!

    Lo! Niko mbali ugahibuni kwa Rais mpenda vita "George Kichaka" lakini navutiwa mno na biriani hii na hata jinsi mabwana hawa walivyojiandaa vilivyovyo katika mikeka...coke na maji ya baridi pia? Kama alivyogusia mwenzangu hapa juu...pamekosa ndizi tu!!

    Picha zako kama kawaida ni poa kabisa!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 10, 2006

    Wataalam mnanifurahisha mno. Eti hao wako high table.
    james

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 11, 2006

    Sifa 10 za kula pilau:

    1. Kukaa mkekani
    2. Unatumia mkono na si kijiko
    3. Usivae viatu
    4. Lazima mkao wa kula kama huu
    5. Spidi yako iwe bomba
    6. Maji ya kunywa muhimu, kuna kukwamwa
    7. nimesahau!!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 11, 2006

    kutokana na vumbi la TZ huo mguu lazima uanatema uchafu katika chakula, vipi huyo mwingine anaogopa soda yake itachukuliwa maana kaiweka karibu sana na mguu wake kama imefunguliwa aombee asitokee pusi ama kuku maana akishtuka kidogo tu basi itakuwa sadaka.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 11, 2006

    Hapo wangekuwa wamewekewa na safari mbili mbili ingekuwa mlo umebance kikweli kweli.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 11, 2006

    Safari mbili mbili kweli ingekuwa "balance diet" (kwa lugha ya ki bbc. Maana hata viinilishe vya jamii ya hamilojo vingekuwepo. Lakini kofia na kanzu haviruhusu

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 11, 2006

    Nyie Anony wawili hapo juu Takbiri.

    ReplyDelete
  10. Kwa kweli nilitazama picha na kushikwa na njaa ghafla! Okay hapa Boston karibu ni lunchtime na niatambulia li-sandiwichi! Lakini nimeamua jumapili napika Biriani! Kaka Michuzi asante sana kwa picha!

    Lakini nami naona watakuwa ni wageni wa heshima hao. Kila mtu ana sahani yake na wamepewa drinks mbili mbili!

    Tuelezee zaidi kuhusu picha basi, ni sherehe ya nini, nk...

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 16, 2006

    Huyo Anonymous No. 1 hapo juu kabisa anaonyesha kakulia Mburahati, Mbagala, Vingunguti au ni Al-watan la Ilala maana description aliyotoa ya mnuso wa Uswahilini hauna cha kuongeza!

    Jamaa wenye masinia wanaitwa "wandazi".

    Regds,
    ../mdosi xp.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...