haya haya tena wadau... mbiu ya mgambo ikilia ina jambo - tarehe 29 na 30\06\2007 kutakuwa na upigaji kura kupata viongozi wa jumuya ya wanablogu tanzania (JUMUWATA). Hivyo wadau someni taratibu zote za shughuli nzima zitakavyokwenda kwa kubofya hapo chini...
hima hima tumia haki yako na kupiga kura kupata viongozi wetu wa mtandao wa wabongo
imetolewa na idara ya uhusiano
JUMUWATA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2007

    ungegombea wewe ningepiga kura

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 21, 2007

    Hiyo ni club au ni jumuiya ya kisheria? Yaani ukiblog mpaka big brother awe anakuwatch?
    Na ukiwa unaishi nje ya nchi lakini unablog mambo ya bongo unatakiwa uwe mwanachama au...hebut tuambie basi?

    Tusije tukakamatwa tukitia tu mkuu hapo airport

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 22, 2007

    Eee bwana mbona mi hawa jamaa siwafahamu wanablog kweli hawa????, au wamebuni mbinu ya kujitangaza kupitia kwako Michu maana wanablog wa TZ ninaowajua mimi sioni hata mmoja kugombea au si lazima uwe mwanablog kuwa kiongozi basi kama ni hivyo ngoja nikutumie na picha yangu uniweke mi nagombea "Uhasibu" wa wanablog.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 22, 2007

    This is a great example of "ideas gone bonkers", just my own view.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 22, 2007

    Wagombeaji wenyewe wamenuna sijui wamnunia nani? Wanategemea mtu awapigie kura wakiwa wamenuna, wanacheza.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 22, 2007

    Mheshimiwa Issa..HABARI ZA LEO KAKA.."..kasi mpya.."..NAONA MAMBO "..YAENDA YAKIONGEZEKA.."..UMOJA NINGUVU UTENGANO NI UDHAIDU... WATCH UR BACK MZEE MICHUZI..

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 22, 2007

    nevermisskwamichu,

    Hao usio wafahamu baadhi yao ni veteran bloggers na wana very seriuos blogs. Nakuomba uzitembelee blog zao. Pia nakuomba utuorodheshee wanablog wa Tz unaowafahamu.

    Asante.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 22, 2007

    wadau naomba msinishambulie mie msema kweli, huyo dada shija ana sura nzuri sijui umbo.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 22, 2007

    Aaaaah mmeanza ... hii kuchagua viongozi wa jumuiya ya wanablogu ... viogozi wa nini tena jamani? Mara mtaanza ooh, ngoja tujiandikishe kama NGO, ooh ngoja tuombe michango sijui wa kuendesha jumuiya ... mambo hayataisha!
    Hamna chochote ... mnataka tu kuona nani zaidi kati yenu ... hachane na mambo yenu hayo!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 22, 2007

    Mimi ninavyojua kublog ni hobby sasa sijui kuwa na jumuiya ya nini tena? Na hiyo jumuiya itamsaidia nani au ni kupoteza muda wa watu?

    Na live broadcast kama podomatic na Utube nazo zikiwa popular bongo wataweka jumuiya nazo.

    Mwishowe mtaharibu vizuri vilivyopo kwa vile baada ya hapo mraanza kuwa na sheria. Oh usifanye hivi ...fanya hivi tu ...usifanye hili....

    msianze kuanzisha indirect control au kutafuta marketing kwa kupitia migongo ya wengine. kama blog zenu hazipati watu basi hamna la maana mnalo blog.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 22, 2007

    Bongo mnapenda mambo sijui gani vile. na uongozi vile Blog nayo jumuiya!!!!!!!. mweka hazina kwenye blog !!!!! si ndio mwanzo wa kugombana? mnataka kuwa na mweka hazina wa nini? katiba ya nini?

    Nini kitakuafaida ya jumuia hii. Mimi kama mbongo nikiamua kujiunga na hii jumuia mafanikio yake yatakua nini?


    Ha ha ha aha ha aha ha mimi yangu macho...

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 24, 2007

    bongo wanajua ulaji ni kwenye vyama tu. Mtu ukitaka kutoka pitia kwenye chama au jumiya yeyote.

    Mwenyekiti, katibu, mweka hazina ...jumuitaya ya blob....

    blog soon itakua the thing of the past jamani...mbona mlichelewa kuanza

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...