Home
Unlabelled
mayenga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
na kulia nani? Au hiko toka Arabuni kupata ubunge? Au ndio fadhili ya huyo Lushy make nilifikiri Oshama yahye?
ReplyDeleteAnony huoni shati ya kijani, ni mjumbe wa sekretarieti ya uwezashaji wa akina mama wa ccm pemba
ReplyDeleteMichuzi, huyo mwenye madevu ni nani?
ReplyDeletetena huyo myenga mrembo kuliko amina ha ha ha ha ha angalieni msije kuwa chakula ya vakuba hapooo chimwaga.
ReplyDeleteDu! Jane Mihanji yuko serious!
ReplyDeleteHuyo Madevu anaitwa Amar.Alisomea Tambaza enzi za 90's
ReplyDeleteShukrani kwa kutuletea Lucy Mayenga.
ReplyDeleteSijajua saaana kama kunyoa ndevu ama kufuga ni utamaduni wa watu flani ama la. Ila kitu kikizidi nako haipendezi. Jamaa ashauriwe kupunguza angalau kidogo, maana duh, zikiendelea atajikuta mdomo na macho tu ndio vinasalia. Huyo Jane anatia huruma !!!!!!!!!!!
ReplyDeletendesanjo, kama anony 6:29 alivyosema, huyu ni amar; mwanaharakati mashuhuri wa ccm vijana dar. baba yake ndiye aliyeendesha islam bucha pale mtaa wa aggrey na pia ni mlezi wa timu ya vijana 'kabaka yeka' ya ilala mtaa wa shauri moyo.
ReplyDeleteNa Osama pia alialikwa ! anaona anacheka hapa mi nakwenda kugombea ubunge kwao sasa nione itakuwaje
ReplyDeleteShukrani Michuzi na anony 6:29.
ReplyDeleteNaomba kuuliza "Hivi wawakilishi wa vijana bungeni ndio Lucy na Amina peke yao au?" Bora Lucy angalau nasikia ana Diploma ya uhusiano wa kimataifa na diploma ya uandishi wa habari lakini bado anatakiwa kwenda shule ili aweze kuendana na hali halisi. Naomba mumshauri nae Lucy afanye mipango ya shule ili aweze kutuwakilisha inavyotakiwa na aweze kuendana na hali halisi ya mazingira ya kisasa dunia.
ReplyDeletevipi lucy ameshaolewa? nataka niwe kama Mpakanjia, mume wa muheshimiwa.
ReplyDeletelakini tanzania ina utani tutakuja tawaliwa na kopo we acha tu.
ReplyDeleteHivi vyote VITAFUNIO vya wazee hapo Dom hakuna cha uwakilishi wala nini.
ReplyDeleteGrill naona una matatizo, mtu ana diploma bado unataka aende shule. Hebu tupe kiwango cha elimu ambacho mtu anapaswa awe ili uridhike kwamba amefuta ujinga. Vile vile sio vibaya nikijua wewe una ka basic degree, ka masters au una RI PHD. Natanguliza shukurani
ReplyDeleteHivi anony hapo juu ordinary diploma na form six au form four kuna tofauti.Naomba utofautishe Advance diploma na ordinary diploma. Mie elimu niliyo nayo ni ile inayokubalika popote pale dunian bila vimaswali maswali.
ReplyDeleteMarehemu Walter Sisulu hakwenda shule lakini alifanya kazi kubwa za ukombozi pamoja na kumfunza Mandela kazi ya sheria.
ReplyDeleteMwandani
ReplyDeleteUnazungumzia dunia ipi ya leo au ya zamani? Tuwe na uwezo wa kutofautisha utawala wa akina Kawawa na Nyerere na utawala wa Lowassa na Kikweke. Mazingira tofauti kabisa.
Grill nina wasi wasi si ajabu una degree kama za Mrema. Eleza vizuri elimu inayotambulika duniani ni ipi na umeipata wapi? Sio unakuwa na degree za online halafu unabaki kukosoa wenzako
ReplyDeleteWe anony naona una matatizo, sasa sikiliza nenda mlimani ulize profile za watu waliokaa room 31 hall one block A, ukitoka mlimani nenda Glasgow University ulizie jamaa waliokuwa na admin no inayaishia 86, waulize glasgow jamaa alikaa muda gani na aliondoka lini na sasa yupo wapi, sawa DOGO.
ReplyDeleteNaona mnatamba na degree uchwara wote hee mmara mlimani hoo mara glasgow university, je tutafute jina lako kwenye internet una chochote au degree tu basi. Profile bwana umefanya nini, sema tu. Weka kikwete uone bwana kila yahoo, google, hata ka search engine kadogo katakuletea.haina haja ya kwenda kwenye mafaile. hapa hapa google tupe, jina na reg.mambo kwisha. Siku hizi mambo ya mtandao type Mrema lakini lazima umalizie Agustino na Lyatonga.
ReplyDeleteNyie watu humu ndani ni kama wapumbavu, diploma ni elimu ya juu sana kumfuata mtu ujinga, sasa nyie kazi kumuandama amina na huyo lucy... Mbona maprofesa wenu kama mbilinyi ambao wamesoma mpaka wameota vipara hawana chochote hikija kwenye swala la uongozi. Kuna mtu anaitwa Mtikila (mtanganyika halisi) Hana elimu ya chuo kikuu wala nini wala nini lakini anajua sheria kama nini... Humu kuna watu wanawivu wameenda shule mno na wanashindwa kupata kazi kwahiyo wakiona mtu kayatoa na elimu ya chini kushinda wao wanakuwa na roho ya kwanini. Pumbavu kabisa
ReplyDeleteWewe anon wa 9.00 ni mshamba wa kijijini kabisa... Sasa kumtafuta mtu kwenye google na kumpata nado inamaanisha kafanikiwa.usiwe mjinga wewe kuna watu kibao wamefanikiwa na majna yao hayapo. Kupata jina la kikwete kwenye search engine ni lazima kwasababu ni kiongozi wa nchi. Sasa kwasababu wewe ni mpumbavu mno mimi ni mtoto wa bakhresa na nimesoma hili niendeleze mali a nyumbani sasa andika kwenye google jina langu ni khalid kama utanipata.Nina mba mnayoisema kwamba hukiwa nayo ndo umefanikiwa na jina lako litakuwa kwenye google.
ReplyDeletesawa bwana wewe toto la basesa ulizo wewe soma glasglow shijui iko nhi gani shomea bunge au wajiri au nini? mimi jua Kidiploma tosa kabisha fanyikiwa siyo pesa. Mimi hapa kijijini nilipo nalima ukijua kusoma tuu mkubwa. sasa Diploma naona huyo yuko mbali mno. Hila wewe una online course make pale mlimani hakuna mtoto wa Bharesa amesomea pale. Toto bharesa pata degree nje tu soma sekondari gani wewe. Ni rahisi kukupata. On line siyo kufanyikiwa ukisoma chuo fulani siku hizi unakuwa online tafuta mwanafunzi wa University of Dar type utampata. Online hawapatikani wenye pesa au wanasiasa tuuuuuu.labda kama arobaini na saba sijui.Ukisoma especially masters Unaandika diserta..., inakuwa kwenye database usionekane. Tena chuo cha majuu we naona unacheza kweli vyeti vya online tuuuuuuu.
ReplyDeleteGrill acha kujifagilia, nafikiri bado na wewe unahitaji kujiendeleza hako post graduate diploma sidhani kama kanatosha. Record za mlimani zinaonyesha kwamba room uliyokuwa unaishi wanafunzi walipigana kugombania house girl waliyekuwa wamemwajiri kuwapikia. Hebu jisafishe kwamba sio wewe. Natanguliza shukurani
ReplyDeleteHaki ya nani watanzania tunatakiwa kuanza kuchapana viboko angalau tutakuwa na mawazo tofauti. Watu wengine argument zao Mmmm! Hawa wote ni vijana ambao Mama Tanganyika inawategemea kwa maendeleo ya siku zijazo. Halafu tunakimbilia tupunguze wazee kwenye system, kwa vijana wepi hawa wanaotoa mawazo humu au tukaazime nchi nyingine?
ReplyDeleteHuyu anon wa online ni mshamba mno sasa kumpata mtu kwenye search engine ndo nini mbona wanafunzi uni of dar wapo online type liberatus kaegele uone basi.Inaonekan wewe ni wakuja kweli. Umeanza kutumia mtandao karibuni nini
ReplyDeleteMimi na huyo anayejihita amesoma master kama ni wewe bahati mbaya hujanielewa kwanza wewe pumzika kabisaaaa. Hata siasa huziwezi wewe muulize mzee msekwa atakwambia. Umeambiwa degree ya online matusi debe. Hiyo tu inaonyesha hiyo degree ilivyo nayo kweli ya online. Hata uvumilivu huna. Kwa taarifa yako ukisoma nje ya nchi siku hizi unaandika kazi ya mwisho ambayo huwa kwa vyuo vya kisasa vinaweka kumbukumbu na kumbukumbu zinawekwa kwenye mtandao hata ka kichwa. Lakini ukipata zile degree za mtu kutoka marekani akakuletea huku kwetu karagwe cheti huwa hakiandikwi popote. Ndio nilicho maanisha. Kutumia enternet siyo dili kubwa mimi nimeona computa juzi tu kwa hiyo siwezi kuwa na uwezo mkubwa wa kutumia internet. Chuo kikuu cha Dar bahadhi ya wanafunzi wanatumia Teil(sijui kama nimepatia), kama ipo mpaka sasa kwa hiyo ili uwezi kupata material lazima ufanye registration, na master time table inakuwa na wanafunzi ambao huwa wanachukua somo fulani. Ni rahisi kupatikana. Enewei mimi sasa hivi kama nilivyosema niko kijijini nalima matunda mambo ya mjini siyajui vizuri ndo maana naweza kuwa mshamba kwa bahadhi ya mambo. Lakini sijalala sana, kama nilivyosema uchaguzi ujao najiandaa kugombea katika shina langu. kama umepata degree ya online huna haja ya kuletewa cheti naweza kukuvisha taji na kukupa cheti kwa kutumia msword. Hii ni burudani asante mzee Michuzi!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteHahahahaha Anony wa 10:29 yaelekea hata pale mlimani unapasoma tu kwenye magazeti kule kwenye vile vyumba tulikuwa hutujipikii kaka, sasa sijui hiyo ya kuajiri msichana ni ya wapi. Yaelekea ule mlima unausoma kwenye magazeti tu. Lakini hata vilaza wenzio ambao hawakufanikiwa kwenda pale huwa wanapitaga na kuuliza kuwa watu wanaishije pale.Kuweza kuupanda ule mlima sio lelemama. Uwe unapita pita pale na kuangalia mazingira yake hawatakufukuza.
ReplyDeleteJamani hii issue mnayochokonoa ya degree za online mtafanya mawaziri wenu wafe kwa pressure maana kibao wanazo hizo Dr za online. Msije mkamshitua JK akapitia CV zao upya na kuleta balaa. Mie hapo sipo shauri yenu. Angalieni hilo baraza la mawaziri lina DR wangapi wenye elimu za online.
ReplyDeletempenzi wake yuko marekani ni kijana wa mheshimiwa mmoja aliyekuwa enzi za Ally Hassan Mwinyi
ReplyDeleteHIVI NYIE MANONY MNAOBISHANA HAPO JUU NI HUYO HUYO MMOJA ANAANDIKA NA KUJIJIBU AU NDIO KUNDI LA WATU KILA MTU AMEKAA KABISA KWENYE MTANDAO KUJIBISHANA NA MTU ASIYEMJUA? HA HA HA HA HA KUMBE WOTE MAZUMBUKUKU KABISA TAFUTENI MENGINE YA KUFANYA ETI MTU ANAKAA KUJAZA PAGE KUJIONYESHA YEYE ZAIDI,NINGEPENDA KUJUA NI MMOJA TU NDIO ANAPOTEZA MUDA KUANDIKA NA KUJIJIBU LAKINI KAMA NI WENGI KALAGHABAHO.
ReplyDeleteHuyu Dada anaonekana ametulia lakini DUh sio kama AC. Kwa hiyo hajaolewa maskini wee mie namshauri aingalie sana hiyo mizee ya ssm isije kumharibia maisha huko Dom.
ReplyDeleteMAVI MATUPU ETI NINI???????? AWE WAZIRI WA MAMBO YA NJE?????? ATAONGEA NINI NA MATAIFA YA NJE??? ACHENI AKILI FINYU NYIE HUYO BADO KABISA NA ATA UWAZIRI HAUMFAI.BONGO VIONGOZI WOTE SIFURI NDIO MAANA MIKATABA MNAYO INGIA, NCHI ZA NJE NDIO WANANUFAIKA BADALA YA WABONGO.YOTE HII NI KUWA NA WABUNGE, MAWAZIRI, MARAIS MBUMBU TU. ZIRO ZIRO KILA KONA
ReplyDeletezemarcopolo tunaomba fungua brogi yako nguvu haitoshi kuishia kutoa maoni tu.tunasubiria
ReplyDeleteKuna mtu eti tikila wa watu ana kadiploma lakini hoja nzito. We ni mtanganyika kweli au umechanganyikiwa. Wengine eti elimu ya huyu dada tosha tosha kabisa. mimi siwaelewi kabisaaaaa!!!!!!!!. Usilinganishe Diploma ya Mtikila na huyu dada nenda kamuulize mtikila mwalimu aliyekuwa anamfundisha alikuwa anaishi wapi? hata wa primary tu. Kama hakuwa ndo bora sehemu aliyokuwa anaishi mtikila. Kwa sasa hivi ukiwa na diploma saizi yako ni kugombea mwisho udiwani tena tutapiga kelele ili watu kama hawa wasitumie bule pesa za walipa kodi. Tena kipindi cha vyeti feki sikia mwingine anasema hata mawaziri wana vyeti vya PhD ya online. Maskini ndo maana mashirika na mikataba feki imejaa bongo.
ReplyDeleteKweli Zemarcopolo wewe inabidi kweli sijui tukuiteje, make nashindwa. Unajua mpaka mtu unampa Waziri wa mambo ya nje? Wakati hakusoma. Mimi hizi zootee za kuweka watu ambao hawakusoma katika ngazi kama hizi naziita kama robbery. Haiana tofauti na wale wanaotafuta hela kwa mkato na kuamua kwenda kuiba. Hebu fikiria nilisikia Eti Amina kaenda pale chuo kikuu. Kama siyo kuua elimu nini? Wewe mtu hakusoma anaenda chuo kikuu kuwaambia nini watoto wa watu waache shule wamfuateee? Badala ya chuo kikuu kumfuata wakamwambia akasome?. Mimi nafikiri kuna baadhi ya akina mama wameteka dhana nzima ya upendeleo. Sasa siyo upendeleo hila ni kupendwa.
ReplyDeleteGrill mmhhhhhhh!!!! mbona uko so negative! dada ana diploma nafikiri inatosha. Kumbuka uongozi sio elimu eg prof. sarungi et al. Hauitaji shahada kumi kuongoza watu ni kipaji. I rest my case! mzee michuzi pole sana na kazi kuna bin adam wa ajabu sana hapa.
ReplyDeletelucy is now going to school for political science, she is a very good candidate for secretariate position in the future.
ReplyDeletehuyo lucy hajaolewa wala hana mchumba wala hana wazo. yeye na kazi tu. laiti mngemjua ni dada poa saaaaaannnnnnaaa. nilisoma na mdogo wake kilakala.
ReplyDeleteI can agree with the last comment. if she has decided to go for further studies, that good option. Mtoto wa watu wasimudanganye kuwa diploma inatosha. Ilikuwa inatosha zamani kwa baba zetu na babu zetu. Lakini kizazi hiki sina uhakika kama inatosha. Mweshimiwa anaweza kusoma wakati anatumikia bunge. Na pia utakuwa mfano mzuri hata kwa vijana wanasiasa ambao wanafikiria kama mk na ambao hawajafikiria kujiendeleza. Shule zipo nyingi tunataka vijana wetu waige mifano mizuri. Good mweshimiwa mbunge na kila la kheri katika kuendelea na degree yako.
ReplyDeleteSafi sana kama ana wazo hilo, ubunge na shule poa sana. Mk nadhani humtakii mema Lucy na vijana wote wa Tz. Hivi unadhani sisi vijana tusingefurahi sana mwakilishi wetu angechaguliwa kuwa waziri wa kazi na vijana vile. Sasa kwa nini wawakilishi wetu hakuna hata mmoja alichanguliwa waziri au JK alipendelea. Lucy tunakutegemea sana wewe piga shule na huo uzoefu wa ubunge baada ya miaka mitano utaona matokeo yake achana na mawazo ya akina MK wasiopenda kuwaona wenzao wakielekea njia nzuri.
ReplyDeleteWaliosoma na kupata ma degree yao kama Grill hakuna lolote la maana wanalofanya kwa jamii, wamebakia kujisifia tu. Kuingia kwenye siasa hawawezi, wamebakia kukosoa kuwa wabunge hawajasoma. Jitokezeni basi ili bunge la 2010 liwe la wasomi waliobobea. Itapendeza kama Mheshimiwa Dr (PHD) Grill atakuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge ya kupitia upya mikataba yote ya madini. Anza kujipanga mapema
ReplyDeleteWewe anony hapo juu umeshaona maisha ni siasa peke yake pole sana. Sio lazima wote tuwe wanasiasa kaka kuna sector nyingi.
ReplyDeleteKuna sector nyingi kwa sababu wewe umesoma, tuachie ambao hatujasoma tushughulike na siasa kwa sababu kazi za professional hatuziwezi
ReplyDeleteanony wa juu umetoa pnt kishenzi ni kweli maana watz tumezidi sasa tunapenda sana kupiga madomo ya chinichini tu kila wakati hakuna move tunayofanya ni kulalamika tuu kama ''vibibi vizee'' ahh mimi wananiuzi sana nenda gombea na kama huoni sababu basi mwenzako aliyetumia haki yake kagombea kapata unalalamika nini sasa? ahh mnaboa bwana na ndio maana ukimchunguza huyo mtu ana mastress kibao ktk maisha sababu kila siku analalamika tuuuu kama una professional yak otulia basi nayo kama huitaki unataka siasa nenda pigania pata chance hiyo ni haki yako.
ReplyDeleteMimi nashanga mtu anayesema kuwa hakuna haja ya mbunge kusoma. Hivi kweli huyu anafikiria sana mimi namshukuru sana huyu dada yetu kuamua kusoma waka anatumikia bunge. Nafikiri atatupa uzoefu wa kutosha. Nyie mnaosema katika siasa hakuna haja ya kusoma nafikiri hamuoni mbali. Ni mawazo gani, mbinu zipi utazitumia kuendeleza jamii kama huna fikra za shule? Au unatapa kututumbukiza kwenye shimo?. Mimi naomba watu hawa watueleze ni nchi gani imeendelea kwa kutawaliwa na watu ambao hawakusoma? hapa hapa tueleze. Na ni nchi gani ambazo zimeeendelea kwa kutawaliwa na watu waliosoma? Na nchi ambazo watu wake wamepata elimu zimeendeleaje? na ambazo hawakupata elimu zimeeendeleaje? mkijibu maswali hayo tutamaliza ubishio na badala yake tutabakiza kitu kimoja tu nacho ni ni kiwango gani cha elimu kinahitajika kwa mtendaji wa kata, diwani, Mbunge nk. Asanteni wote kwa mawazo yenu.
ReplyDeleteUmesema, CV za wabunge wetu zinasikitisha!!!!!!!!!!!!!(ni suala la kuangalia sana kama tunataka nchi yenye maendeleo lazima tufike wakati tuainishe sifa za mbunge). Tukiachia kuwa mbunge ni yule tu mwenye uwezo hatutafika kokote. Tutapeleka hata wanaofanya ujambazi ubungo. Tuangalie sana suala la uwakilishi. Halafu hatujasema vijana ni akina nani na wazee ni akina nani. Na mtu wanamna gani kweli anaweza kuwakilisha mawazo ya makundi mbalimbali. Kwa sababau hata ukisema vijana tuko tofauti. Kuna vijana wako mashuleni, kuna vijana wamachinga nk. Je ni mwakilishi gani anaweza kujua matatizo ya haya makundi. Mwisho kujisomea vitabu kama upeo wako ni mdogo vile vile elimu utakayo ipata ni ndogo mno. Siku hizi kuna open University, kuna na njia nyingine nyingi za kupata elimu.
ReplyDeleteNinyi nyote mnaopiga kelele na hivyo vijiusomi vyenu hamna lolote! Msomi kweli hapo angerudi nchini kwake kupata kazi zilizoenda shule. Wengi wenu hapo na hizo PHD uchwara zenu mnafanya kazi za kusafisha tu huko Marekani sijui wapi mlipo. Kama kuna msomi kweli arudi Bongo akaendeleze Taifa. Sio tu kukaa mnakandia wenzenu wakati nyie mnafanya kazi za usafi tu huko majuu!
ReplyDeleteWee anon wa 1.41AM kweli umepitwa na wakati unafikiri kila nayetoa mawazo ana PhD? halafu yuko marekani? Ulaya? Mimi sikuelewi? kabisaaa? kama huna cha kuchangia we lala tu maana kila jambo lina watu wake. Wanakwambia mziki ukiujua huna haja ya kutafuta jinsi ya kuucheza. Hata ukiinia mguu wanasema siyo mchezo. Kwa taharifa hawa watu wako bongo tu na hizo elimu zako unazozitaja sidhani kama wanazo. Hila wewe huna cha kuongezea unabakia kulalamika tu.
ReplyDeleteWewe Anony wa 1.41AM sio lazima uchangie mada ambazo zipo nje ya uwezo wako. Yaelekea wewe uwezo wako kwa haya watu wanayochangia hapa bado sana.Aliyekuambia ukisoma lazima urudi nchini kwenu kupata kazi zenye shule ni nani. Kwanza unaposema kazi zenye shule una maana gani? Kwani hapo Tz kuna watu wangapi wa nchi nyingine wanapiga kazi hapo? Usikimbilia masuala yaliyo juu ya uwezo wako.
ReplyDeleteTatizo la Tz kila mtu ana mawazo kuwa siasa ndio last resort, kitu ambacho ni hatari sana kwa maendeleo ya taifa changa kama letu. Imefikia kipindi sasa cha kuweka vigezo vilivyo wazi na vinavyoeleka kwa mtu yeyote anayegombea uongozi wa aina yeyote. Sio mtu ukishaona mambo yamekugomea kote unaona kimbilio la mwisho ni siasa hii ni hatari tutaendelea kupiga makitime hapo hapo.
ReplyDeleteJamani samahani wengine tunafanya research, tafadhali naomba Anony wa 1:41AM anisaidie kiwango chake cha elimu. natanguliza shukurani.
ReplyDeleteAnony wa 3.03am jifunze kiswahili "Kazi zilizoenda shule" Maana yake kazi za maana.
ReplyDeleteMfanya research, Anony wa 1:41AM ana elimu ya Shahada ya Uchumi, na hivi sasa anachukua MBA. Yuko mbioni kumalizia MBA yake arudi Nchini. Ni mtumishi wa Wizara ya Fedha.
ReplyDeleteAnony wa 1:41 AM - Masikini WIZARA yetu ya FEDHA kama mtaalamu wetu mtaarijiwa ndo wewe mwenye point mavi (fake) kama hizo. Yaani unatoa vapour tupu. Aisee wewe hiyo itakuwa siyo MBA bali ni DUM yaani Degree ya UMbeya. Pole sana ndugu. Jaribu kuwa na busara kama mtumishi wa umma. Reve. EVM
ReplyDeleteWabongo wengi elimu ya ulaya haiwasaidii sana kwa sababu wanatumia muda wao mwingi kufanya kazi ambazo hazihitaji akili. Sababu ni kwamba hawana uhakika na kazi gani watapata huko bongo hivyo wanaamua kutafuta hela kwa nguvu zote na kusahau elimu, kwa kufanya hivyo wanabaki wababaishaji kwenye professional zao. Kwa maoni yangu bora hata wasomi wetu wa UDSM wanaweza wakawa wazuri pamoja na matatizo ya allowance kuliko hawa ninaowaona huku ulaya wanafanya usafi.
ReplyDeleteACHENI BWANA MSICHEZE NA KUVUKA ATLANTIC KWA NAMNA YOYOTE HUWEZI KUMLINGALISHA MTU ALIYETOKA BONGO AKAENDA ULAYA NA HAKUSOMA HAWAWEZI KUWA SAWA LAKINI ALIYEKWENDA NA AKASOMA PIA HAWALINGANI TZ ELIMU BADO SANA YAANI MIMI NIMESOMA UDSM NA NIKAENDA NJE KUSOMA NAJIONA KABISA NINA TOFAUTI KUBWA SANA NA WENZANGU WENGI WALIONIZUNGUKA HIVYO NAWATIA MOYO SANA MLIO UGHAIBUNI HAKIKISHENI MNASHIKILIA ELIMU
ReplyDeleteOk kwanza huyo wa MBA na yuko wizara ya fedha ningelikuwa mimi ningemfukuza kazi. Ndio wanarudisha maendeleo ya nchi nyuma kabisaa. Au anataka awadanganye wengine hili ajisafishie njia na ka MBA kake, wewe unaona eti MBA unasema elimu haisaidii hiyo akiri kweli.
ReplyDeletePili mimi ninachojua kusoma bwana ni kusoma unaweza ukawa bongo pamoja na matatizo ya alawance ukapata elimu ambayo ni bora kuliko vyuo hata vya marekani.Na unaweza ukawa japani, marekani, Uingereza na ukapata elimu hafifu zaidi ya aliyesomea bongo.
Mimi nimeona mfano mzuri kwa watu waliosomea bongo(hapa na zungumzia elimu za under na post) na wameenda katika nchi mbalimbali na wametesa sana. Kuona wanajua mambo mengi mno. Kwa hiyo suala la kusoma kwa kweli sana sana ni juhudi binafsi. Hila nguvu anayoitumia mtu aliyesoma bongo akiitumia mtu anayesoma nchi za nje matunda yatakuwa mazuri sana kwa mtu wa nchi za nje kwa sababu kila kitu kiko kwenye imaya yake. Lakini katika enzi hizi za utandawazi-Mawasiliano(Internet Resources) watu hata bongo wamepanuka katika wigo wa elimu.
Mwisho namtakia huyo jamaa wangu wa 1.41Am asiturudishe nyuma leo hii kenya tu wana wanafunzi karibia mia moja na kuendelea wa Masters/PhD katika kila chuo kilichoko South Africa- hizi ni data nilizoziona miaka mitatu iliyopita, lakini tanzania kama kuna mmoja ni bahati. wanafanya kazi katika sehemu mbalimbali.
Kwa hiyo kwa watanzania mlioweza kupata bahati ya kuona mbali muwe let encourage watanzania wasome. Watu wengi wakisoma tutaendelea taratibu. na kuchangia katika uchumi siyo lazima ufanye kazi tanzania. hata ukiwa ulaya ukatuma dola moja tanzania umechangia.
Anony wa hapo juu unaweza ukawa na akili
ReplyDeleteAnony wa 11.25pm ningekuwa Mimi huyo wa MBA sio ningemfukuza kazi tu pia ningemkumu apigwe risasi hadharani ili liwe fundisho la wenye akili kama za kwake. Mawazo mengine yanatia hasira, kwa hasira niliyopata kwa kusoma comments za huyo wa MBA inanibidi nifunge siku moja kunywa wiski.
ReplyDeleteclass elimuYaWabungeTz extends GraphicsApplet{
ReplyDeletepublic void run(){
Point jinaLaMbunge = getName ("Please enter the name of Mheshimiwa");
Point kiwangoChaElimu("Please enter the level of education");
line result = new result(jinaLaMbunge,KiwangoChaElimu);
result.draw();
}
}
Grill siyo mchezo sasa hii ni nini? make niko hoi. Na anony wa 11.56Am naona kweli umekasirika angalia make hiyo wiski inaweza kukutoa roho jamaa wa MBA akaendela kutesa make ndicho anacho taka abaki tu peke yake tanzania mwenye elimu.
ReplyDeletekaa andika taka taka tu au ndo kujifanya code breaker. teteteteh
ReplyDeleteDuu mbona watu mnahasira hivyo yaani MBA tu isababishwe mtu apigwe risasi.. Duu yaani kukaa nje kunawaharibu kweli wengine. Hata roho ya kitanzania hawana tena wamekuwa wakatili kufikia hadi kutaka kuwapiga risasi wenzao..
ReplyDeleteSiyo nje tu bwana kwani waliopiga wenzao ubungo walitoka nje? hau ujambazi wa siraha bongo wanatoka nje? Mbona watu wa nje tunawasingizia bure?
ReplyDeleteWe anon wa 3.56AM si unajua gllil ana masters? au hujui? huyo jamaa siyo mchezo? hizo ndio technologia bwana? Si unajua pale gloshopper? Uk kapata ki master pale bwana.Hiyo inaitwa intanet bwana.
ReplyDeleteHii yote nadhani ni ukosefu wa ajira tu watu wana nyanga kibao kichwani sehemu ya kufanyia implementation hakuna. Eee mola tunaenaelekea wapi?
ReplyDeleteKuna mtu alitoa wazo lakini hakumalizia je mbunge anatakiwa awe na elimu gani ili kujua hili tunaomba kujua kazi za mbunge, diwani tukijua hivi tutaweza kujua elimu yake inatakiwa iwe kiwango gani. Unajua tulipumuzika ili watu wapate mawazo mapya.
ReplyDeleteMbunge angalau awe na degree ya kwanza au mnasemaje waungwana.
ReplyDeleteNafikiri kama anany wa 12.26AM alivyosema naomba mtu anieleze kazi za mbunge kabla hatuja ingia katika kiwango cha elimu.
ReplyDeleteKwa mfano najua moja Kuangalia na kupitisha sheria za nchi.
wabunge hawana majukumu ya lazima...majukumu yao ni ya kisiasa.kuleta maendeleo.how?its not explained anywhere.jukumu lingine ni kuhakikisha kuwa hawakosi vikao vitatu mfululizo bila kutoa taarifa.sio lazima wachangie chochote katika hivyo vikao,sio lazima walione jimbo lao,sio lazima wawe na ofisi.ofcourse wabunge wengi hawana ofisi kabisa.ingawa wana allowance za kuendesha ofisi.
ReplyDeleteKama majukumu yenyewe ya wabunge ndiyo hayo basi mie naona hatuna haja ya kuwa na wabunge wanapata mshiko wa bure. Kwa nini tusipendekeze wabunge wasiwepo kama kazi zao ndio hizo?
ReplyDeleteunakumbuka ubunge ilikuwa ni kazi ya kujitolea.sababu yake ilikuwa ni hii.sasa tangu maslahi yalivyoongezwa mapak ubunge ukawa biashara bado majukumu hayabadilishwa.nadhani cha muhimu sio kupunguza malipo ila ni kuwapa majukumu yatayoendana na malipo.
ReplyDeleteNaona sasa ndio tumefika penyewe kumbe ndio maana kila mtu anakimbilia bungeni kumbe hakuna kazi yoyote iliyoainishwa kufanya na wabunge? Unaona sasa, huu sijui niuite nini. make zamani kama sikosei huu ulikuwa uwakilishi wa watu wa aina mbalimbali hivyo mbunge alikuwa katika jamii inayohusika anatoka anakuja dodoma kuleta matatizo wa wakazi wake. Sasa Hivi kinachofanyika ni kinyume mno, mtu anakaa DAR masaki, na ni mwakilishi wa nanyumbu mtwara, je tutafika? Either wapangiwe majukumu au Wafutwe badala yake tuwe na wawakilishi wa wakulima wa chai, Mihogo, Kahawa, wawakilishi wa wachimbaji wadogowadogo, wamachinga nk ndio waunde bunge na kuwepo watu waliosoma hawa nafasi zitangazwe waombe kazi na wawe wanawasaidia hawa wasiosoma.
ReplyDeleteMie nadhani wabunge tulionao ni wengi sana kwa kazi wanazotakiwa kufanya. Wabunge wanachukua sehemu kubwa sana ya pato la Taifa bila kuzalisha chochote. Nikiuliza mtu anipe contribution ya wabunge kwenye pato la Taifa sidhani kama ipo. Imefikia kipindi tupunguze idadi ya wabunge tuwe nao wasiozidi kama 50 hivi. Wewe fikiria mashangingi, mishahara yao, posho zao na pension yao halafu linganisha ni real contribution kwenye national cake is nothing.
ReplyDeleteGrill nimekupata umesema kweli, mimi nafikiria tuanze hivi wabunge wawe wanafanya kazi. Kwa mfano bunge lina maprofesa wengi mno wakati vyuo vyetu walimu hakuna kuna madaktari wengi kwa hiyo hawa watu warudishwe kwenye kazi zao. Harafu tubakize watu wachache ambao ni sawa na kamati za bunge zilizopo sasa hivi. Kama watu hawana kazi na wanachukua kiasi hicho cha pesa mimi nafikiri hawa ndio wanaturetea umasikini. Mimi sijaona mchango wao uliomkubwa katika jamii ukilinganisha na matumizi yao.
ReplyDeleteWatu bwn.. Picha ya Lucy maoni ya MBA
ReplyDeleteSafi sana Anony wa 1:41 AM. wengi huko ughaibuni wanachuma machungwa kufagia barabara, kuosha masahani mahotelini, kufua chupi za wazungu nk cha maana wanachofanya huko hakuna wakirudi huku wana vyeti fake sio wabunifu kazi kudharau walioko bongo. Hivi mtaendelea lini? Kurudi makwenu hamrudi kisa mnawaonea haya walioko bongo manake wamepiga hatua mbili tatu mbele zaidi ya mliojichimbia ughaibuni mbona wenzenu tunakuja kusoma na tupo makazini huku bongo na tunaelewa kuwa tukija huko tunakuta hakuna cha maana mnachokuwa mnafanya kazi kuzidanganya familia zenu kuwa mnasoma kumbe maisha magumu mnaogopa kurudi kwenu. Tukija mnatu bom kila kukicha. Nyie si mme opt kuishi huko kisa maisha ni bora? Sawa basi mkirudi msianze kuomba hifadhi kwenye vibanda vyetu tulivyojijengea? Kaeni kwenye maghorofa yenu basi.Ila wakumbukeni hata wazazi wenu huku nyumbani sio kelel nyiiiiiiiingi vitu vyenu mnavyofanya huku nyumbani hatuvioni wazazi wenu wanalalamika kila kukicha.WAJAMENI NYUMBANI NI NYUMBANI HEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!Anony 1.41 AM soma rudi zako Wizarani achana na wachuma machungwa wanokulaumu.
ReplyDeleteANONY 2:02 AM UMENENA. NIKO UGHAIBUNI NA NIMESHUHUDIA YOTE HAYO. TUTARUDI MZEE. WENGI TUMESHACHEMASHA.
ReplyDeleteHakuna aliye mzuia kurudi nyumbani. Na kuhuza machungwa mimi sioni kama ni shida ili mradi anakula anaishi. Suala zima la huyo bwana alionekana kudharau elimu, mimi sioni kama dhambi mtu kusoma mpaka kiwango cha juu. Ukimutetea bila kuangalia kwa makini hata mimi nafanya kazi bongo lakini nafikiri suala la kusoma na kuelimika halina mjadala. maana hata unaweza ukasoma bila kuelimika. Hilo limewakuta watanzania walio wengi. Matokeo wake huwa linakosesha ubunifu kwa kufikiria tu kuwa nimesoma. Cha muhimu huyu jamaa arudi tu wizarani na MBA yake lakini ajue kuna kitu anakosa katika usomaji wake na kama atajirekebisha atapata shida katika maisha yake. Maana inaonekana amesoma lakini ni vitabu tu, kuelimika hakuna. Wewe ulieandika 2.02AM niushauri mzuri kwa watu ambao kidogo mwelekeo wa ulaya kama haupo lakini kama kuna mtu mwenye mwelekeo haina haja ya kuangaika make hata Bongo kazi siyo kwamba zimeweka kwenye mto kiasi kwamba utachota tu. Si mnajua nchi yetu tuviwanda tulikufa tukabakia kuwa wachuruzaji? Kwa hiyo kazi ni kama kufuta vyumbi computer(Computer Engineer), Kupangusa mtambo wa mawasiliano(Tel. Eng.), kuangalia kama watu wanalipia umeme(El. eng.) na nyine za waasibu ni pamoja na kurushiwa mia tano kila check unayotoa, Kudanganya danganya nk. na mwisho kugombea ubunge, hizi ndio aina za kazi tulizo nazo . Vinginevyo karibu sana.
ReplyDeleteNadhani tukiwa na mawazo kuwa mtu ukisoma lazima ufanye kazi Tz ni mawazo finyu. Kwanza tujiulize kwa nini Maprofessor na Dr kibao kutoka vyuo vikuu Tz wanaondoka na kwenda kufanya kazi nje. Sidhani kama kuna Dr atakubali kuacha kufundisha TZ aende nje akauze machungwa au akafue chupi za wazungu.
ReplyDeleteSuala sio kuja kufanya kazi bongo bali suala ni pale mtu anpoogopa kurudi TZ kulitumikia taifa akaamua ku opt kufanya kazi za kuchuma machungwa na kufua chupi zao wakati ni msomi bora arudi nyumbani hata akifundisha itatusaidia kuwaongezea ujuzi wabongo wengi nyumbani ambao hawakwenda shule.
ReplyDeleteUrudi kufanya nini bongo jamani kama issue ni maisha. Sidhani kama kuna mtu anayeogopa kurudi kwao. Ajira Tz zipo wapi wakati Tz ni miongoni mwa nchi zinazongoza dunia kwa kuwa na rate kubwa ya unemployeed. Rais mwenyewe anatuomba tuwe tunawashitua kukiwa na vinafasi vya kazi huku. Sindhani kama kuna mtu kweli ana shule yake safi alafu anaishi maisha kama aliyosimulia Anony hapo juu. Sijui labda nchi nyingine lakini mimi huku niliko kama huna kipato cha kueleweka sijui utaishi wapi kodi yenyewe ya chumba kwa mwezi ni sawa na kodi ya nyumba nzima kwa mwaka hapo tz.
ReplyDeleteWe anony 9.20 inaonekana uko UK.
ReplyDeleteSasa kuna haja gani ya kung'ang'ania huko ulaya kumbe maisha yenyewe mnaishi kwenye kichumba... duuu
ReplyDeleteTukirudi tutaanzia wapi, wakati tulishajipakulia kwamba huku maisha yetu yapo bomba sana. Nimekaa miaka kadhaa huku ulaya halafu nirudi niwe nalala sebuleni kwa brother??? Bora niwe naosha vikonjwe na kufanya usafi pamoja na masters yangu lakini bongo hakanyagi mtu, piga ua
ReplyDeleteUnajua wakati ninaandika 3.31AM, nilikuwa namaanisha hali halisi iliyoko bongo, kama mmoja wetu alivyosema chumba tu mwezi dola mia tano(hii ni mishahara wakati mwingine ya miezi miwili tanzania), kama mmoja livyo sema pia siyo rahisi kukuta mtu ulaya, marekani, japani na kwingineko amesoma vizuri hana na akakaaa huko atakula nini mimi siko bongo kama nilivyosema hapo juu lakini nina uelewa wa maisha ya bongo vizuri sana. Na nina uelewa wa nchi takribani kama 20 duniani, ukianzia RSA, USA, Sweeden, Japan, Uk, na nchi nyingine nyingi. Maisha kama hujishughulishi kweli yanaweza yakawa magumu lakini mtu kama ana kazi yake ulaya bwana piga ua bongo hawezi kwenda. hata mfagizi mimi kwa nchi ninayokaa sasa hivi(samahani sitaweza kuitaja) anapata kama milioni mbili za kibongo kwa mwezi lakini ndo hivyo nyumba laki kama tano. Kwa hiyo kazi zenye akili za bongo wakati mwingine siyo kazi za kuaminika. Ukitaka kazi yenye kueleweka labda serikalini. mshahara laki moja/mbili(dola mia moja/mbili).Lipa nyumba, maji, umeme mwisho frustrations, kufa tu. labda tumuombee JK atusaidie bwana vinginevyo sijui.
ReplyDeleteIla jamani nipo Ughaibuni na japo sijaamua kurudi bongo lakini mmh bora bongo jamani.Huku kwanza nani akusaidie hata kama huna chakula utajiju no msaada.Upendo umetoweka. Bora bongo hata muhogo wa kuchoma na kisamvu utapata.Huku limkate kila saa, asubuhi, mchana jioni. Aliyesema EAST OR WEST HOME IS BEST HAKUKOSEA JAMNI TUWE WAKWELI.Ila acha tu tukaekae kidogo tutarudi.
ReplyDeleteHapa comments zinatosha hamieni kwingine mmesikiae tosha kabisa. Asanteni sana kwa mawazo yenu yatafanyikiwa kazi.KWA JINA LA MICHUZI:AMEN
ReplyDelete