maprodyusa hodari wa filamu wa kibongo waishio ukerewe nassir mohamed (shoto) na mwanga kirahi wakimalizia kuhariri filami mbili moto ambazo zitakuwa sokoni hivi karibuni. habari zaidi soma chini hapo. wote wawili wako masomoni na hizi filamu ni moja ya mazoezi ya masomo yao...




Jina la Filamu:................. THE VICTIM OF LOVE
Mtengenezaji...................TIMELINE MEDIA
Waongozaji......................NASIR MOHAMED & AMRI BAWJI
Waandishi........................NASIR MOHAMED & AMRI BAWJI
Muigizaji kiongozi...........RIYAMA ALLY
Waigizaji..........................MAHSEN AWADHI(DR CHENI), CHAUSIKU SALUM
(BI. CHAU), RAHIMA KIPOZI, SAIDA YAHAYA, MARRY
FEDRICK,JUSTINE MHINA,FAIZA ALLY, ISSA MUSSA
(CLAUDE), MWINYI AHMED,FATUMA WAYMACK


Maudhui............................Tofauti na matarajio ya wazazi wake,binti Tausi( Riyama Ally) anakuwa ni mtoto wa shule anaeathirika na penzi la mwalimu wake, penzi ambalo linamsababishia ujauzito na aibu katika jamii pale kijijini kwake..

Baada ya miaka minne ya kutelekezwa Tausi anaweza kujipanga vizuri kimaisha akiwa na mtoto wake Majaliwa. Mwalimu Adam(Dr. Cheni) anarudi tena katika maisha ya Tausi na ujio huo ni wa kudai kupewa haki za mtoto na si kuwa pamoja kimapenzi na kulea mtoto wao kama Tausi alivyo tarajia na kusubiri kwa kipindi chote walichokuwa mbalimbali.

Penzi la Tausi kwa Adam linapelekea Tausi azidi kudhalilishwa na Adam kiasi cha kumplelekea Tausi achukue uamuzi utakao badili maisha yao milele,maisha ya Adam ,mtoto Majaliwa na maisha yake mwenyewe.

Sokoni:.............................. Inategemewa mwishoni mwa March(2007)
Msambazaj:.......................Tutawafahamisha baadae


OTHER INFORMATION
Filamu ilianza kushootiwa July 2005

Sound Tracks by: Allan Kalinga, Juma Kwiku, ENKAT

Sound designer: Mwanga Kirahi
walioshiriki katika utengenezaji: Mr. Amri Bawji,Mr. Kassim El siagi, Mr. Nasir Mohamed. Mr. Kulwa kikumba, Mr.John Lister

Camera men: Florian Lawrence(Ray), Abdulhakim Bayakub & Rashid Mrutu

Edited by Mbwana Kidato & Nasir Mohameed

Waigizaji wengine ni :
Bakari Baringo,Juma Ramadhani,Mama Abijani, Zena Jumbe, Moza Salim, Abdulrahman Zimbwe

LOCATIONS: Kijiji cha Amboni (Tanga) Tanga mjini, Dar es salaam


----------------------------------------------





Jina la filamu:.......................SUPER MODEL
Mtunzi...................................NASIR MOHAMED
Watengenezaji.......................TAWOMA & TIMELINE MEDIA
Muongozaji............................NASIR MOHAMED & KASSIM EL-SIAGI
Muigizaji kiongozi.................CUTE MALISA
Waigizaji................................KHALFAN AHMED(KELVIN)MRISHO ZIMBWE(TITO)
CHUCHU HANS,SAIDA YAHAYA,CHRISPIN NG'WENGWE,
VIOLET MUSHI(RADHA)MWANSITI MOHAMED(CHICHI)
FATUMA MAKONGORO(BI. MWENDA,MAHSEN AWADHI
(DR. CHEN)BARKE MZEE

Maudhui:Sasha, mlimbwende aliye juu katika fani, Sasha alikuwa na kila kitu mwanamke wa kileo angetamani kuwa nacho ikiwemo afya nzuri, mume mzuri, nyumba nzuri na magari ya kifahari.

Sasha alikosa kujiamini katika kazi yake kutokana na wimbi la warembo wanaoingia kwenye fani. Hofu hiyo iliyumbisha ndoa yake na kumfanya ajiingize kwenye dibwi na utumiaji wa madawa ya kulevya na hatimaye kupoteza kazi na mume aliyempenda.

Hata hivyo Sasha alifanikiwa kupata tiba na kubadili muelekeo wa maisha yake pale alipotambua kuwa umaarufu na urembo ni vitu vya kupita.Sasha aliweza kuanza maishi yake upya, maisha ambayo aliona ni ya furaha na amani yaliyomfanya asitake kurudi tena kwenye fani ya ulimbwede.

Sokoni:..................Mwezi wa April 2007
Msambazaji...........Tutawafahamisha

OTHER INFORMATION
SHOOTING:APRIL 2005
LOCATIONS: Dar es salaam & Bagamoyo
CAMERA MEN: Mwanga Kirahi and Hisani Muya
SOUND TARCK BY: Banana Zoro
SOUND DESIGNER:Mwanga Kirahi
EDITED BY : Nasir Mohamed & Mwanga Kirahi
WAIGIZAJI WENGINE: Abdulrahman Zimbwe, Chava Limembe,Athumani Issa(Mwalubadu)



f

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. tunafurahi kuona wabongo wakijitahidi katika fani mbalimbali. tatizo nilionalo mimi ni moja ambalo linajirudia kila siku. kwa mfano katika hizi filamu hatuoni kama kuna Casting Designer, makeup artist, costume designer, set-up producer etc.

    Kuna mambo mengi sana katika filamu ambayo ni muhimu. Utakuta hizo location walizopigia hizo filamu zinahitaji usanii na ubunifu wa hali ya juu katika kuijenga filamu hiyo, so tulihitaji maproducer na madesigner wa set-up. pia kuna tatizo ambalo kila siku tunaliona kwenye filamu za bongo, ambalo ni costumes. tunataka kuona filamu ikiwa na mahadhi gani, kama ni mapenzi, na wale washiriki wawe kweli wanavishwa katika nguo, au mahadhi fulani. kama ni bagamoyo, ni ya wakati gani, na mahadhi gani, so hapo tunataka kuona costume designer anaingia katika kuamua na kupanga waigizaji wavae nini na wakati gani, na siyo kutuletea filamu ambayo haivutii.

    jamani kuna vitu vidogo vidogo vingi ambavyo ni muhimu, na msichoke kuwashirikisha wasanii na wabunifu wengine wa nchini. kwa mfano katika costumes, kuna watu kama akina manju, nk.

    jamani tutumieni wengine mnapoandaa projects zenu, tupo tayari hata kwa bure, ili mradi tufanye kitu kiwe kizuri. utakuta hata sound haifanywi vizuri. jaribuni kuangalia Post production ya hizo filamu zinafanywa wapi na kwa ustadi gani. mkihitaji ushauri tupo jamani.

    haya sisi tunasubiri tuone filamu hizo, tutazinunua, na nia ni kukuza maendeleo ya ubunifu nchini mwetu.

    ReplyDelete
  2. issa michuzi mwangu wee blog yako kiboko yao nakufagilia mwanangu kwa sana waaa waah waaa

    iam sure itaku bab kubwa movie hii maana bi tatu yumo je nassir mohammed na mwanga kirahi naweza kupata copy yangu mimi niko ughaibuni new york, na je number ya bichau naweaa kupata nijibuni tafadhalini.

    ReplyDelete
  3. must begin by saying ni watu kama nyinyi Nassir Mohammed and Mwanga Kirahi. Mntatupa hope ya Entertainment Industry ya Tz. Nassir greets from NY keep up good work. Ya'all work hard from what i had heard during shoot

    ReplyDelete
  4. Hongera kwa ma-producer wa sinema hizo za Ki- Tanzania. Kwa vile kuna watanzania kibao hapa Uingereza na nyie ma-producer mnamalizia ukamilishaji wa sinema hiyo hapa Uingereza, mimi kama mkazi wa London napendekeza pia muangalie uwezekano wa sisi wakazi wa Uingereza kupata hiyo sinema kwa maajenti wenu hapa hapa London. Naomba majibu kupitia blogu hii.

    ReplyDelete
  5. Asanteni wote kwa maoni yenu mazuri. Kwanza mvuvi nitafurahi sana ukinitumia cv yako na sample ya kazi zako ili nione. Pili mimi mwanga napenda kusema kuwa ninachofanya ni kujaribu kurekebisha hizo filamu kazi ambayo si rahisi wakati mwingine kwani ubora wa filamu kiufundi ni pale unapoanza kupiga picha kuwa na uhakika wa kufanya kila kitu sahihi kwenye editing unamalizia kazi.
    kwa ndugu yetu wa NY unaweza kupata copy wasiliana na michuzi atakupa contact.

    Kwa mkazi wa uingereza tupe contact zako tutawasiliana.

    ReplyDelete
  6. ongera sana kakazangu kwa kazi nzuli mnayo ifanya watu wana ponda watu kujiliupua sasa haya ndio matunda ya kujilipua sasa mwambieni raisi wakimbizi sasa wanatoa ajira kwa kina bi chau nk

    ReplyDelete
  7. Mhh! kazi nzuri lkn bongo creativity Zero! hizo filamu zote ni copy ya filamu za ki nigeria. wamecopy mpaka majina! sasa kama Tz nao wanataka ku win soko la kimataifa nafikiri wanatakiwa kuwa wabunifu. hapo swala la haki miliki sijui linakuwaje.. Nigeria walitoa filamu zote hizo, Victim of love and super model. au kina cheni watuambie kwamba wameamua kutafsiri Nigerian films kuwa kwenye lugha yetu. vinginevyo soko la kimataifa still a long way to go.
    Mama Ushauri

    ReplyDelete
  8. we need more people like, keep it up.

    ReplyDelete
  9. Nunueni hiyo sinema halafu mrudi hapa tujadiliane mi niliapa kutonunua tena mpaka viwango viongezwe kidogo, nilinunua sinema moja nikajutia time and money.
    labda ilikuwa first bad experience kunawezekana kuna muvi nyingine ziko makini ila hiyo dogo ndo aliyoiamini kuwa bomba ndo kanitumia, anyway i would like to hear your experience after watching it

    ReplyDelete
  10. Producers wachovu tu hao!!wanasoma au kubeba boxes ughaibuni tu!!Angalia wapo wametulia kwenye council flats kisanii hapo basi mtu rundo

    ReplyDelete
  11. Producers wachovu tu hao!!wanasoma au kubeba boxes ughaibuni tu!!Angalia wapo wametulia kwenye council flats kisanii hapo basi mtu rundo

    ReplyDelete
  12. Hawa maproducer kwanza si wazamiaji kwa taarifa yako halafu la pili hawakai kwenye council flat jamaa na wafahamu shule imepanda na wanarudi Tanzania mmoja wao ni mtaalamu wa siku nyingi katika maproducer wanaofanya kazi nyingi nje yumo na anaijua kazi yake. Tusiwe na tabia ya kutukana waswahili wenzetu tubadilike tupeane mawazo ya kujenga mwenzako akifanya kitu mpe mawazo ya kumsaidia aboreshe pale alipokosea. Mawazo finyu hayatatufikisha mbali.Mwanga na Nasir mkirudi bongo muwasaidie na wengine keep it up.

    ReplyDelete
  13. Ma-producer wa sinema tuwasiliane na mimi mkazi wa Uingereza kwa simu 07903244977 ili nipate movie zenu hapa hapa Uingereza. Tunakumbuka sana nyumbani na waigizaji kama kina Bi. Chau na wengine. Pia kuwapatia watoto wetu wa kitanzania hapa Uingereza hamasa ya kupenda na kutambua kuwa ki-swahili pia ni lugha mojawapo kubwa ulimwenguni.

    ReplyDelete
  14. shukran anonymous wa feb 24 at 2:11 kwa kuweka number ya simu na nimatarajio yangu kwamba tutapata direct line ya nasir mohammed au muhusikia ili tuagiziye hizo movie zetu. isije ikawa tena ohoo fulani katoka kabaki fulani na fulani hajui fulani atarejea saa ngapi etc. shukran tena sawa tutapiga simu sawa na michuzi pia shukran kwa kuweka number hii kwenye blog yako ya kimataifa, mwana michuzi umetoka mbali mwanangu mungu hamtupi mja wake usisahau kupiga msalaa na kumshukuru ALLAH kila leo mwanangu eeh.

    ReplyDelete
  15. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...