leo asubuhi kuna miss amafunga pingu za maisha. gesi hu?

wakati huo huo kuna mdau kanidondoshea hii hapo chini sasa hivi...

Bwana michuzi hongera kwa kazi nzuri.Kwa kuwa glob yako inasomwa sana,naomba utafute nafasi uyaweke maoni yangu haya;

Jana,tar 16/02/07 majira ya saa moja usiku,Mtangazaji wa Kipindi cha Jahazi cha clouds FM (Gardner Habash) alikuwa na mgeni wake studi, (Wema Sepetu). Sasa akasoma tangazo la shule ya sekondari inaitwa Masinde Juu,inatangaza kuanza kwa muhula wa Form 5,pamoja na combination wanazotoa ambapo walizisoma PCB, CBG.CBN etc.

Kilichonikera,mara baada ya tangazo huyu Gardner akaanza kusema,' dah,hii combination ya CBG mimi mbona siijui?au mpya? itakuwa inamaanisha chemistry,Biology na Geography nadhani.Mimi sijawahi kuisikia hii.'

Wema nae akarukia,'hata mimi siijui,mimi navyojua combination yoyote ya science lazima iwe na physics,kama PCM,PCB etc.hizi CBN na CBG sijawahi kuzisikia,sijui zimetokea wapi'.

Gardner akamalizia,'labda siku hizi kila shule inaruhusiwa kutunga combination zake'. wakamalizia kwa kucheka kwa dharau.

Mimi namshauri Gardner kama kitu hakijui anyamaze kimya,hizi combination za CBG )chemistry,biology na Geography) na CBN (chemistry,biology na Nutrition) zipo miaka nenda rudi,zaidi ya miaka kumi na Jangwani kuna darasa kubwa tu la CBN.Ofcourse tunajua Gardner elimu yake,kwa hiyo sishangai sana kutokuzifahamu,lakini kwa nini atoe comment kwa Tangazo?shule imeilipa redio itoe tangazo kwa nini wakae kulijadili,tena mambo wasiyoyajua?

Huyu Wema ndio anasikitisha kweli,inaelekea IQ yake ndogo sana.Si katoka shule juzi tu huyu idiot!

Naomba unitafutie nafasi Michuzi,liwe funzo na kwa watangazaji wengine.WANAPOTOSHA JAMII NAMNA HII,NA WANAJIPUNGUZIA UMAARUFU. AHSANTE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. mmhhh tena huyo Gardner usimzungumzie kabisa IQ yake ni ndogo sana kupita kiasi... ni huo uzaramo wake tu ndio unamsaisia kusema sema humo redioni lakini hajui kitu kabisa kabisa.....Wema sepetu yeye ndio bongolala kabisaaaaaa inatia hata kinyaa. Watu wamelipia tangazo wewe unalijadili tena maana yake nini??? ingekuwa ITV yule mama MD angemtimua huyo

    ReplyDelete
  2. Saida Cessy au Miriam Ikoa

    ReplyDelete
  3. WAANDISHI VIHIYO BOMU KULIKO WAGANGA WA KIENYEJI

    that's no surprise at all.i've been saying time and again, most of these radio stations in dar can't afford to hire professional broadcasters [be they news readers, producers and presenters].

    majority ya hawa wanaojiona "stars" wa broadcasting ni announcers, hawana tofauti na wale wanaotangaza list za wachezaji kwenye viwanja vya mpira - just that.

    inakuwaje mtangazaji akajadili tangazo la biashara? ethically, kama kweli hilo lilitokea, basi ina maana huyo mtongozaji....mtangazaji alikiuka maadili ya utangazaji.hutakiwi kujadili commercial yoyote hewani, labda iwe ni sponsorship na kwa makubaliano kwmaba ijadiliwe.

    tukazanie mafunzo kwa taaluma zote, tatizo ni kwamba taaluma kama waandishi inaonekana kama siyo lazima mtu apitie mafunzo maalum.kisa sababu hakuna hatari kama madaktari na wanasheria - lakini waandishi na watangazaji vihiyo ni hatari kuliko waganga wa kienyeji.

    ReplyDelete
  4. Hili tatizo la watangazaji kuwa VIHIYO ni kubwa sana sana hapo Nchini. Nakumbuka wakati Amina Chifupa alipokuwa akitangaza Radio hiyo hiyo, alikuwa anasema vitu vya jabu sana mpaka kwa hakika nilikuwa naona aibu kabisa! NInasoema vitu bya ajabu ni kwamba inapofika wakati wa kipindi cha kutoa facts, alikuwa anasema uowngo tupu ikimaanisha kuwa hajui chochote. Kuna siku alitumia kipindi kizima kuelezea MIJI mikuu ya kusini mwa Africa. Yote ilikuwa wrong! SIjajua hata humo bungeni kama wanatuwakilisha kweli sisi vijana au ndo basi tena! Sidhani kama anaweza kuchambua issue za miswada na kuiwakilisha itakikanavyo. Lakini ndo tatizo la bongo. Radio imemnyanyua, na wengine wakashinwa kufikiria, wakampa UBUNGE. Haiko hivi DUniani. Tumebakia sisi tu.

    ReplyDelete
  5. Hayo ndio matunda pale zinapokutana divison 0 za point 34. Kwa maana hiyo IQ ilikuwa -68.

    ReplyDelete
  6. michuzi maaharusi wamependeza kupita kiasi HAWAONEKANI!!!

    ReplyDelete
  7. Wema Sepetu...WTF?Gardner Habash..rudi shule kabla hujasema kitu chochote. CBN na CBG have always been there, kwa mtu ambae umeenda shule na unajua nini kinaendelea..you should know, CBN and CBG are part of the science subjects.Inasikitisha Lundenga na kamati yake sat na kumpitisha huyo bongo lala...who as of to date, I havent heard anything positive about her..apart from kuendekeza umalaya.Mwangalie Faraja Kota, better yet Nancy Sumari..they have it all but they are smart enough to know, wat to say and wat not to say wakiwa kwenye sehemu kama hizo.We need watu who are professionally trained for their job..sio vipaji tu vya kuongea...and Gadner Habash..u have very much lowered your dignity. Shame on you all

    ReplyDelete
  8. Michuzi unatuyeyusha, hiyo picha ulisahau kuwasha flash!

    ReplyDelete
  9. michuzi,umeonyesha kiwango chako cha kupiga picha,maana wa nyu,anaonekana kuna mwanga lakini mbele kiza,usisubiri ufe watu tuanze ulizana ulikuwa unafanyaje

    ReplyDelete
  10. Yeah!hii ni kweli kabisa.Nakumbuka na mimi niliwasikia.it's shame kwa kituo cha redio na mtangazaji pia. Clouds FM watch your self,kuna hawa vihiyo watawaharibia sifa ya redio yenu.Ku discuss tangazo lililoletwa na institution nyingine ni vibaya sana,na ni vibaya zaidi kuli discuss vitu ambavyo huvijui na vinavyopotosha!Yaani unawaharibia biashara wanaoleta matangazo kwako??!u should be ashamed of yourself!

    ReplyDelete
  11. michuzi huyo mrembo ni Jenifa aliyeolewa na inno...lete hiyo zawadi sasa

    ReplyDelete
  12. Picha ni nzuri ila Michuzi umemiss kitu kimoja, outline ya bibi harusi, kwa sababu aliangalia mkangafu. Picha ya kiza kuchukuliwa wakati maharusi wameangaliana, ili kupata outline kama ulivyoipata ya bi harusi.

    ReplyDelete
  13. Hiyo harusi ni ya Jenniffa John,anaingia kanisani na mdogo wake ILA flash na mwanga kidogo ulipiga chenga.

    ReplyDelete
  14. Kwa kweli nimekereka sana na hilo Swala la CBG, CBN!!! NI JAMBO LA AIBU NA KAMA HAWAJUI WAFUNGE MIDOMO YAO WASIOONGEE REDIONI MAMBO WASIYOYAJUA MAANA WANAPOTOSHA JAMII. Mimi nimemaliza CBG mwaka 1995 na ninachokifanya sasa ni "medical Geography"-
    (Hybrid research between Geography and medicine) Hii inamuwezesha huyo huyo mtangazaji asiyeijua CBG akiumwa Malaria apewe dawa ambayo itaweza kumponyesha.Kuna uhusiano mkubwa sana wa mazingira(geographical aspects of location) na vijududu vinavyo sababisha magonjwa. Naomba hao waelimike kuwa haya Maosomo wasiyoyajua ni muhimu kuliko hata yale wanayoyajua.
    (Tanzania YWA-Canada)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...