
wakati wengine tukisherehekea kurejea kwa staaz wadau wengine ilikuwa taabu kidogo. huyu mdau kaleta kisa hiki kilichomkumba na stori hii chini
Habari Issa..!!
Napenda kutoa ushauri na kupenda kuwakumbusha wenzangu wote tunaotumia vyombo vya moto. Tukumbuke kufunga mikanda yetu wakati wa safari bila kujali umbali wa safari yenyewe.
Hizo picha ni ajali tuliyoipata jana jumapili, tar. 17/06/2007 mishale ya saa 10 jioni wakati tunatoka Geita na kuelekea Kahama na hapo Pembeni ni mimi mwenyewe.
Ajali ilitokea baada ya watu waliokuwa wamepakizana kwenye baiskeli.Mama mmoja aliyepakizwa kiti cha nyuma aliruka na kuanguka katikati ya barabara. Dereva alivyomkwepa ndipo tukapata hiyo ajali.
Tulikuwa watatu kwenye gari hii na tulikuwa wote tumefunga mikanda hivyo tulitoka salama bila hata mchubuko ila na Mungu naye alisaidia sana.
Napenda kutoa ushauri na kupenda kuwakumbusha wenzangu wote tunaotumia vyombo vya moto. Tukumbuke kufunga mikanda yetu wakati wa safari bila kujali umbali wa safari yenyewe.
Hizo picha ni ajali tuliyoipata jana jumapili, tar. 17/06/2007 mishale ya saa 10 jioni wakati tunatoka Geita na kuelekea Kahama na hapo Pembeni ni mimi mwenyewe.
Ajali ilitokea baada ya watu waliokuwa wamepakizana kwenye baiskeli.Mama mmoja aliyepakizwa kiti cha nyuma aliruka na kuanguka katikati ya barabara. Dereva alivyomkwepa ndipo tukapata hiyo ajali.
Tulikuwa watatu kwenye gari hii na tulikuwa wote tumefunga mikanda hivyo tulitoka salama bila hata mchubuko ila na Mungu naye alisaidia sana.
Aisee poleni sana na mpe hongera sana dereva kwa kuwasisitiza mvae mikanda na pia kwa kuthamini maisha zaidi ya gari maana tunashuhudia maisha ya watu wanne yakiokolowa, yule mama aliyekwepwa na ninyi mliokuwa ndani ya gari. huyo anatakiwa kuwa dereva wa kwanza kupewa leseni ya juu katika mfumo mpya leseni baada ya serikali kukusudia kufuta leseni zote.
ReplyDeleteIla pia anaonekana hakuwa kwenye mwendo wa kasi maana hata chombo hakijaharibika hapo ni kubinua na kuendelea na msafara.
Mungu awaepusha watanzania na ajalizenye maafa. Amin
bwana michuzi huyu jamaa ninampata sana,anaitwa a.k.a mzee sengasu,anapiga job pale kahama mine,baada ya kumaliza udsm miaka michache iliyopita,si mchezo hayo maeneo anayotaja yanapanda sana kabla sijaja ughaibuni.
ReplyDeletemzee Rabson pole kwa ajali hiyo,bado upo kahama? mbona umepinda kidogo vipi mzee?
madereva wa bongo bwana, mchana mzima huwezi kumuona mtu yuko na baiskeli kati kati ya barabara ukapunguza spidi? au ndo ubabe wa njia
ReplyDeletePoleni sana kaka zangu, lakini pamoja na mikanda pia Mungu alikuwa bado anawahitaji duniani. Poleni sana
ReplyDeletePoleni sana na tunashukuru mlisalimika. Lakini wangetakiwa kuwa na sheria ya seat belts kwa kila biria kwenye magari ya kawaida.
ReplyDeleteNinaishi NJ na kuna law ya click oor ticket fine mpaka $200. Kwa hiyo ukija NJ kila mtu an seat belt. Na kwa vile kama wee dereva na abiria wako wako under 18 unapigwa ticket wewe. Hivi kila mtu yuko macho macho. Ila cha kusikitisha ni Govenor wetu alivyopata ajali na hakuwa amevaa seat belt..Ilikua noma kishenzi. Lakini alilipa fine
We anony hapo juu acha ulimbukeni ..eti oo ninaishi NJ..governor WETU.. we huyo ni gavana wako kivp? we ni m-bantu unatoka ktk top ten ya nchi masikini duniani huo ndio ukweli utakaobakia. usijipendekeze huko eti ooh governor wetu, huyo ni governor wa wamarekani weusi na wazungu limbukeni wewe. Nyie waafrika sasa ni wakati wa kuamka jamani
ReplyDeleteHuko Nyujese si ni ndio gavana wenu alikuwa anasafiri huku akiendashwa na polisi wakati hajavaaa mkanda matokeo yake alipopatwa na ajali akavunjika vunjika.
ReplyDeleteWe mdau wa michuzi endelea kufunga mikanda na Mungu pia anakupendeni maaana hata hiyo mikanda saa zingine ndio hio hio inayokunyonga shingo mara ajali ikeapo. All in all ukifunga mkanda unakuwa angalau salama zaidi kuliko kutoufunga kabisa. Il amikanda ya ndege mmmh mie huwa nafungaga tu kufuata mkombo manake hata yale maelekezo yao ya nin cha kufanya ikitokea ajali huko anangani kwa sipidi yao wanavoeleza mie huwa siyaelewi kabisaaaa badala yake natumia muda huo kusali Mungu aepushe lolote baya liwezalo kutokea ktk chombo iko cha usafiri
Michuzi,
ReplyDeleteNinampa pole huyu jamaa lakini ukweli ni kwamba deleva wa hiyo gari alikuwa ni mzembe. Sheria inasema lazima uwe umbali ambao chochote kikitokea unaweza simama bila tatizo. Hiyo ni hapa marekani au bongo sasa had this guy kept his distance hayo yote yasingetokea. Pia inaelekea spidi alikuwa anaendeshea ilikuwa haiendani na mazingira--had it been so angeweza simama bia tatizo. For the same reasons nimekwisha wai angusha gari bagamoyo, huko sikupewa adhabu kwani niliongea fresha na trafic. PIa for the same reason niligonga mtu wa pikipiki hapa states---jamaa alikuwa anacheza barabarani na akasimama gafra---nilipata ticket ya $90 for following too close and my insurance had to cover his bike.
so jamaa pole sana lakini kosa ni lako---na utakuwa na bahati kama trafic hawatakulima zaidi coz they should kwani umehatarisha maisha yako na ya airia uliobkuwa umebeba.
KJ-204
Pole sana kaka. Kusema kweli kuendesha gari Bongo ni kama ndoto ya jinamizi. Dereva unatakiwa uwe muangalifu ujikinge kutokana na madereva wengine, wapanda baiskeli na waendao kwa miguu, hasa ukiwa katika barabara za kuelekea mikoani. Mara nyingi, hasa waendesha baiskeli wana tabia ya kurudi barabarani gari moja likiwapita, bila kujali kuwa kuna magari mengine yanakuja. Ukimpigia honi, yeye anakuonyesha ishara ya 'pita tu'! Unakuta jamaa anaendesha baiskeli kapakia mzigo ambao umetokeza hadi nusu ya barabara! Mambo!
ReplyDeleteHey kwani nikisema govenor wangu kinakuuma nini? Jamani watanzania!!! I am a legal citizen and I pay my tax. Sasa sijui tatizo liko wapi....Wewe kama hutaki shauri yako but he is my govenor na nilimpigia kura. Sasa sijui lipi nilikosea...
ReplyDeleteMichuzi wee
ReplyDeleteMpe jamaa pole!
Cha kufanya hapo nikuomba washikaji walisukume na kuligeuza upande wa kushoto ili kioo cha dereva kisivunjike likae wima tena. Aangalia kama tenki la mafuta halijatoboka na kwa vile siioni kama kuna vioo vilivyovunjika basi ni kuwasha moto na ngoma itakubali tu. Hakikisha ukifika mjini uwaone wale mafundi wa kunyoosha vyuma.
Hilo likilala hapo .....
All the best !!
jamani kwani tena blog ya michuzi mekuwa ukumbi wa malumbano? kila mtu ashike zake jamani.
ReplyDeleteDogo pole sana. Inawezekana ni matunda ya defensive driving hayo!
ReplyDeleteTulikuta jioni pale mess lakini hukuniambia kuwa kulikuwa na disaster ..au ndio ulikuwa unatafakuri baado?
Nadhani kwa mtindo huu utaratibu wa kupumzika Geita kila weekend utaubadili make hata hiyo njia si nzuri. Jaribu hata Kahama town siku 1..1 panalipa tu halafu kunaendeka.
Hivi hivi tulikuwa tunawapoteza, Jamani!!!!
Pole!
Wabongoo wivuuuu wakiona mbongo kawa raia wa nchi nyingine hawapendi kusikia. Afadhali umempa ukweli wake kwani nani kamwambia wamarekani weusi na wazungu tu ndio raia wa huku. Jinga hilo halina akili.
ReplyDeletePole uliyepata ajali
Kaka Michuzi Vatican imetoa amri 10 kwa madereva na watumiaji wa barabara nadhani itakuwa vyema ukiweka ukurasa wa mbele kabisa huenda ikasaidia hasa ukizingatia ajali ambazo zimejitokeza ndani ya kipindi hiki kifupi cha mwezi huu.
ReplyDeleteNawasilisha.
THE HIGHWAY TO HEAVEN
1 You shall not kill
2 The road shall be for you a means of communion between people and not of mortal harm
3 Courtesy, uprightness and prudence will help you to deal with unforeseen events
4 Be charitable and help your neighbour in need, especially victims of accidents
5 Cars shall not be for you an expression of power and domination or an occasion for sin
6 Charitably convince the young and not-so-young not to drive when they are not in a fit condition
7 Support the families of accident victims
8 Bring guilty motorists and their victims together so they can experience forgiveness
9 On the road, protect the more vulnerable party
10 Feel responsible towards others
Jamani watanzania hivi huyo anony angesema anaishi tunduma au sehemu yeyote ungemuita limbukeni. Watanzania mnamind ndogo sana. Manazania kuishi nje ya nchi ni beag deal sana. Kumbe wenzenu wanaona ni jambo la kawaida tu. sasa wewe anony 1.46 unamlipukia mtu kwa vile amesema anaishi sijui wapi. Ulimbukeni mnao nyie kwa tunaoishi nje ya nchi wala hatuoni ni la ajabu lolote.
ReplyDeleteWe limbukeni wa NJ na we anony wa 11.54, hapo hakuna cha wivu wala nini. Ukweli ni kwamba nyinyi ni wabongo tu na mtaendelea kuwa wabongo mpaka siku ya mwisho. Hapo NJ sijui wapi sio kwenu na wewe si mmarekani mweusi au mzungu. Utaendelea kubakia MLUGURU maisha yote na unatakiwa ujivunie. Kuhusu kulipa tax kila mtu anayefanya kazi huku mtoni analipa tax. Jiangalieni sana msije mkapoteza hata jinsia zenu.
ReplyDeletePole uliyepata ajali!!
Wasema sana tu lakini wengi walishakana uraia wa Tanzania na wengine wazaliwa huko sasa wasumbua wa nini? Wahindi wajiita watanzania hapa kila siku mbona hamuwafagilii. Walah waswahili mna maneno marefu sana. Siye macho tu lakini tabia yenu inasikitisha sana.
ReplyDeleteMind your business