wadau hii imeingia sasa hivi nami kama tarishi ambaye kiinglishi iz noti richebo naimwaga kama ilivyo...
Michu!
Nakutumia hii kali ya wacamerron. najua bongo hatukawii kuiga hii tabia but may be by the time nakutumia hii kuna watu tayari wameshalizwa. Ipe kipau mbele.. as usual majina tusitajane pls

Please be aware of a new fraud carried out by Western Union Employees in Cameroon.

Western Union employees in Cameroon have begun stealing from their customers, precisely deceiving Recipients of funds from the US that the Money Transfer Control Number (MTCN) is inaccurate after the form has been filled out and the receiver has signed as having recieved the money.

How it works:

The Reciever of funds fills out the form and hands it to the WU employee. The Employee collects the form from the Receiver, interrogates the system and tells the receiver that the MTCN is inaccurate, and requests that the receiver should call his or her contact in the US to get the correct number. The form is not retruned to the Receiver by the Employee.

While the Receiver goes to make the call, the Western Union worker now collects the money from the system using the form that was filled with the Receiver's signature. The Receiver returns with the same number that was given to her before, but WU employee sticks to the story and a frustrated Receiver now thinks the relative in the US never sent the money, and gives up.

What to do:

**Always advise relatives receiving money not to leave behind a filled-out, signed form if the MTCN can't not be verified.

**To sign the form only when the money or MTCN is verified.

Should this happen to your relative, immediately call WU 1800-325-6000 option 4, then 5, and ask for the Fraud Department. They are very helpful most of the times and report the case. It takes about three (3) weeks to get a refund from WU after several follow-ups from the US end.

I hope this will help prevent fleecing someone's innocent relative out there.
hapa chini kuna mdau kale ushauri nasaha kwa hili jambo....
Michuzi,

Kama unaweza, naomba ubandike hii kitu kwenye blogu yako. Huu ni ushauri tu kwa waTanzania wenzangu ambao wako majuu na wataka kutuma pesa nyumbani. Ushauri wangu unatokana na habari uliyoitoa kutokana na stori ya Western Union huko Cameroon.

Njia mbadala ya kutuma fweza nyumbani ni kutumia kadi ya benki (Debit au ATM Card). Kwa sababu kuna mashine za ATM lukuki Tanzania, unachoweza kufanya ni kufungua akaunti mahsusi kwa ajili ya kutuma fedha nyumbani, halafu utume kadi pamoja na PIN nyumbani. Baada ya hapo, unaweka pesa kwenye akaunti na kuagizia tu kiasi unachataka nyumbani watoe. Mara nyingi kuna kiwango cha mwisho cha utoaji wa pesa kwa siku (nadhani Bongo ni laki nne kwa siku).

Kwa wale ambao wako Marekani, gharama ya utoaji wa pesa kwenye ATM ambayo sio ya benki yako ni dola mbili ($2). Hiki ni kiasi kidogo ukilinganisha na dola kumi na tano ($15) za utumiaji wa dola mia moja ($100).Huu ni mfano tu.

Tatizo ni kwamba ukiwa na ndugu ambao sio makini, utaanza kupigwa zile overdraft charges (wastani wa dola 39). Kwa hiyo inabidi utafute njia ya udhibiti wa utoaji hela holela.

Metty
http://mettyz-bongoland-reflections.blogspot.com/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Nashukuru kwa ushauri wako; ushauri mzuri sana huu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2007

    DEBIT card nyingi hazina overdraft facilities hapa UK, kwa hiyo ukimtumia card nduguyo tanzania yeye anapeta bila wasiwasi,ila tu unamstua umeweka ngapi sababu yeye hawezi kuona balance,ni cheap na mshiko unaingia instantly

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2007

    Ushauri mzuri huu, Dar nako kuna utapeli unapewa pesa lakini wanapiga panga (WU Tawi la Kariakoo)haswa wakati kuko 'busy.'

    Usipohesabu pesa zako kabla ya kutoka umeliwa imeshatokea kwangu, ndugu yangu ilikuwa apokee Tshs.480,000 akapata 470,000.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2007

    Yes ushauri mzuri,but mimi nimeibiwa na Western Union kwa njia nyingine kabisa,but nilichokifanya ni kustop kutumia huduma hiyo,May mwaka huu nilimtumia ndugu yangu euro 800,kutoka Paris kwenda Dar,wakati naenda kutuma nilikuwa nina copy moja ya exchange rate ya BOT,ambayo ilikuwa inaonesha 1euro=1665.83Tsh,baada ya kujaza sender form na kulipia,gharama ya kutuma ilikuwa ni euro42,jumla nikalipa euro842,cha ajabu akanirudishia copy yangu wakiwa tayari washa convert into Tsh,huku wakiandika atapokea (1,272,000)badala ya (1,332,000) yaani 1euro=1590.nilipowauliza kwa nini mmetumia rate hii,wakasema ndo iliyopo kwenye system,nikawapa website ya BOT na kuwaonesha exchange rate kwa wakati ule ,lakini walibisha na kusema wao wanafata system yao,uvumilivu ulinishi na kuwatukana na kutaka nirudishiwe pesa yangu nitaute njia nyingine,wakasema washaingiza kwenye system haiwezekani,nikiwa nimeliwa karibu 60,000/=,labda wadau mshauri tena juu ya hili,hawa jamaa wanapo convert hizi pesa,rate wanasoma wapi? maduka ya fedha ya mtaani hapo hata mimi ningewakubalia,but BOT nayo hawaitaki,je au ndo njia nyepesi ya kuiba?mbana gharama yao ya kutuma hawakunitajia in Tsh? sasa sijui wale wanaotuma from Tanzania kwenda sehemu nyingine,nafikiri in case of euro unaweza kuta anaambiwa 1euro=2000tsh ili system iibe rahisi,
    Kamtu-Chui,Paris

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2007

    safi kabisa,haya ndo mambo ya kupost kwenye blog ya michuzi,tunaelimishana vizuri sana,keep up issa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 05, 2007

    Ndugu yangu kama hulikuwa hujui kuwa western union wana rate yao basi umeliwa. uwe unatuma kwa njia ya Money gram, wao rate yao ni bomba. Halafu kwa kukufahamisha kuhusu western union, huwa wana rate tofauti. Kwa mfano rate ya wakati unatuma inaweza kuwa 1euro = Tshs 1,650 by the time huyo mtu bongo anakwenda kuchukua wanampa rate ya Tshs. 1,630. Ukiuliza unaambiwa system inaonyesha rate hiyo. Wanachokifanya ni kwamba mtumiwaji atapokea pesa kutokana na rate ya muda alipokwenda kuchukua hizo pesa, na si rate ya kwako ambayo wewe uliikuta ulipokwenda kutuma hizo pesa.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 07, 2007

    Na kwa mnaozituma hizo Debit Cards, chonde chonde msitume Card na PIN/Code katika bahasha moja. Mtawapa posta pesa za bure, maana bahasha zenye kitu ndani utakuta zimefunguliwa kidoooogo, wanapiga chabo kuna nini ndani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...