
asili ya handakizz dar ni hawa wadau ambao kwa vile plani ya mabomba na mifereji wakati wa ujenzi wa barabara haikuwa nayo inabidi wachimbe baada ya ujenzi, ama kuna nyumba mpya imejengwa karibu na inahitaji bomba la maji. ubaya wa zoezi hili ni pale wanapoacha kurudishia lami. matokeo ni handakizzzz
Mamlaka zinazohusika na usimamizi wa miundombinu zinapaswa kulitazama kwa makini suala la watu kukata barabara za lami kwani ujenzi wa barabara za lami hugharimu fedha nyingi mno. Ingekuwa vyema kama kungekuwa na utaratibu wa yeyote anayetaka kupitisha bomba (kwa kukatiza barabara ya lami) aombe kibali kutoka mamlaka husika na awajibike kulipia gharama za matengenezo ya hiyo sehemu ya lami aliyoharibu. Sina hakika na hili, lakini kwa sasa inaelekea yeyote anaweza kubomoa barabara ya lami kwa visingizio mbalimbali na kurudishia udongo jambo ambalo linasababisha mahandaki na uharibifu mkubwa wa barabara.
ReplyDelete