*Awapongeza kwa uzalendo wao kujadili masuala ya kitaifa
*Awaasa kutofanya masikhara na siasa wala viongozi
*Watanzania walio mtandaoni wamjibu, wengine wamwuliza maswali kedekede


Katika hatua ambayo imeonyesha kuwafurahisha watanzania watumiao mtandao wa intanet walio ndani na nje ya Tanzania, Mhe. Freeman A. Mbowe amejitokeza na kujisajili katika Mtandao mmoja na kutoa maoni yake kama watanzania wengine wafanyavyo.

Hali hii imewafurahisha watanzania walio wengi kwani badala ya kuendelea kuongea mambo bila kuwa na mlengwa wa kuelekeza maswali yao na kero zao kwake wamempata kirahisi na kumwuliza au kumpa ushauri wao harakaharaka.

Tarehe 2, Desemba 2006 Mheshimiwa Mbowe alijisajili katika www.JamboForums.com na kueleza hisia zake & shukrani kwa watanzania ambao wamekuwa wakichangia katika mijadala mbalimbali mtandaoni.

Baadhi ya watanzania waliomhoji au kutoa shukrani zao wamempongeza Mhe. Mbowe kwa kutumia njia ya mtandao na kujiweka bayana. Wengine walionekana kutofurahishwa na kitendo chake kujiweka bayana wakidai kuwa inaweza kumwaribia jina.

Maoni mbalimbali yametolewa na Mhe. Mbowe aliahidi kutoa majibu moja baada ya jingine (hasa yatakayoonekana ya msingi).

Tunapenda kuungana na watanzania wenzetu kumshukuru Mhe. Mbowe kwa kuingia mtandaoni bila kujificha ili watanzania waweze kumwuliza maswali mbalimbali na tunamwomba asiwadharau au kuchukia pale atakapoulizwa maswali yanayoelekea kuwa na dhamira mbaya. Atambue wazi kuwa wanadamu hatufanani na lazima kuna wanaomuunga mkono na wasiomuunga mkono.

Aidha ingependeza viongozi zaidi wa kitaifa wangetumia fursa hii ya mtandao kuweza kuwafikia wananchi mbalimbali kwani wanakuwa wanatoa dukuduku zao bila kificho na bila wasiwasi.

Kupata kujua watanzania wamemwuliza maswali gani na amejibu nini Bofya hapa: www.JamboForums.com

http://jambotanzania.net/v2/content/view/923/2/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hakuna haja ya kwenda www.JamboForums.com
    kuzungumza na Mbowe wa Chadema! Chadema yetu imo mtandaoni, na mlango wake uko wazi mithili wa hekalu: http://www.chadema.net

    ReplyDelete
  2. BANK FREEZE FOR CORRUPT OFFICIALS COMING...

    Officials in the public and private sectors who are involved in grand corruption and looting of public resources will have their foreign bank accounts frozen and properties confiscated, once the review of the anti-corruption law is completed.

    The draft bill is ready. The government is finalising formalities for its approval before it is tabled in Parliament, the Minister of State in the President Office (Good Governance), Philip Marmo, said in Dar es Salaam yesterday.

    ’’Preparatory processes have been completed?the bill will be presented to the cabinet for preliminary approval this week,’’ said Marmo in an exclusive interview at the anti-corruption forum in Dar es Salaam.

    The minister spoke after officiating at the National Anti-Corruption Strategy and Action Plans II (NACSAP II).

    After the cabinet approval, he said, the bill would be tabled in Parliament for deliberations and final endorsement, before being assented to by the President to become law.

    Once it becomes law, it will contain provisions that will take to task corrupt government officials and other people involved in grand corruption, theft of public properties and resources, and international crime.

    The new law will seal loopholes used by people employed in the public service and the private sector who steal and deposit government money in bank accounts outside the country.

    ’’With this legislation, we freeze their accounts and confiscate their suspected ill-gotten wealth, pending completion of investigations,’’ said Marmo.

    Anti-corruption crusaders described the document as a fresh government resolve to crack down on grand corruption, which has cost the country billions of shillings.

    Current anti-corruption laws could hardly touch big shots black listed by the anti-corruption watchdog.

    ”Big shots involved in corrupt acts will face a difficult situation once the law becomes operational,” said Marmo, without providing more details.

    The new legislation encompasses international conventions against transnational crimes, corruption, money laundering and related practices.

    The new document incorporates the Southern African Development Cooperation (SADC), African Union (AU), United Nations conventions and other international agreements on corruption and related vices.

    ’’These are new components in the country’s anti-corruption law. We are faced with difficulties in punishing people stealing money within the country and depositing it in foreign bank accounts,’’ said the minister, ’’such cases can easily be handled and the stolen money recovered.’’

    Earlier, the Chairman of the Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture, Elvis Msiba, said developing new anti-corruption legislation was useless if the anti-corruption watchdog has no teeth to bite.

    ’’We cannot win the war if senior government officials and others in the private sector are suspected to be corrupt but left untouched. Let’s take it seriously, and make sure that law bites the culprits,’’ said Musiba.

    Speaking at the same occasion, the Chairman of the Media Owners Association of Tanzania, Reginald Mengi, pushed for enactment of a law to protect whistleblowers as a strategy of intensifying the fight against corruption.

    ’’Whistleblowers need protection?and their information on corrupt people should be treated as confidential.

    Disclosure of sources of information will amount to silencing free speech and corruption cover up,’’ said Mengi.

    He challenged the government to act timely on bribery scandals exposed by the media in a drive to crack down on grand corruption in government circles and the private sector.

    ’’Timely action by relevant state organs in relation to corruption scandals exposed by the media will prove the government’s resolve to eradicate bribery and build government credibility,’’ Mengi said

    ReplyDelete
  3. Napenda sera za mzee mzima Mbowe ana sera nzuri sana.Nilibahatika kuongea nae kidogo pale Protea Hotel Machame....Watu/Vijana kama hawa wananchi wanatakiwa wawaangalie maana wana upeop mkubwa sana kulingana na viongozi wengine wa CCM eti wanakaa madarakani miaka 40 na zaidi kwa lipi zuri walilolifanya?Muone Mzindakaya au Makweta...ndio wamejenga shule au kuimarisha kilimo ila miaka yote hiyo yangetakiwa yafanyike makubwa zaidi...
    Wapi Amina Chifupa?keshazimwa kama kawaida ya CCM?Wapi wabunge kama akina Njelu Kasaka au Tuntemeke Sanga?

    ReplyDelete
  4. Habari


    Ndio kukata tamaa kwa Boys II Men?
    Mwanzoni kabisa baada ya Boys II Men kutwaa madaraka, walikuja na ahadi za suluhisho la kero kibao zilizotolewa wakati wa kampeni ya Uchaguzi Mkuu 2005.

    Boy II Men (Rais JK na PM wake Lowassa) baada ya kuenea katika safu za uongozi waliahidi kukabiliana kichwa kichwa na lundo la ahadi alizotoa JK akigombea Urais.

    Sasa maneno yanatakiwa yabadilike kuwa vitendo na hali inaanza kuwa ngumu na wananchi inabidi waelezwe nini kinaendelea au waanze kuona matunda ya kero walizotoa.

    Katika hili tutaongelea suala la umeme tu ambalo PM Edward Lowassa amerejea nchini kutoka Canada na kuibuka na ule utetezi wa mwaka 47 kuwa tatizo la umeme tumelirithi kutoka serikali ya awamu ya tatu.

    Kwa maneno mengine tatizo hilo lilitoka ndani ya serikali ya Rais Mstaafu Benny ambayo Rais JK na PM Lowassa walikuwa vijana wake wa kazi.

    PM Lowassa alisema vilevile kuwa kuna nchi nyingine zenye tatizo kama hili kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani na utegemezi wa mabwawa kama njia ya kutoa umeme.

    Kwa hali ilivyo Bongo hakuna nchi yenye hali mbaya ya umeme kama ilivyo mgawo wa umeme hapa Bongo, labda Somalia ingawaje PM alizitaja Ghana na Uganda kuwa tatizo ni hilo hilo.

    Utetezi wa Lowassa unaanza kututia shaka juu ya uwezo wao
    kukabiliana na tatizo hilo kwani anadhihirisha kulinyooshea mikono pamoja na ahadi bomba walizotinga nazo kuwa ifikapo Desemba (ndio hii) tatizo hilo lingekuwa limeisha.

    Ingawaje hali ni mbaya walau Mh Lowassa jaribu basi kutupooza na kutupa moyo kuwa hali itakuwa bomba

    ReplyDelete
  5. This on has surely made my ribs ache..

    MAKE SURE YOU READ IN LUHYA ACCENT this interview between BBC (PPC) and Mr. Baraza Shituma (the Luhya fellow who dared to milk an elefant.)

    BBC: Sisi ni watu wa BBC na tunge penda kukuhoji kuhusu kilicho fanyikahivi majuzi.


    Baraza: Asandeni sana. Nimesichia sifa sa PPC kwa muta murefu sana na sichawahi fikiri ati siku espressowatanihochi.


    BBC: Sasa bwana Baraza unaweza kutueleza ni nini hasa kilichofanyikasikuhiyo.


    Baraza: Mimi nilikuwa katika siara sangu sa kawaita sa mtaani wakatiambapo niliona kandofu na katoto kake katoko, nasichia munasiita chumbo. Hapo hapo nikaamua kutafuta katepe katoko ntiyo niwese kwenta kwa hako kachumpo nikamue ile kanipatie masiwa kitoko nichipurutishe nayo na watoto pia wapate chitu cha kunywa. Sasasi ntiyo nilikuwa katika ile hali ya kukamua matiti sa nyuma sa yule ndofu ntiyo nikastukia kamenikapa kwa mapua yake na kunirusha chuu chuu. Sichui kalichuache kwamba nilikuwa nakamua, lapta kalisense tu. Muta simuta niliruti jini na ntiyo nikachimbilia ile muti ilikua karipu niwese kuipandeko. Kumbe yule ndofu alikuwa amecham sana, kakanifwata spitisana na kung'oa muti na misisi yake yote na muta si muta nikachipata chuu tena,lachini nikaamua sitawacha ile pranj ya muti nilikua nimesichilia. Niliporuti jini nilikua na pahati kwa file yule ndofu alikua tistractet (distracted} na wamama ambao walikuwa wakisumbua kachumbo kake katoko, ntiyo kakaamua kuwachana na mimi kuchimbilia mtoto wake. Ile chitu sielewi ni kwampa nimekamua ndofu sa Amposeli, Masai Mara,Tsafo na hata sa kutoka Tee Seti (Tanzania), rachini sicha wahi ona ndofu chisirani kama hii. Sichui hii ilikuwa inatoka wapi, hata tepe ya masiwa akapika teke na kumwaka masiwa yote, po!! Chiisirani tuu!


    BBC: Na sasa unajisikia aje mwili?


    Baraza: Mwili ni msuri tu ichapokua fiungo na mkongo ntiyo sitaumakitoko kitoko rachini nitakua sawa tu, inkawa sichui kama nitaruti kukamuachumbo tena. Wacha hiyo masiwa ikae. Na pia ninge penda kutumako salamu kwa nduku Elicha , akiwa huko Shamakhokho, Ingo, tata Truphena akiwa Shivaale Ingo, Na pia mchomba Cheremia akiwa kakameka Ingo,........uchumbe , kale kangompe ka chirani, kalisaako mtoto ? Niwekeeko hako kakuku nitakucha krismas Tesemba. Na pia muchuwe kwamba KPC , aiii....( BBC reporter
    Grumbles) , ooh sorre, PPC ndio nusu ya kuonana

    ReplyDelete
  6. HAYA TUTAENDELEA KUONA MENGI,MICHUZI MBONA HAMNA HOT NEWS TATIZO NI NINI??TUNATAKA KUJUA VITU VIPYA.

    ReplyDelete
  7. Mzee mbona kimya kama mimi bloguni. Au mambo ya Kinshasa hayo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...