Home
Unlabelled
chidumule
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Kama kuna mtunzi aliyestahili awards Tanzania basi huyu jamaa yumo ingawa ndio hivyo tena,walioimba tungo zake ndio wanazoa sifa
ReplyDeleteRufaa ya Kifo.
ReplyDeleteMbali na utunzi wa Neema. Cosmas Thobias Chidumule iliyoshinda tuzo ya muziki bora Tanzania kwa miaka miwili mfululizo 1985 na 1986, Cosmas pia ni mtunzi wa miziki ifuatayo akiwa na kundi la Mliman Park Orchestra:
ReplyDelete1)Mnanionyesha njia ya kwetu
2)Ubaya
3)Nalala kwa taabu
4)Usitumie pesa kama fimbo
5)Ugomvi wa baba na mama
6)Epukana na maneno
Hapo bado hatujarudi kwenye zile alizotunga akiwa Dar International na zile za alipokuwa kwa muda na Orchestra Vijana Jazz.
Ninasema bila kuogopa kwamba Cosmas ndiye mtunzi pekee wa muziki wa dansi wa Tanzania aliyebaki baada ya kuondoka Hayati King Michael Enoch.
F MtiMkubwa Tunagaraza.
Nilisahau na alipokuwa na wana Matimila:
ReplyDelete1)Dodoma
2)Kidogo kidogo
3)Bwana mdogo
Halafu nakumbuka kuna jamaa yangu mmoja alitaka kumfananisha Cosmas Chidumule na Shaban Dede. Sikutaka kubishana naye nikanyamaza, kwa sababu kufananisha kichuguu na mlima, au mtumbwi na manowari, bwawa na bahari sijui utakuwa unatafuta uwiano gani? Kwa ufupi: Cosmas is the best no protest!
F MtiMkubwa Tungaraza.
MtiMkubwa,
ReplyDeleteHapo umenifanya niingilie kati kidogo. Kwanza kabisa, hayati King hakuwa mtunzi bali ni arranger, jamaa alikuwa anafanya arrangement zote za vyombo pale Nginde kuanzia magita, drums, Horns mpaka uimbaji,, baadhi ya wanamuziki walikuwa wanatunga mashairi tu ya nyimbo lakini arrangement zote wanamwachia King amalizie. Alikuwa anapanga hadi nani aimbe wapi,, alikuwa wizard.
Nikiwa mshabiki mkubwa sana wa Sikinde na kuwa karibu sana na baadhi ya wanamuziki wa Nginde nyakati hizo, nakubaliana nanyi kwamba Chidumule ni mtunzi mkali sana, ingawa Shaaban Dede na Max Bushoke ni watunzi wa kaliba hiyo hiyo ya Chidumule. Kwa kuongezea kuhusu vibao alivyotunga Chidumule ni kama:
Nina maneno nataka kusema na wewe
Taxi Driver
Gama
Nawashukuru wazazi
Majirani huzima Redio
Sasa Nitakupa mfano wa tungo za Dede na Bushoke, tukianzia Dede
Talaka Rejea
Pole mzee
Diana
Tafuteni Darubini muone mbali
Nelson Mandela
zote hizo akiwa na Sikinde achilia mbali alizotnga akiwa Msondo kama Kimwaga n.k
Ukija kwa Bushoke ndiyo kabisaa, huyu jamaa watu walikuwa hawajui tu undani wake, alikuwa mtunzi wa kutisha, mfano:
Patapotea
Shemeji Issa
Aza
Christina Bundala
Clara
Kiu ya Jibu
Penzi kileo Cha fikara
Telegramu
Siyo wivu mke wangu,,,,naona uchungu kusikia
Na alikwenda Ndekule akashuka na:
Kata ya maji ukweni
Kuna maneno
alipokuwa Bima akatunga vibao kama
Mesenja n.k
Kwa kifupi ni kwamba wote hao Chidumule , Bushoke, Dede wako kundi moja ni watunzi wakali sana.
MtiMkubwa kama unataka maelezo zaidi tutafutane.
Baba G
ndugu zangu mimi sina hata la kusema kuhusu hawa magwiji wa3 kwani wote ni hatari hakuna wa mbele wala wanyuma mimi wote nawafagilia.
ReplyDeleteGrill, kama unataka kusikiliza nyimbo hizo jaribu www.youtube,com nyingi utazikuta,
ReplyDelete