wadau kunradhi. shirika letu la posta limetutumia majibu kufuatia waraka wa malalamiko uliobandikwa kwenye hii blogu yetu hivi karibuni. naomba tuusome kwa makini na kueelewa kama tulivyofanya kwenye ule waraka wa malalamiko
Habari ya kazi Bw. Michuzi,
Tumepokea malalamiko ya mteja wa Posta kutoka US kupitia blogspotyako.Tunakupongeza kwa kuanzisha mtandao kama huu ambao mbali nakuwafahamisha watanzania popote walipo kuhusu masuala mbalimbaliyanayohusu nchi yetu, mtandao huu pia unawawezesha watanzania hao kutoamaoni na kero mbalimbali wanazokutana nazo katika maisha yao ya kila siku.Tumejibu malalamiko hayo na tunakutumia ili yamfikie mteja huyo nawatanzania wengine wenye matatizo kama hayo.Aidha tunakaribishamalalamiko, maoni na mapendekezo mengine ili tuweze kujua hatua zakuchukua ili kuweza kukidhi matakwa ya wateja wetu.Namba zetu za simu ni +255 22 2118280 Ext: 336, 637 na 642 au 2121591
Fax: +255 22 2113081J. Bujiku
customer.care@posta.co.tz
YAH: MAJIBU YA ‘WARAKA KWA WAFANYAKAZI WA POSTA’
Tumepokea ‘Waraka kwa wafanyakazi wa Posta’. Tunasikitika sana kwa matatizo yaliyokupata kutokana na kutokupata huduma ambazo zingekidhi matarajio yako. Pole sana ndugu mtumaji wa waraka huo kwa yote yaliyokupata. Tunapenda kukufahamisha yafatayo:
Usambazaji wa barua ndani ya jiji la Dar es Salaam hufanywa ndani ya masaa 12 iwapo itapostiwa mapema katika masanduku ya barua yaliyo katika ofisi za Posta au yale yaliyoko mtaani (‘street letter boxes’).
Barua zinazotoka nje ya nchi (inbound) kwa kawaida huchambuliwa na kupelekwa maeneo husika mara moja baada ya kufika Posta Kuu ya Dar es Salaam, hii ikiwemo kusambazwa katika ofisi za Posta zilizoko Dar es Salaam au zile za mikoani.
Barua kutoka Dar es Salaam kwenda/ kutoka mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya na Ruvuma, zina uhakika wa kufika ndani ya masaa 24 kama zitakuwa zinaenda makao makuu ya mikoa hiyo au maeneo mengine ya mikoa hiyo ambayo yana uhakika wa usafiri. Shirika la Posta lina utaratibu wa kusafirisha barua hizo kwa kutumia magari ya Shirika yanayosafiri usiku (overnight mail vans) kuelekea/ kutoka mikoa hiyo. Usafiri huo pia hutumiwa na wachapishaji wa magazeti ambapo wasomaji wa magazeti wa mikoa hiyo huweza kusoma magazeti ya siku hiyo hiyo sawa na wale walioko Dar es Salaam.
Kuna uhakika pia wa barua kufika ndani ya masaa 24 kwa ile mikoa ambayo kuna usafiri wa ndege kutoka/ kwenda Dar es Salaam kama vile Mwanza, Bukoba, Shinyanga, Tabora, Mtwara, Lindi, Kigoma kutegemea na ratiba za ndege zinazoenda katika maeneo hayo.
Barua kutoka Dar Es Salaam kwenda Zanzibar nazo zina uhakika wa kufika ndani ya masaa 24 kutokana na kuwa na usafiri wa uhakika wa boti ziendazo kasi.
Tukirudi katika suala lako, nyaraka na vipeto vya EMS husambazwa kila siku vinapopokelewa iwapo vitakuwa na ‘physical address’ ya mtumiwa. Iwapo mtumaji atakuwa ameandika anuani ya sanduku la posta (P.O BOX), mtumiwa huandikiwa ‘calling notice’ ili aje kuchukua barua hizo katika ofisi ya Posta. Iwapo mtumiwa hana kawaida ya kufungua sanduku lake binafsi mara kwa mara hapo uchelewesho unaweza kutokea. Sababu nyingine ya kuchelewa ni iwapo mtumiwa anatumia sanduku la posta la mtu mwingine au la kazini ambapo si yeye anayeenda kulifungua; uchelewesho au upotevu unaweza kujitokeza. Hivyo ni muhimu sana kwa mtumaji wa barua kuandika anuani sahihi na kwa upande wa nyaraka na vipeto vinavyotumwa kwa EMS kuandika physical address ili kurahisisha usambazaji kwa kuwa kwa kulipia EMS ina maana nyaraka au kipeto chako ni cha haraka na kinatakiwa kufikishwa hadi ofisini/ nyumbani kwa mtumiwa.
Kuhusu suala la kifurushi/ barua kukatiwa bima (insurance) na haijafika ilikokusudiwa, kwa kawaida kama itakuwa imepotea/ kuharibika ni lazima mtumaji arudishiwe kiasi cha fedha kulingana na bima aliyokatia barua/ kifurushi chake.
Kuhusu suala la kuwa huenda mzigo huo umeshikiliwa na watu wa forodha (customs), Posta haina mamlaka ya kuzungumzia masuala ya forodha kwani shughuli za forodha ziko chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), hata hivyo jukumu la customs ni kuangalia kama mzigo huo unapaswa kulipiwa ushuru au la. Habari za kiusalama pekee ndizo zinazoweza kufanya mzigo ukashikiliwa kwa uchunguzi iwapo itabainika kuwa kuna vitu vya hatari. Hata hivyo kwa kuwa wewe ulituma zawadi za birthday hatudhani kuwa hiyo ni sababu ya kushikiliwa zawadi ulizotuma.
Kutokana na maelezo hapo juu tunaomba kupata particulars za vifurushi/ barua ulizotuma na kutokufika ili tuweze kufuatilia (track and trace) na kujua tatizo liko wapi. Maelezo hayo yawe na tarehe uliyotuma, nambari ya kifurushi hicho (ipo kwenye risti uliyopewa na ofisi ya posta ya huko), jina lako kamili na anuani yako kama ilivyo kwenye barua/ kifurushi ulichotuma, jina kamili la mtumiwa na anuani yake. Maelezo hayo yatume kwenye customer.care@posta.co.tz
Ushauri wetu kwako ni kama ifuatavyo:
Ø Ni muhimu kuandika anuani sahihi za mtumaji na mtumiwa katika barua/ kifurushi ili kuondoa uchelewesho usio wa lazima kwa kuwa inapotokea anuani imekosewa mwenye sanduku la posta anaweza kuandika try P.O Box………. (nina maana anuani nyingine ambayo yeye anaweza kudhani kuwa huenda inaendana na yake kwa kufikiria kuwa mtumaji anaweza kuwa amekosea). Danadana kama hiyo inaweza kuendelea kwa barua kutoka sanduku moja hadi nyingine na nyingine hupotea kwa mtindo huo. Barua kama hiyo inapoingia kwenye sanduku la barua ambalo anayelifungua sanduku hilo si mwaminifu anaweza kuichana na kuitupa au kuchukua mali zilizopo.
Ø Pamoja na anwani sahihi tunashauri nyaraka na vipeto vinavyotumwa kupitia vya EMS ziandikwe physical address (jina la mtaa na nambari ya nyumba) pamoja na simu ya mtumiwa ili kurahisisha usambazaji.
Ø Tunashauri vitu vyenye thamani vitumwe kwa njia ya EMS au kwa kusajiliwa (registered) au kukatiwa bima (insurance) ili kudhibiti usalama wake na pia kurahisisha ufuatiliaji.
Ø Aidha ni muhimu kuhakikisha kuwa kifurushi au kipeto kinafungwa vizuri (properly packed) ili kisipasuke wakati kinasafirishwa. Ni muhimu kufunga vizuri kwa sababu usafirishaji wa barua, nyaraka na vipeto/vifurushi kutoka nje ya nchi hususan Ulaya, Marekani, Asia, n.k hushughulikiwa na makampuni mbalimbali kabla ya kufikishwa Posta ya Tanzania.
Ø Ni vizuri zaidi kwa mtumiwa kuwa na sanduku lake binafsi la barua ili kuweza kudhibiti barua ziingiazo katika sanduku lake. Gharama ya sanduku binafsi la kupokelea barua kwa mwaka ni sh. 12,000/- kwa Ofisi Kuu ya Posta Dar es Salaam, sh. 9,600/- kwa ofisi za Posta zilizoko miji mikuu, sh. 7,200/-kwa Ofisi za Posta Wakala (Franchised Post Offices) na zile zilizoko wilayani na sh. 1200/- kwa ofisi za Posta zilizoko vijijini. Gharama hizi zimejumuisha ongezeko la thamani (VAT).
Mwisho tunaomba uendeleee kutumia huduma za Posta na usisite
kutufahamisha matatizo yoyote yanayojitokeza wakati wa kutumia
huduma za Posta kupitia e-mail address tuliyokupatia. Kwani kwa
kufanya hivyo ndiyo tutaweza kujua matatizo yaliyopo na kuchukua
hatua zinazofaa ili kuweza kukidhi matakwa ya wateja na wadau
wanaotumia huduma za Posta.
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA
17, MEI 2007

Hehehe....hawa jamaa wanaboa !
ReplyDeleteNawapongeza posta kwa majibu yao, kwa kweli huduma kwa wateja zinastahili kuwa namna hii. Nadhani tukifuata ushauri tuliopewa hapa basi kutakuwa hakuna upotevu wa barua na vifurushi vyetu.
ReplyDeleteAma kweli nchi yetu inasonga mbele! Kweli posta hongera kwa kujaribu kuweka mambo bayana hapa. Lakini tatizo langu linabaki TRA wanatoza ushuru ambao uko unjustified kabisa. Mtu unatumiwa pair moja ya viatu lets from US unaambiwa ulipe ushuru ambao ni mara mbili ya gharama za hivyo viatu!
ReplyDeleteAnyway, again Michuzi na hawa jamaa wa posta thats a good job. Hongera.
Nashukuru bwana michuzi kwa kufikisha ujumbe kwa walengwa. Upigaji wa Domo bila vitendo hauleti maendeleo.
ReplyDeleteKuhusu Posta-nashukuru pia wamechukua muda wao kujibu malalamiko na kutoa ushauri wa jinsi ya kufanya.
Asante bw MICHUZI kwa kufikisha ujumbe. Tunashukuru kusikia toka kwa Bw BUJIKU pia.
ReplyDeleteHaya maelezo yote yaliyoandikwa ndivyo inavyopaswa posta zetu kuoperate kwa namna hiyo --- hayo yote yaliyotajwa ni SHERIA ZA KWENYE VITABU ambazo wafanyakazi wa posta hutakiwa kuzifata. Tatizo hapa tulilonalo ni kwamba hizo sheria HAZIFUATWI na matokeo yake ndio hayo ya watu kupoteza ama kuibiwa vifurushi vyao.
Tunashukuru sana kwa Bw BUJIKU kutupatia info zake, kila mtu kwa wakati wake ataweza kuwasiliana na huyo bujiku na kumweleza shida zake (BUJIKU kaa tayari kusikia malalamiko mengi toka kwetu) labda bujiku ndio atakuwa muokoaji wetu mara vifurushi vyetu vitakapotea kiajabu.
MICHUZI hongera sana kwa kuwa na blogu ya KIMATAIFA tunafarijika sana kuona wazalendo wanasoma hii blogu yako. Kazi nzuri kaka!
Michuzi,
ReplyDeletehuyu aliejibui hii kitu ni mbavu sana tena siajabu ndie mwizi mkuu. Huo utaratibu na ujinga wote alioandika hapo tunaujuwa lakini tatizo ni kwamba hayo matatizo bado yapo. Ukituma barua zingine hazifiki---mimi binafsi nimetuma kadi za x-mas hadi leo ni hadithi---kati ya hizo kadi moja niliweka US $50, na nyingine niliwekamkitu kama 20,000/= au 15000/= (TZsh) ambazo nilisahau nikaondoka nazo---nikasema ngoja niwapatie washkaji--sasa wewe nikalipie western unioni kutuma $50-----. kutuma kwa hii njia ni kosa langu--lakini the fact is there posta ya bongo ni wasenge wote---maana ya customer service hawajui---kuna wakina mama wamekaa hapo ukiwauliza swali wanajibu kama unawataka kimapenzi na wanaangalia pembeni----nilikuwa hapo sep/2006 na nimeona kwa macho yangu sio kuambiwa.
Anasema anaomba tuendelee kutumia huduma zao---what other option is there---fedex, dhl,.
wewe ulioandika hii kitu kwa michuzi----tunachotaka ni kwamba hicho mlichoandika ni kwamba kitekelezwa.
Do not get me wrong I can point watu wawili au watatu hapo posta (majina siwajui) ambao wamekwisha kwenda an extra mile kunisaidia mimi binafsi--lakini the majority ni wapunmbavu tu--na wezi.
Wengine ndugu zetu wapo vijijini hakuna e-mails sasa tutawasiliana vipi kama nyinyi mnachana barua zetu.
KJ-204
Kama mteja serious Posta Nawaonya hakikisheni shirika linafanikiwa.
ReplyDeleteShirika likifa hakuna sababu kwa ninyi mlipwe mafao yenu.Kampuni ikifa kwenye utandawazi mnatakiwa muachishwe bila chochote sababu mumeua mtaji wa mtu hivyo haiwezekani mpongezwe kwa kuua mtaji wa mtu kwa kulipwa mafao shirika likifa.
Kwenye utandawazi mtu ukiua kampuni ya mtu unaondoka mikono mitupu tena ukikutana na wenye hisa wakorofi utaishia mahakamani.Ndio maana wawekezaji hawataki kulipa mafao ya watu kwenye mashirika na viwanda vilivyokufa ambavyo wamenunua sababu hawaoni sababu ya kuwalipa wauaji kama hao.Na ndio maana mara ingine hawawataki hata wafanyakazi waliowakuta, hawataki kuendelea nao sababu hawataki kuendelea kufanya kazi na wauaji walioua kampuni au kiwanda walichonunua hapo kabla.Wanakuwa na hofu kuwa ukiwachukua waweza ua tena na mitaji yao ikapotea ndio maana wanaleta watu wao na kuajiri wengine wapya.
Wawekezaji wanaishangaa sana Tanzania kuona eti mtu anaua kiwanda au shirika halafu anaandamana hadi kwa waziri wa kazi au mahakamani eti anadai mafao yake kutoka kiwanda au shirika lilokufa au linaloelekea kufa na waziri na mahakama wanawasikiliza badala ya kuwakoromea na kuwafokea na kuwaambia watoke.
Huwezi kudai haki kwa marehemu kiwanda au shirika uliyemmwua.
Niliwahi pata nafasi ya kuangalia baadhi ya mabango sikukuu ya mei mosi.Unakuta watu wamebeba mabango yanayodai eti wanataka Raisi awasaidie wapate mafao kwenye viwanda au mashirika yaliyokufa!
Raisi aingilie!Walioua mashirika hawana haya kabisa.Wanathubutu kubeba mabango kama hayo kweupe bila hofu wala haya tena mbele ya Raisi.
Watanzania tuwe wakali.Mtu akiua biashara yako au kiwanda chako hakuna haja ya kumlipa mafao.Kama ni hasara keshakutia hasara anataka nini kwako tena.Mwambie akukome.
Kodi za wanachi ambao ndio mtaji wa kuanzisha haya mashirika ya serikali Posta ikiwemo mkiuua lazima muondoke mikono mitupu.Kama munaona ushindani hamuuwezi jiuzuluni chapchap mpishe wengine.Kama menejimenti au mfanyakazi ni goigoi timuaneni haraka kabla shirika kufa.Bodi kama haiko commpetitive mamlaka husika ibadilishe haraka.
Watanzania tusioneane aibu.Let us be serious with our resorces.
koloboi@yahoo.com
well, kazi nzuri sana michuzi , nakuhakikishia siku hii blog yako inakuwa ya kitaifa. hihihihihi
ReplyDeleteAisee BIG UP kwa Shirika Letu la Posta, kumbe mnajali. Michuzi sasa Tanzania tunapiga hatua za maendeleo. Huu ni mfano wa kuigwa.
ReplyDeleteNatamani sana PCB, na TANESCO nao wangekuja hapa kujibu hoja
THREE WISE WOMEN
ReplyDeleteWhat would have happened if it had been the three wise women instead of three wise men?
1. They would have asked for directions
2. They would arrived on time
3. They would helped deliver the baby
4. They would have cleaned the stable
5. They would have brought practical gift
6. And final they would have made a casserole
But what would have they said as they left?
1. Did you see the sandals Mary wearing with that gown?
2. I heard that Joseph isn’t even working right now?
3. That baby doesn’t look anything like Joseph
4. And that donkey they are riding has seen better days too.
5. You want to bet how long it will take before you get your casserole dish back
6. Virgin my *%@$! I knew her in school
Wewe mshamba unayetuma pesa kwenye barua hata huku ulaya wanachukua!!
ReplyDeleteBig-up customer care POSTA TANZANIA
Koloboi umeongea very sensitive issue ni kweli tanzania kuna uzembe mkubwa wa aina hiyo.
ReplyDeletehebu angalia sasa huyu jamaa wa posta maelezo yake ya utendaji kazi wa shirika ni mazuri na yanavutia tatizo ni hao wasenge wezi,sasa watu wakikacha kutumia posta shirika likafa hao hao wezi watarudi kudai mafao wakati wao ndo wameliua shirika kwa wizi wao.watanzania inabidi tugrow up na huyu jamaa afuatilie hao wezi sio anatupa sera za shirika HAISAIDII.
Kwa kweli nimefarijika sana na hili jibu la posta ingawa haiwezi kurudisha mzigo wangu lakini imenipa Moyo, Michuzi imekuongeza thamani hii kaka yangu. si mchezo nimewasiliana na huyo bwana sijui kama atanipa jibu la kufaa.
ReplyDeleteTunamshukuru kwa majibu lakini bado jambo kubwa linalosikitisha na hakugusia mambo ya ushuru kabisa amewatupia sijui nani.
ReplyDeleteKwa wale ambao tumeshatuma vitu mara nyingi na mara zone ninabahati havijapotea tunalia na ushuru. Ni wapi au ni kiasi gani kinatozwa kwa ushuru halali? Angalau kungekua na mahali pakusoma mtu afahamu kabisa kama akituma mzigo wa kilo kumi kama haja declare value yake basi atatozwa ushuru kiasi fulani na kama akideclare value basi ushuru unakua kutokana na value ya mzigo.
Mimi nilimtumia mama yangu nguo ya kinigeria. Na kwa vile nilitumia ems (7 days) na insurance nilibidi niandike thamani yake. Ukweli ni kuwa walitowa 50,000 ushuru na hata risiti sikumbuki kuwa walipewa au la. Jamani nguo moja ya $150 wacharge shilingi 50,000????
Nilishikwa na hasira sana na toka siku hiyo niliamua ni heri nikusanye vitu vingi nitumie cargo au kama ni mzigo wa haraka basi natumia njia ambazo ninalipa kila kitu huku wao wanapokea tu. Wakati mwingine ni ghali sana lakini ina worth peace of mind na kuwakomesha hao wala rushwa hapo posta.
USA kitu chenye thamani ya less than $200 au 50 pounds hawacharge ushuru kukipokea na wanakuletea mpaka nyumbani for free box lako. Hiyo ndio good customer service na ukiangalia ushindani ulioko wa service hii saa hivi posta ya bongo itakufa tu siku moja hizo nyodo sijui mtampelekea nani.
ReplyDeleteHuo ushuru mnaotucharge ni kutukomoa tu sisi watu raia wenu tunaotuma vitu vidogo vidogo kusaidia ndugu zetu wakati matajiri na watu wasio raia wanaingiza mabidhaa mengi tu for free hapo na kuviuza na kutia faida mfukoni kwao au kushare na baadhi ya viongozi hapo. This is not fare at all
Shirika la posta Tanzania wanatakiwa kutolewa nishai au kutandikwa viboko kabisa. Tena wee ngoja tu nikiulamba uongozi unaoeleweka siku za usoni watajuta kuzaliwa. Manyang'au kabisa, walafi,wavivu,na wenye dhuluma. Siwasifu hata kwa kitu kimoja hawa kwani wamekwamisha vifurushi vyangu kuwafikia walengwa all the time nilipotuma.
ReplyDeleteMfano: nilimtumia mtoto wa sekondari kamera ili tu aweze kujitafutia lolote kwa kujikimu na mahitaji ya hapa na pale akiwa masomoni. lakini alipoenda kuichukua akaambiwa alipe ushuru wa laki mbili na nusu. Ajabu mno- yaani pesa hiyo ni zaidi ya ada na matumizi ninayompatia anapokuwa shule kwa term moja. Posta wanawaumiza mno maskini. Mtoto kama huyo angepata wapi hiyo hela? Nadhani angeachwa achukue mzigo wake. Cha ajabu, ilishindikana kabisa na mzigo ukarudi kwangu. Sasa nchi hii tutajikomboaje? Ningedhani nchi yetu wangejali watu wake kipita anything na hasa wanapoingiza vitu toka nje. Concept ingekuwa kwamba watanzania waliosambaa nje ya nchi- wapo kule kukusanya kurudisha chochote kile nchini mwao. Sasa vitu vidogo kama kamera, kakiatu, planner,video camera nk; watu wa posta wakiviona basi inakuwa nongwa. Tabia hii ya posta haiwezi kabisa kuingia katika ushindani na makampuni mengine. Nilipokuwa mlimani katika seminar zetu nilikuwa mpinzani mno wa ubinafsishaji kumbe nilifanya hivyo kwa kuwa sikuwahi kupatwa/kushuhudia fika huduma mbovu za makampuni yetu. Shuleni tulifunzwa hata kama ukiwa maskini na ukawa una pea moja tu ya uniform itunze na kuisafisa vizuri, hata aliye tajiri akikuona atavitiwa kuwa hata kwa kidogo ulichonacho unakipenda na kukitunza.
Waajiriwa wa posta wangekuwa wanapewa safari za kwenda kujifunza kwa wenzao. Wenzetu hawa wamepiga hatua mno na kuondokana na viulafi na uroho wa vitu vidogovidogo. Lakini nyumbani bwana loooo! Mungu apishe mbali. Wizara inayohusika inatakiwa kuwarusha watu hawa vichura. Kulilia uwekezaji tu kwenye mgogoro wa utendakazi kama huu unaotutesha hata sisi wazawa utamvutia mtu wa nje kweli hasa aliyezoea smoothness ya services!!!. Basi tu- nakuja though one day posta mkae chonjo-ni kuwachapa bakora tu.
good response from posta tanzania, ila kuna walafi wachache ndo wanawaaribia jina. fukuza kazi
ReplyDeleteAkhsante sana Bw Bujiku kwa kuamua kutoa maelezo,kwani ungekuwa kama watendaji wengine wa serikali na mashirika ya bongo ungeanza kutoa lawama na kuficha UOZO huo..akhsante sana kwa hilo.Kwa uzoefu wangu,hapo bongo kuna mambo mawili ambayo ni UPOTEAJI WA VIFURUSHI na USHURU.Watanzania wengine wanachanganya masuala ya ushuru na Posta...Posta hawana mamlaka na masuala hayo,na hili limekuwa tatizo la muda mrefu sana.Hao TRA wanatoza ushuru mkubwa usioendana na thamani ya mzigo.Mimi nina ushahidi hai,kwani nina ndugu yangu aliwahi kutuma cds mpya kutoka States,zilipofika hapo dsm,ushuru uliopangwa siusemi,na vilevile eti wakasema quality ya cds ni low...mpaka leo hizo cds ziko mikononi mwa TRA!!!!.Suala la uwizi liko mikononi mwa Posta,ni lazima mlishughulikie.Nina ushauri wa bure kwa shirika la Posta...kaeni na TRA muongee masula haya,kwani yanaharibu image ya TZ na Posta.
ReplyDeleteHingera sana Posta kwa maelezo mazuri na ya kuridhisha. Lakini bwana Bujiku nafikiri hujaelewa kilio cha watanzania. Tatizo ni kwamba hao watumishi wenzio wanaiba vifurushi vya watu, maelezo uliyotoa ni mazuri sana, lakini ndani ya shirika hakuna uaminifu. POSTA WIZI MKUBWA tafadharini jamni rekebikeni.
ReplyDeleteUshuru baba ushuru baba
ReplyDeleteNchi nyingi zinaweka ushuru mwingi ili kudiscarage importation na kufanya watu wanunue vinavyozalishwa nchini. Lakini kwa sisi hata vinavyouza hapo mlimani city vyote ni vya nje sasa mbona bado mnatucharge ushuru mwingi tu. Au mnatudiscarage tusitume vitu nyumbani ili watu wanununue kutoka kwa hao wasouth?
Ni kweli ratio ya ushuru na mzigo tutumayo hapo bongo havinauwiano kabisa. Sijui ni kukomoana.
Mini nimeuliza swali hili siku za nyuma bado sijapata jibu. Hivi sisi watanzania kwanini hatuheshimiani hivyo???. Ukifika posta unamkuta mama wa makamo, unamsalimia na kusubiri huduma, anaangalia pembeni na kukuignore kabisa. Kama anataka usubiri si akuambie vizuri tu?. Kama hatuheshimiani wenyewe, waje wazungu ndio watuheshimu? Sisi vijana wenu tumetembea duniani. Jamani, wenzetu wanaheshimiana na kuthaminiana sana. Ukifika posta, au dukani, au bank unasalimiwa sana na kusikilizwa kwa makini na haraka! Tukiweza kuheshimiana, tutapeana huduma nzuri, tutaacha kukomoana kwa ushuru ambao ni mara mbili ya bei ya "zawadi", n.k.
ReplyDeleteje nitajuaje mzigo wangu umekwama kwa watu tra forodha
ReplyDelete