mojawapo ya somo nililopata hapa dumila ni kwamba kuna haja jamaa wa bandari na watunza fukwe wa dar, mwanza, kigoma, kagera na itungi watembelee wenzao wa hapa wanafanya nini na sehemu hizo. sio kukalia kuzipiga senyenge kwa kisingizio eti wabongo waharibifu...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Na wewe nkumbe mkabila kama tulikuwa tunazungumzia kule JAMBOFORUMS.COM

    yaani katika bandari zote mbona TANGA HUJAITAJA? uNGUJA JE? PEMBA JE AU WAO HAWASTAHILI KUTENGENEZEWA?


    acha hizo

    ReplyDelete
  2. Duh! garden bomba sana, huko dumila kumbe kuzuri namna hii? itabidi nijikusanye holiday moja niende, Michuzi aminia mazee hatukuwezi.

    ReplyDelete
  3. Broo Michuzi, kama bado uko Dubai pita kule barabara inapopita chini ya maji halafu unatokea kwenye daraja linalo funguka utueleze kuna mdau mmoja anabisha

    ReplyDelete
  4. Mwanangu Michu, hapo umecheza kama Edson Arantes Des Nascimento au kwa kifupi~Pele. Ni ukweli ulio wazi kwamba tatizo letu kubwa katika matatizo mbali mbali ni kutotaka kujifunza toka kwa wenzetu.

    Hapo kuna kazi kibao zimeshakuwa created na wananchi wanapata sehemu mwanana ya kutulia, kupumzika au kuvuta pumzi bila ya bughudha yoyote.

    Lakini bongo yetu wanafunga kila sehemu nzuri, pale mnazi mmoja pamefungwa na beach nyingine nzuri tu pembeni ya Indian ocean wabongo haturuhusiwi kutia mguu.

    Unajua wewe unabonga na wanene, hebu mwambie Kandoro aende dumilla aone wenzetu wanavyopendezesha miji yao na kuwaachia wananchi wafurahie usafi wa miji hiyo. Hata Mnene kuliko wote wabongo pia unaweza kumuonyesha picha kama hizi na kumnong'oneza jinsi wenzetu wanavyofanya.

    Ahsante sana Michuzi.

    ReplyDelete
  5. Issa, sio kisingizio, bali ukweli ni kwamba Wabongo ni waharibifu!. Wewe fikiria kabla ya pale ufukwe wa bahari posta ya zamani kupigwa seng'enge palivyokuwa pananuka kwa sababu watu wanajisaidia ovyo( ingawa pia site yetu haikuwa na mipangi mizuri ya kuweka vyoo sehemu muhimu). Pia watu wana tabia ya kutupa takataka ovyo hata pale unapokuta wamewekewa vyombo vya kutupia takataka mitaani, lakini cha ajabu utakuta mtu ana kunywa maji halafu ile chupa badala ya kuibeba akatafuta mahali pa kutupia takataka anatupa tu ovyo.
    Sasa kwa kuwa tumekuwa na dhamira hasi ambayo kwa bahati mbaya imewakumba hata watendaji wetu serekalini tumeshindwa kupata ufumbuzi wa matatizo ambayo yangeweza kutatuliwa kwa kuwaelimisha tu wananchi wakaelewa.

    Mimi kuna wakati nashangaa hasa nyie akina Issa ambao mmekuwa kwenye misafara ya viongozi wetu wanapotembelea nje, hivi hawa viongozi wanapotembelea huko nje nao wanabaki tu kushangaa tu na kurudi wakisifia jinsi wenzetu walivyoendelea tu, hivi hakuna wanachojifunza huko wakarudi hapa wakajaribu waone matokeo yake.

    Angalau hata marehemu Baba wa Taifa alipoenda China mwaka 1968 alirudi na vijiji vya ujamaa akajaribu, ingawa alitumia ubabe bila ya kujaribu kwanza na matokeo yake walio wengi wanayajua.

    Serekali yetu kwa kushindwa kutafuta ufumbuzi wa matatizo, kwa mfano imepiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki!!. Hii ni ajabu!. Wewe Michuzi naamini umetembelea huku Marekani na pia umeingia katika maduka makubwa hapa. Bila shaka uliona wanatumia mifuko ya aina gani kubebea bidhaa. Tena ukinunua vitu watakupakilia mifuko kibao tena ya plastiki. Juzi nimepigwa na butwaa waziri katika serikali eti anashangaa maduka makubwa Tanzania bado wanatumia mifuko ya plastiki!!!!.

    Hivi ni kweli kwamba viongozi wetu hawajui kwamba mifuko hiyo inaweza kuwa recycled?, wameshindwa kweli kuhamasisha viwanda na wawekezaji kuwekeza katika kurecycle hiyo mifuko. Wameshindwa kweli kuhamasisha wananchi katika kuhakikisha kuwa hiyo mifuko haitupwi ovyo na badala yake iwe ni chanzo cha ajira?!!!.

    Wakati mwingine mtu unashikwa na hasira mpaka basi tu. Yaani tumekuwa wavivu wa kufikiri mpaka inatia aibu. Jamaa kila siku mko majuu tu lakini mnachorudi nacho kutoka huko hakijulikani.

    Kuna jamaa mmoja alitoa hoja juu ya barabara ya kuelekea kwetu Mbagala inayojengwa sasa hivi( Kilwa Road).Leo mwaka 2007 bado tuna mipango ya mwaka 1980!!. Yaani hatuangalii mbele. Baada ya miaka michache ijayo tutaambiwa msongamano wa magari katika barabara hiyo ni tatizo.

    Wakati Morogoro Road inajengwa tuliambiwa itapunguza msongamano lakini leo angalia hiyo barabara inavyokuwa kero wakati wa asubuhi na jioni!. Badala ya sasa kufikiria zaidi ya hapo kwa kujenga flyovers na kupanua barabara ziwe njia mpaka nne kwa upande moja, bado tumeng'ang'ania njia mbili!. Aliyesema kuwa watanzania wanaohitaji magari yao binafsi wanapungua badala ya kuongezeka ni nani. Dar es salaam Business District tunayo moja tu. Kwa hiyo watu wote wanaelekea sehemu moja asubuhi na kutoka sehemu hiyo jioni.

    Tunahitaji, kuona hiyo kasi mpya, nguvu mpya na hari mpya kweli, siyo maneno ya kupatia kura halafu tunasubiri kutafuta maneno ya kutafutia kura uchaguzi unaofuata.

    Issa nimesema sana lakini ukweli ni kwamba tumekuwa wavivu wa kufikiri. Acha tu wapige seng'enge labda itasaidia hata kuifadhi hicho kidogo kinachoonekana kabla hakijapotea kabisa.

    ReplyDelete
  6. du kwa misela ya bongo hiko ni choo kimoja safi sana,mpaka mauwa yataungua hayo.

    ReplyDelete
  7. Wewe Amoko nyie ndio watu msiopenda maendeleo siku zote mnaangalia mambo on negative side instead of a positive side. Ulifanya lini hiyo study ambayo ilikufikisha kwenye conclusion yako kwamba wabongo ni waharibifu.

    Nakumbuka wakati Mrema alipokuwa Waziri wa mambo ya ndani alifanya kampeni ya kuliweka jiji la Dar katika hali ya usafi. Wenye maduka walitakiwa kupaka maduka yao rangi na kuweka mapipa ya uchafu ili watu waweze kutupa uchafu kama maganda ya ndizi, karatasi za kufungia karanga n.k.

    Na kampeni ilifanikiwa sana na hata soko la kariakoo likawa safi. Mimi naamini kabisa wabingo wanapenda mazingira mazuri na yanayopendeza. Ikiwekwa kampeni kali ya kulipendezesha jiji la Dar na majiji yetu mengine na kuyaweka katika hali ya usafi kama majiji ya wenzetu hili litawezekana bila tatizo lolote. Kumbuka Mrema 1991/92 alifanikiwa sana. Sioni kwa nini tusifanikiwe tena.

    Acha hizo za kuangalia mambo kwa kukata tamaa

    ReplyDelete
  8. Msongamano wamliza Lowassa Dar
    na Mwandishi Wetu

    WAZIRI Mkuu, Edward Lowassa, ameuagiza uongozi wa Jiji la Dar es Salaam kuchukua hatua kadhaa za haraka, kuboresha mazingira ya jiji, ikiwa ni pamoja na kupunguza msongamano wa magari jijini na kuimarisha usafiri wa abiria.

    Katika barua aliyowaandikia Meya wa Jiji na wa manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke, Lowassa ametaka apate taarifa ya utekelezaji wa maagizo hayo ifikapo Mei 15, mwaka huu.

    Pamoja na kupunguza msongamano wa magari barabarani na kuimarisha usafiri wa abiria, Waziri Mkuu ameagiza kusimamiwa kikamilifu sheria na taratibu za barabarani na kuweka taa sehemu mbalimbali, na hasa barabarani.

    Maagizo mengine ni kuanzisha usafiri wa “tram” (mabasi kama treni yanayokwenda kwa umeme jijini), kusafisha jiji, kupanda miti na maua, kupaka majengo rangi na kuweka utaratibu wa kuwaonyesha watalii maeneo ya jiji.

    Alisema kuwa maagizo yote hayo yatekelezwe mara moja bila ya kusubiri, na kwa yale mengine ambayo yanahitaji muda zaidi kama vile kuwatembeza watalii na usafiri wa “tram”, mikakati ya utekelezaji ianze.

    Waziri Mkuu alitaja agizo jingine ni kuwaondoa mara moja wafanyabiashara ndogo ndogo “machinga” waliorejea katika maeneo ambayo wamefukuzwa, kama vile kwenye kituo cha mabasi cha Mwenge.

    Katika barua hiyo ya Machi 9, 2007, aliyoinakilisha pia kwa rais, Waziri Mkuu aliwataka viongozi hao wa Jiji la Dar es Salaam washirikiane na taasisi zake, sekta binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kuandaa na kutekeleza maagizo hayo.

    Barua hiyo pia imenakilishwa kwa Makamu wa Rais, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Uratibu), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, wakuu wa wilaya na halmashauri za manispaa. Alitaka barua hiyo isomwe kwenye vikao vya Baraza la Madiwani.

    Waziri Mkuu alisema kuwa, kero nyingi katika Jiji la Dar es Salaam, kama vile utupaji ovyo taka, zinaweza kupatiwa ufumbuzi kwa kutumia sheria ndogo zitakazowabana wauzaji na watumiaji wa vitu vinavyochafua mazingira.

    Hata hivyo, aliupongeza uongozi wa Jiji la Dar es Salaam kwa kufanikiwa kuwaondoa wafanyabiashara ndogo ndogo katika maeneo ambayo hayakuruhusiwa kufanya biashara hizo na kuwapeleka kunakohusika.

    Lakini alisema wale wanaorudi kwenye maeneo walikoondolewa, kama vile kituo cha mabasi cha Mwenge wakati wa usiku na kusababisha msongamano wa magari na vitendo vya wizi wa mifukoni, waondolewe mara moja.

    Alisema taa za barabarani hazipo, majengo hayapakwi rangi, sehemu nyingi hazikupandwa miti wala maua, taka zinatupwa ovyo, hakuna utaratibu wa kuwatembeza watalii na tatizo kubwa la usafiri wa umma katika jiji.

    Waziri Mkuu alisema anaelewa kuwa kuna mipango ya muda mrefu ya kuanzisha usafiri unaoeleweka na kuondoa mabasi madogo, lakini haiwezekani kukaa kimya na kuwatazama wananchi wakipata shida.

    “Yapo malalamiko mengi ya magari ya abiria kukatisha njia na madereva na makondakta kuwa jeuri kwa abiria. Ni wajibu wa mamlaka zinazohusika kuhakikisha kuwa sheria zote zinazohusu usalama barabarani na hasa zinazohusu magari ya abiria, zinasimamiwa vizuri,” alisema Waziri Mkuu kwenye barua yake hiyo.

    ReplyDelete
  9. watu awajastaraabika,wache serikali iweke uzio,binadamu anataka aendeshwe kama punda!kila kitu mpaka uambiwe,sisi watu weusi popote duniani tuna matatizo sana na dawa ya mtu mweusi ni kumpeleka kibabe kama anavyofanya PM lowasa,sababu tuna desturi ya kuto starabika,wazungu walituachia nchi safi lakini ona sasa,kama unabisha nenda harare utajua nasema nini, ni tofauti kabisa na ile aliocha mwingereza 84.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...