WADAU. HII IMEINGIA SASA HIVI. POLENI WAFIWA NA MOLA AKILAZE KICHANGA CHETU MAHALA PEMA PEPONI - AMIN.
Ndugu zangu wapenzi:
Tunasikitika kuwatangazia kifo cha mtoto mchanga Tatum Rehema Hiza aliezaliwa Jumapili Februari 4, 2007 na kufariki jana Jumamosi tarehe 10 Februari 2007 kwa matatizo ya mapafu.
Tatum ni mtoto wa Aisha Mboza Hiza ambae ni mtoto wa marehemu Bwana Norman Mhilu Hiza na bibi Rehema M.K. Hiza wa Amherst, Massachusetts.
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa Bibi Rehema Hiza Amherst, Massachusetts.
48 Harkness Road, Pelham, Mass 01002

Tafadhali wasiliana na wafiwa kuwafariji katika kipindi hichi kigumu.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Bwana Stephen Tomi
(413) 658-5253 cell
(413) 772-6838 nyumbani
Aunt Diana T. Kibodya
(413) 210-3372 cell
(413)782-6310 nyumbani
Bwana Kawala Mgawe
(413) 330-1609 cell
(413) 783-6156 nyumbani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Michuzi asante sana kwa hili. Blog yako itanifanya niingie kila siku. Nipo NY City na habari hizi wala nisingezipata mpaka labda miezi ipite vile si unajua maisha yetu ya huku. Huyu aunt Rehema namwonaga tu ni mdada mmoja poa sana tu lakini sikujua kuwa anaweza kuwa na mjukuu. It is a shock to me.

    Aunt Rehema "While your are mourning the loss of your grand daughter other are rejoicing to meet her in heaven. May you find the courage to face tomorrow in the love that sorounds you today. May God rest her soul in peace. My sincere condolences on your bereavement.

    ReplyDelete
  2. Nawapa pole sana wafiwa, katika huu wakati mgumu.Lakini bwana Michuzi je hii Blog ni ya kutangaza Matangazo yote ya vifo vinavyotokea UGHAIBUNI au ni aje?Au hata misiba ya Nyumbani tukuleletee?Au ni kwa unaowafahamu tu?Tafadhali tufahamishe.

    ReplyDelete
  3. Poleni sana wafiwa, Mungu awape nguvu na mshikamano katika kipindi hiki kigumu na wakati wote. Mungu amlaze Little Angel mahali pema peponi.

    ReplyDelete
  4. Nawapa pole zaidi wazazi wa huyu mtoto, mungu alimpenda zaidi huyu malaika wake na akamtwaa, nina imani atawabariki na kuwajaalia watoto wengine maishani POLENI SANA WAFIWA WOTE

    ReplyDelete
  5. Poleni wafiwa. Mungu amlaze pema baby.

    swala la kipi kitangazwe na kipi kisitangazwe, maoni yangu ni ujumbe wowote ambao unatakiwa uwafikie watu haraka, maana watu wengi wansoma "michuzi" hata kumtafuta ndugu/rafiki aliyepotea zamani ukitangaza hapa labda kuna mtu atakusaidia. Sijui lkn hayo ni mawazo yangu tu Issa unasemaje?!
    Aurely

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...