mdau born again pagan ametoa maoni bomba sana kwenye picha yenye kichwa cha habari 'gwaride' hapo chini ambayo nimeyapenda na nadhani ni mojawapo maoni bora toka kwa wadau hadi sasa. na amenihamasisha niwe natoa zawadi mara moja kila mwezi kwa maoni kama yake ili iwe changamoto kwa wadau wote ambao nashukuru kwamba sasa wameanza kuja na maoni yenye ukomavu wa mawazo na hisia.
asante sana born again pagan na hongera kwa kuwa mtu wa kwanza kupokea zawadi kwa maoni bomba. maoni yako ni mfano wa kuigwa na wadau wote. naomba unambie ungependa zawadi ya picha gani nikutumie ama niibandike humu bloguni mwenu...
na hapa nawapa pia taarifa ya habari ya leo tvt kwa hisani ya jambovideo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Michuzi naomba nitofautiane nawe kidogo katika hili. Born again Pagan hajaniridhisha katika maoni yake mpaka kustahuli kupata zawadi, kwa kipi hasa alichokisema hapo!!.

    Ni ukweli usiofichika kwamba blog kama hii inatakiwa itimike ipasavyo kwa watu kutoa maoni yanayojenga na wala si ya kukurupuka tu.

    Ukweli ni kwamba watu wengi wamemchoka Mzee wetu Kingunge. Na kumchoka mtu si kutokumuheshimu. Huyu Mzee amekuwa katika medani ya siasa za nchi yetu kwa muda mrefu sasa, na mimi kwa maoni yangu sijaona kitu ambacho tunaweza kujifunza kama taifa kutoka kwa Kingunge as Kingunge. Kwa kupitia katika serikali zote za awamu tatu zilizopita mpaka awamu nne na wakati mwimgine akiwa kama mshauri wa Rais katika masuala ya kisiasa, pengine nchi yetu ingekuwa mbali sana katika kupambana na maadui watatu ambao toka nimekuwa na akili sawasawa nimekuwa nikisikia nchi yetu inapambana nazo yaani, Ujinga, Maradhi na Umaskini. Kama kweli Kingunge ni bingwa wa ku-blow minds, nadhani mpka leo, nchi yetu watoto wasingekuwa wnakaa chini madarasani,Akina mama wajawazito na watoto wangekuwa hawafai kwa magonjwa yanayotibika na vituo vya afya na madawa yasingekuwa tatizo katika nchi yetu, na wakulima wetu kilimom chao kingekuwa kimebadilika kutoka kutegemea kilimo cha jembe la mkono na njaa kutupiga kila mara tukisingizia hali mbaya ya hewa wakati kuna mito na mabonde yanayotiririsha maji mwaka mzima miaka nenda miaka rudi.

    Kama kweli Mzee huyu ni analyst(mchambuzi) mzuri,nchi yetu isingekuwa tayari kununua rada iliyopitwa na wakati na kununua ndege ya Rais na magari ya kifahari kwa gharama kubwa wakati matatizo ya maradhi, ujinga na umasikini hayajatutoka!!!!!.

    Tumechoka na watu ambao wamekaa madarakani muda mrefu, wakati hatuoni wnachokifanya kufanya maendeleo ya kweli katika Taifa letu. Hakuna cha maana ambacho mimi nakiona ambacho kinastahili sifa kutoka kwa huyo mzee.

    Wazee kama akina Kingunge wameziba nafasi za watu amabao wangeweza kufanya mambo makubwa zaidi katika Taifa letu.

    Na Hiyo zawadi ya Born Again Pagan, mimi sikubaliani nayo hastahili hiyo zawadi.

    Tumechoka na huyo Mzee akapumzike.

    ReplyDelete
  2. Acha ulumbukeni wewe Issa, vigezo gani umetumia kusema maoni bora zaidi? Je ni kwa sababu yanasifia watawala? Hakuna cha ajabu alichosema huyo Born again Pagan zaidi ya Ngonjera za kila siku, ati Ngombale-Mwiru Kichwa, ameifanyia nini Tanzania zaidi ya kushirikiana na mafisadi? Tunaona watu wanajipatia haki miliki kwa kusanya mapato ya parking kwa parking ambazo hawakuzijenga, na wala hawaboreshi parking hizo au kujenga nyingine, halafu tunaambiwa watu waandike thesis kuhusu Kingunge, loooh huku kujipendekeza huku sijui kutaisha lini. Na usitoe maoni yangu haya lakini najua ujumbe utakuwa umekufikia.

    ReplyDelete
  3. CHELSEA CARLING CUP WINNER,NEXT BARCLAYS PREMIER LEAGUE(WITHIN 10 GAMES),FA CUP.
    THIS YEAR UEFA CHAMPIONS LEAGUE TROPHY TO STAMFORD BRIDGE.
    HALLELUJAH...!!!!!OUR CAPTAIN... JOHN TERRY IS OK FOR NEXT MATCH.
    MICHUZI LIVERPOOL YENU WASINDIKIZAJI TUU,KUTUFUNGA SISI NA KUMFUNGA FRANK RIJKARD CHA MTOTO.
    STAY TUNE ..SENTATA CHANNEL.

    ReplyDelete
  4. KUWA MSHABIKI WA CHEALSEA RAHA SANA.....HATA KAMA UNAPRESSURE ...MAMBO RAHA BILA KICHEKO.

    ReplyDelete
  5. Asante sana, Michuzi, sikujua kuwa tundiko langu litasitahili hiyo "onorari rekognisheni"!

    Kunizawadi, umeniomba nichague picha niipendayo. Kwa unyenyekevu, kama kuna picha ambayo ningependa kuiona kwenye blog hii, ni ile ya Jengo la Elimu ya Watu Wazima, Barabara ya Lumumba, Jijini Dar es Salaam.

    Kuna majengo mengi nchini. Mengi tunayachukulia ki-granted. Jengo hilo nililolichagua ni mojawapo ya majengo ya kihistoria katika jiji la Dar es Salaam, hasa, na Tanzania, kwa ujumla. Jengo lenyewe lilijengwa na TANU kuwa Makao Makuu yake.

    TANU, ikiongozwa na Mwalimu Nyerere, ilitilia mkazo umuhimu wa elimu katika kuleta mabadiliko katika nchi yetu changa. Jengo hilo liliteuliwa kuwa Chuo Kikuu cha kwanza nchini, kuanzia na Kitivo cha Sheria, kabla Mlimani kujengwa.

    Wanasheria wanafunzi hao walilala na kusoma hapo jengoni. Walikuwa wakipata mahitaji yao ya mlo hapo Dar es Salaam Technical College.

    Uongozi huo huo ulitambua pia nafasi ya elimu ya watu wazima. Wakati Mlimani inajengwa, TANU iliamua jengo hilo libakie sehemu ya Chuo Kikuu (ingawa Idara ya Elimu ya Siasa ya Chama iliendelea kuwa na ofisi zake hapo jengoni) na kuwa makao ya Idara ya Extra-Mural Studies, na baadaye kubadilika kuwa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ya Chuo Kikuu. Mwaka 1975 ilijitenga kuwa taasisi inayojitegemea.

    Nakumbuka miaka ya kati ya 1970-75, contributions za yale yaliyokuwa yakitendeka katika jengo hilo (pamoja na zile za Wizara ya Elimu (Idara ya Elimu ya Watu Wazima) katika kuinua kisomo cha manufaa (functional literacy), zilikuwa zinailetea Tanzania sifa kubwa duniani kwa kushinda kila mwaka zawadi ya kwanza ya UNESCO ya elimu ya watu wazima duniani.

    Tanzania ilifikia kiwango cha juu cha %-age ya kupambana na umbumbu wa kutojua kusoma, kuandika na kuhesabu kushinda nchi zote za sub-Saharan Africa.

    Kiwango hicho sasa kimeshuka!

    Uongozi huo pia ulitambua nafasi ya elimu kwa njia ya posta katika kuimarisha elimu ya sekondari na ya juu.

    Chuo cha Elimu kwa Njia ya Posta cha Tanzania, chenye makao makuu yake Barabara ya UWT sasa - karibu na Maktaba Kuu ya Taifa - kilizinduliwa katika jengo hilo hilo na kuambatishwa kama sehemu ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.

    Hatuna budi kuwapongeza wafariji wetu, hasa wa Uswedeni (SIDA) na Ujerumani (Frederich Ebert Stiftung) na wengineo, katika mafanikio hayo.

    ReplyDelete
  6. Tunakubaliana sana na maoni mazuri lakini tatizo linakuja kwako michuzi kwani maoni mengi hasa yale ya kuikosoa serikali wewe huwa huziweki ndipo hapo watu wanaanza kukutukana.Swali langu kwa wana maoni ni lini sisi wakazi wa kanda ya ziwa tutaweza kusafiri toka Dar/mwanza,Dar/Bukoba,Dar/musoma bila kupitia nchi jirani ya KENYA.Maoni yenu wananchi na ushauri.

    ReplyDelete
  7. Mdau Born Again Pagan!

    Asante kwa ujumbe na kukubali zawadi. Naandika kukuarifu kwamba kazi ulonituma naifanyia kazi.

    Kwa idhini yako naomba pia kuwashukuru wachangiaji waliopita na wajao kwamba sina nia ingine ila kuanzisha huu mchakato wa kutoa zawadi kwa maoni ambayo MIMI nadhani ni bora. Sisemi kwamba mengine ni pumba, la hasha. Nayaheshimu yote na wadau wote wanaonitembelea nawavulia kofia. Ila kuna sehemu ilibidi nianzia na kwa bahati mbaya ama nzuri ni kwako. Japo ni kweli kuna mawazo tofauti lakini pia si uwongo kwamba angalau umejarfibu kuangalia upande mwingine wa shilingi. Aghalabu maoni mengi yamekuwa ya upande mmoja tu wa hiyo shilingi na wewe umeweza kupuliza pumzi mpya katika hili.

    Hongera kwa mara ingine na wadau mnaotofautiana na Born Again Pagan kwa maoni yake; na mimi kwa kumpa zawadi naomba msijihisi mko ofendedi. Nawaheshimu wote kama ninavyoheshimu mawazo yenu, na tamko hili halimaanishi mwisho wa mjadala. Na uendelee kwa faida yetu na vizazi vijavyo.

    Nawasilisha

    ReplyDelete
  8. Hongera sana Born Again Pagan! Zaidi kwa kuchagua hiyo zawadi ya Jengo La Elimu ya Watu Wazima na kutolea historia yake kwa ufupi. Umenigusa maana hilo ndilo eneo langu pia.

    ReplyDelete
  9. Hongera Born again, hongera Issa pia.

    Born anatoa mawazo yake bila kumkera mtu na isitoshe anaelimisha. Haonyeshi chuki wala kutukana mtu. Kondeni tu Born na Issa keep Up!

    ReplyDelete
  10. Nafikiri jengo aombalo Born Again Pagan si Jengo la Elimu ya Watu Wazima, Barabara ya Lumumba, Jijini Dar es Salaam bali ni jengo la SUKITA (Shirika la Uchumi na Kilimo Tanzania) mali ya CCM. Jengo la Taasisi ya Elimu ya Watu wazima lipo pale Barabara ya Bibi Titi, mkabara na Uhasibu haouse!

    ReplyDelete
  11. Kamanda mirojo unakumbusha sana taarifa za habari....ningependa kuchukua nafasi hii kukuomba rasmi uwe angalau unatupostia hizi taarifa za habari mara kwa mara na kutoka vituo mbalimbali vya habari vya nyumbani maana zinakumbusha mno homu...Ahsante

    ReplyDelete
  12. Michuzi naomba utueleze kipimo cha maoni mazuri ni kipi?
    Kama maoni mazuri ni kujua historia ya mtu basi itabidi watu wengine tuliozaliwa majuzi tukae kusoma tu humu bila kueleza yaliyopo moyoni. Na kama maoni nikusifia kila kiongozi wa nyuma basi tutakua tunatoa maoni kwa unafiki huku tu ili kufurahisha ulimwengu.

    Mimi regadless of your awards...ninachosema wazee wazamaani tutanawapa heshima zao kila siku. Lakini ni vizuri wangeachia hizo nafasi wawape vijana..halafu wao wawe maconsultants tu. Kuna leo na kesho...na maisha sio kuwa tutaishi duniani siku zote. Sasa mpaka mtu Mungu amuite mtu mbinguni ndio aachie uongozi na wapi tutajifunza na wapi watapata muda wa kutukosoa?
    Ndio maana kuna pension funds, HMO, 401K na mengineyo na ndio maana kuna umri wa kuretire kila mahali duniani hii. Watu wanatakiwa kupumzika na kufurahia matunda waliyoyatengeneza na kuangalia watoto waliowakuza na kuwafundisha wakifanya kazi.....

    ReplyDelete
  13. Michuzi kweli wewe kada wa CCM, yaani maoni yote yanayofagilia CCM na uongozi wake wewe ndo mazuri saana kwako yanayostahili zawadi.

    Zaidi zaidi alichofanya born again pagan ni kutupa historia tu (ambayo mtu yeyote anaweza kutupa kama alikuwepo enzi hizo) hakuna critical thinking wala analysis katika cooment yake, mbona kuna analytical thinkers wengi wanatuma comments hapa lakini hawapewi recognition? au sababu wao wana criticize government na CCM.

    Michuzi jitahidi kutokuwa biased katika hii blog yako, ndiyo ni yako wewe mwenyewe lakini na sisi kwa ku visit hii blog yako kila siku ni wadau muhimu.

    Usitoa hii comment basi nitaprove kwamba blog yako imenunuliwa na CCM kama walivyolinunua gazeti la rai, na NITAHAMA! freedom of speech Ustaadh

    ReplyDelete
  14. Michuzi mbona hujapost comment yangu? Au sababu nimekuita kada wa chama cha mapinduzi? Najua hautaposti na hii lakini point taken!

    ReplyDelete
  15. Born Again Pagan,naomba nikuite chemba kwa majadiliano juu ya Kingunge.tafadhali niandikie kwa email: zemarcopolo@yahoo.co.uk

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...