nani kasema mwalimu hajawahi kukaa kiti kimoja na idi amin dadah? hapa ni algeria wakati wa mkutano wa nchi zisizofungamana na upande wowote septemba 1973. aliyetupa kisogo ni waziri wa mambo ya nje enzi hizo john malecela, kushoto ni mama maria

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Michuzi,
    Hiyo picha inanikumbusha mengi. Ni wakati ambao E.A.C ilikuwa iko katika kipindi kigumu mno kiuchumi. Kenya wao walikuwa wanaoina bora kwa sababu uchumi wao ulikuwa stable mno na ulikuwa ukikua, na ndo maana Jomo Kenyatta nafikiri hayuko hapo. Tanzania ndo kwanza mambo yalikuwa yamekolea ya ujamaa na kujitegemea (sera iliyokufa kifo cha mende) ambayo makali yake kiutekelezaje bado tunayaona hadi sasa. Uganda nayo huyo bwana unayemwona ndo kwanza alikuwa kaanza kulewa Ikulu, akifikiri kuwa rais wewe unakuwa Mungu.

    Katika picha hiyo sijui wanaongea nini, nafikiri labda Idd Amin anamuuliza mwalimu kama alishawahi kushika hata bunduki, wachilia mbali kuitumia.

    Kihistoria hiyo picha inatuonyesha kwamba your best friend could your worst enemy and your worst enemy could be your best friend..

    Kwani nani alikuwa bora zaidi Uganda, Obote au Amin (wote ni marehemu - tuko free ku wajadili).

    ReplyDelete
  2. Wamewahi kukutana mara kadhaa tu, at one time Amin showed up un announced pale Mwanza wakati Mwalimu yupo pale..na Addis OAU summit Amin alikwenda kumshika mkono Nyerere

    ReplyDelete
  3. Idi aliwahi pia kujikaribisha mjini Mwanza na kukutana na Nyerere! lakini Nyerere aliwaagiza walinzi na ma-protokali kuwa hataki kamwe Amin alale Tanzania!

    ReplyDelete
  4. pamoja na mabaya aliyoyofanya huyo bwana Obote ambaye kwa ujumla ndie aliyesababisha tule sana Yanga( unga wa farasi) aliua zaidi aliporudi au tuseme tulivyomrudisha mara ya pili, hamna tofauti kati yao zaidi ya kwamba Obote alikuwa ni msomi hivyo mwenye upeo mkubwa zaidi ya mambo kuliko huyo bwana mkubwa hapo na ndiye aliyemjenga na kumtuma kuua hadi mambo yalipomgeukia mwenyewe, taifa zima likafungishwa mkanda kwa ajili tu ya kutetea interest za mshikaji mmoja, ama kweli.

    ReplyDelete
  5. Licha ya matatizo yake, Amin kaisaidia sana Uganda. Pia ni kweli Obote ndiye aliyeua sana kuliko Amin na pia hakuwa na shukrani kwa TZ ndiyo maana alipopinduliwa mara ya pili hakukimbilia TZ.

    ReplyDelete
  6. Amin na mabaya yote atakubukwa kwa moja kubwa la kuwawezesha waganda kumiliki biashara kubwa kwa kuwanyang`anya wahindi.Laiti serikali ya Tanzania ingeamua kuanza kuwapa watanzania wazawa tenda kubwa na kuacha kuwapa wahindi huo ndi ungekuwa uwezeshaji mkubwa kuliko hizi kelele za Saccos.Kumwaga mapesa kila mkoa ni kuongeza inflation tu watu wataolea,watazinywea n.k hakuna uzalishaji wa maana utaoongezeka.Idd Amin kwa hilo la kuwawezesha waganda kiuchumi alijitahidi pamoja na uuaji,ujinga wake na ujahidina wake uliojificha nyuma ya kombati za kijeshi na uraisi uliowapa kichefuchefu wengi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...