Home
Unlabelled
MECHI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hilo wazo lishindwe. Kushinda mechi moja kusifanye watu waone kama ndio tumetwaa kombe la dunia. Bado tunasafari ndefu mno. Serengeti, Kilimanjaro au hata Twiga ni majina yanayofaa kupewa timu ya taifa badala ya kuibambika jina la mpita njia mmoja.
ReplyDeleteBad suggestion Michuzi! What do you tell the oppositions, that they are not a part of this team ? We have to be fair to both sides here, (Tanzanian) is no longer a single party State, therefore to call a Our National Soccer Team J.K Eleven will not be a good idea. We have so many names we call call the team, Taifa Stars, TZ Eleven, Tanzania Stars, Kilimanjaro Stars and so forth.
ReplyDeleteMhh unaamn gani ya "JK ELEVEN" tunaomba ufafanuzi kama nikumuenzi Kikwete sio wakati muafaka sasa kwani bado Yuko hai.Nashauri libaki na jina lake la asili"Taifa Stars"
ReplyDelete'jk ileven' NI UFALA NA KUJIPENDEKEZA KWA MTU KISA TU NI RAIS WA NCHI!! KWA MAMBO GANI ALIYO YAFANYA YA MAANA? KWA KUWA MMOJA WA WALA RUSHWA NCHINI? KWA KUWAFUMBIA MACHO WALA RUSHWA? KUNA WATU WENGI TU WA MAANA KTK TAIFA HILI AMBAO TUNAWEZA ATA KUSEMA KUTUMIA MAJINA YAO KTK KUITA TIMU YA TAIFA, KAMA HAIWEZEKANI KWA MAJINA KAMA NYERERE N.K BASI TUITE MAJINA KAMA TWIGA, KILIMANJARO, AU ATA KUTUMIA JINA LA NCHI YETU TANZANIA NA SIO KUIITA HII TIMU JINA LA MLA RUSHWA ALIYE KUWA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA SASA RAIS. HACHENI KUJIPENDEKEZA WATANZANIA KWA WATU AMBAO WANAPITA. TAFUTENI MAJINA MENGINE NA SIO HILO LA 'jk ileven'
ReplyDeleteMimi nafikiri Ingekuwa vema kama tungeiita John Malecella 11, ama Kingunge Ngombare mwiru stars, Mrema Stars, Rashid Kawawa 11,Mwalimu Nyerere Juniors,Anna Abdallah Starz ama hata baba yangu Samwel Sitta Starz, mnasemaje waungwana? Haya ni baadhi ya majina mazuri ya kujivunia na wamefanya mambo mengi tu muhimu katika nchi yetu tangu tupate uhuru kumbe jamani tuwa enzi hawa ndugu siyo lazima awe baba yangu lakini hao wote hapo wamelifanyia taifa letu mambo mengi jamani.
ReplyDeletemi binafsi sina interest na mabadiliko ya jina la timu .. ila kutokana na MAUMIVU ya kuangalia mechi wima taifa.... noma zaidi ni pale unapolazimika kwenda kiwanjani saa sita mchana...tiketi za kununua mkononi mwa askari mwenye njaa.. mnasukumana mlangoni mpaka mnakoma... halafu ukifanikiwa kuingia uwanjani unasimama mpaka mechi ianze.. kama hiyo haitoshi.. mechi ikianza lazima uwe mrefu ili uone vizuri..... vyoo hakuna... taabu TABU tupu!!! polisi milangoni ndiyo walikuwa wanasababisha kero hii k*manina zao wakome sasa!
ReplyDeletekinachonivutia zaidi nikiangalia hiyo picha hapo juu ni hiyo background ya kiwanja kipya. napata uthongo wa kwenda mpirani kwa ari mpya. hebu niambieni.. ina maana kila atakayenunua tiketi atakuwa na kiti chake? thiamini.. walahi! ila itabidi tuwe wastaarabu.. tusije tukawa tunagonganishwa kiti kimoja watu kibao... ndiyo usishangae.. ish ...kwa sababu enzi zile mabasi ya mikoani walikuwa wanakatiwa tikiti moja watu 3!! halafu mbabe ndiye atakayekaa.
hebu niambieni,,, itakuwa vipi?
ameifanyia nini huyo jk hata timu ya taifa iitwe jina lake,wabongo na nyie kwa kujipendekeza,kesho mtaipa majina ya mademu zake sasa.
ReplyDeleteWewe John Sitta unachemka. Kwa nini team ya taifa ipewe jina la watu wa CCM wanaologana, na kuuana. Waulize Sokoine, Kolimba, na Mwaikambo walikufaje. Wachawi tu hao CCM.
ReplyDeleteKuiita TAIFA STARS JK eleven ni ujinga amabao nisingependa utokee wakati bado naishi afadhali nife kwanza alafu watu waiite timu kwa jina hilo. Hebu angalieni , mnakimbilia kuwaenzi wapenda MISIFA, tunaacha watu muhimu sana kama akina Mzee Morisi NYUNYUSA, MAKOPNGORO,RAJAB HERI DIWANI, SOKOINE,BIBI TITI, KAMBONA,THABIT KOMBO,Kasela Bantu, Fundikira, tunakimbilia hawa ambao hawajafanya lolote la maana, TAIFA STARS si mara ya kwanza kushinda angali nyuma awakati wa akina Mahadhi, Tino, Kibadeni, Sembuli n.k leo hii badala ya kuwaenzi hao tunataka kufanya mambo ya MISIF TU, acaheni hizo, hakuna cjochote tungojee kipigo kule Bukinabe, tushukuru kwa vile ni ligi ingekuwa mtoano mngeona safari yetu ya wendawazimu.MAGAZETI ya TZ nayo yaache ujinga kuandika andika mambo ya MISIFA
ReplyDeleteAIBU AIBU TUPU MUHESHIMIWA KIKWETE HAO UNAOWASHANGILIA TAIFA STARS MMESHINDWA KWELI KUWANUNULIA SARE ZA VIATU HADI KILA MCHEZAJI ANAVAA CHAKWAKE NA ISIKOSE WAMEAZIMANA AIBU AIBU, HADI JACK PEMBA ATUTUMIE MITUMBA YA VIATU JAMINI.MHESHIMIWA RAIS KAMA TUNAPATA PESA ZA VIINGILIO KWA NINI VIATU VISIPATIKANE VYA TIMU YA TAIFA JAMANI? AIBU AIBU....
ReplyDeleteKwenye soka kila mtu anavyaa viatu anavyopenda, dunia wanafanya hivyo. Angalia Ronadinho anavyaa viatu gani na Ronaldo anavyaa viatu gani.
ReplyDeleteangalia viatu we mshamba lunyamila
John Sitta, umeamka nazo nini babu, ndio comments gani sasa zile?? anyway tunakuelewa, si wewe, ulabu unaongea.
ReplyDeleteEdibily Lunyamilla, sijui nyie wachezaji wa zamani mmeingiwa na kitu gani kama mwenzio Mgunda, kati ya watu wote wewe ndio ulitakiwa uelewe vizuri kabisa kuhusu issue ya viatu, kulaleki!! jamaa kakupa mfano hapo DINHO, rooney, beckham, ukiangalia timu zote za taifa siku hizi kaka viatu sio tena standard kama 47 kila mtu anavaa alichokuwa comfortable nacho, you should know better, kina Song wao ndio kabisa wanavaa rangi mbili, chekundu na manjano, hivi huwa mnafanya nini mkiacha soka? inaonekana hamna habari kabisaaa.....umekaa mjini miaka mingi sasa Lunya au usharudi Kigoma??
Nimefurahishwa kuona watu wanatoa mapendekezo tofauti kuhusu timu yetu ya taifa ambayo kwa muda mrefu mafanikio yake yamekuwa hafifu.tukumbuke hii siyo timu ya mtu mmoja ( privately owned team)!!! Wachezaji 11 wanawakilisha taifa la Tanzania lenye watu zaidi ya million 35....jina muafaka lenye kuweza kuwakilisha watu wote bila kujali kabila , mkoa au sehemu ya nchi ambayo inajulikana zaidi (kilimanjaro,serengeti, meru au victoria) liatakuwa ni bora zaidi.jina "taifa stars" ni muafaka zaidi kwani lina maana ya National stars lakini kwa lugha ya kiswahili ambayo ni lugha ya taifa(our identity). lakini kama tunataka kutofautisha mchango maalum wa kiongozi au wakati fulani kimafanikio au matatizo tunaweza kui-nickname accordingly!!!
ReplyDeletemfano kwa wakati huu wa kikwete...."Taifa Stars-the JK Eleven":"Taifa Stars-Kakakuona"....inakuwa rahisi kwa watu kuikumbuka timu ambayo ilifanya vizuri zaidi.mfano...taifa stars-jk eleven ni bora zaidi kuliko the Kakakuona!!!
Kuhusu swala la wachezaji kuvaa viatu tofauti si la msingi zaidi. tunaweza kuweka umuhimu kwenye rangi moja au zinazofanana na jersey colors....kumbukeni wenzetu wa mataifa mengine wana wachezaji wa-kulipwa ambao wana-shoe contracts ambazo zinawabana kila waendapo na timu zao za taifa zina-adjust to accomodate michango yao katika timu.Wataalamu wa soka pia wamegundua kuwa tofauti ya rangi za viatu zinawa-identify team stars bila ya mchezaji wa timu pamoja kuanza kufikiria ni nani anayempasia mpira na ni jinsi gani anapenda mpira utumwe kwake.(fast,slow,away or close)....Tukumbuke jersey zinawafanya wachezaji wote kuonekana wanafanana ...number ndio kitofautisho rahisi.(viatu na jersey za mikono mirefu au mifupi kwa position zinatumika zaidi siku hizi za karibuni-mfano long sleeves for defenders)
Naungana na maoni ya anony hapo juu umeongea pointi tupu, sio mastaa wetu wa zamani, anyway, jina ni Taifa STARS, Period!!! raisi akibadilika je baada ya hiyo miaka kumi? mambo ya Kaunda na Chiluba hayo.
ReplyDeleteJamani hamjambo ?
ReplyDeleteNani atanisaïdiya kupata picha za "MZEE MORISI?"
tafadhali saana.
Jr