Home
Unlabelled
nyirenda
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
mzee michuzi shukrani kwa kuweka hii picha, maana inatukumbusha utanzania wetu. ingawa tuko nje ya nchi but tanzania is our home and mother land. we luv Tanzania. God bless Tanzania.
ReplyDeleteaisee mzee michuzi kama unaweza tuwekee picha ya uwanja wa Taifa wakati wa uhuru(late Mwl. Nyerere akiapishwa). kama unaweza ndugu yangu. uk
Hii picha ni muhimu kweli katika historia ya nchi yetu.Chakusikitisha mpaka leo Tanzania tumeshindwa kufikia uhuru kamili.Mpaka leo tunategemea misaada hata kuendesha serikali yetu .Ningependa picha hii itukumbushe kuwa uhuru wa nchi yetu ni jambo la kupigania bado.Na wanajeshi ni mimi na wewe.
ReplyDeleteSimon Kitururu kwa maoni yako mafupi sidhani kama unaelewa maana halisi ya uhuru wa nchi. Tanzania tuna uhuru kamili...kutegemea misaada ili kuiendesha nchi yetu ni uchaguzi wetu wenyewe kutokana matendo yetu wenyewe kupitia kwa viongozi tuliowachagua wenyewe kama wawakilishi wetu.
ReplyDeleteKwa mtazamo wangu sidhani kuwa Watanzania tunaweza kuamua tu nchi yetu itegemee misaada kwa kupenda au kuchagua.Na pia ninaamini hii misaada imepunguza uhuru wa serikali kujiamulia mambo.Kwani hata wakati Nyerere anapinga masharti ya IMF na world bank ikafikia kushindikana kutokana na ukweli huwezi kubishana na watu ambao wanaweza kuidhoofisha serikali yako kwa kuinyima pesa za kuendeshea nchi.Angalia kama Zimbabwe ilivyofanyiwa na haya mataifa ambayo yanamiliki pesa za misaada. Sasa mimi naamini uhuru halisi wa nchi utapatikana pale tutakapoweza kutotegemea cha mtu.NI sawasawa tu na uhuru kutoka kwa wazazi unavyopatikana pale mtoto anapoondoka nyumbani na kuanza kujitegemea.Ni mtazamo wangu tu huu mzee Anonymous!
ReplyDeleteBwana Simon Kitururu, mtizamo wako una ukweli fulani ndani yake lakini ukitumia maana hiyo ya uhuru basi ni nchi cheche sana duniani zenye uhuru kamili maana hata Urusi wanategemea misaada ya Marekani...waingereza wanalazimika kupigana vita bege kwa bega na marekani kwa manufaa ya uchumi wao...Nadhani ni vizuri utofautishe uhuru wa kweli na uchumi tegemezi. Sisi ni masikini na tegemezi japo tuna uhuru wa kweli, Cuba ni masikini...wana uhuru wa kweli kisiasa japo raia si huru na hawana uchumi tegemezi kama tulivyo nchi nyingi za africa. Kwa ufupi uhuru ni tungo tata na inategemea unalenga na kujadili nini. Kwa hiyo ni vema tukasema nchi yetu ni huru japo uchumi wake siyo huru kama zilivyo nchi takribani zote duniani.
ReplyDeleteCaptain Nyirenda kwasas yuko wapi na kama yupo Jeshini bado ana rank gani na kama kastaafu aliishia rank gani/ huyu ni muhimu sana na ni mtu wa kumuenzi kuliko JK Eleven!
ReplyDeleteNyirenda aliacha jeshi baada ya wazawa waliokuwa jeshini kumpiga vita kuwa atakuwaje na wadhifa mkubwa jeshini wakati yeye ni mnyasa wa Malawi by origin. Nilisikia kuwa yuko Dar bado, huwa anasali pale St. Columbus Church, Upanga, opposite na(Formerly) Palm Beach Hotel.
ReplyDeleteMichuzi,
ReplyDeleteNani alikuwa mpiga picha wa picha hii?Nadhani huyo aliyepiga picha hii naye ana umuhimu wa aina yake achilia mbali ushujaa wake wa kuukwea mlima Kilimanjaro na pia kuhakikisha kamera inakuwa salama.