
niko na wakongwe wa muziki bongo. toka shoto ni kikumbi mwanza mpango a.k.a king kikii, shem ibrahim karenga wa tabora jazz na dk remmy ongala. wakongwe hawa ni kati ya wasanii 711 ambao leo chama cha haki miliki bongo (cosota) kimewapa mgao wao wa mirahaba (royalties) kutokana na kazi zao kutumiwa. kikii kaondoka na laki nne na ushee, shem karenga kalamba milioni na dk remmy kabeba laki tisa na ushee hivi...hii ni mgao wa awamu ya pili ambapo kila baada ya miezi zita cosota hugawa mirahaba kila baada ya miezi sita. safari hii ilikusanya kama milioni 75, na baada ya kukata ganji lake na la mawakala wakusanyaji ikagawa milioni 46 zilosalia.
athante kaka michudhi kwa picha ya wazee wetu ambao nyimbo zao haziwezi kumchosha mtu kamwe.nawapongeza pia COSOTA kwa kukpigania haki za wanamuziki wetu kwani wananyonywa sana na watu wanaotumia kazi zao za sanaa,kama tu vile wanavyopunjwa wachezaji mpira,hasa wa miguu ambao wanaweza kuingiza milioni 70 uwanjani ila timu mbili zikaambulia milioni 30 tu.nawashauri COSOTA na wadau wengine wenye uchungu na unyonyaji wa kazi za wanamuziki wakaze uzi sana hadi haki ipatikane.kuna watu wasio na huruma wanadurufu kazi za wasanii bila idhini zao na kuziuza.mikoani hali ni mbaya kutokana na kutokuwa na ufuatiliaji wa kutosha hivyo kwenye kumbi za disko,mashindano mbalimbali ya muzikina urembo na hata ktk vituo vya redio(hasa za masafa ya FM) kuna wizi mkubwa unafanywa wa kazi za wasanii.kuna watu wako huku Ulaya wanauza albums za wasanii wetu nadhani hawana ridhaa wala idhini za wenye hati miliki hizo.tuendeleze utamaduni wa kuwasaidia wanaonyanyaswa,hasa watu kama hawa wanamuziki mabao hawana hata sh el 30 kwa mwezi za pensheni pale nguvu zinapowaishia au umri kuwatupa mkono na kushindwa kuendelea na kazi zao.tununue kazi halali na halisi za sanaa.JJ.
ReplyDeleteHatutarajii 'teni pasenti' ya mirabaha COSOTA
ReplyDeletemaoni,Mwananchi 02/02/2007
JANA kulikuwa na zoezi la Chama cha Haki Miliki Tanzania, COSOTA kutoa fedha za makusanyo, mirabaha ya kutumika kwa kazi za wasanii katika maeneo mbalimbali nchini.
Shughuli ya kukabidhi fedha hizo, ilifanyika kwenye Ofisi za Baraza la sanaa la Taifa, BASATA.
Awali COSOTA ilitangaza kupatikana kwa sh80mil. zilizokusanywa kutoka kwa wahusika wa utumiaji wa kazi za wasanii ambazo tayari zimeshawekewa utaratibu na wasanii kufaidika nazo.
Fedha hizo ambazo tayari zimeshakatwa asilimia tano kwa ajili ya shughuli za COSOTA licha ya katiba kutaka zikatwe asilimia 30, wahusika watalipwa mirabaha ya sh75m.
Ilielezwa kwamba, vikundi vya kiinjilisti vya Angaza (SDA), Muungano Christian vya jijini Dar es Salaam na Kwaya ya Kiinjili ya Habari njema ya jijini Arusha vilitajwa kuwa miongoni mwa vikundi vitakavyopata mgawo huo.
Mbali na vikundi hivyo, ilielezwa pia kuwa vikundi vya muziki wa dansi na wasanii mbalimbali pia walikuwa katika fungu la kupata fedha hizo ambazo zimekusanywa kutoka sehemu mbalimbali za starehe zilizotumia kazi ya sanaa.
Katika mpango mzima, kati ya fedha hizo, sh72m ziligawiwa kwa wasanii wa muziki na sh3m zilienda kwa wasanii wa michezo ya kuigiza, Angaza SDA ya Manzese, Dar es Salaam ilipata sh2.6m, kwaya ya Muungano sh2m na kwaya ya Habari Njema ya Arusha sh1.4m.
Tunawapongeza COSOTA kwa kazi ya kukusanya mirabaha kwani ni kazi nzito ambayo inahitaji somo na kuwapata waelewa kiasi cha kupatikana kwa fedha hizo ambazo ni neema kwa wasanii japo ni kidogo.
Ni imani yetu kwamba, bado kuna fedha nyingi zinzoweza kukusanywa tanzania nzima kutokana na kutumika kwa kazi za wasanii.
Kwa upande mwingine, hatudhani wala hatutarajii, lakini hadhari yetu ni kwa wahusika kuwa isije kuwa 'dili' ya 10 pasenti na baadaye kuondoa wazo zuri ambalo hata wasanii watakuwa wakifarijika na kuona faida ya kazi zao.
Hakika ikiingizwa 'teni pasenti' katika hili, ni dhahiri itavuruga utaratibu mzima, itatoa maswali mengi ikiwa wasanii ambao pengine hata kusikika hawasikiki ama vikundi havipo badala yake utasikia wamepata mrabaha.
Uaminifu wa COSOTA utafanya wahusika wa wasanii kuwa na imani na chama chao na kuwavuta zaidi na kujiandikisha kwa ajili ya kusimamiwa kazi zao za sanaa endapo majangili wa kazi za wasanii watachukua nafasi.
Watendaji wa COSOTA na mawakala wao, bado wana jukumu la kuhakikisha upatikanaji wa fedha zaidi za wasanii kupitia mirabaha hiyo.
Ikiwa mambo yatafanyika kwa uwazi, mfumo mzima utasaidia sana wasanii kwani inawezekana kazi zao zikaibwa, lakini bado wakaoinyesha nafasi katika kukusanya fedha za mirabaha.
Inafahamika kuwa ni kazi nzito kupitia kila mahali na kukusanya mirabaha, mfano kuanzia Mikindani Mtwara hadi Kanyigo mkoani Kagera na kuanzia Moshi, Kilimanjaro hadi Namtumbo, Songea, lakini kubwa ni uaminifu wa watendaji wa COSOTA na mawakala wao katika kuwafikishia wahusika malipo yao bila kuwa na 'teni pasenti'.
This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteDu Remmy kawa kingasti!!!kweli kumrudia yesu kuna faida kwake sio kama alivyokuwa kwa shetani bado kidogo awe mr ubaya nakumbuka alikuwa mshindi wa pili
ReplyDeleteGym na mahala pako pa kwenda hivi sasa kaka Michu, naoan katumbo kidogo kanakwenda sambamba na mkulu Ongara!!! AKd
ReplyDeleteHongera COSOTA kwa kuwakatia haki ya wasanii. Nawaomba wasanii wakongwe Shem Karenga, Kikii, Remy Ongala na wengine wengi mbuni mbinu zingine zaidi za kuongeza mapato, mfano mkongwe Tabu Ley Rechereau ametoa DVD zenye nyimbo nyingi za miaka ya 1960-1990. Hakika watu wengi wamependa huu ubunifu wakongwe kama Rechereau kutoa DVD za nyimbo za zamani katika mazingira ya kileo, hivyo wazee wangu wasanii wa Tanzania lifanyieni kazi hili suala muongeze kipato kwa DVD na Video.
ReplyDeleteMilioni 45 kwa watu 711 kila mtu wastani elfu 60, du kweli noma imekuwa noma!
ReplyDelete