gwiji la kuimba cosmas thobias chidumule sasa sio tu amezaliwa upya bali pia huimba nyimbo za injili kwa mafaniko makubwa kama alivyokuwa dar international, sikinde na kwengineko. hapa ni daimondi jubilei wakati wa tamasha la nyimbo za injili karibuni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 12, 2006

    Kama kuna mtunzi aliyestahili awards Tanzania basi huyu jamaa yumo ingawa ndio hivyo tena,walioimba tungo zake ndio wanazoa sifa

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 12, 2006

    Rufaa ya Kifo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 12, 2006

    Mbali na utunzi wa Neema. Cosmas Thobias Chidumule iliyoshinda tuzo ya muziki bora Tanzania kwa miaka miwili mfululizo 1985 na 1986, Cosmas pia ni mtunzi wa miziki ifuatayo akiwa na kundi la Mliman Park Orchestra:
    1)Mnanionyesha njia ya kwetu

    2)Ubaya

    3)Nalala kwa taabu

    4)Usitumie pesa kama fimbo

    5)Ugomvi wa baba na mama

    6)Epukana na maneno

    Hapo bado hatujarudi kwenye zile alizotunga akiwa Dar International na zile za alipokuwa kwa muda na Orchestra Vijana Jazz.

    Ninasema bila kuogopa kwamba Cosmas ndiye mtunzi pekee wa muziki wa dansi wa Tanzania aliyebaki baada ya kuondoka Hayati King Michael Enoch.

    F MtiMkubwa Tunagaraza.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 12, 2006

    Nilisahau na alipokuwa na wana Matimila:

    1)Dodoma

    2)Kidogo kidogo

    3)Bwana mdogo

    Halafu nakumbuka kuna jamaa yangu mmoja alitaka kumfananisha Cosmas Chidumule na Shaban Dede. Sikutaka kubishana naye nikanyamaza, kwa sababu kufananisha kichuguu na mlima, au mtumbwi na manowari, bwawa na bahari sijui utakuwa unatafuta uwiano gani? Kwa ufupi: Cosmas is the best no protest!

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 13, 2006

    MtiMkubwa,
    Hapo umenifanya niingilie kati kidogo. Kwanza kabisa, hayati King hakuwa mtunzi bali ni arranger, jamaa alikuwa anafanya arrangement zote za vyombo pale Nginde kuanzia magita, drums, Horns mpaka uimbaji,, baadhi ya wanamuziki walikuwa wanatunga mashairi tu ya nyimbo lakini arrangement zote wanamwachia King amalizie. Alikuwa anapanga hadi nani aimbe wapi,, alikuwa wizard.
    Nikiwa mshabiki mkubwa sana wa Sikinde na kuwa karibu sana na baadhi ya wanamuziki wa Nginde nyakati hizo, nakubaliana nanyi kwamba Chidumule ni mtunzi mkali sana, ingawa Shaaban Dede na Max Bushoke ni watunzi wa kaliba hiyo hiyo ya Chidumule. Kwa kuongezea kuhusu vibao alivyotunga Chidumule ni kama:
    Nina maneno nataka kusema na wewe
    Taxi Driver
    Gama
    Nawashukuru wazazi
    Majirani huzima Redio

    Sasa Nitakupa mfano wa tungo za Dede na Bushoke, tukianzia Dede
    Talaka Rejea
    Pole mzee
    Diana
    Tafuteni Darubini muone mbali
    Nelson Mandela
    zote hizo akiwa na Sikinde achilia mbali alizotnga akiwa Msondo kama Kimwaga n.k

    Ukija kwa Bushoke ndiyo kabisaa, huyu jamaa watu walikuwa hawajui tu undani wake, alikuwa mtunzi wa kutisha, mfano:
    Patapotea
    Shemeji Issa
    Aza
    Christina Bundala
    Clara
    Kiu ya Jibu
    Penzi kileo Cha fikara
    Telegramu
    Siyo wivu mke wangu,,,,naona uchungu kusikia


    Na alikwenda Ndekule akashuka na:
    Kata ya maji ukweni
    Kuna maneno
    alipokuwa Bima akatunga vibao kama
    Mesenja n.k

    Kwa kifupi ni kwamba wote hao Chidumule , Bushoke, Dede wako kundi moja ni watunzi wakali sana.
    MtiMkubwa kama unataka maelezo zaidi tutafutane.


    Baba G

    ReplyDelete
  6. ndugu zangu mimi sina hata la kusema kuhusu hawa magwiji wa3 kwani wote ni hatari hakuna wa mbele wala wanyuma mimi wote nawafagilia.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 30, 2014

    Grill, kama unataka kusikiliza nyimbo hizo jaribu www.youtube,com nyingi utazikuta,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...