
basi la scandnavia likiwa eneo la ajali sehemu ya kijiji cha kisasa nje kidogo ya mji wa dodoma hivi majuzi baada ya ajali iliyohusisha basi hilo na daladala aina ya hiace ilosababisha vifo vya watu wanane papo hapo, wakiwemo mtoto wa mwaka mmjoa, wanafunzi wanne wa shule ya sekondali ya doreta iliyopo kisasa, pamoja na raia mmoja na dereva na konda wa daladala ambalo halipo pichani


MICHUZI, WALIOKUFA NA FAMILIA ZAO WANAFIDIWA? SHERIA INASEMAJE KAMA WENYE MABASI WAKIWAUA ABIRIA WAO? TUNAJUA M-TZ WA KAWAIDA HANA LIFE INSURANCE, JE INSURANCE YA MWENYE BASI INA-COVER ABIRIA?
ReplyDeleteHAYA NI MASWALI MUHIMU KWA WEWE KUFUATILIA, KWASABABU WATANZANIA WANAUWAWA BARABARANI MNO KILA SIKU NA HAKUNA AMBAYE YUKO RESPONSIBLE.
KWA MFANO, SHERIA MPYA INAYOWABANA WENYE MABASI KUWA DIRECTLY LIABLE WAKIUA BIRIA ITAWAFANYA WAWE MAKINI SANA. ITAWAFANYA MADEREVA WAO WAWE MKINI SANA, ITAPUNGUZA VIFO VYA ABIRIA WASIO NA HATIA.
KWA MFANO, SHERIA MPYA KWAMBA UKIUA ABIRIA KWENYE AJALI YA KUGONGANA USO KWA USO, LAZIMA UILIPE FAMILIA YA MFIWA MIL. 30 ITAWAFANYA WENYE MABASI NA MADEREVA WAO WAANZE KUTUMIA AKILI KAMA BINADAMU, SIO KAMA SASA AMBAPO WANAUWA WATU KIZEMBE KAMA NG'OMBE NA HASARA YAO NI MABASI YAO TU!!!
KUNA MWENYE BASI HATA MMOJA AMEFIDIA FAMILIA ZA ABIRIA WANAOUA KILA SIKU TANZANIA? HILI HALIWEI KURUHUSIWA KUENDELEA. SISI SOTE NI BINADAMU, SIO NG'OMBE, LAZIMA TUULINDE UBINADAMU WETU. KAMA HATUWEZI KUJILINDA WENYEWE, TUSUBIRI MISAADA KUTOKA NJE WAJE WATUSAIDIE TUSIUANE BARABARANI KIZEMBE?
Nafikiri kuna kitu kinaitwa third party liability.
ReplyDeleteLakini kwa uzoefu wangu mdogo, kwenye insurance za magari huweka kiwango kidogo cha fidia, ila kwenye mfano viwanda nk, utakuta wameweka hata milion 100.
Inabidi serikali sasa iangalie ni vipi itaanzisha sheria ya fidia
Ni hayo tu
kusema kweli migari ya scandinavia ni bomu sana kwa sasa,ingawa ajali haina kinga na inaweza kutokea hata kama gari jipya lakini huyu jamaa sasa magari yake mara nyingi hayafiki mwisho.Kuna wakati nilikuwa naenda moshi na basi lake la class ya juu nauli 27,000/ kwanza kufika hapo wame tu dereva kazima AC kama haitoshi kufika njia panda ndo ikawa mwisho wa safari,.Na watu walisha nionya kwamba magari ni mabovu sikusikia......atengeneze basi au akpoe tena mengine
ReplyDeleteKwakweli hali ya usalama wa vyombo vya kusafiria inasikitisha sana, hasa pale ajali inapotokea. Nimependa mawazo na maswali mazuri ya hapo juu lakini naona nikumbushe wasomaji kwamba maswala ya fidia bongo bado yako kwenye vitabu tu! Ukweli wa mambo ni kwamba makampuni ya Insurance yanapenda kukwepa kulipa ili yapate faida mara dufu. Kinachotokea ni kwamba ili kupata hiyo fidia, familia huenda ikalazimika kujikokota mahamani kwa miaka hata mitano na hata sijui fidia yenyewe kama kweli inakuja kuwa na kiwango kinachoendana maana inflation nayo haiwekwi maanani katika mambo mengi ya malipo bongo - hasa hasa utaiona kama ulikopa benki!
ReplyDeleteKwakweli hayo mambo ya fidia yamekaa vibaya hata sijui watu wanaweza kupewa msaada gani! Inasikitisha....