wana jeiwii wakicheza ngoma ya kinyakyusa. samahani nimesahau kuuliza jina lake.wadau naomba msaada...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Hiyo sio ngoma ya Wamanda Michuzi, sidhani kama ni Ngoma ya Wanyakyusa kwa jinsi walivyovaa hao jamaa watakuwa wanatokeo mwambao wa ziwa Nyasa

    ReplyDelete
  2. ukimaanisha niya wanyasa??? basi "mganda"

    ReplyDelete
  3. Haloo bwana Michuzi, salam sana. Nimefurahi sana kuijua blog yako, inanivunja mbavu, kwa lugha yako. Hiyo ngoma wanyakyusa tunayo inaitwa "Mapenenga" lakini sisi hatuvaagi sare kwa hiyo hao watakuwa ni wangoni na mganda, its the same thing though.

    ReplyDelete
  4. Hiyo ngoma inaitwa Ling'oma.Ni maarufu Unyakyusa, Undali, Ungonde, na Ulambya katika wilaya za Rungwe, Ileje na Kyela.Hata upande wa Malawi mpakani na Tanzania wanacheza ngoma hii. Na ngoma hii inachezwa zaidi wakati wa kiangazi, shughuli za kilimo zikishapungua.

    ReplyDelete
  5. Hii ngoma ni bomba. Hivi wewe michuzi mbona unaleta vitu vizuri sana! yaani sio tu Bongo flava ambazo watoto wa sasa hawajui tumetoka wapi?

    ReplyDelete
  6. kazi nzuri michuzi

    ReplyDelete
  7. MICHUZI hongera kwa kazi nzuri,Ngoma ya KINYAKYUSA inaitwa ING`OMA na huo urembo mwekundu unaitwa PATESI,Yaani Nimefurahi sana huku ughaibini,Ikiwezekana tupatiwe na DVD kabisa.

    ReplyDelete
  8. HAO VIJANA POA WASIJE WAKAWA KAMA DADA KING ANATULETEA MITINDO YA NYWELE TU NA MASTAILI YA KUIGA KWA WAKINA MAREHEMU TUPAC NA WASANII WENGENE WA AMERICA HUKU NI BONGO WAJE KIBONGO BONGO TUTA WAKARIBISHA UJUMBE WAO TUTAUSIKILIZA KAMA TUKIUKUBALI POA TUTAPITISHA FAGIO NA KUWAFAGILIA WA WA

    ReplyDelete
  9. ISSA hilo ni lipenenge la wanyakyusa?

    ReplyDelete
  10. Issa Miposi (ooh naomba uniruhusu nitumie hilo maana ndio michuzi kwa kinyakyusa.

    Ngoma hiyo inaitwa ling'oma, ngoma hiyo inafanana sana na mganda ya wanyasa tofauti pekee ni kuwa wanyasa wanaimba lakini wanyakyusa ktk ling'oma ni ngoma tu pamoja na ndululutilo.

    ReplyDelete
  11. Hallo Michuzi nimekukubali kazi yako siyo mchezo.Maana umenikumbusha mbali sana,ngoma hiyo inaitwa Ling'oma.Mtu mchafu hachezi ngoma hiyo.

    ReplyDelete
  12. Jamani hili kabila kwa kuji proud hadi wanakera. Wao na Wahaya baba mmoja mama mmoja.

    ReplyDelete
  13. hao wa Zambia,kweli nyerere alikua na roho nzuri.kawaleta toka jirani hao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...