mapicha ya mwalimu na jk yakiuzwa mitaani dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 02, 2006

    Mungu alitubariki watanzania kwa kutupatia nyerere. Sijui baada ya karne ngapi tutampata mtu mwingine kama Nyerere.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 02, 2006

    Tunaye sasa kijana wake JK. Usiwe na wasiwasi wote ni ma- JK
    Huyu wasasa atafanya makubwa zaidi ya yale ya JK mkubwa.Tusubiri

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 02, 2006

    tusahau kumpata mtu mwingine kama mwalimu nyerere. cha kwanza sisi wabongo hatukuthamini hata kidogo mwalimu zaidi zaidi ya kumuita majina ya ajabu ajabu (mchonga, musa) na kumlaumu kwa kutuletea ujamaa ambao ulidumaza uchumi wetu. haya sasa siku hizi bongo imejaa makaburu kibao, tumepata simu za mikononi, magari ya fahari, tv, nk ila watu ndo hawana kazi, tunakufa na njaa, elimu ya bure ndo imekwisha na joto ya jiwe ndo kwanza ndo inaanza.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 03, 2006

    kumfananisha kikwete na kambarage ni ukosefu wa akili. Kikwete ni mtanzania tuu, nyerere alikuwa mwafrika. upeo wa nyerere wa kufikiria ulikuwa ni wa kidunia na wa kiafrika; upeo wa kikwete ni wa kitanzania tuu. kwa watu Pan Africans, kumfananisha Nyerere na Kikwete ni matusi makubwa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 03, 2006

    annoy2:46 am umechemsha sana, ulichofanya hakina tofauti na hicho alichofanya mwenzako hapo juu, na kwa vile wewe ni wa pili basi wewe una makosa zaidi.Kuzungumzia swala la wakati huo wa Pan-Africanism kwa nyakati hizi ni kuturudisha mika ya 60 tulipodai uhuru, sasa tunaangalia kitu kitwacho global-concern chini ya Globalization.Mtu atakuwa na akili nzuri zaidi pale atakapotumia Global -concern katika kufikiria nchi yake, yaani kutumia globalization kujenga nchi na siyo tena mambo yako ya Pan-Africanism. Ebu lete stori ya haya ya kidunia ambayo JK mkubwa yamempa impact!Kwa nyakati hizi JK mkubwa asingeweza kufit kama angeng'ang'ania mawazo yake.Tembelea ubishi wake na Kwame ama Kenyata alafu utaona ni kwa vipi ambavyo asinefit kwa sasa ila Mkapa ama Kikwete ndio hasa wanafit. Ni matazamo makini.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 03, 2006

    Annoy 2:26 am ulichofanya pia ni ukosefu wa akili.Haipandi kichwani kupuuzia tofauti za nyakati katika hayo uliyoainisha.Huo pia ni ukosefu wa akili, na ni mbaya zaidi kuliko niliofanya mimi maana wewe ungetumia akili zaidi kutofananisha ,badala yake umeingia katika kosa lile lile kwa ubaya zaidi.POLE,hata mimi namheshimu sana Mwalimu na mchango wake ndio maana nina imani kwa JK-mdogo kwamba aytaweza na zaidi sana ataweza.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 03, 2006

    asante sana anony wa 1:24 hapo juu. Ndo uzuri wa blogu hii ni kuwasilisha mawazo tofauti ya watu tofauti, na siyo kukosoana kwa kutukanana. Narudi tena kwako, kwanza unatakiwa ujuwe kwamba Pan Africanism ni ni kujikubali, na kujivunia wewe mwenyewe uafrika wako, na kuhakikisha kwamba "race ya kiafrika" inabakia kuwa ndo yenye nguvu ndani ya Afrika. Sasa kama unasema kuwa Pan Africanism ni mambo ya 1960's, tafadhali fikiria tena.
    Na hii globalization yako pia iangalie, kiukweli hii ni "ghost and fictious idea" ya kumfunga kamba mjinga ili aishi na umasikini wake huku akiwa na "hope and dreams", Globalization is not a real thing, na kama utachunguza vizuri, utakuta kwamba Globalization ni Americanization. Kwa mfano, kama ulimsikiliza George Bush kwenye "speech" yake ya States of the Union ya mwaka huu 2006, ilikuwa na kila kitu kizuri kwa ajili ya America, na hakukuwa na chochote kizuri kwa ajili ya Globe. Angalia, ukiwa adui wa America leo hii, basi wewe ni adui wa Globe. Kwa mfano, bin laden, Hugo Chavez na Fidel Castro. Lakini, adui wa Greece ni Turkey, na wala siyo adui wa Globe. "Pan Africanism is not only an idiology, it is a state of being". Sasa kama "existence" yako wewe ni kitu cha 1960's, fikiria tena. KUMBUKA, KUJIKATAA HAKUTOKUFANYA UPENDWE, BALI UDHARAULIWE.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 04, 2006

    For an African to suggest that Pan africanism is a thing of 1960's is an act of degrading your self, and not recognising the value, dignity, pride and existence of Africans. It is true that Africans today refuse themselves, no wonder they are refused by their "masters".
    By. Sammy Amankwah of UDSM Tanzania

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 04, 2006

    Tanzania now is so poor kwamba raisi mzuri ni yule atekayejipamba kwa america na european union wampe misaada other wise funds ni ndoto!nchi zilizondelea sasa hazitaki mambo ya internationalism wanataka wadeal na watu wao tu unless umejikomba sana.lkn baba Kikwete naamini brazamen atafanya mambo kwani sio mjinga ila sio wa kumfananisha na nyerere !yule mtu hafananishiki misingi yake ni ya haki za binadamu ukiifuata unakufa!ila ndio right way

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 04, 2006

    Nyie vipi! mbona wabongo wengine kama mume pagawa. toka lini mkamringanisha Julias mchonga meno na kijana kama Jk, JK ni wale wabagaizaje fulani wa maskani tu waliokuwa wanashinda kwa macheni magomeni na waliowahi kwenda shule, kumbukeni wakati alivyokuwa jeshini enzi hizo kuna matawi ya CCM kila corner ndio JK akapanda chati, Mchonga ana mavitu yake makubwa na ma-ideology yake mengi aliyotufanyie wabongo hatutawezi kuyasahau´. mfano, wewe leo ni msukuma unaweza kumpenda mchaga na kumuoa... nenda kwa bwana NYAYO kama utasikia mkikiyu na mjaruo wanaweza kula sahani moja......

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 04, 2006

    Mimi naona kuna mambo mawili yamejitokeza kwa wle wanaopingana kati ya Annoy 2:26 am na annoy2:46. Watu hawa wamekua wakichuana naweza kusema kuhusu Nafasi ya Pan Africanism na nafasi ya Jk ati anapuuza hiyo Pan Africanism kwani anaangalia sana Nyumbani. Kwanza labda niwakumbushe kwamba kama Kuna enzi za watu kuchapukia katika Pan Africanism basi ilikua wakati wa Ujana wa kina JK na JK alikua ni miongoni wa Vijana hao. Wengine ambao vitabu vya Historia havitawasahau ni kama akina Jenerali Ulimwengu. Pili HAUWEZI ukajiita mwana Mapinduzi(Pan Africanism) kama nyumbani kwako hakuna maendeleo yoyote. mama Theresa anasema Charity Begin At home na kama tunataka kuwa maPan Africanism basi lazima tuhakikishe kila nchi yetu kuanzia Nyumbani kwanza inajenga misingi thabiti ya UTAIFA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...