Franco the Great aja kukuza utalii

Mwana Sanaa maarufu duniani wa Kimarekani, Franklin Gaskin, anayejulikana kwa jina la Franco the Great, anaingia Jijini Dar es Salaam Jumatatu (Juni 25) kwa ziara ya wiki moja kwa nia ya kutafuta njia ya kukuza utalii wa Tanzania nchi za nje kwa njia ya sanaa.

Ziara yake inatokana na mpango uliobuniwa na kampuni moja ya kitalii ya New York nchini Marekani iitwayo Time Warner Safaris ikishirikiiana na makampuni matatu ya humu humu nchini Tanzania yanayojishughulisha na masuala ya utalii.

Habari zilizopatikana Jijini Dar es Salaam zinasema makampuni hayo ni Discover Tanzania Heritage inayosafirisha watalii, Stan Ad & Consultancy Ltd, ambayo inatoa chapisho maalum la Kili Album, kwa ridhaa ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Ujumbe Inc. Ltd inayotangaza utalii kwa njia ya mtandao wa Internet.

Mtendaji Mkuu wa Time Warner Safaris, Bw. Bill Mushi, ambaye tayari yuko nchini, amesema Tanzania mpaka sasa ilikuwa haijachukua fursa mbadala ya kutangaza vivutio vyake vya utalii kwa njia ya sanaa. Utalii wa aina hii, alisema, umetokea kupendwa na umechangia sana mapato ya nchi mbalimbali.

Franco the Great, ambaye amewavutia watalii wengi kutembelea sehemu anayoishi Jijini New York, Harlem, amekubali kutengeneza michoro ya vivutio mbalimbali vya utalii vya Tanzania ambavyo vitaonyeshwa nchi za nje.

Mushi amesema ujio wa msanii huyu maarufu utasaidia kukuza utalii wa Tanzania kwa sababu umaarufu wa Franco umeenea katika nchi nyingi na ana uvuto wa kipekee.

Mkurugenzi Mtendaji wa Discover Tanzania Heritage, Bw. Saleh Dola, amesema kuwa akiwa nchini, Franco atatembelea mji mkongwe wa Bagamoyo, hifadhi ya Ngorongoro na hifadhi maarufu ya Serengeti ambayo hivi karibuni ilitangazwa kuwa mojawapo ya maajabu mapya duniani. Dola pia ni kiongozi wa asasi ya Bagamoyo Cultrural Heritage Tourism Cluster.

Msemaji wa Stan Ad & Consultancy Ltd amesema “ujio wa Franco, licha ya kusaidia kukuza utalii ni mfano mkubwa kwa wajasiliamali vijana wanaojibidisha kujikwamua na umaskini nchini Tanzania.”

Akiwa na miaka mitatu, mtoto Franklin alianguka toka ghorofani na kupoteza fahamu kwa mwezi mzima. Watu wote, hata madaktari, walikata tamaa isipokuwa bibi yake. Baadaye alikataliwa na watoto wenzie shuleni. Kutokana na msaada wa padri mmoja wa Kikatoliki aliwekza kutimiza azma yake ya kucheza mazingaombwe.

Miaka 40 iliyopita, bibi yake alimkaribisha Jijini New York kutoka mashambani alikokuwa akiishi na akaanza kuchora picha mbalimbali bila malipo. Kipaji chake kilionekana. Jamii ikampenda.

Hivi sasa Franco the Great ni jina maarufu duniani. Amepata tuzo nyingi za kimataifa. Serikali ya Ufaransa imewahi kumpa kazi ya kuchora vivutio vya utalii vya miji minne.

Kufuatana na ratiba iliyotolewa na waandalizi, Franco pia anategemewa kukutana na Waziri wa Masliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, na viongozi wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na hifadhi ya Ngorongoro na Bodi ya Utalii Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 23, 2007

    huyu ndio nani vile. Tupe basi background yake.
    Unjua huku hata makanisani kwetu mtu akija kuhubiri lazima waseme ni nani, alisoma wapi na anaujuzi gani...ha ha ha ha like neno la mungu llnahitaji PhD....lakini basi tutel tell kidogo ni nani. Unajua sanaa inanoga tukijua mwanzo wake.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 23, 2007

    Huyu the great mwenyewe atachukua kidogodogo kutoka goverment au bill na wenzake ndo wano mlipa?Kama goverment inchip kidogo basi huo ni ulghai.Ila rai wa kawaida hatuna choise.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 23, 2007

    FRANCO KAZI YAKE NI NZURI NA TUUNAZIONA HAPA HARLEM.JAPO SIO MKALI WA KUTISHA KWANI PALE TZ KUNA VIJANA WANAWEZA KUM-CHALLENGE.
    KAMA HUO MCHORO NYUMA YAKE HAPO JUU ULIOPO KONA YA 123 ST. NA MALCOM X. BLVD/LENOX AVE./7TH. AVENUE,WATU ALIOWACHORA HAWAJAFANANA SANAAAAA NA WATU HALISI NA MAARUFU TUNAOWAJUA.
    KUFIKA KWAKE TZ KUTAISAIDIA NCHI YETU NA WACHORAJI MAKINI.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 23, 2007

    ANON WA 1:46 AM,UKIONA KITU HUKIJUI NINAKUSHAURI KUINGIZA HILO JINA KWENYE SEARCH ENGINE.SASA SEARCH JINA FRANCO THE GREAT UTAPATA HABARI ZAKE.HATA KAMA UNATAKA KUMJUA NDUGU AU RAFIKI KAMA AMESHAWAHI KUSHTAKIWA KWA HAPA USA,AU ANA MAMBO YA MITANDAO...JUST SEARCH HIS OFFICIAL AU POPULAR NAME.
    FOGO.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 23, 2007

    Nyie afrika leo takoma mimi,iko penda sana tangaza inchi,hilo kazi kama anapewa janja kutoka India tatangaza dunia kote,kwani yeye iko kila mahali,lakini kama nachukua toka marekani tu,seem that the targeted market will be USA,canana and part of europe.Lete hiyo kazi kwa mtu kama sisi bana taona fanikio zake zinazokuja hapa TZ

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 23, 2007

    hii ni fursa nzuri kwa wasanii waketu kujua kwamba kazi wanazo zifanya ni mzuri na zina dhamani kubwa sana duniani, mimi nina wapongeza hao walio leta wazo hili ni zuri na litawajenga wachoraji wa tanaznia kiakili na kiusanii kama watapata nafasi kama hizi zakuonana na wasana sanaa wengine kutoka nje pia kupandisha chati kazizao za uchoraji FRANCO karibi bongo karibi sana unaweza kuona ni aina mpya ya kutangaza utalii wetu nje kama FRANCO ATAKAPO ENDA KUCHORA MLIMA KILIMANJARO NA MBUNGA ZETU HUKO MAREKANI NA NCHI NYINGINE BASI NIFURUSA NZURI KUJITANGAZA,unapotaka kuangalia picha NA VIDEO za FRANCO ANGALIA WWW.JAMBOVIDEO.COM NA WWW.JAMBOPHOTOS.COM nimejionea mwenyewe sasa hii ni njia mpya kabisa ya kujitangaza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...