f.mtimkavu upo???

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kwa kweli kazi zako za zamani zinavutia hivi huwezi angalau kutukumbushia zile picha za akina Chakubanga, Polo na Bushiri ambazo zilikuwa zinavuma sana na kutufundisha mengi, iwe changamoto kwa vijana wa sasa wasanii wanaochipukia naamini hazikosekani katika maktaba yako.

    Wakatabahu

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 12, 2006

    Muhidin,

    Haya maweekly na monthly siku hizi hakuna tena. Namkumbuka na yule mtoto Lemmy kwenye Spear.

    Enzi hizo kuna Spear, Drum:Mwaka 2004 ilitoka dokyumentari moja ya muziki wa Afrika ya Kusini, ndiyo nikajua kama Drum lilikuwa gazeti la Marebels fulani. Halafu kulikuwa na African Women, Baraza, Fahari, Nchi Yetu, Sani, Shoot, makomiki ya Chakubanga, Topper, Beano, Beezer, Tin Tin, nk.

    Jamani mnakumbuka Dar es Salaam Elimu Supplies, Dar es Salaam Bookshop, International Bookshop, Cathedral Bookshop, na ile bookshop nyingine pale pale Mtaa Mansfield ilikuwa inatazamana na Kanisa la Mtakatifu Joseph kwenye jengo la Tume Ajiri. Mnamo miaka ya 70 kwenye ile bookshop nilikiona kitabu Mirela Ricciad, Vanishing Africa. Mwaka 1998 nikakinunua hicho kitabu toka kwenye bookshop moja Manchester, Uingereza. Kitabu hiki ni moja ya masterpiece collection item yangu. Zile bookshop zingine zote zilikufa zikabaki Dar es Salaam Bookshop na Cathedral Bookshop ambazo zote zinamilikiwa na makanisa.

    Baada ya kufa kwa mabookshop wakaibuka books streets vendors. Miongoni mwa wa kwanza kabisa alikuwa Omar Mruguru wa pale Empress Cinema. Muhidin, hebu tafadhali naomba kwanza utuletee picha ya Moses/Musa mpiga brashi wa Empress. Kila nikifika TZ lazima nikapay respect kwa Moses/Musa na pia kupewa hala hala za jiji.

    Ukipita Empress naomba uwape kina Moses, Omar, Chauda, Zandoro, Mchizi Somo muosha magari na wana kijiwe kikongwe wote salamu zangu za dhati.

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...