hili ndilo lango kuu la makaburi ya gombe, kinshasa,, jiji lenye watu takriban milioni 10.

naam! makaburi hayo yaliyo mtaa wa barabara ya juni 31, ambapo kama yalivyo makaburi ya kinondoni, huzikwa watu ambao ni kwamba tu. yaani unaambiwa mtu mwenye nazo hata afie wapi lakini atakodi ndege aje azikwe hapo.

hivi sasa, kama yalivyo makaburi ya kinondoni, sehemu hiyo imejaa na inasemekana kulikuwepo na mtindo wa watu kufukua maiti na kupisha mazishi ya mtu mwingine kinyemela, na maiti ilofukuliwa kutupwa kusikojulikana.

ikalazimu pawepo na ulinzi ili balaa hilo lisiendelee!

basi siku hiyo mien na chuwa tukaamua kwenda kutembelea makaburi hayo, hususan pale alipozikwa kabaselle yampanya pepe kale na pia franco lwanzo makiadi, wanamuziki ambao wabongo wengi tunawafahamu.

tulipofika tulikuta askari kibao wanayalinda makaburi hayo. Mwenyeji wetu alisema wenye jezi ya buluu ni askari wa serikali na wenye kijani ni wa bemba. Ila wote lao moja; huingii makaburini hadi utoe faranga.

tukajipigapiga na kuwapa kitu kidogo, tukaruhusiwa kuingia. Lakini tulipomaliza kutoa heshima kwenye kaburi la pepe kale na kutaka kwenda kwenye kaburi la lwambo, tulizuiwa kwa maelezo kuwa mapatano na thamani ya faranga nilotoa ni kaburi moja tu.
yaani ilikuwa kama tukitaka kwenda kuona kaburi la lwambo basi tutoke na kupatana upya.

kwa vile hatukuwa na faranga za kutosha tukaishia kupiga picha ya wizi na za mbali za kaburi hilo la lwambo. zilitutoka kama dola tano hivi za kimarekani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Bw Michuzi,Maelezo yako yanaonyeha kwamba bado Zaire hakuna serikali hila kuna magenge ya wahuni wanaoongoza nchi.Wahuni wapo busy kuvuna rasilimali asili za Congo kamam vile madini na bidhaa zitokanazo na misitu.God tusaidie TZ tusifikie hapo ilipo Congo. Angalau dalili zinaonyesha tunaelekea huko ilipo Congo-DRC.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...