nimefurahi leo kikutana na senpai wangu geoffrey shoo mahakama kuu leo hapa dar. huyu bwana ana mkanda mweusi wa karate staili ya goju ryu. ukimwangalia vyema utakuta ana makovu karibu mwili mzima. makovu hayo ni ya ushujaa. acha niwasimulieni...
senpai shoo alipata ajali ya moto siku moja na kuungua karibu mwili wote. na baada ya kupata ajali hiyo ilibidi apelekwe hospitali kwa matibabu ya haraka. bahati mbaya hakukuwa na usafiri, hivyo yeye na senpai ilungu aliyekuwepo baada ya ajali, wakaamua kupiga mbio kama alivyofanya umsolopagazz alipompandisha allan quatermain juu ya farasi na kupiga mbio.
kitendo hicho kilichotokea miaka ya 70 huko kiliokoa maisha ya senpai shoo na kutudhihirishia wanafunzi wake wa sanaa ya kujilinda kwa mikono mitupu kwamba kwenye shida, weka moyo wako juu. yaani pamoja na kuungua vibaya alitroti kiasi cha kilometa 10 hadi hospitali ya muhimbili kupata matibabu.
tukio hilo la kishujaa limempatia heshima ya kipekee senpai shoo ambaye kwa sasa anachukua shahada ya sheria udsm na kapania kufanya mtuhani mwakani na kuwa wakili wa kujitegemea. ni watu wachache ambao wangeweza kufanya kama yeye, kupiga mbio akiwa ameungua vibaya mwili mzima badala ya kusubiri usafiri. hongera senpai shoo, najivunia kuwa mwanafunzi wako hususan pale ulipokuwa ukitusaidia sie wanafunzi wa awali pale zanaki, ukisaidiana na senpai ilunga, senpai heri, senpai mbezi, senpai (marehemu) bofu, senpai mkekena, senpai malekia, na ma-senpai wengineo wengi tu. hapo simsahau senpai magoma nyamuko ambaye hana mfano katika fani hii. sote tulilia ilipobidi uhamie moshi ambako uliendeleza libeneke pale ymca.
nakumbuka ulivyokuwa ukitufundisha nguzo kuu za ukumbi wa mafunzo (dojo) na nidhamu ya kupiga deki ukumbi kabla ya kuanza tizi. sisahau jinsi ulivyokuwa ukituimbisha nyimbo wakati wa mazoezi ya kukimbia mitaani tukiwa pekupeku. na je, unakumbuka wewe ndiye uliyenifundisha kwa mara ya kwanza aina ya stensi, mirusho ya mikono na miguu, na pia kucheza kata kama geki-sada-ichi na geki-sa-dan na pia zile ushiro, mawashi na nsanzu geri?
wadau naomba mnisamehe kama leo napitiliza. huyu mtu kanikumbusha mbaaaaaaaali. noamba mumone kama alivyo; si mtu wa kawaida....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 14, 2007

    duh huyu jamaa ni shujaa kweli kweli, kwahiyo na wewe michuzi una mkanda gani? maana umesema ulikua mwanafunzi wake au unatutisha tu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 14, 2007

    Sasa michuzi mbona tunafungana kamba sana ndugu yangu, huyu jamaa ni Senpai wangu kwa muda mrefu toka pale moshi YMCA na sikumbuki kama darasani tulikuwa na mtu kama wewe, au mwenzetu wewe alikuwa anakufundishia nyumbani kama tution.aah kama hivyo sawa sawa nitakuwa nimekuelewa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 14, 2007

    Naona leo Michuzi umeandika ujumbe wako kwa heshima sana inaonekana huyu jamaa alikupiga mitama kupita kiasi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 14, 2007

    New Zealand, Geofrey alianzia Zanaki kabla hajaja dojo la Moshi - YMCA. Akiwa Zanaki ndiyo alimfundisha Mi-soup.

    Mi huyu jamaa namfahamu pia kwa kuwa alinifaa sana kwa chakula cha kuku pale Moshi miaka ya 80s. Kama sina usafiri alikuwa akipeleka order yangu kwa pikipiki yake hadi nyumbani.

    Kweli tumetoka mbali. Michudhi, mpe salamu sana.

    ReplyDelete
  5. Sempai Magoma Nyamuko yuko wapi?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 14, 2007

    MZEE WETU WA MOSHI SOWETO NA DOJO LA PALE YMCA MAISHA MEMA.....HUJABADILIKA MZEE !!!!.....MARK(NDUGUYE MASHAKA WA USHIRIKA NA KHALIFA WA MTAA WA CHINI) UP000000000 !!!!!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 14, 2007

    Sir ISSA HABARI YA LEO KAKA..KAMA ULIVYOMUELEZEA HUYU ..SEMPAI.."..WASIFU WAKE WANJE..." ..TUNAUONA..AKSANTE.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 14, 2007

    Kaka Michuzi unanikumbusha mbali sana enzi zetu za YMCA na DarTech. Msalimie sana brother na mpe salaamu zangu. Salaam toka Dallas,TX

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 14, 2007

    Do!Michuzi ndio unataka kutuambia watu wakuogope n a sio kukuingia kiasarahasaran maana wataumia!
    Ongera mkubwa maana nimeanza kukufahamu siku nyingi tokea miaka ya themanini kweye mitaa ya Mazengo(Upanga)hila sijapata kukuona kwenye mazoezi Zanaki,anyway ongera Sempai Michuzi.

    ReplyDelete
  10. Jamani nagombea nafasi ya ukatibu jumuwata - naombeni kura zenu ili tuweze kushirikiana katika kuleta mapinduzi ya upashanaji habari. Uchaguzi utafanyika tarehe 30 Juni 2007.

    Anuani ya Blogu ya JUMUWATA ni: -
    http://www.blogutanzania.blogspot.com

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 14, 2007

    Michuzi mbona nilivyokuwa nakuomba uweke picha za Sensei Bomani zile ulizokuwa ukipiga pale anaposhuka toka Unyamwezini na stori ulizokuwa ukifanya kwenye Sunday News hukujibu kabisa na wala hujawahi kugusia kitu. Vipi leo Sempai Shoo amekupiga Msubidachi nini? Au Mawashi geri? Hizo kata naona moja umechanganya, ni geki-sada-ichi na geki-sa-danii halfu seifa..kama kuhesabu ni .1ichi..2.nii ...3.sanii ...4.shii..5.goo..6.rokii--7.shijii..8.hajii..9.kuuu..10.juu

    "Nguzo za ukumbi wa mafunzo:
    1: Kwa uadilifu, Chunga tabia yako.
    mwili na fikra zako zile kitu kimoja.
    Mafunzo hayana mwisho."
    Sempai Heri Kivuli yupo wapi siku hizo? na Sempai Mbezi? Kulikuwa na jamaa mmoja anaitwa Benson? duh! jamaa hizo nguzo yeye anataka zisemwe kwa Lugha, ngeli babake sasa enzi hizo miaka ya 80s, 90s duh watu ngeli ilikuwa haipandi basi balaa tupu! Pia kulikuwa na sempai mmoja Mhindi nimesahau jina lake. Duh kweli tumetoka mbali..!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 14, 2007

    New Zealand nina wasi wasi wewe ni Sunday Pesa MR ARUSHA No. 90's au sio!!!!!????

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 15, 2007

    DO MICHUZI SASA UNAINGIA DEEP,MAANA SIKUTEGEMEA KITU KAMA HIKI HIVI KARIBUNI KWELI DUNIA MDUARA.HUYU MTU (SEMPAI)KAMA MASHUJAA BASI HUYU NI MMOJA WAO NINAMAANA HISTORIA YA AJALI YAKE NA MPAKA ALIVYO SASA NI MFANO HAI KWA WATU WENGI,SIO KAMA NASIFIA HAPANA KWA SABABU NAKUMBUKA ALIPOPATA AJALI HIYO ALIKUWA KWENYE GARAGE YAKE ILALA MOTO ULITOKEA NA MLNGO WA KUTOKA ULIKUWA MMOJA TU,WAYU WALIJARIBU KUVUNJA DIRISHA IKASHINDIKANA NA MLANGONI KULIKUWA NA PIKIPIKI NAPIPA LA MAFUTA VYOTE VINAWAKA MOTO NDIPO ALIPOAMUA KWAMBA HAKUNA JINSI NI KUPITA KATIKA MLANGO ULIYOKUWEPO BILA KUJALI MAUMIVU NA MAANA UNAMWONA SASA NDIO ALIVYO.NA CHA KUFURAHISHA NI KWAMBA ALIPOKUWA HOSPITALI ALIKUWA HAPENDI UUMWONEE HURUMA ANATAKA UKIFIKA KUMWANGALIA UANZE KUTANIANA NAYE KAMA AKIJAMTOKEA KITU CHOCHOTE(TULIKUWA TUNAMWAMBIA KWAMBA AMEKUWA HANGSOME KWELI NA MABANDAGE YAKE HAPO MUHIMBILI)

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 15, 2007

    Kaka Pori, nimeenda kwa blog yako CV yako kali: SINGLE with 1 KID

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...