jk akipozi na wahariri wa habari wa vyombo mbalimbali akiwa na waziri wa habari, utamaduni na michezo mh. mohamed khatib (wa nne shoto mbele) na naibu wake mh. daniel nsanzungwanko (shoto kwa jk) ikulu leo katika utaratibu aliojiwekea wa kuongea na taifa kwa njia tofauti. leo amelihutubia taifa kupitia wahariri ambapo amesema vyombo vya habari ni nyenzo muhimu katika kufikisha ujumbe. mada kuu za jk leo zilikuwa utoro na mimba mashuleni pamoja na gonjwa la ukimwi ambapo ametaka kila mmbongo ajitokeze kupimwa ngoma kwa hiari ili kujua statasi yake na kuisaidia serikali katika kutoa huduma kwa waathirika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

 1. AnonymousJune 07, 2007

  Mimi sio staiisti wala nini lakini hii staili ya JK inachosha. Sijaona raisi akaitisha mkutano na kuvaa huu upuuzi. waachie watu wa fleva na wanamichezo wavae hivyo.

  ReplyDelete
 2. AnonymousJune 07, 2007

  inaonesha jinsi mfumo dume ulivyokomaa vyomboni vya habari... hakuna wahariri wanawake, isipokuwa hao wawili tu, tena nadhani wanatoka majarida maalum ya wanawake. TAMWA mpo??

  ReplyDelete
 3. AnonymousJune 07, 2007

  Mie nampongeza yule tu wa gazeti la MwanaHalisi aliyeuliza swali kuhusu "Mr. Clean" na Kampuni yake. Nakufagilia babake!
  Wengine wote WAOGA nyinyi!

  ReplyDelete
 4. AnonymousJune 08, 2007

  Wanawake wanachallenge sana...ndio maana wamewaweka wawili tu....Hawa wote unawaowaona ni yes sir people.

  Put women and see how the job will be done..

  ReplyDelete
 5. AnonymousJune 08, 2007

  enyi wahaririwatukufu,mi naomba mnijibu swali moja kupitia hii blogu.JE MMEKAMATISHWA KITU KIDOGO NA JAMAA WA TBS/WTM? HOW COME STORY YA UTAPELI WA HAWA WATU HUKO UINGEREZA MNAIBANIA?HAMUONI KWAMBA NI SERIOUS STORY?AU MPAKA WATU WAANDAMANE WAPIGWE VIRUNGU NA WENGINE LABDA WAPIGWE PI HUKO UK NDO MSHTUKE NA KUANDIKA.ACHENI HIZO UR GROWN UPS!

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...