kila mahali bongo kuna mabango ya matangazo kama hili hapa ilala

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Huu uchafu unapatikana bongo peke yake zunguka dunia nzima kuanzia Nairobi, kiwango cha haya mabango ni kikubwa mno,kinaharibu sura ya mji, wataalam wa mazingira mtanisaidia hivyo vyuma vinavyopotezwa hapo vingetumika kwenye ujenzi wa madaraja n.K, hata lingekuwa robo yake lingeonekana vizuri, huu ni UCHAFU.

    ReplyDelete
  2. hilo bango lenyewe liko wapi? na watweka mapicha ya cowboy...sanasana usumbufu tu kwa wananchi hebu ona walivyobanwa...na hapo daladala hizo zipe siku chache tu, zitalivaa hilo bango kama hazina akili nzuri...hivi nani anyetoa ruhusa ya mambo haya?

    ReplyDelete
  3. kikwete ndie anayetoa ruhusa !!

    ReplyDelete
  4. Mnashangaa mabango, hamjaona nyumba za serkari zikipakwa rangi ya matangazo kama vodacon? Nakumbuka mwazoni mwa mwaka huu jengo la sayansi lilikuwa na rangi hiyo, pale msimbazi centre kuna jengo pia lina rangi hiyo. Nadhani huo ndio uchafu zaidi kuliko haya mabango.

    ReplyDelete
  5. Waweke matangazo madogo kiasi na yanayovutia. Hayo yamezidi sana ukubwa ingawa ni mazuri. Ujumbe kwa kampuni ya AI Outdoor.

    ReplyDelete
  6. Anony 2.30 am acha uongo niko Nairobi na mabango ya aina hiyo ndo yaliyoenea. Au ni Nairobi ipi unayoizungumzia? Watu bwana!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  7. Mkubwa mzima ovyooo, unafikri kuwa Nairobi ni sifa? mimi nilijua upo viwanja kumbe upo Nairobi..!

    ReplyDelete
  8. Hayo mabango mimi sioni shida. Unayaona meupe, ushahidi kuwa biashara ya matangazo hakuna.Hivyo wenyewe msiwasumbue kuwa wayang`oe. Hapo walipo wamechoka kipesa hata kutuma kibarua wa kutindua na nyundo hawawezi kumlipa! Labda city Council wayatoe.Wenye hayo mabango Walipata pesa nyingi wakati wa kampeni za uchaguzi. Kikwete alijaza picha zake za Ari mpya,Kasi mpya,nguvu mpya sasa na yeye kaishiwa hoja hana jipya la kutangaza kwenye hayo mabango na pesa kaishiwa sasa anahangaika kuzurura kwenye vichochoro vya nchi za watu na kopo la kuombea misaada kubwa kidogo kuliko lile la ombaomba wa kigogo Matonya wa Dodoma.

    ReplyDelete
  9. HAYO NDIO MAMBO YA KUCHIMBA DHAHABU KUONDOKA NA KUWAACHIA WENYEJI USHUZI.
    SASA ANGALIENI HIYO NYUMBA HAPO AROUND, NA NYINGINE ZOTE ENEO HILI NI USHUZI HUU HUU.
    HIYO HELA MATANGAZO INAENDA CITY NA CITY INAFANYIA NINI KWA WANANCHI WALE WANAOSUMBULIWA NA HAYO MABANGO USIKU NA MCHANA?
    KWA NINI WATU WOTE WANAOKAA MAENEO YA THAMANI HUWA WANAONEWA KAMA HAWANA KITU? MWISHOWE WATAWATRICK MPAKA WAUZE NYUMBA WAHAME!
    WE KIKWETE VIPI WEWE?

    ReplyDelete
  10. haya mabango poa sana huwa yanatupa kivuli wakati wa jua kali tukiwa tunasubiria kupanda ma daladala

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...