
wadau, mna habari kwamba mzee justin dotto mayagilo, yule kiongozi wa brasi bendi ya polisi mwenye mbwembwe nyingi enzi hizo kalazwa muhimbili? basi ndo hivyo tena. babu wa watu yuko wodi 10 mwaisela anasota kwa maumivu ya mguu, na ukiacha familia yake ni watu wachache wanamtembelea mzee wetu huyu ambaye sifa za kazi yake haina mfano na anafananishwa na mashujaa wengine kama kina mzee makongoro, morris nyunyusa na wengineo wa aina hiyo. chozi lilinitoka nilipomtembelea na kumkuta mkiwa pale kitandani, na ukizingatia haoni sawasawa ndio basi tena. alizaliwa mwaka 1922 na kujiunga na polisi mara tu baada ya vita kuu ya pili ya dunia. alistaafu mwanzoni mwa miaka ya 80 na kwenda kula penshini yake kijijini kwake tinde mkoani shinyanga. ana siku kadhaa hapo muhimbili sasa...
Mungu ampe nguvu apone haraka.
ReplyDeleteahsante kwa kutuwekea picha hii mheshimiwa Michuzi.Nimefurahi mno.Ni miaka mingi nilikuwa tu nasikia habari zake toka kwa baba yangu ila leo naiona sura yake.Mwenyezi Mungu amjaalie kheri mzee wa watu kwani ameitumika nchi yetu muda mrefu na kwa uhodari na uadilifu mkubwa.Nadhani anastahili matuzo na kuthaminiwa sana na serikali yetu na watu wake.Sikuwepo miaka hiyo ila nilisimuliwa alivyoing'arisha nchi ktk maonesho ya biashara ya Expo '70 Japan na hata ktk wimbo wa hayati Mbaraka Mwinshehe Mwaruka(Soloist Internacionale) uitwao Epo 70 alilisema hili: "...Maenyesho Japan yalifana sana,banda la Tanzania limetia fora,mzee Morris na ngoma zake kumi,mzee Mayagilo na bendi ya polisi...eeeh.." Michudhi tafadhali endelea kufuatilia afya yake huyu mzee wetu na pia ukipata wasaa utuwekee picha zake na wasifu wake,na wa wa hayati mzee Morris pia na wakongwe wengine kama Mbaraka,Salum Abdallah Yazide,Ahmed Kipande,King Michael Enock na wengineo.Mwenyezi Mungu amjaalie afya nzuri ili mzee Mayagilo arudi nyumbani ili tunaompenda tusihuzunike zaidi..Ameen! JJ.
ReplyDeleteMICHUZI WEKA PICHA HII NA HABARI KWENYE GAZETI WATANZANIA WAFAHAMU KUHUSU MZEE MAYAGILO.MTU KAMA HUYU NI MIONGONI MWA "GREAT TANZANIANS" LAKINI WATANZANIA HATA HATUNA MAZOEA YA KUENZI WATU WENYE ACHIEVEMENTS KUBWA ZA KIHISTORIA NCHINI KWETU.WENGI WANAJUA NYERERE TU NDIYE MTU WA MAANA WAKATI KUNA MZEE KAMA HUYU NA WENGINE WENGI TU WALIOSAHAULIKA NA PENGINE HATA HAWAJULIKANI,HEBU WAPASHE WANANCHI HABARI HII.
ReplyDeleteGet Well Soon.
ReplyDeleteWananchi ni wakarimu sana wa Tanzania but it is a shame the way our country/Govt don't know how to honor people who have bring so much to the country or the Name TANZANIA.
Inamaana hata wewe Michuzi kuna wakati ukifika jamii pia itakusahau? inabidi tubadilike sana na kuanza kuwaenzi watu kama hawa, mwenyezi mungu amjaalie apatekupona haraka AMEN.
ReplyDelete"Ask not what your country can do for you - ask what you can do for your country." John Kennedy
ReplyDeleteGet well soon, your legacy shall always be remembered by the people of Tanzania who make up Tanzania
Apewe pole nyingi. Ndivyo tulivyo binadamu. Kisichokuwapo machoni hata moyoni hakipo. binafsi sikuwahi kumfahamu si unajua tema wengine tumekulia huuuko halafu wakati huo huyu ndugu akikamua vilivyo pengine hata ka-umri wengine kalitukaba.
ReplyDeleteBaada ya kusema hayo, umenikumbusha huyu jamaa Morris Nyunyusa. Nae kama huyo bwana enzi zao za makamuzi, lakini Morris Nyunyusa ananyunyiza kila leo pale RTD, mara saba kwa siku! Hivi kapicha kake (Morris) kanaweza kupatikana hivi?
Wengi wa watoa maoni wameilaumu serikali kwa kutokumuenzi vyema Mzee Mayagilo lakini sijaona hata mmoja aliyeomba apewe Acc No. ili amtumie pesa za kumsaidia. Kabla ya kusonta kidole kwa yeyote ni bora nasi tuonyeshe tuliyo/tunayo/tutakayofanya kwa mzee huyu. "Kwa Muungwana ni kitendo...." Tafadhalini nisaidieni kumalizia hiyo methali.
ReplyDeleteAnony wa juu ya rhxoqsa, mbwembwe nyingi kuandika ung'eng'e wakati ni mashuzi tu, kwa nini usitumie kiswahili? "who have bring" ndio Kiingereza gani hicho?
ReplyDeleteWanablogu wenzangu,
ReplyDeleteNinakubaliana kabisa na huyo anon wa Saturday, February 03, 2007 5:57:00 PM. Sisi kama watanzania na wanablogu tusisahau utamaduni wetu, ni vizuri tukasaidia kwa hali na mali ingawa kwa kidogo tulichonacho kwa watu ambao michuzi ataona/atachagua kuwaleta katika blogu hii ambao wanahitaji msaada kwa mambo kama matibabu.
Mimi kama mwanablogu najitolea kumchangia kiasi kidogo cha kumsaidia mzee Mayagilo wakati akiwa hospitali. Michuzi nimekutumia email kuhusu mchango wangu. Nafikiri hii itasadia kama shukurani zetu kwa michuzi ambaye anatuletea burudani na habari za nyumbani bure.
Mzee Michuzi,wewe ni mtu mzuri sana kwani katika hii Blogu yako unaonyesha mambo mengi ambayo yanamkumbusha Mtanzania yeyote duniani tulikotokea.Hata mimi nimetoa machozi kuona picha ya Mzee Mayagilo akiwa katika hali hiyo.Watanzania tumechenji lakini wengine wamebaki nyuma na roho mbaya ya kutafuta makosa kama huyu Anonym ambaye anamkosoa mwingine eti kwa kuandika umombo mbaya "who have bring".I think he missed the point.pointi ni Mzee Mayagilo sio nani anaandika vizuri.Anyway,namuombea mzee Mayagilo nguvu na afya,apone na kuinjoi maisha yake yaliobaki.Pia nataka kuunga mkono kwamba Mzee Nyerere si pekee ambae anapashwa kukumbukwa,wako wengi.
ReplyDeletewewe anony wa saa 10:20 acha ujinga kukosoa kitu kilichowazi tangu lini ikawa roho mbaya? Mbona imekusaidia kuandika kwa Kiswahili? Acha uongo wako ati machozi yamekutoka wapi? Hiyo picha unataka kutuambia inaonyesha hali mbaya kweli kulinganisha na wagonjwa wengi kwenye hospitali zetu. Unafiki mtupu
ReplyDelete