wadau, blogu yenu hii imepata habari na picha kwamba wakati taifa staaz ikimenyana na senego juzi huko huko mwanza shindano la aina yake lilifanyika chuo kikuu cha mtakatifu agostino cha nyegezi (saut) ambako dada celina luhazo (akitoka kuchukua zawadi meza kuu pichani) alijishindia taji la 'saut decent girl 2007' na kuzoa kitita cha shilingi laki moja toka kwa waandaaji ambao ni walimu wa hapo. azma ya shindano hilo ambalo mpashaji habari anasema litakuwa la kila mwaka ni kuhamasisha kinadada wawe na tabia njema na pia kuendeleza mshikamano, upendo na tabia nzuri katiak jamii wanayoishi. masharti ya shindano hilo ni kwamba mshindani hatakiwi kuwa na rafiki wa kiume yaani boifrendi na awe mcha Mungu anayehudhuria sala kanisani na pia limelenga kuondoa tabia ya utoaji mamba, kutumia mihadarati na kuelimisha wanafunzi juu ya ukimwi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2007

    Thats excellent. Yaani dada mwenyewe anaonekana decent kweli kweli. Atakuwa Muha huyo! Good girl. God bless you.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2007

    Kwa hiyo Mshiriki/Mshindani akiwa na rafiki wa kike yaani Lesbian au Bisexual ni pouwaaa tu. Inajulikana sana hizi shule za boarding mambo ya Usagaji yanavyofanyika kila siku na tena siku hizi ni kama fashion. Nadhani waandaji waweke wazi vigezo vya hilo shindano na sio kutubania sisi Wanaume pekee.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2007

    Tamasha na changamoto ni nzuri lakini masharti yao hayana ukweli ndani yao.

    Kwanza wakumbuke kuwa hata mapadri wengi hawana girlfriends lakini kesi zao ziko mahakamani nyingi tu na wengi wana watoto kila kona.

    Pili ni umri gani wa washiriki? Msichana hatakiwi kuwa na boyfriend na wanaume je nao hawatakiwi kuwa na girlfriend?

    Kama ni below 20 yrs nitakubali lakini kama hata ukiwa above 21 basi usiwe na boyfriend huo ni uongo. Msichana atamfahamu vipi mwanaume kabla hajamuoa? Au ndio hiyo bado ukandamizaji wa wanawake kuwa wanawake hawana saying ya kuchagua mwenzi wake.

    Kuwa na rafiki wa kiume sio lazima sex itahusika. Labda kwa vile tunatumia lugha ya kizungu (boyfriend). Lakini mimi na amini unaweza kuwa na marafiki wa kiume wengi tu na bila kuhave sex at all. Na living example ni mimi mwenyewe.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2007

    mie nafikiri hili wazo la kutoa zawadi kwa msichana mwenye "tabia njema" ni la kipuuzi:
    1. msichana ambaye ana rafiki mmoja tu wa kiume-naye anaweza kuwa na tabia nzuri tu. Sema kwa sababu hicho chuo ni cha kidini-hakiruhusi mapenzi
    2) mie nafikiri wangesisitiza masomo zaidi ya tabia njema
    3) elimu ndio itamkomboa mwanamke sio tabia njema tu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2007

    Vilevile msichana anaweza kuwa na boyfriend na walimu wasijue. Mambo hayo hufanyika kwa siri na wakati mwingine usiku. Watakuwa wanamfuatilia kote huko? Mfano mzuri ni nyumbani-bint anaweza kuwa na boyfriend na wazazi wasijue, kufikia hata kupata ujauzito ndo wajiuliza ameupataje huyu.
    Walimu hao wanatuletea longolongo hapo. Sidhani kama zoezi hilo litakuwa linafanyika kwa haki, ufasaha na accuracy. I doubt!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 05, 2007

    "utoaji mamba". Michu hapo unamaanisha nini? mimi mswahili ninafahamu unaeleza nini lakini je kwa yule anayejifunza kiswahili si atachukulia kama ndiyo neno sahihi?
    Nafikiri ukiwa unaandika kitu ni vema ukisome ndipo ukipeperushe kwa wanabblog. na hili tatizo unalo sana. angalia siku unaweza kuandika matusi badala ya kuweka n ukaweka m.
    NOPE

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 05, 2007

    Jamani nikakipeleka hicho chuo mahakamani.

    Mimi ni mwanamke bikira kabisa sijawahi pata mimba wala toa mimba hata wanablogu mkitaka nifunue mhakikishe kuwa mimi bikira naweza funua muone kama michuzi ataruhusu naweza waonyesha.

    Sina bwana chuoni na nilikuwa nasali sana ila sisali hapo wanaposali hao mapadri nasali kwenye dini yangu mjini sababu dini yangu iko mbali haipo hapo hivyo hawanioni hao mapadri sababu ninakoenda wao huwa hawaendi kutokana na tofauti za imani.

    Sasa mchumba wangu ambaye ni mdogo wake Issa Michuzi aliyetaka kunichumbia katoroka baada ya kuona hii picha na maelezo yaliyoambatana na hii picha..

    Anasema ana ushahidi kuwa nilikuwa na mabwana wengine,nilishatoa mimba,na nilikuwa na tabia mbaya,na ni kafiri wa kutupwa nisiyejua tofauti kati ya Mungu na Ibilisi ndiyo maana nilikosa hiyo zawadi!

    Wasichana wote tuliobakia tunaonekana kwamba ni wapenda ngono! na mfano mbaya usiofaa kuigwa!mapadri mna mambo!

    Nimechafuliwa jina langu!na hiki chuo wallah!

    Tunaomba shindano hili lililokaa kimfumo dume safari ijayo lifanyiwe marekebisho ili litupatie mwanaume bikira ili tumjue!Hata kama ni padri tuonyeshwe!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 05, 2007

    hii chata ya iringa hii

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 05, 2007

    mhh!!! kusema ukweli labda alipoenda huko st. augostino ndio akaamua kutokuwa na boyfriend lakini before................

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 05, 2007

    Kweli huyu dada anaonekana mtiifu maana anaona haya kuangalia watu. hii ni tofauti kabisa na akina dada ambao washafurahia utamu wake! wangekuwa na sura kavu ka dagaa! I like that

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 05, 2007

    wamesahau kigezo kimoja muhimu saaaaaaaaaana,awe bikira.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 05, 2007

    we anon unayesema ni mha huyu,kakwambia nani?huyu anaonekana ni mhehe bwana (ah!we fanya tu,sambi sako mwenyewe!)

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 05, 2007

    Lazima awe na tabia njema. Shape ziro nani atamhitaji? Sijui labda taster wetu "M.I.M".

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 05, 2007

    anoy 4.20 speak for yourself
    kwanza wenye kuangalia chini ndio wabaya sana.

    Nina binamu yangu alikua mpole kama nini. ukitaka kwenda kwenye party ukienda naye hata mkichelewa kurudi hamtagombezwa na waazazi...yaani sauti yake ya upole na watu wakajua huyu ndio mtoto mtakatifu kweli...bomu lilikuja alipopata mimba kila mtu macho wazi..Siye tuliokuwa tunaonekana vicheche bado bikira zipo mpaka kesho

    Usimjudge mtu kwa jinsi anavyoweza kusocilize na watu wengine..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...