jk akiwa na joji kichaka majuzi nyumba nyeupe. jamani eeee... vipi tena huko? soma chini kwa makini. inglishi mwenzenu iz noti richebo, la sivyo ningewatafsilia...kunradhi



NINE CHARGED IN MULTI-MILLION DOLLAR THEFT CONSPIRACY FROM HOUSTON CAMPUSES OF HEWLETT-PACKARD AND EXEL LOGISTICS...

HOUSTON, TX , May 22, 2006

Nine persons were indicted for conspiring to transfer in interstate commerce servers, processors, hard drives, and memory strips stolen from the Houston campus of Hewlett-Packard (HP) and the Houston facility of HP’s logistical partner Exel Logistics (Exel). United States Attorney Don DeGabrielle announced today that the nine charged are Njaidi Othman Njaidi, 35, of Houston; Franklin Lauwo, 35, formerly of Houston; Wasia Kessi Maya, 28, formerly of Houston; Abby Hussein Omari, 24, of Houston; Misso Canute Temu, 30, of Houston; Ahmed Juma Khalid, 30, of Houston; James Mtae, 27, of Houston; Frederick Omondi, 31, of Houston; and Jamese Hill, 25, of Houston. The indictment, returned by a Houston grand jury under seal on May 16, 2006, was unsealed on Friday, May 19, 2006. Njaidi, Khalid, Mtae, Omondi, and Hill are alleged to be current or former employees of HP or Exel.
On May 18 and 19, law enforcement personnel from the Federal Bureau of Investigation (FBI), Houston Police Department, and the Harris County Sheriff’s Department arrested Njaidi, Maya, Omari, Khalid, Omondi, and Hill. With the exception of Hill, who has released on bond following her initial appearance in court on Friday, all others arrested have been ordered to remain in federal custody without bond pending a detention hearing scheduled for Wednesday, May 24, 2006, at 10:00 a.m. before United States Magistrate Judge Mary Milloy.
Arrest warrants remain outstanding on Lauwo, Temu, and Mtae. It is believed that Lauwo and Temu may have returned to Tanzania. Mtae is believed to be in the Houston or Dallas area. Anyone with information concerning any of these three defendants should contact the FBI at 713-693-5000. Photos of these three fugitives are attached.
According to allegations in the indictment, Njaidi and Lauwo recruited individuals working at HP or Exel to steal processors, hard drives, memory strips, and other items. Njaidi and Lauwo, along with Maya, Temu and Omari, allegedly paid sums ranging from $20,000 to in excess of $100,000 to Hill, Omandi, Mtae, Khalid and other HP or Exel employees who provided them with stolen products. It is further alleged that the next step of the scheme involved employees Omondi, Khalid, Hill, Mtae and others changing the shipping labels on outgoing shipments from HP and Exel, redirecting the shipments from customers to Njaidi, Omandi and other members of the conspiracy. Another part of the scheme involved charged employee defendants and others removing the processors from their packaging at the computer company facility, secreted the stolen goods in their shoes or clothing, and leaving the premises with the stolen goods. According to the transactions alleged in the indictment, Njaidi, Lauwo, Maya, Omari, Temu and Khalid sold more than $2.9 million of the stolen products to purchasers in Minnesota, California, and other states.
All nine defendants are charged with conspiring to transfer stolen products in interstate commerce, a crime that carries a punishment of up to five years in prison and a fine of up to $250,000 upon conviction. Njaidi, Lauwo, and Maya are also charged in two separate counts, and Temu with one count, of transferring stolen products in interstate commerce, a crime that carries a punishment of up to ten years in prison and a fine of up to $250,000 upon conviction. The indictment also seeks a forfeiture judgment from all the defendants of approximately $3.25 million, alleging this sum constitutes the proceeds of their alleged illegal conspiratorial conduct. The case was investigated by the FBI and the Houston Police Department’s Major Offenders Division, Cargo Theft and Fence Detail, and will be prosecuted by Assistant United States Attorney Gregg Costa. An indictment is a formal accusation of criminal conduct, not evidence. A defendant is presumed innocent unless and until convicted through due process of law.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 62 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 23, 2006

    mhhh makubwa michuzi ushapata news?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2006

    Haya ndio mambo yanayozidi kututilia watanzania kiwingu kila kukicha.Tamaa za utajiri wa haraka haraka,usiokuwa na jasho hautufikishi popote na wala sio ujanja.Fanyeni kazi halali jamani,kwa bidii na maarifa.Aibu

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2006

    Michuzi naona habari hii imekuchanganya mpaka umesahau kuweka picha ya George Kichaka au ni kompyuta yangu tu ndio haioni?ee bwana hiyo aibu...sio ujanja kabisa

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2006

    Samahani hapo juu nilimaanisha tusianze kuwasemea vibaya

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 23, 2006

    Kitendo cha kutajwa tajwa tu kinaonyesha kwamba njia zao sio nzuri.Kwanini wao na sio wengine wengi wanaoishi Marekani?

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 23, 2006

    tamaa bwana inauwa sana,hao watu ndio wanaotuwaribia maisha yetu ulaya na america.utakuta unaelimu yako lakini unashindwa kupata kazi ya maana kutokana wao walituharibia mwanzo , mfano kwa hapa uk wabongo wanajulikana sana kwa kuchanja[wizi wa credit card] basi utakuta vijana wengi wenye elimu ndogo wanaishia ktk kazi hazieleweki na hata kama unaelimu nzuri ukitaja tu umetoka tanzania wanakuogopa wanakuona mwizi.mimi nashangaa sisi watanzania sijui tuko vipi wenzetu wengine kutoka afrika wanafanya mambo yao kwa kutulia sisi tunaaribu kila siku, shule hawapendi wana baki wizi, starehe,ngono,kazi hawataki kufanya wanabaki kuchanja siku inapofika wanarudishwa nyumbani wanabakia si lolote na si chochote,huo ndio ukweli wake bwana michuzi.

    bora niishie hapa na nibaki Anonymous ili nisijenge maadui.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 23, 2006

    Uingereza sikuhizi wizi wa credit card umeisha, hata kama hupo hauna faida kama zamani. Vijana nawaomba muanza kufanya kazi sasa,zile hela za ujanja ujanja tuache sasa na tuanze kuwajibika.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 23, 2006

    wewe usiseme hakuna huo wizi, wizi upo na utaendelea kuwapo labda usiwe na supplier mzuri na wa kuaminika.

    kwa kweli hawa vijana wanatuharibia maisha hasa hasa wabongo wajinga sana ukiwa na dili moja ina ambiana au yote inataka kufanya hizo hizo dili na wakifanya wana haribu au kukuaribia jina. mi na kwambia wabongo kote kule mlipo acheni hizi ishu na anzeni kufanya kazi mambo yana badilika kila siku mtajikuta dsm ndio mlie kwa sana.

    na hapa usa ndio sio mchezo wabongo wezi hao. ngoja nikae kimya wasije nipiga risasi za kichwa

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 23, 2006

    Wewe I.M unasema nini hapa? Hawajashitakiwa au hawajahukumiwa? Umen'gang'ana tu hawajashitakiwa hawajashitakiwa sasa hiyo indictment ni kitu gani kama siyo kushtakiwa? Sitaki kuwahukumu hawa jamaa lakini kwa utendaji kazi wa wenzetu kama wameaamua kwamba hawa sasa ni washtakiwa asilimia 95 ni kweli wametenda. Jamaa hawakurupuki tu na kukamata kama polisi wa Bongo. Kinachoweza kuwasaidia ni kupata Mawakili kawa Simpson O.J kama bado wanazo hizo hela. Lakini ndio matunda ya Bongo hayo wote ni wezi tu, wewe mtu na familia ya watu saba utaishije kwa mshahara wa elfusitini na tano kwa mwezi

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 23, 2006

    Inashangaza sana wabongo huku ugahibuni, hii ni aibu kubwa na kuzibiana kwa uwazi. Wewe MTZ kama ulikuja huku hata kwa kuzamia basi tafuta kazi halali ya kufanya sio unaharibia WaTZ wengine. Huo ni ujinga tu hakuna kingine. Mimi nitawahukumu tu moja kwa moja kwa nini wakimbie sasa!

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 23, 2006

    Ni safi sana, hayo ndiyo wanayotenda hata viongozi wetu. Sema wao inakuwa kwa namna nyingine. Ukipata udiwani marupurupu yako ni kwenye viwanja vinavyogawiwa mara mbili mbili. Ukiwa katibu mkuu wa wizara, kula yako ipo kwenye mikataba ya madini nk. Ukiwa daktari uza dawa, hivyo siwashangai. Hiyo ndiyo tabia ambayo hata mdogo akipewa hela kwenda dukani anafikiria ni jinsi gani atapata cha juu. Usipoiba kwenye sehemu yako ya kazi wewe ndiye utakayeonekana FALA. Haya sasa matunda ndiyo hayo!!! Ujanja ujanja kila sehemu

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 24, 2006

    Kuna proof gani kwamba hao ni 'watanzania'? Kuna uwezekano mkubwa tayari wana makaratasi hao kwahiyo siyo wenzetu hata kama wamezaliwa huko!

    Hivi ni coincidence kwamba hao fbi wametoa hizi taarifa wakati wa ziara ya kikwete au?

    Msiwe na wasiwasi bwana, hizi ni rare cases kuiona tanzania kwenye news, wanigeria mbona wanajulikana kwa wizi wa billions kwa miaka mingi na bado wanapeta tu, kazi wanapata, wamarekani wanakwenda kufanya nao biashara etc. Wewe soma kazi watu watakupa acheni visingizio!

    ReplyDelete
  13. Wanigeria wanapeta? Si ukweli. Wanigeria wako wengi sana katika watu weusi. Leo hii hii nilikuwa na Wanigeria wengi ambao kutokana na kuwa na sifa mbaya hakuna anaye taka kuongea nao mambo ya maana.Kila mtu anawaona matapeli. Na hawa Wanigeria naowaongelea ni watu bomba.Kumbuka katika waafrika watano , Mnigeria mmoja.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 24, 2006

    Pole Mkurugenzi(NJAIDI ATHUMANI)Ndio ukubwa huo!
    Salaaam zao Mung'anda.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 24, 2006

    Watanzania wa Houston wanatia aibu. Maswala ya wizi ugenini yanawaharibia watu wengine nafasi za kupata kazi na vyuo.
    Mkumbuke hapa Houston Mtanzania alimuua mwenzake mwaka jana tu, na akaingia mitini hajapatikani hadi leo. Anyway, wengine hapo Houston wamefanya wizi wakafanikiwa kurudi
    na Limo nyumbani. tulieni vijana msiwe kama wanzetu wa West Africa(Nigeria) hawapati admission kwenye colleges tele kwa ajili ya vitu kama hivi.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 24, 2006

    Mnawasema wazungu wa chip. Sawa wameiba, watatumikia vifungo vyao na watatoka na kuendelea na maisha. Wakati sie wabongo tunaka kuwakandia, kuwasagia na kusema maneno machafu wengine wanaendelea na maisha yao na biashara zinazidi kuzaa.

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 24, 2006

    KWELI UGHAIBUNI KUMETUSHINDA MPAKA TUMEKUWA WEZI. KAAAAAAAAAAAAAZI KWELIKWELI.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 24, 2006

    Mimi kuna watu nawashangaa kabisa, kuweka Tanzania kwenye miskendo,tu mimi kwangu ni pigo. Huyu anony wa 6.34AM simuelewi, inawezekana na wewe uko vilevile. Jamani mkisha wekwa kwenye system sijui. watanzania wenyewe hatujaweza kuwa na Elimu za kutegemewa sana kama Nigeria.Vile vile kauchumi kachanga tunategemea hao. Vile vile mimi huwa nikimuona mnageria namuogopa sana na siyo mimi tu ni kila mtu, pamoja na kwamba ni mwafrika mwenzangu. Juzi juzi nilikuwa sehemu nikakutana na mnageria akataka kunitembelea nyumbani, sikumpeleka, tanzania tukifikishwa hapo tutapata shida sana.

    Marekani,Mtu akisema TAnzania unapokelewa utafikiri ni mwizi(bahadhi ya sehemu) nilishangaa. Kumbe ndo tulivyo. Inasikitisha.

    Michuzi inabidi tupige kelele pasporti wafanye utafiti wa kutosha inawezekana wengine si watanzania, pia watoe utambulisho kwa watanzania. Vinginevyo bwana dunia hii watu wangapi wamesoma, Hata ukiwa na Elimu yako kama nchi yenu haina maana na wewe hauna maana.

    Msituharibie nchi yetu maisha yakikataa huku ugaibuni twende nyumbani, kwani si kuna wazee wetu wako vijijini wanalima kahawa, korosho na maisha yanakwenda tu.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 24, 2006

    Nyie aachewani hayo vijana wa chips walitesa sana Houston lakini helewa mmarekani haujamwibia hata kama ni 5yrs watakupata tu. Wanakupa mda utumie ujisahau halafu wanakutokezea .Sasa nawaonea huruma sana hao wabongo sipati picha hapo ndani ya Harris County Jail toba wameshakuwa nyama ya BATA UTAJIJU.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 24, 2006

    Samahanini wananchi, naomba kufahamishwa tafadhali. Huyo Othman Njaidi ndie yule aliyekuwa Radio Clouds?

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 24, 2006

    Ndie huyo huyo aliekuwa wa CLOUUUDS FM.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 24, 2006

    Nyinyi acheni kupiga makelele, tatizo kwamba dili hiyo imegonga lakini ingefanikiwa jamaa wangekamua kwa ajili ya kurudisha TZ hiyo mitaji kama tulivyoshauriwa kufanya na viongozi kuwekeza nchini. Alafu WATZ bado hatuwafikii Wanagireria katika mambo kama hayo hivyo msijisikie vibaya kiasi hicho.Ni dili ya akili labda tu kwa vile zali limeshika moto.tuwaombee jamaa wasipatikane na hatia za kurudishwa nyumbani maana watatiwa kibano sana.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 24, 2006

    Hii habari kutoka darhotwire, inasemekana picha zimechapishwa kwenye magazeti yote ya bongo leo.


    Wabongo waibua usanii kwa Bush USA
    Wabongo wengine maarufu sana huku Bongo wamejaa katika vyombo vya habari kutokana na kuhusika kwao katika skendo la wizi katika kampuni ya Hewlett Packard HP ya Houston.

    Picha za jamaa hao Wabongo hao zimejaa katika magazeti ya Bongo na aliyesuka misheni hilo ametajwa kuwa ni Njaidi Othman Njaidi (35) aliyekuwa mtangazaji maarufu sana nchini.

    Wengine ni Frank Lauwo (35), Misso Canute Temu (30), James Mtae (27) ambao bado hawajakamatwa na wanasakwa kwa udi na uvumba kwa kushiriki katika deal hili.

    Watuhumiwa hao walidaiwa kusuka misheni za kukomba vifaa vya kompyuta, seva, processors, hard drivers, na memory strips katika kampuni hiyo na nyingine ya Exel Logistics (Exel) vyenye thamani ya mamilioni ya dola.

    Njaidi Othman Njaidi, vijana wa FBI wanakula naye sambamba


    Taarifa ya Mwanasheria Mkuu wa Unyamwezini Don DeGabrielle iliwataja Wabongo wengine kuwa ni Wasia Kessi Maya (28), Hussein Omari (24), Ahmed Juma Khalid (30), Frederick Omondi (31) na James Hill (25).

    Kesi yao imefunguliwa Mei 19 mwaka huu ambapo watano katika orodha hiyo; Njaidi, Khalid, Mtae, Omondi na Hill wanadaiwa aidha walishawahi kupiga mzigo katika kampuni hizo au wanaendelea kuchaka kazi.

    Shauri la mmoja wao (Hill) lishatinga Mahakamani na wengine wanatarajiwa kutinga mbele ya jaji Mary Milloy jijini Houston wakati Lauwo na Temu wanadaiwa kuwa wamerejea home TZ.

    Misheni lenyewe lilikuwa kuwa Njaidi na Lauwo walikuwa wanawatumia wenzao kukomba vifaa hivyo kwa kubadilisha lebo na kupelekwa kwao badala ya wateja halisi na kisha kuwapooza kwa mishiko ya kati ya $20,000 hadi $100,000/-.

    Uhalifu huo ulikuwa mbaya hadi baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hao walikuwa wanaficha baadhi ya vifaa vidogo sehemu zao nyeti, kwenye viatu na kutoka navyo kuwauzia jamaa hawa wa Kibongo.

    Soo hili linachunguzwa na kufuatiliwa kwa karibu na Wazee wa kazi FBI na ndembwela hilo linaendelea.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 24, 2006

    anoy 2:08pm.Usia wa kuwekeza nchini haina maana pesa za wizi na kama wakipatikana na hatia lazima jela wataonja na wakitoka wanapigwa bomba bongo..tamaa mbaya sana na ni aibu.Hata kama hatujafikia wanageria ndo tunakoelekea sasa..hata aiport wale immigration officers wanajua tu watanzania nuksi..usishangae kuambiawa hiyo ni aibu kweli fikiria ni jina la raia wa kitanzania linavyoweza kuchafuka ...kumbuka unatolowa hiyo kuna watu pembeni wanasikia na kukupiga macho ya kiwizi and roho juu!!

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 24, 2006

    nafikiri kuwekeza Tanzania siyo kuleta mali za wizi. Tunataka wawekezaji wa kweli, lakini kama unaiba na unasema unakuja kuwekeza ukaende huko watapokaa na wezi. nafikiri hapa lazima watanzania tuelewe kuwa jamani hii ni aibu tupu kwa Tanzania na watanzania wote kwa ujumla yaani ulimwengu wote ujue sisi ni wezi. Kundi hili kutoka Tanzania ni kubwa mno. sasa maskini ya mungu sehemu yoyote tukionyesha kitu Tanzania imani na hawa watu hakuna. badala yake tutaanza kujiita wazanzibar ili kuficha jina la nchi. Kwa hiyo anayesema kuwekeza mali za wizi nafikiri ni mvivu wa kufikiri.

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 24, 2006

    Kama tuhuma hizi ni za kweli, mie nawapa pole waliyofikwa. Hopefully wameweza kufanya ya maana Tanzania kwa hela walizokuwa nazo kama mambo yao kuharibika (if it is the case).

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 24, 2006

    wewe anony wa 2:08 pm walah una matatizo. Ila Watanzania ndio mlivyo wizi mnaita dili. Huo ni wizi ubumbuluke usibumbuluke ni wizi wala mtu huwezi kujisifu kwa kuwa mwizi. Upuuzi mwingine ni kudai eti kwa sababu hatujawafikia Wanaigeria hakuna shida, yaani wewe unaona saifa kushindana na wanaigeria kwa kuwa na sifa mbaya? Ndio maana ujambazi bongo unaota mizizi kwa sababu wenye mawazo kama yako wewe anony ni wengi mno: rushwa, ujambazi, wizi, mikataba feki n.k ni dili na ni sifa

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 24, 2006

    Stealing because of being trusted is awful bacause at the end of the day you will loose that trust. Most of the time the outcome results affect majority in the certain group of people. Sometimes are wrong assumptions. Just think about the permeant global assumptions about Nigerians.
    Most of the stuffs you guys are saying are not far from some kind of truth. But the question is "is this The Breaking News?". Absolutely NOT. So what real happened? The package includes the hatred which was generated from the act, foolishness, behavior, and the talk of the alleged thieves after being mini-millionaires.

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 24, 2006

    Vijana wanaokaa marekani wanasema huo siyo wizi hila ni vipanya panya tu. vilikuwa vinachukua kidogo kidogo. Lakini hili liwe fundisho kwa wazazi/walezi wa watoto bongo msikimbize watoto wenu majuuu wafundishe tabia nzuri hapohapo bongo. Mambo ya kuwapeleka Marekani/Ulaya watoto matokeo yatakuwa hayohayo. Hao wote ukiwafatilia utakuta kuna tatizo.Just wote tuangalie katika kuimalisha chekechea, Msingi na Sekondary zetu, pamoja na vyuo na industries in General hili kuwapunguzia watoto tamaa.

    Wakati mwingine hawakupenda ni matatizo yanayotokea nchini mwetu na kufanya vijana wakakosa matumaini.

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 24, 2006

    Wewe anon wa 7 40 acha kuongea vitu ambavyo havina maana,kupata msingi mzuri sio kwamba wewe ndo hautaweza kuwa mwizi, wazungu ulaya wapo ma seria;l killers, paedophile, bulgrars na ma fraudsters pia...asilimia kubwa hawa wana misingi mizuri... Hiyo ni tabia ya mtu mwenyewe, au makundi anayo ji associate nayo. siyo malezi... Kikwete alikuwa na malezi duni leo mnamheshimu hapo kwenu, na mmepa dhamana ya kuongoza nchi

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 24, 2006

    Huyu anony hapo juu nadhani anaongea pumba kabisa.Huyu nadhani ni Emergencypoison ila anaona nona kuweka tena lile jina lake.Kama sio yeye basi huyu mdogo wake.Malezi huchangia sana yakifuatana na mazingira yanayomzunguka mtu.Ukichunguza behind the curtain ya hao serial killers na wengineo uliowataja utagundua kwamba kuna kitu kilikwenda kombo katika maisha yake.Ila hiyo isiwe excuse,no matter what,mtu anatakiwa kuwa imara zaidi baada ya majaribu na sio kufanya upuuzi kama huu wa kina Njaidi halafu wasingizie eti Tanzania haikuwapa msingi bora au familia zao...

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 24, 2006

    Sawa wameiba hawajafanya jambo zuri, lakini tukumbuke na sisi kwetu tunaibiwa sana na wazungu hasa migodini, hujichotea madini yakutosha na kuondoka nayo kinyemela kwa madai wanaenda kufanya majaribio, majaribio gani mchanga ndege nzima?

    Haya na hawa wizi wa mali ya umma hatuwaoni...tunawaona kina Njaidi tu!!

    Kina Njaidi hawajaiba walikuwa wanajaribu kurudisha kile kilichoibiwa Tanzania.

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 24, 2006

    Huyo Anony wa 7:40 Ana mtindio wa akili. kichwa chake kitakuwa hakifanyi kazi vizuri tunaomba mola amrehemu.

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 24, 2006

    Wengi wa hawa watuhumiwa ni watu wazuri kitabia na kiroho sasa kilichopo hapa ni majungu na wivu usio na msingi na hii inatokana na wenzetu kujijenga haraka haraka kimaisha ni hakika yangu watatoka na kuchukua chao tayari kwa safari ya kwenda nyumbani Tanzania.

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 25, 2006

    Leo hii ujambazi umeshamiri bongo kwa sababu ya mawazo kama yako wewe anony wa 11:19 pm may 24. Watu wanakuwa mamilionea kwa kuazimisha silaha kwa majambazi na kuongea na wakubwa wa polisi ili vijana wao wa kazi wasikamatwe, watu kama wewe mnasifia wana akili na mtu akihoji nyendo zao mnasema wivu!!Hovyo!

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 25, 2006

    Kwani mkurugenzi wa dtv mbona alikuwa na kesi ya wizi kwao huko ugiriki sijui, laknii mzee alikuja kuwekeza bongo, u can't hate on that. Hamna mtanzania aliyeumia kutokana na wizi huu na kuna uwezekano jamaa wangekwenda kuwekeza bongo. Watz tuache wivu na kuchukiana, hatutaendelea kwa hali hii.

    STOP SNITCHING!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 25, 2006

    hao hao wafanyabiashara wa kibongo mnaowa-idolize either wameepuka kodi au wanawalipisha watz 300% over cost kwa sababu wanunuzi wana uelewa mdogo wa bidhaa hizo. Watu wanapeleka bongo limos za '47 na kuweka fees ambazo ni kubwa kuliko limos kali za usa.....utaelezeaje hilo?

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 25, 2006

    Anony 11:19 unasema watatoka na kuchukua kilicho chao nakurudi Bongo? Hiyo sahau. Labda kama wame weka vitu vyao katika jina lamtu mwingine. Na huyo mtu awe ana aminika. Kila kitu wame freeze. Kwa hiyo wakitoka hawa kitu. Inasikitisha sana.

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 25, 2006

    Mimi anony 7.40PM, Nimefurahishwa sana na wale walionishambulia sana lakini warudie kusoma vizuri sentens zangu. niliona jana jioni mawazo yenu anony 8.01Pm, na Anony 8.57PM.

    Anonoy 8.01PM,24 anasema hii inategemea na makundi anayoshirikiana nayo. Na anamuhusisha rais wetu na malezi duni!!!!!!!!!(Amesoma UDSM).

    Anony 8.57PM, 24, Ananifananisha na sumu, amemjibu 8.01PM na kusema kuna kitu kilichokwenda kombo ktk maisha yao na ukiangalia nimesema hicho ktk malezi na akagusia mazingira.

    Anony 10.08PM, 24 nashukuru kwa maono yako.

    Hoja, angalia msemakweli 8.57PM, may 23, Anony 9.17PM, anony 5.56AM may 24, 8.22AM, 9.44AM, 4.02PM, 5.17PM. ukisoma vizuri utagundua kuna tatizo kubwa linaibuka katika jamii ya vijana wa kitanzania wanaokaa ugaibuni.(Mpaka watalii wanaokuja tanzania watatukimbia)

    Hatujaguzsia kuna nchi moja sitahitaja jina waliotembea wataijua, kila kukicha lazima kijana mmoja wa kitanzania afe katika ujambazi.

    Leo hii Sisi wenyewe vijana hata tunakosa imani na bahadhi ya vijana wenzetu tunaoishi nao bahadhi ya sehemu na kusema msituharibie nchi yetu.

    Mimi nina mfano mmoja katika nchi ninayo kaa kuna vijana baada ya kufika hapa walikuwa wameletwa kusoma lakini wakawa hawafanyi kazi yoyote zaidi ya kuwa na waarabu, lakini waarabu wanaweza kusoma mazingira na kujua kama kuna tatizo au la. Maskini watanzania hamna kijana alipokamatwa akataja yeye mrundi. Alifikiri atasamehewa, siku hiyo alifika Burundi, sijui iliishaje.

    Sasa ningependa katika kujibu hoja zangu tuambizane kabla hamjanitukana mngenieleza background ya hao jamaa waliokamatwa then tungeelewana.Kwa sababu nimezungumza kwa kifupi lakini ukiingia kwa undani ukachambua nina maana nyingi. Actual I can write a book on those three words.

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 25, 2006

    anony 1:22am umenifurahisha sana sana kwa sentensi moja tuu kubwa kwamba...WATZ ACHENI VISINGIZIO kamaKAMA UNAQUALIFY KWA NINI USIPATE KAZI? watz kwa kupenda kujiconsole hawajambo bwana wasipate kitu cha kuzungumzia tu utawasikia wameshachukua kama sababu ya FAILURE zao ktk maisha sawa nakubaliana na wote kwamba kitendo walichofanya si kizuri lakini chukua mf. wa ndugu zetu wanigeria kila siku wanaiba tena kwa kiwango cha juu lakini ndio tunasikia kila siku wanagraduate lawyers,doctors na kazi za kumwaga, watz wakati umefika kuamka na kuface reality kwamba sisi ndio tatizo tufanye nini tuwe kama wenzetu wengine wanaondelea kwa kukubali kukutana na magumu mbele yao ilimradi tu wafanikiwe ktk wayatakayo? (CHEAP IS EXPENSIVE)na kila jambo linatokea kwa sababu watz muache mawazo ya kukalia kufanya kazi za kwenye mawarehouse fikirieni zaidi nini mfanye mfanikiwe.

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 25, 2006

    big deal?
    nasikia wote wapo hapa Milton keynes UK wamejilipua

    ReplyDelete
  42. AnonymousMay 25, 2006

    Duh nusu yao ni WACHAGA duh sasa...........Je sisiiii wachagaaa tutapata Visa kweliiii

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 25, 2006

    Wapumbavu sana nyinyi mnaolalamika hapo juu. Wazungu wanatuibia sisi kila siku, sisi tukiwaibia wao ndo mnaona ishu. Hawa jamaa wa kibongo kwa mtazamo wangu ni mashujaa na wanastahili sifa, heshima na msaada wa kisheria kutoka kwa Tanzania na Watanzania wote. Ondokaneni na utumwa wenu wa kiakili wa kuabudu wageni.

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 25, 2006

    Zote hizo ni style ya struggle ya maisha duniani humu tu. Amekwapua prof Mahalu 2 billion ubalozini Italy hamjaona wizi huo ila huu wa hawa vijana mnawaona hawafai. Nani asiye na mission ya maisha anakofanyia kazi aorodheshe jina lake hapa. Watanzania serikalini wanaisha kwa mshahara wa sh 67,000 kwa mwezi na mtu ana watoto saba, anaishi nyumba ya kupanga na watoto wote wanaenda shule anaishije mtu kama huyu kama sio mwizi.Tuache kuongea tu kwa vile tuna midomo na vidole vya kutype hapa. Asiye mwizi aorodheshe jina lake hapa na sehemu anakofanyia kazi. Hata wabeba Mabox na waosha vikongwe wana mission za ajabu kazini kwao.

    ReplyDelete
  45. AnonymousMay 25, 2006

    Unajua Grill umekosa mwelekeo. Huwezi kuhalalisha wizi kwa kuwa mwizi. Aliyekwambia wizi wa Mahalu watu hawakuuona ni nani, au ulitaka wamchome moto ndio ujue kuwa wamekerwa na kitendo hicho? Unachotuambia hapa hata wale majambazi wa pale Ubungo nao walikuwa na mission ukianzia na watu wandani walioshirikiana nao? Wewe ndio unatype kwa vile una vidole. Ila mawazo yako ni hatari kama ukoma. Nakataa katakata kuwa sehemu ya watu wanaojitaqmbbulisha na wizi kuwa ndio sehemu ya maisha yao.

    ReplyDelete
  46. AnonymousMay 25, 2006

    He bwana Grill naye tena kahalarisha ujambazi? ndugu yangu hii haifai unafikiri hawa jamaa hizo hela zingeishia wapi ka si kuharibu watoto wa watu tu????????+

    ReplyDelete
  47. AnonymousMay 25, 2006

    Taratibu tunaanza kuona rangi zao. Huyu Grill naye kutokana na mawazo yake ni mwizi. Bila shaka ndio master mind wa tukio lile la Ubungo. Kumbuka lakini za mwizi ni arobaini, ukiiba nikakuona lazima niwatonye FBI, kwanza hapa mimi nitapa hela halali siyo ya wizi kama yako.

    ReplyDelete
  48. AnonymousMay 25, 2006

    NYIE MWASEMA TU HAPA NAANGALIA BREAKING NEWS YA ENRON TRIAL JAMAA IS GUILTY FOR WHAT HE DID,sasa huyu naye alilelewa vibaya huyu mtu usikute alikuwa na malengo yake na hela ya haraka haraka, sio nzuri lakini msijifanye hapa mnachonga sanaa ohh malezi sijui yamefanyaje? mara msikimbize watoto ulaya na kwanini mkae mnaongelea ambao wanamess maisha na kuacha wanaofanya mazuri? acheni kujifariji kwa situation za kijinga,kuna watz majuu wanafanya mambo makubwa wana income za .08m to 150 na zaidi in a yr HALALI ambazo hata prof achia mbali mawaziri tz hapati unless kaiba..... hivyo wazazi wala msistushwe na haya kuna vijana wenu wanafanya vizuri tu na pia si kufanya vizuri ktk kupata mkate wao wa kila siku bali wanapata exposure ya juu sana asikudanye mtu kuna mambo mengi sana unaweza ukadhani unayajua ukiwa huko mwanangu ukikanyaga arhi za wenzetu na kupata challenge kubwa unashangaa ni kweli wenzetu wameendelea hata katika mambo madogo madogo sana ambayo huwezi kudhani ni ustaarabu tukiwa nyumbani lakini pia si kwamba ni wote hivyo kila mahali kuna watu wa kila makundi.

    ReplyDelete
  49. AnonymousMay 25, 2006

    Hawa watu kama Grill ndio watamu sana kuchoma moto ngoja tukushike tu pale mitaa ya posta ukiwa kazini tutakushughulikia! Hawa waliofanya upuuzi huku US ni sawa tu na vibaka pale bongo ila wanaigharimu zaidi nchi yetu na vijana wake kwa hiyo wanatakiwa wachomwe taratibu ili wapate fundisho. Acheni tamaa za fedha na kufananishana na wanigeria ili tu ku "justify" ukibaka wa akina njaidi

    ReplyDelete
  50. AnonymousMay 25, 2006

    Anony. 7.25PM nafikiri hakuna ambaye hajui kwamba watu wapo ulaya /marekani na wanafanya vizuri wanachotaka kusema ni vizuri ukienda huko uwe umekomaa kimawazo/umeisha elewa unafanya nini. Kuna watu wanafanya vitu ukimuona unajua tu lazima akamatwe na anaendelea kufanya.nafikiri hiki ndicho kinaongelewa hapa.Kuna watu wengi wanafanya mambo mazuri mazuri tu na hata Anony mbalimbali wanaolalamika wako ulaya/marekani na wanafaya vizuri tu. lakini kuna wazazi wengine mtoto anamaliza darasa la saba anakimbilia ulaya/marekani si vibaya lakini mpime kwanza na ujue je ameisha komaa. Miji hii ni migumu sana. lakini si migumu kwa watu wenye elimu zao. hata hao wanageria wanaofanya mambo yao wanatumia utaharamu wa hari ya juu(siwasapoti) wanageria.

    ReplyDelete
  51. AnonymousMay 25, 2006

    Jamani nimesema na anayejiona anafanyakazi haki bini haki aandike jina lake hapa na anakofanya kazi mbona mnaishia kuongea yanayoelea hewani tu. Hawa jamaa usiwalinganishe na majambazi, hawajavunja na hawajatumia nguvu ila ubongo tu na shule walionayo.We unafikiria bila michoro ya kueleweka unaweza kufanya kitu kama hicho. Hata yesu alisema, NA ALIYE SAFI AWE WA KWANZA KUMTUPIA JIWE MWANAMKE YULE MZINZI. Hakujitokeza hata mmoja watu mnaishi maisha ya mnayoyajua wenyewe siku likimbumburuka ndio kama hivyo tena vijana wananyea ndoo.

    ReplyDelete
  52. AnonymousMay 25, 2006

    Grill unataka tukutajie kazi zetu ili uje utuibie? Hapo umepiga chini hutajiwi hapa. Ila wewe na wenziyo endeleeni na sitaili yenu hiyo ya maisha. Lakini usianze kutuletea hekaya hapa ati kwa sababu kuna wengi wanaiba ndio uwe mtindo wa maisha ya Mtanzania. Wewe unayechafua jina la Watanzania kwangu ni sawa tu na jambazi maana kula ya halali ya Watanzania inategemea jina hilo likiwa safi.

    ReplyDelete
  53. AnonymousMay 26, 2006

    Yaani wewe Anony wa hapo juu na wenzio mnanisikitisha sana.Unajua wote mnaopinga kitendo cha hawa jamaa ndio njie mnaoishi maisha ya kufikiria kuwa mnaishi kwa kupendelewa kumbe ni haki yenu. Kama mtu una utaalamu wa kueleweka na shule unayo ya nini kufikiria kuwa hawa jamaa wanawaponza. Shule yako itaditamin maisha yako. Kama una utaalaamu unaoeleweka hakuna atayeangalia unatoka nchi gani.Suala ni is your competence jamani.Hawa wazungu wanatuibia sana na hakuna fairness huku duniani. Unajua 23 to 87% ya natural resourses za dunia yote zinatoka africa? kwa nini sisi africa ni maskini kuliko mabara yote?.Mimi hapa nilipo nafanya kazi kama developer na napata pound 60,000 p.a lakini ukiangalia saving nayofanya hakuna. Natumia hela hiyo hiyo kuishi na familia yangu na kutuma kwa wazazi wangu walio bongo na migarama mingine ya kuishi nchi za watu.sasa fikiria ningekuwa nipo kwetu na mshahara kama huo ningesave kiasi gani. Naomba muache mawazo kuwa mnachofanya huku kuwa ni fever ni haki yako kutokana na ujuzi wako. Kama unaishi maisha unayofikiria kuwa ni fever bora urudi kwenu ukawe machinga utaishi kwa furaha zaidi.

    ReplyDelete
  54. AnonymousMay 26, 2006

    Haya mambo ya kuwa Jina la Tanzania linachafuliwa inabidi tuache kujidanganya wizi wa watu wachache hauna uhusiano na Tanzania. kama ni hivyo basi Wahindi na Wanageria wasigefanya kitu hapa duniani na hao ndio wako world bank nakila sehemu muhimu.Hii ilikuwa very assoleted move vijana wakibongo wamesogezana katika kibarua kimoja wakataka kutumia wingi wao kujinufaisha maji yakazidi Unga,"Period" Tuache ujinga na Ujamaa wakiali.Tanzania haitachafuliwa jina na watu 9

    seti mbili zangu..

    ReplyDelete
  55. AnonymousMay 26, 2006

    wewe anony 5.08PM umeandika bila kufikiri kidogo, wazungu wanachotuibia sisi waafrica ni katika mikataba ambayo sisi kwa njaa zetu na upumbavu wetu tuna sign kwasababu ya 10% na ndio maana hawakamatwi! sasa wewe mswahili unaiba kwa kupindisha address na kuweka processor kwenye mifuko ni upumbavu na hakuna haja ya kuwatetea hawa watu.

    ReplyDelete
  56. AnonymousMay 26, 2006

    Mimi nafikiri tunawaonea wahindi na wanageria kufanya kazi katika mashirika makubwa wakati ni wezi. Kuna mtu mmoja amesema kitu cha maana sana hawa jamaa wameweza kwa sababu ni competent. Nenda dunia nzima kila sehemu utamkuta mhindi angalia wanajua nini they are real competent. Vile vile nafikiri wanageria wengi wameweza kusoma vya kutosha na kufikia wakati wa kuwa vinara. michoro niliyoiona hawa jamaa wanafanya kwanza siyo ngeni kwa tanzania ilikuwa inafanyika wakati wa mwinyi sasa hivi imepitwa na wakati na ndio jamaa walikuwa wanafanya marekani.

    jamani tutafika ulimwengu wa sasa. Mimi nafikiri tukubali mahisha ni magumu lakini vilevile kuwa magumu kuna njia nyingi sana za kujipatia kipato, watanzania tufanye planning. Tuwekeze katika akili zetu vya kutosha hili tuweze kufanya kazi zinazo dhaminika. anayeniambia kuwa jina Tanzania likialibika siyo yeye anajidanganya. wewe ukifika marekani ukaambiwa kama ni mtanzania njia yako ni hii ambayo ni tofauti na wengine kweli unajisikiaje. analess wewe siyo mtu wa kawaida. wengine huwa tunajisikia vibaya.

    Je hilo siyo kuaribu jina la nchi pamoja na watanzania kwa ujumla?

    nafikiri tutafte njia halali za kuishi na kupambana na karne hizi za sayansi na tech lakini tukiwa na mawazo kwamba wizi/ujambazi utatufikisha mbali hatutafika kabisaaaa. Naomba wote tuupige vita na vijana mlipo tafuta mbinu mbalimbali za kusaidiana kufika mbali na zisiwe ujambazi. grill saidia kwa hili na si vinginevyo.

    ReplyDelete
  57. AnonymousMay 26, 2006

    Jamani mie sijasupport wizi na ujamabazi ila nachosema tusiwakumu kuwa hawa jamaa hawafai kwa waliofanya, tujiangalie na sisi tunayofanya lolote laweza na kukupata kwenye shughuli zako na sisi tukakuhukumu vile vile. Usihukumu kabla hujahukumiwa.Suala la nationla reputation mimi siliafiki kabisa ingekuwa matokeo kama haya yanamata watu wa nigeria na india wangekuwa na hali mbaya sana dunian. Wewe lalia kwenye utaalamu wako tu utakubalika bila kuangalia unatoka wapi bwana.

    ReplyDelete
  58. AnonymousMay 26, 2006

    Nafikri tumemuelewa gril na anony 11.32AM, ni kwamba katika ulimwengu wa sasa ambapo kuna kusigana katika maendeleo mambo kama akina njaidi hayaepukiki. Ni mambo ambayo tutakuwa tunatembea nayo kama ilivyo india na Nigeria. Kwa maana hiyo katika ulimwengu huu ukitaka nchi Tanzania ndio iwe kioo chako cha kukusaidia katika kuishi umeliwa.

    Kinacho hitajika wewe jitahidi ulipo ufikie wakati hata kama kwenye kampuni unayofanyia kama mtanzania amefanya kosa wewe ubaki unapeta.

    Na hili kufikia hapo pigana kufa na kupona kama wewe ni programma piga code, kama wewe ni researcher piga kitabu gundua, kama wewe ni mfagizi bwana fagia mpaka watu wapende(hata maji waweze kunyea chooni), kama wewe ni mcheza mpira cheza tuu kama maradona.

    Hakuna atakaye kufukuza kwa sababu fulani mtanzania kaiba chaki/stationale shule za marekani/uingereza. Piga mzigo wanangu. Hata kwa mzee bush utakaribishwa tu pamoja na kuwa mtanzania

    ReplyDelete
  59. AnonymousMay 26, 2006

    Wewe anony wa 7:14 na Grill mnapenda sana majibu rahisi kwa maswali magumu. Hiyo dunia yenu mnayoishi ni ya utopia na kusadikika. Mnatuleta habari za ukishakuwa ndani ya sisitimu wakati siye tunakuelezeni habari ya first timas. Kulinganisha na Wahindi na Wanaigeria ni upuuzi. Hawa watu tayari wako wengi mno kila sehemu, iwe vyuo vikuu na kwenye makampuni. Unatarajia Mhindi anayeeenda kuomba kazi kwenye University anakutana na asilimia 50 ya falkati ni Wahindi anyimwe kazi ati kwa sababu jina lao ni chafu? Vivyo hivyo Mnigeria. Sasa wewe mbongo unayetegemea credential zako tu plus sifa mbaya ya wizi utaweza kushindana na watu hawa? Kuna Watanzania wangapi nje wanaoweza kupambana na Wahindi na Wanaigeria?
    Hata hapa nyumbani Tanzania tunajua kabasi kuna makabila yana julikana kwa sifa mbaya, kabila fulani wana roho mbaya, kabila fulani wezi, kabila fulani wavivu, ni ujinga kudhani sifa hizi haziathiri nafasi za watu. Lakini ndio kusema watu kutoka makabila yanayotajwa hawapati kazi? La hasha unakuta ndio wanaongoza kwa wingi makazini. Kwenda kuomba kazi na mtu ambaye anasifika kwa ubaya lakini ana Godi fazas unatakiwa uwe na sifa ya ziada nayo ni jina zuri. Vinginevyo hizo mnazotuambia kuwa eti kisomo chako, sijui nini ni takataka, Watanzania siyo watu pekee waliosoma hapa duniani, na tena elimu iko chini sana.

    ReplyDelete
  60. AnonymousMay 26, 2006

    Wewe Anony wa 9:37 Pm kwa nini na sisi WaTZ tusiwe wengi kwenye hizo sehemu ulizotaja kama wanaigeria na waindia. Hivi unategemea kama umeitwa kwenye interview na mnaigeria na mhindi basi wewe MTZ utakuwa huna chako? hilo sio kweli kabisa. Naomba WaTz tuache kujiona inferia ukilinganisha na watu wengine.Sioni kuna sababu gani inayotuzuia tusicompiti na hao wengine. Watz tuache ubabaishaji kama wewe ni mtaalamu jitahidi uwe mtaalamu kweli kweli si issue ya kubabia babia tu. Naomba tuondoe hayo mawazo ya infiria tafadhali kwa sababu tutaendelea kuishi maisha ya kutegemea zaidi fever.

    ReplyDelete
  61. AnonymousMay 27, 2006

    Wewe Anony wa 9:37 Pm tunacho sema sisi nikuwa huu Uguilty by assocition sisi ndio tunapinga hatusemi kuwa hawa watu 9 hawakufanya makosa lakini tusijishushe Utanzania wetu "eti Tunaharibiana" ukiweka list ya nchi wezi duniani tanzania itakuwa karibu na mwisho kama si mwisho kama ilivyo katika list ya umasikini.Usiwatie Fear wabongo na wezi wa 2.9m ,WaNageria,wahindi Warusi wanapeta hata baada ya kuibia CityBank,Social security System Na Pentangon(Sana sana walipewa kazi huko huko ya kulinda wasiibiwe tena).

    Seti mbili zangu...

    ReplyDelete
  62. AnonymousMay 27, 2006

    Mimi anony wa 7.14Pm 26, Anony wa 9.37Pm unachosema ni sawa lakini siyo practical kwa sasa. Ukiangalia mbali wote na wengine hata na mimi tulikuwa na mawazo kama ya kwako. Lakini sasa hivi tunaishi katika jumuiya kubwa mno, ambapo watu tuna background tofauti, kipato tofauti, elimu tofauti. Wewe ukitegemea Mtanzania ambaye amebahatika kufika ulaya aishi kama wewe ambaye ni haki labda umekuja kimasomo/ umesoma unakazi yako, itakuwa ni kujidanganya haitawezekama ndugu yangu. Ukifika hapa wanakwambia maji ukiyavulia huna budi kuoga.

    Unatafuta solution, solution iliyopo bwana ni kufanya kweli, mambo ya godi farther/kujuana yako sana sana lakini kuyavuka tu ni kuhakikisha bwana unajiweka sawa. Katika group nililokwambia usitegemee wahishi ulaya/marekani kwa kukufikiria wewe unayeenda kuomba kazi.

    Kwa maana hiyo ndugu yangu cha kutusaidia wewe ukibahatika ukapata sehemu ya kujibanza piga mzigo hata mnageria/Mhindi atamani kukuweka kwake.

    Watanzania tukifikia hapo tutashindana taratibu na kadri miaka inavyokwenda wote tukipigana tutafika mahara hata huku majuu tutasaidiana. lakini hakuna atakayesaidia mwenzake kama wote tunategemea godi father.

    Piga mizigo wajomba/ uchumi wetu bado ni tegemezi hata wamarekani wanaiba madini congo/Mafuta Irak na kwingineko lakini sijasema watanzania muibe. halafu ni vibaya kuiba kwenye nchi yako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...