barabara ya nyerere (zamani pugu) hapa dar karibu na njia ya kwenda keko kuna msikiti na kanisa ndani ya kiunga kimoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Tanzania ni mfano wa kuigwa kwenye mambo ya dini.

    ReplyDelete
  2. michuzi naona umeshuka kwenye benz....big up!

    ReplyDelete
  3. Kwakweli Kaka Michuzi, mimi nina mtazamo tofauti kidogo kuhusiana na hili. lakini ni mtazamo wangu tu na si vinginevyo.
    kwanza kwakweli ningeonelea kwamba serikali iingilie kati ujenzi wa makanisa, na misikiti hovyo, kwani tunakoelekea sasa ni hatari hasa mijini, na jiji letu la Dar. mfano ni huo hapo ambako kila siku huwa naangalia na nashangaa, kwani misikiti ni lazima iwe na loud speakers zile za mnanda, ambapo kila ikifika muda wa swala mhadhini huadhini kwa sauti kubwa mno na kuleta kelele kubwa sana hasa kwa wakazi wa jirani. Tunakuja kwa makanisa, nayo ni hivyo hivyo, kwani utakuta wenzetu sisi tuliookolewa hukesha tukiimba na kulia usiku kucha tena kwenye maloud speaker hayo hayo. Sasa basi siku zinavyozidi kwenda tutajikuta tunatengeneza Istanbul na Rome ndani ya Dar es salaam. tena afadhali na Rome hakuna makelele ya kukesha usiku kucha, kwani utakuta wengine wa akina Kakobe huwa wanaweka redio kwenye loud speakers wakati wahusika wamekwenda kulala nyumbani, sasa zile kanda zitaimba na kuhubiri usiku kucha kwa sauti kubwa wakati hakuna muumini hata mmoja. sasa sijui tunaelekea kwenye ustaarabu gani.

    Kama speed ya kujenga misikiti na makanisa ingekwenda sambamba ya ujenzi wa mashule na viwanja vya michezo nadhani nchi hii ingeendelea sana. naiomba serikali iangalie sana utoaji wa vibali vya ujenzi wa makanisa na misikiti kwenye makazi ya watu. Imejazana mno na kutupigia kelele. Utakuta maeneo ya sinza, kumeongezeka na mabaa, afadhali makamba alikuja juu na ufungaji wa baa mapema, la sivyo ingezidi kuwa kero. Au la makanisa na misikiti yenye maspeaker ya mnanda yawekwe mbali na jamii. utakuta umezungukwa na makelele kila mahali unashindwa kulala. ukitoka unakutana na kelele za makonda, ukirudi za makanisa na misikiti, ukipita ni mabaa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...