aboubakar liongo akibarizi na charles Mwabeya, mtangazaji marufu wa radio kwizera ya kule ngara ambaye kwa sasa yuko redio dw huko ujeremani kwa mafunzo ya miezi sita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Ngara ndio wapi?

    ReplyDelete
  2. hicho ni kifaa bwana kikikamata kipaaza sauti ebwana tunakumiss sana mdau liongo hata hivyo big up ,pull up your socks

    ReplyDelete
  3. Hapo ni Dom Cathedral, Köln, karibu na Hauptbanhoff (relwe stesheni)

    ReplyDelete
  4. mhh mhhh mhhh Cute TZ guys!!!!! I hope mlivyowazuri hamna kiswahili kirefu though.....

    You guys look so good for really.....Call me....

    ReplyDelete
  5. watu wengine bwana!, ngara ni WILAYA ilioko mkoa wa KAGERA, si u search hata kwenye google, watu hamkui ee, ndo unajiita mtanzania, 'eti ngara ni wapi?', ntakusamehe kama wewe sio mtanzania au wewe kama ni mtoto kuanzia darasa la 3 kuchuka chini,

    aboubakar liongo, mtangazaji wa siku nyingiii, ana sauti nzuri sana

    ReplyDelete
  6. Duh! anon wa kwanza,Ngara ni moja kati ya wilaya iliyoko mkoa wa Kagera ulioko Kaskazini magharibi mwa Tanzania na iko mpakani na Rwanda na Burundi ndio sehemu iliyopokea wakimbizi kutoka Rwanda mwaka 1994 kipindi cha Genocide.Na wakazi wake ni kabila la Waangaza ambao lugha yao ni sawa kabisa na Kinyarwanda na Kirundi.

    ReplyDelete
  7. Abou! Jamaa hana makuu, hana kinyongo. Nakumbuka jumamosi moja mwishoni mwa miaka ya 90 aliwahi kuniita studioni pale Radio One na kufanya mahojiano nami kupitia kipindi chake cha African Panorama. Hiyo ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuzungumza redioni. Kwa approach yake niliweza kufikiri kuwa angefika mbali sana katika taaluma yake.Najivunia mafanikio ya kijana mwenzetu huyu.

    ReplyDelete
  8. Abuu ni mmoja ya watangazaji wazuri tulionao asiye na mtu ,huyu bwana ndiyo aliyemfundisha kazi yule kijana aliyeoa wake wawili wa pale redio one kwani jamaa aliiga hadi sauti safi saaaana ABUUU

    ReplyDelete
  9. Naomba ku-intervene, huyo mdau aliyeuliza ngara iko au ni wapi hakumaanisha eti Ngara ya Bongo haijui; bali alifikiri Ni mfano wa majina aliyovumbua na kutumia ndg michuzi, mathalani, ukerewe (UK), newala (NY) n.k. kwahiyo mdau alidhania ngara labda ni mahali kwingine ulaya au amerika. Kwa hiyo tusimshambulie bila sababu ya msingi!

    ReplyDelete
  10. Anony. wa kwanza yuko sahihi kuuliza. Si kwamba hapajui Ngara ila ni KUTOKANA NA LUGHA YA KIMICHUZI.

    Naona mmemtolea macho ili-hali angeuliza Ukerewe ni wapi basi wote mngesema ni UK.

    Zika likwelikwe.

    ReplyDelete
  11. Kama sikosei walikuwa Chuoni TSJ na kina Susan Mungi na pascal Mayala au walifuatana miaka

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...