
kwa heshima na taadhima naomba nitangaze kwamba rev. evm ndiye mshindi wa shindano letu la mwezi huu la 'jengo gani hili' lililotoka januari 8.
hongera sana rev. evm sio tu kwa kupatia bali pia kueleza kinagaubaga ni jengo gani hilo na zamani lilikuwa nini na mtaa wake. tafadhali wasiliana nami kupitia issamichuzi@gmail.com na utamke picha gani unataka nikutumie kama zawadi.
JIBU: HAPA NI MAKAO MAKUU YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI BARABARA YA SAMORA, ZAMANI MAKAO MAKUU YA TANESKO, MKABALA NA BRITISH COUNCIL NA STEERS.
kunradhi kwa kuchelewa kutoa matokeo mapema. hii ni sababu za kiufundi.
Hongera zako Revd. EVM, inaonekana kuwa wewe upo Ughaibuni, lakini hujatupa kwenu! Keep it up!! Nakuaminia mwanangu. NB: Naomba jina lako kamili, please!!
ReplyDelete