jk akiangalia mitambo mbalimbali ya kuzalisha bia katika kiwanda cha kampuni ya bia bongo, ambapo alifungua mitambo mipya ya kisasa ya kupikia bia wikiendi hii. tbl sasa wamezindua upya bia aina ya ndovu na inaonesha kupendwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Bongo hajachacha tuliokuwa huku ughaibuni tukija tutaonja hiyo ndovu.
    Namuona rais wetu hapo anazidi kupendeza mungu ampe afya njema.

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli Bia hiyo ya NDOVU PREMIUM LAGER imeletwa kuimaliza Serengeti (SENGE)kama inavyoitwa na watu wa TBL... Ni tamu sana Bia hii...Associated Breweries kazeni buti....

    ReplyDelete
  3. Wamejaribu sio mbaya sana, ila bado wana kazi hadi kuifikia Serengeti, hili bia lao lina hang over kinoma wakati serengeti asubuhi unaamka kama jana yake hujanywa. IDUMU SERENGETI LAGER

    ReplyDelete
  4. Mambo gani haya kumfanya Rais kama mtoto kazi hiyo ilitakiwa aifanye waziri au wengineo

    yaani rais kawa cheap hivi?

    duh!
    noma

    ReplyDelete
  5. Wewe anony hapo juu unayesema rais kaa cheap una maana gani?ulitaka raisi afunguwe kiwanda halafu aondoke bila kukagua halafu waziri ndiyo aje akague nadhani un muone finyu wa mambo nyie ndiyo mliozoea kuwa viongozi wa kwenye viyoyozi unataka kila kitu uletewe taarifa!utaharibikiwa na mambo kwa kujonga kila kitu uletewe.Kama raisi mwenyewe alivyosema kwamba ukingoja itifaki ya ving'ora kwa kila jambo utaharibikiwa na mambo kwa hiyo rais yupo sahihi kabisa

    ReplyDelete
  6. Michuzi mfikishie Rais Kikwete Ujumbe huu tafadhali. Mwambie simfundishi kazi lakini ni ushauri tu.

    Nchi hii ina mambo mengi sana ya kushughulikiwa naye kama kiongozi wa nchi. Asipokuwa mwangalifu atamaliza muda wake bila kufanya cha maana kwa watanzania wengi. Najua ana nia ya kuitoa TZ katika matatizo mengi hasa UMASKINI. Apange vipaumbele (priority) ktk mambo ya kushughulikiwa kwa ukaribu na bidii sana. Afanye japo tu yafuatayo na atakuwa ametenda mengi sana kwa nchi yetu:

    1. Apiganie sana ELIMU katika ngazi zote na ajali SANA UBORA wa elimu.
    2. Apiganie sana miundo mbinu hasa barabara. Ahakikishe barabara ZOTE zinazounganisha mikoa na hata wilaya ziwekwe LAMI.Nchi kama Afika ya Kusini wana msemo (slogan) kuwa Transport is the Heartbeat of SA economy. Ktk miundombinu aangalie sana masuala ya nishati, mawasiliano,maji n.k.
    3. Akomalie afya na usalama wa nchi na raia wake.

    Mambo hayo ni ya msingi kwa kuwa yatapelekea watanzania kuamka na kuwa na uwezo wa kutumia raslimali zao nyingine vizuri na kwa ufanisi zaid, kuzalisha na kuuza bila kunyanyasika. Kilimo, kwa mfano, kamwe hakiwezekaniki bila miundombinu.

    Mambo mengine yatafanyiwa kazi kadri hali inavyozidi kuruhusu usoni. Mwambie rais akumbuke wahenga walisema mshika yote kwa pupa hukosa yote. Vipao mbele ni muhimu sana na ni LAZIMA kwa maendeleo ya nchi.

    Msalimie sana Rais.

    ReplyDelete
  7. Mtoa Maoni hapo juu, Hayo yote uliyosema au kuorodhesha, yanafanyiwa kazi kila kukicha, kati spiidi ile ya kasi mpya, Na kadiri yatakavyokuwa yakikamilika tutapata taarifa zake, Ila baada ya kasi kubwa ya kujenga nchi, hutakiwa kupumzika, na pumziko bora ni kupata the laga yenye ubora wa hali ya juu...

    ReplyDelete
  8. Michuzi, naomba hili Rais alisome ama alisikie.AFANYE ZIARA VIJIJINI, TANGU APATE MADARAKA HAJAFIKA HATA KIJIJI KIMOJA KUKAGUA MASHAMBA AMA KUANGALIA WANAKIJIJI WANAENDELEAJE, YEYE KAZI YAKE MIJINI TU, AFIKE HATA KIMBIJI AMA KIBUGUMO AONE KILIMO, AMA AENDE KULE CHAKWALE, YEYE ANAHITAJIKA ZAIDI VIJIJINI KULIKO AMERIA AMA MWANZA MJINI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...