gavana wa benki kuu mh. daudi balali amemaliza mkutano wake na waandishi wa habari hivi punde na kwa haraka haraka nawapa pinti kadhaa za yaliyojiri.

1. Kuhusu tuhuma dhidi yake katika mtandao kasema ni za uwongo mtupu na hazina ukweli wowote na unatokana na watu ambao wanagombana ama wanagombania kitu, na kwamba mwandishi wake ni 'selfish' na ana 'malice' pia. na pia kasema kama kuna waliozoea kukopa na kutorudisha huko zamani sasa inabidi wafanye financial adjustment na akikopa na kushindwa kulipa benki inambana na akija kwa gavana hatopata msaada kwani ndo hali halisi. na kwamba hawezi kuongelea zaidi kwani jambo lenyewe ninafanyiwa uchunguzi na serikali.

2. amesema hawezi kujiuzulu ili kupisha uchunguzi unaoendelea kwani haiwezekani mtu akaachia ngazi kwa tuhuma na uzushi ambazo sio tu hazina uhakika bali zinachunguzwa ili ukweli ujulikane.

3. Kuhusu gharama za ujenzi wa twin tawa kasema amesema hizi tuhuma na kelele zipo wazi kwenye ripoti ya matumizi na ziko wazi kwa kila mtu kusoma. amesema pia hazikuanza leo bali toka 1984 jengo la zamani lilipomalizika ambapo gavana wa wakati huo hayati nyirabu alipigiwa kelele kuwa kavuta, hivyo ujenzi ukasismama. gavana rutihinda naye alijaribu lakini kelele kama hizo, amesema, zikafanya ujenzi usimame tena, pia, aliongeza, gavana rashid alipokuja naye alijaribu kupanua ujenzi wa benki kuu, lakini ujenzi ukasimama kwa tuhuma za aina hiyo hiyo. anasema alipokuja yeye mwaka 2000 amefufua mradi huo baada ya uchunguzi kufanywa na kukutwa tuhuma za uwongo baada ya upelelezi kuhitimisha kazi yao.

4. amesisitiza haya sio mambo mapya na yamekuwa katika benki kuu kwa miaka takriba 20 sasa. na amesema kama kuna mtu ambaye ana ushahidi wa kwamba kuna mtu ni mhalifu aletwe na ushahidi ili achukuliwe hatua na kwamba hawezi kufanyia kazi tuhuma na uzushi. alisema kwamba yuko komfotebo sana tu, hali yake nzuri na anaendelea na kazi kama kawaida, baada ya kuulizwa anajisikiaje-sikiaje kisaikolojia kufuatia hizo tuhuma kwamba yeye na washikaji kibao wamevuta.

5. pia amesema huyo mtu ambaye kasambaza waraka kwenye mtandao hamjui ila alimtaja kuwa si mzalendo, ana chuki binafsi na mbinafsi. 6. gavava bilali pia alizungumzia hali ya uchumi ni nzuri na kwamba hali ya inflesheni hadi jaanuary 1995 imedondoka hadi asilimia 9.1 na ilipanda hadi asilimia 6.1 hadi April 2007 na kufikia 5,0 mwezi mei mwaka huu.

7. pia amesema akiba ya taifa ya fedha ya kigeni imepanda toka dola 270 milioni mwisho mwa 1995 hadi kufikia dola 2,260 milioni ambayo inatosha kukava kwa angalau miezi 5

8. amesema pia kafurahishwa kwa uteuzi wa manaibu magavana wengine wawili kufuatia mapendekezo yake ya muda mrefu ambapo sasa kuna watu wanne akiwemo yeye na manaibu wake watatu akisema hii itasaidia kurahisha baadhi ya kazi.

WADAU MKUTANO UMEDUMU KWA DAKIKA 90 NA SIWEZI KUELEZA YOOOOOTE KWA SASA NA NDIO MAANA NIMEWEKA YALE YENYE KUTAKIWA KUJULIKANA NA MAPEMA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 58 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 12, 2007

    Bomba sana Michu, nilikuwa nakusubiria utupe vitu vya huko! Kwa kweli point moja tu ni kwamba huyo jamaa anayesambaza huo waraka sio mzalendo! Mi nimeuona na unaoneka kuandikwa na wale wenye asili ya...!

    Mi namsapoti 100% Gavana achape kazi aache majungu yapite!!!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 12, 2007

    Hata mie ningesema ni uzushi. Thanks Misoup for flashy update.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 12, 2007

    Asante Michu kwa Taharifa.

    Vipi kuhusu zile pesa zilizopotea kwenye account ya NJE hata IMF nao wanamsingizia?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 12, 2007

    JAMANI TUMECHOKA MBONA TUNAFANYWA HATUNA AKILI. KILICHOMFANYA SIKU ZOTE ASHINDWE KUONGEA NINI? AU NDIO ALIKUWA ANAPATA USHAURI WA KISHERIA KWANZA. BALALI HELA ZA WAFUJA JASHO HIZO HAYA.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 12, 2007

    UNAFAHAMU TANGU JANA ULIPOTOA PICHA YA BILALI NA KUANDIKA BREAKING NEWS, NILIDHANI JAMAA AMEKUFA AU MEJIUZULU WADHIFA WAKE.
    NILITAKA KUKUELEZA KITU KIMOJA TOFAUTI YA BREAKING NEWS NA PRESS CONFERENCE.
    HUYO JAMAA TAARIFA YAKE YA KUKANUSHA KASHFA DHIDI YAKE, HAIWEZI KUWA BREAKING NEWS HATA KWA MIAKA ELFU KUMI IJAYO. HIYO NI TAARIFA YA KUKANUSHA NA ITABAKI HIVYO.
    KIFO CHA AMINA, HIYO ILIKUWA BREAKING NEWS.
    SIMBA KUTWAA UBINGWA; HIYO NI NEWS ALERT.
    NIMEKUPA MIFANO MICHACHE TU LAKINI KUNA TAARIFA NYINGI UMEKUWA UKITOA KWENYE BLOG YAKO UKIZIPA KICHA CHA BREAKING NEWS.
    TUMIA NEWS ALERT AU UMBEYA ALERT KWANI HUKO KWENU KILA KITU UMBEYA.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 12, 2007

    Bilali amejibu tuhuma because ilibidi ajibu asingeweza kukaa kimya. Ila from your report, Issa, inaelekea issues hazija kuwa addressed bali ni kama vile ame-zipersonalise. Whether huyo mtu au watu ni malicious au selfish au wana chuki binafsi (sounds familiar...) siyo 'issue'; yale mambo yaliyotajwa ndio concern ya wa-TZ. Pengine sio kweli lakini kwanini tuhuma kama hizo zi-surface? Kama watu wanakopa pesa nyingi hivyo bila kurudisha au wanajaribu ku-fix papers ili wasirudishe(typical behaviour ya wengi wetu), basi ni tabia ambayo haifai kabisa and such people (if he knows them) should be brought to task. Ni wezi!! Ubadhilifu wa pesa za umma umezidi whether justified or not and someone has to pay for that.

    Kuhusu jengo, kuwepo kwa cost kubwa ya ujenzi, na kuwepo kwa accounting nzuri inayo onyesha kwamba hamna pesa iliyoibiwa hai-justify BOT kujengwa kwa hela zote hizo! Tatizo ni watu wanafikiri wa-TZ ni wajinga, waki-raise issues wanafanya hivyo kwasababu wana chuki binafsi, au hawana kazi nyingine bali kusemasema tu which is an insult to our intelligence! If Bilali is as good as other people have said (alikuwa sijui advisor wa World Bank) basi hiyo response yake kama alivyoandika Issa ni 'below standard'. Unless of course iwe kwamba majibu yake yataingiliana na uchunguzi.

    How can 'tuhuma za matumizi mabaya' ziwe tuhuma za uwongo na kama upelelezi umonyesha ni za uwongo, we don't know that. Wa-TZ hatumnyoshei kidole Bilali, as such, tunasema kwamba 'SOMETHING IS WRONG! AND THIS WRONG THING SHOULD BE ADDRESSED!
    Samahani kwa ku-mix lugha but I am sooo pissed off!!

    ReplyDelete
  7. @Michuzi,
    Summary ya maongezi ya Gavana ni hii: blah blah blah...

    Hakujibu hoja ya msingi. Aliyetoa tuhuma juu ya Gavana hakusema kwamba jengo la Benki Kuu lisijengwe, bali alisema GHARAMA ILIKIUWA KUBWA kuliko sehemu nyingine duniani. Kwa kifupi Gavana hakutoa comparative analysis kujustify majengo ya Benki Kuu kujengwa kwa gharama kubwa. Sana sana, alichosema ni blah blah blah.

    Hilo ni moja tu, mengine ni unafiki. Kama vile "kufurahi kuteuliwa kwa manaibu magavana". Really? We all know what that means - it is a clear message to Balali that he is either incompetent, au siku zake zinahesabika.

    Anazungumzia uzalendo. Does he really know what uzalendo means? Yaani Bongo kweli maajabu. Wezi ndo wazalendo?

    Na hii ya "waliozoea kukopa na kutorudisha". Hivi ni wangapi hao? Halafu kuna suala la "mazoea". Ina maanisha kuna watu lukuki walifanya BoT kama kapu lao. Na Balali alikuwa anawasapoti, ila noma ilipofumuka anajifanya kwamba hao "waliozoea" wafanye "financial adjustment". Sasa Mzindakaya atafanya "financial adjustment" ipi, wakati BoT wamesaini kumpa udhamini wa mkopo benki nyingine?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 12, 2007

    Wewe Michuzi usiwe kama haupo kwenye karne ya ishirini na moja tuwekee clip hiyo tuone, sio kusema mambo mengi na mazungumzo yamedumu muda wa dakika 90. Kama huwezi muulize MK atakuelekeza jinsi ya kuweka link ya video tumwone mwenyewe kwa mamcho yetu huyu baaa-laa-lii. Ni hayo tu. Asante.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 12, 2007

    Huyu jamaa, kapotezea watu muda wao tu, kwani majibu yake ni ya kisiasa zaidi kuliko tuhuma zilizopo. Swali ni je anahusika yeye au na mekewe na hayo makampuni aliyohusishwa nayo? Swali ni je gharama za ujenzi huo ni halali? kwani kuna majengo mengi kama la PPF na Mafuta kwanini hayapigiwa kelele?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 12, 2007

    He he he, Mh. Balali umefanya kazi ambayo hakuna governor wa tanzania ambaye amewahi kufanya kuwa na reserve ya kutosha na kupunguza inflation toka uwe mshauri wa rais mpaka sasa govenor.Naona wahindi watajuwa kwamba watu weusi sio wajinga kama waliotangulia maana wakati mwinyi walikuwa wanakopa tu hata kama wanamadeni na hawalipi ela za watanzania. Nakutakia kazi njema mheshimiwa

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 12, 2007

    Duuh!! Yaani huyu jamaa ni mzushi. Ina maana hizo habari watu wamezitengeneza from A to Z? Unajua ni rahisi kusema hivyo kwa sababu ana cover up ya serikali au watu fulani wakubwa serikalini kwa manufaa binafsi wanashirikiana au wanajua nini kinachoendelea. Ukiomba hizo gharama za ujenzi wa BOT utasikia stories.
    In short jamaa wamekula vya kutosha na hatishwi na yeyote kwani anaokula nao ndio wanamlinda. Hii nchi imekwisha. Wanasema tembea mendo wa pesa nchi imeshauzwa. Wanachojua ni kuwa Watanzania wanapigaga kelele mwisho wake wanakuwa kimya kwani wameshazoea. Na kuanzia raisi wetu, makamu, waziri mkuu na baraza lao la mawaziri hawana nguvu yoyote ya kutetea masilai ya wananchi. TUMEKWISHA ila nasema MUNGU yupo mtakufa kifo kibaya sana. Nawaombea mfe kifo cha aibu wezi nyie

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 12, 2007

    Siku hizi presi konferensi nje nje; Wataliki wakitaka talaka -Presi knoferensi. Zikikutiririkia tuhuma -Pres konferensi.Rais akitaka kukemea utoro mashuleni, presi konferensi.

    Mtindo wa presi konferensi mzuri kwa sababu kwanza unakupa pablisiti, unakupromote, unakufagilia halafu unakuosha.

    Muhidin, waandishi na wapiga picha wengine, ombi langu kwenu ni kwamba hili dili la presi konferensi lisiwe kwa vigogo tu na jamaa waliopo kule Keko, Segerea, na rumande zingine pia samtaimz muwe mnawatokea na makamera, video, tepurekoda,na vimemo nao pia mnawapa presi konferensi.

    Inawezekana Mheshimiwa Ukiwaona Mzuzuri Ditopile naye anatayarisha presi konferensi lake. Sijui na Rais Mstaafu Mheshimiwa B W Mkapa na foma festi Ledi Mama Anna Mkapa nao pia wataitisha presi konferensi? Gavana Balali katoa pointi nane za nguvu sijui watakaofuata watatoa pointi ngapi?

    ReplyDelete
  13. Asante Michuzi kwa dondoo hii.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 12, 2007

    Hayo ni ya Gavana Balali. Watu watayafanyia uchunguzi zaidi!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 12, 2007

    Kaka Michuzi

    Tunashukuru kwa update kuhusu mkutano wa mkuu wa chombo cha fedha na waandishi wa habari.Kwa mara nyingine tunashuhudia vile waandishi wa bongo wanavyokosa udadisi wa kutosha kwenye mambo yaliyo sensive.

    Kwa mujibu wa dondoo zako, mimi naona kama mkuu wa chombo hajajibu tuhuma dhidi yake na badala yake ametoa majibu, sisi huyaita ya kisiasa. Unless haujatuletea yaliyokuwa yanatarajiwa na wengi.

    Kwanza hauwezi kujibu tuhuma nzito kama hizo kwa kusema ni za kizushi bila kusema ukweli ni upi.

    Pili hauwezi kujibu tuhuma za ujenzi kwa kusema kelele zimeanza siku nyingi bila kusema , pamoja na kelele zile gharama halisi ni kiasi gani kulinganisha na zinazosemwa kwenye hizo tuhuma

    Tatu, hakugusa kabisa issue ya Foreign Debt Account ambayo inasemekana imefujwa vya kutosha

    Nne kama anasema serikali inachunguza tuhuma zake, kwanini aseme kuwa ni za kizushi, ina maana serikali nayo inafanyia kazi uszushi?

    Tano, kwanini asijiuzulu wakati anafanyiwa uchunguzi na serikali iliyomwajiri?

    Sita, anasemaje kuhusu IMF kuagiza uchunguzi ufanyike nao ni wazushi au?

    Saba, anasemaje kuhusu waziri wa fedha ambaye aliliambia bunge kuwa tuhuma zinachunguzwa, naye ni mzushi?

    Kwangu mimi balali bado,bado hajatoa jibu, na wito wa kujiuzulu uko pale pale.

    Sele

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 12, 2007

    ATM ZA BENKI YA CRDB KUNA WATU WAKIKUCHUKULIA CARD YAKO, WANAPATA PIN NAMBA YAKO BILA YA WEWE KUWAAMBIA AU KUJUA NA KUKUIBIA HELA ZAKO !! HII IMESHATOKEA MARA NYINGI TUU, NA WAHUSIKA WAMELIFUMBIA MACHO HILI.LAZIMA KUNA WATU WA NDANI WANASHIRIKIANA NA WEZI.TUNAOMBA UONGOZI ULIFANYIE KAZI

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 12, 2007

    Watanzania wanazidi kuibiwa jamani huku wenyewe wamezubaa kama mazumbukuku. Huyu jamaa hajajibu tuhuma zezote zinazomhusu yeye katika hiyo Press Conf yake.

    Kama hakuna wizi au ubadhirifu BOT, kwa nini serikali inahangaika kutafuta Auditors na wachunguzi wengine kutoka nje?? Si kila kitu kiko shwari jamani??

    Je Foreign Account pesa zilizopotea zimeenda wapi?

    Je ame-justify vipi gharama zote kubwa hizo za majengo ya BOT?? Je ametoa ulinganishi wa gharama za majengo kama ya BOT na sehemu nyingine duniani.

    Je gharama za kusafisha vifaa mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo zilikuwa kiasi gani??

    WABONGO SASA AMKENI JAMANI NCHI NDIO INAMALIZWA NA HAWA WATU.

    Richmond tumeambiwa hakuna rushwa, Rada walisema hivyo hivyo kuwa hakuna rushwa, dili ya Ndege ya Rais nayo ilikuwa safi bila ya rushwa. Sasa kumbe nchi haina rushwa kwa nini kila siku Kikwete anapiga kelele kuwa moja ya malengo yake ni kumaliza Rushwa. Kweli Tanganyika ni ya Wadanganyika.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 12, 2007

    angalia mabongo humu yalivyokuwa marahisi kudanganywa...mengine yameashaanza kusingizia wahindi,shutuma ni majengo yaliyochukua $$ kupita kiasi na wizi mwingine sasa badala ya kuangalia hayo yamewageukia wahindi ambao hata hatuwajui...mimi nasema chunguza huyo balali deeeep na kama kaiba au kuna uzembe fungulia mashtaka na filisi mali yote arudishe,hao wahindi tutadeal nao kama kuna ukweli nao ni wezi ila sasa ni Balali

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 12, 2007

    Wanaodai kwamba Balali hakujibu hoja za msingi wanasahau kwamba yeye ana haki yakutojibu swali lolote, ukiachia mbali haki yake ya kujibu vyovyote atakavyo! Ni aibu kwa watanzania tunaposhindwa kuziheshimu haki hizi na badala yake kulazimisha Balali ajibu kama tunavyotaka, kana kwamba yuko mahakamani. Tuamke na kuheshimu haki za binadamu.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 12, 2007

    Michuzi ,

    Tatizo kubwa la waandishi wa habari wa huko nyumbani amjiaandai kabla ya kukutana na hao wakubwa. Mbona hamjamuuliza maswali ya msingi huyo bwana ... amfanyi homework zenu mnakimbia tuu kwenye mkutano bila ya kujua tuhuma .

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 12, 2007

    Nyie mnaosema balali ajihudhuru mnanishangaza.

    Balali hawezi kujiudhuru ati!

    Inatakiwa asaidiwe kujiudhuru

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 12, 2007

    Mbona anachachawa huyu?? asubiri basi tuone huo uchunguzi asitupe conclusions zake za kidwanzi...anyway mbona hao wa kumchunguza hatujatambulishwa au ndo wanatengeneza cover up?? Mungu pitisha radi wezi wote wakubwa kwa wadogo wafe kifo kibaya sana!!!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 12, 2007

    MI NAOMBA NIMSUPPORT ANONYMOUS NUMBER TANO...MY SENTIMENTS EXACTLY..MI NIKIWA MMOJA YA WATZ WANAOISHI INDIA..NI MUHIMU KURAISE CONCERNS KUHUSU HAWA VIONGOZI WETU KWASABABU NCHI YETU NI NCHI YA DEMOKRASIA..JAMANI NATAMANI MUONE JINSI HUKU INDIA VIONGOZI WANAVYOKUWA SCRUTINIZED NA WANANCHI WA HUKU WANACHACHAMAA KWELILKWELI..OUR GENERATION YA VIJANA SAHV WE ARE OUTSPOKEN AND MORE LIBERAL UKILINGANISHA NA WAZAZI WETU KWA HIYO WE SHOULD NOT BE UNDERESTIMATED IN OUR OPINIONS!!!!

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 12, 2007

    Kaka Michuzi huyu Jamaa mzushi tu,kwa nin amewakataa baadhi ya waandishi wa habari wengine kama sio kuna kitu kinafichwa?embu pitieni www.abdallahmrisho.blogspot.com muone yalioandikwa kuhusu huyu balali kugomea vyombo vya habari vingne,mana wameingia kwa majina kwenye mkutanao na wengine kuzuiliwa.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 12, 2007

    Waandishi wa Habari waulize! Kwani walikwenda kuuliza maswali ama kuambiwa nini cha kutangaza?

    Ni lazima tuwe macho. Waandishi wa Habari fanyeni "investigative reportage"! fanyeni homework" kwanza.

    Msiridhike na hayo yaliyojitokeza na kubandikwa kimatandao!

    Kuna network ya wattu wananyonya pesa za nchi!

    Kwa mfano, mtundiko uliosambazwa ki-Intenet, kuna majina ya baadhi ya Wahindi na makampuni yao ambao wana-donate maelfu ya mapesa na kadhalika katika kumsaidia Mbunge wa Musoma Vijijini na Wakili mashuhuri nchini (ambaye wakati mmoja eti alijitolea kutetea Benki Kuu iliposhitakiwa na foreign interests) kujenga mashule ya sekondari kwao Uzanakini:

    Chief Ihunyo National Secondary School - For Girls.

    Chief Wanzagi National Secondary School - For Boys.

    Busegwe Primary School.

    Oswald Mang'ombe High School.

    Butuguri Secondary School.

    Kuna pia mipango ya kuanzisha Chuo Kikuu cha Nyerere huko huko Uzanakini kitakachounganisha taasisi (kituo) moja ndogo iliyojengwa na Wa-Cuba kwa ajili ya afya ya ng’ombe.

    Sisemi kuwa miradi ya namna hiyo si mizuri; la hasha! Nasema, wakati mwingine the end does not justfy the means!

    Anayebisha, afungue website ya musomarural.org kwenye sehemu ya projects na aone wahisani. Kuna baadhi ya majina ya hao Wahindi, makampuni yao na benki fulani fulani!

    Je, hao Wahindi waliotajwa wanachangiaje mifuko mingine ya "harambee" nchini? Ama wako eclectically selective ni wapi pa kuchangia?

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 12, 2007

    Nawaunga mkono waliotangulia kutoa maoni ambao wana akili na upeo wa fikira. Watanzania tumedanganywa kiasi cha kutosha. Viongozi wetu wamezoea kuwa tuna mbio za sakafuni kelele kidogo kisha tunannyamaza.Sababu wamefanikiwa kutuweka maskini hatuna muda wa kupiga kelele. Ila ninachoamini za mwizi arobaini zimeshafika, kizazi kipya tusikubali upuuzi, tusikubali majibu ya kiburi.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 12, 2007

    Wabongo msiwe mnakurupuka tuuu,hawa wote wanaopiga debe Balali ajiuzulu huwezi jua wanatumwa na hao magabacholi.ajiuzulu kwa kipi?Ameshawaambia ujenzi sio yeye kakurupuka tuu, sasa kujenge walianza muda toka kipindi cha akina Nyirabu, na pia kuidhinisha ujenzi waziri wa fedha lazima aliipitisha.kwa hiyo sio tu mnasema Balali kwani yeye aliinidhinisha pesa hiyo peke yake?

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 13, 2007

    Kaka Michudhi

    Mbona haukusema kuwa Gavana aliamua kuwafunga gavana waandishi wa habari ambao wangembana vizuri kama vile Deutche Well?

    Hii ni aibu kubwa kwa democrasia ya vyombo vya habari kaka. Inaonekana kuna mkwanja umepitishwa kwa hao waliohudhuria na waliokataliwa watakuwa walikataa kupokea mkwanja.

    Hili inabidi lifanyiwe kazi, Gavana hawezi akajiamulia nani ahudhurie mechi kati yake na watu wanaomtuhumu. This is not a fair play kwa kweli

    Sele

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 13, 2007

    Duh, Siku hizi watanzania tunadanganywa kama watoto vile.Kuna haja ya kuungana na Mbowe na tuwaache wakezetu wajane hili tuondokane na hawa wanasiasa batili.Hali hii haivumiliki hata kidogo...Kuna umuhimu wote tuanze level moja kama Ruanda na Burundi.

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 13, 2007

    Mbunge wa Musoma Vijijini na Wakili mashuhuri nchini anadiriki kupitishia kwa waziri wa elimu 'msaada' wa magari na kompyuta kwa ajili ya shule za kwenye mradi wake!

    Sielewi.

    http://www.mkono.com/

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 13, 2007

    selemani mpochi nakuona babake, unawajibika kwa baba mengi. Big up man.

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 13, 2007

    Huyu Gavana kwanza kachagua watu wa kuingia ndani kwani bahadhi ya waandishi wa habara kawapiga panda kama wa idhaa ya kiswahili ya Ujerumani (soma hapa http://www.abdallahmrisho.blogspot.com/)

    Lazima kuna kitu anaficha ndo maana alijibu maswali kisiasa tu hakuna data yoyote

    ReplyDelete
  33. AnonymousJuly 13, 2007

    Michuzi tuna shukuru sana kwa kuweka hii habari hii jamaa balali naongea na fahamisha vizuri sana mimi. mimi kwishaelewa yeye nitajitahidi fanya naye kazi karibu kabla naondoka kwenda zake. Hii balali nakaribishwa CANADA sasa..

    ReplyDelete
  34. AnonymousJuly 13, 2007

    Sikieni wadua acheni kufumba macho hawa watu walio kwenye system tunawachekea sana. Hata hawa waandishi wentu sijui vipi mnashindwa kumbana huyu mbazilifu balali kwanini .....tatizo hamtafuti details za kutosha hivyo mnakaa kuuliza mambo juu juu. Kaja hapo kuelezea kuteuliwa manaibu wake au kujibu tuhuma.....WATANZANIA WENZANGU TUAMKE JAMANI.....Huyu Bil hali anatakiwa atoe maelezo ya kutosha sio anakaa tu na kuiva na wakati si MZALENDO...Fukuza weka ndani Prezident usiwachekee Fanya mambo

    ReplyDelete
  35. AnonymousJuly 13, 2007

    Unajua wa-tz mi ninakiri ni wajinga, cases nyngi za ubadhirifu tumeziona na hatuchukui hatua zozote, tumeona mabo ya BAE na rada, ndege ya rais, n.k na sasa BoT.
    Sasa imefika time kwamba tusiwaruhusu wabadhirifu kama hawa akina Balaa-hili na mawaziri na vigogo wote wanaojenga empires at the expense of us poor tanzaniana sio tu waendelee kuiba bali inatakiwa tuwaondoe duniani kabisa.
    Sorry for being too militant but it is time that tuelewe maendeleo huwa hayaji kwa kukaa na kusubiri kudra za mwenyezi mungu, hata Ulaya wamedevelop baada ya kutwangana sana na kuondoa chuya zote ktk mchele.
    Niko tayari kuongoza mapambano

    ReplyDelete
  36. AnonymousJuly 13, 2007

    Jamani watanzania tufungue vichwa vyetu ndio maana natamani tuingie East Africa ili hao wenzetu waje watuzibue akili zetu. Kweli kweli kuna mtu anaweza kumtetea Balali? Naamini sana uhuru wa mawazo ila kwa hili naomba kudiffer! Mlimwangalia machoni jana wakati wa press conference? It wasnt real unajua utawadanganya watu wote ila hutaidanganya nafsi bwana!! Kwani nani alikuwa anategemea tofauti na kukana tuhuma hiyo jana? Hivi wewe kama waziri mkuu alishasema bungeni kwamba kila receipt ya transactions ipo leo balali atasema ameiba? Tatizo ni receipt au ni justification ya kutumia x instead of y? Nimeumia, nimesononeka news za juzi wale wajawazito kule mawenzi hospital walivyokuwa wamelala chini, na wengine wanne kitandani! Inauma, inakera na cha kusikitisha mno wote tuko helpless and hopeless. Kama waliotoa news sio wazalendo kuna wasi wasi gani sasa wa kuunda tume huria ya bunge? Ili tuwaexpose kwa ulimwengu? Eti walizoea kukopa bila kulipa na sasa wimbi limehamia kwa kina mzindikaya ndio maana wamekasirika, kama hivyo ndivyo tuchunguze ili na wao tuwabring kwenye justice pamoja na hawa kina mzindikaya.
    Anyway muda wake umekaribia ila itamhaunt the rest of his life na laana hii iende hata kwa kizazi chake cha kumi ikawashughulikie na kuwafanya wavuta bangi na watumiaji wazuri wa madawa ya kulevya.

    ReplyDelete
  37. AnonymousJuly 13, 2007

    This guy he is a jock right.... what kind of crap is that? Issa swali la kwanza ni nani alikuwa moderate wa maswali. Hatutaki kusikia history ya Bank kuu and its financial statements, we want to hear about the money, how you spend them? kuwaambia watu history ya buildings ni kupoteza muda, tell us why the price was skyrockets compare to the same building in big city like NY and Tokyo. He just bring a bunch of bull crap. I cant stand Tanzanian and i cant stand this guy..... God, Please Mwalimu Nyerere help us.

    ReplyDelete
  38. AnonymousJuly 13, 2007

    Tatizo kubwa ninaloliona hapa ni kwamba nchini mwetu bado kuna viongozi ambao bado wanadhani nchi ni ya Chama kimoja na Uongozi unaokuwa madarakani ni wa milele. wake up viongozi wa Taasisi mbali mbali,leadership ya sasa ni kwa phase mbili za 5 years.Kiongozi akiwa madarakani asije akakuzuga na kukupa false confindence kwamba 'we fanya tu, mi Pm,au Rais, au waziri nitakulinda'.atakulinda so long as he is in power,baada ya miaka 10 you are on your own.muulizeni Prof Mahalu na in due course mtamuuliza Balali maana atake asitake ataning'inizwa tu,labda hamjui Kikwete anamsikia tu,Mkwere yule akiwaka amewaka,subirini mtaona moto wake,mark my words.

    ReplyDelete
  39. AnonymousJuly 13, 2007

    Lets get our eyes open damn it!!! watanzania tumelala sana kwa nini nchi yetu iendelee kuliwa na mafisadi? Ewe baba wa taifa nchi yako umeiacha kwa wenye uroho wa kuiangamiza. jamani tuachieni japo hicho kidogo tulichonacho, you can not keep doing all these to us.. Mungu Ibariki Tanzania na watu wake na piga radi toka kule Mpanda wote wafujaji wa Mali ya nchi yetu.

    AMIN.

    ReplyDelete
  40. AnonymousJuly 13, 2007

    Tanzania inajengwa na wenye MOYO na INALIWA NA WENYE MENO
    ..poor tanzania,
    ...poor tanzanians
    am feeling pity 4 u guys

    ReplyDelete
  41. AnonymousJuly 13, 2007

    Haya mamabo sisi watanzania tumeyazoea. Tangu tupate uhuru, kumekuwepo na kashfa mbalimbali lakini ni nadra kwa mhusika kujiuzuru. Kuna watu wamezaliwa hata mishipa ya aibu hawana. Gavana, kutuhumiwa peke yake ni kosa la kutosha, na aibu kwa taasisi kama Benki Kuu.

    Lakini tumeyasikia mengi kuwa mapesa ya Twin Towers, sehemu yake ndiyo ilitumika kufanya kampeni za chama tawala. Hiyo inakutosha wewe kutokuona sababu ya kujiuzulu na wala hakuna wa kukushinikiza. Hatuna uwezo wa kukulazimisha kutoka lakini ujue tunakuundia njama za kukulipua na bomu.

    Jichunge namna gani lakini sasa inabidi tutumie njia mbadala mmezidi kutuchezea! Watoto wetu wanakufa kwa maradhi ya kuambukiza na utapiamlo, wanafunzi wa vyuo wanafukuzwa, wengine serikali inawakan kama vile siyo raia wa nchi hii wakati wako ughaibuni, wewe na majangili mengine mnakwiba pesa yote hiyo alafu mnaleta maneno ya kifalambada!

    Sasa ni kazi kwako.

    ReplyDelete
  42. AnonymousJuly 13, 2007

    Ngoja niseme ukweli hao wote wanao waraka za kashfa dhidi ya hawa Wakurugenzi nina wasiwasi nao. Hiyo Twin Tower si ilikuwa na proposal, Mbona hawakutuma hizo query zao before wamengoja hadi sasa. WANAFIKI, hivi Balali awe mjinga kiasi hicho aibe pesa kwa jina la Mkewe mmh!! Naomba viongozi wetu wa upinzani msitukatishe tamaa jaribuni ku raise mijadala yenye vithibitisho halisi... na kama ikitokea mnafungwa midomo kubalini kufa kwa ajili ya fedha hizo za wanyonge acheni UBINAFSI mbona sasa mmekaa kimya kama mlikuwa na uhakika.
    Mimi nachukia sana kwani huku nje ya nchi vijana nakaa tunajenga chuki na serikali iliyo madarakani kumbe mnataka tu publicy ya kijinga na ya kujenga chuki.

    Nadhani sasa WATANZANI ifike hatua kitu kikubwa kama hiki kikisemwa na mbunge au kiongozi kikaishia hewani hivi tumshitaki huyo kiongozi kwa KU-KWAZA NYOYO ZETU kwani wengi tulipata masononeko.

    WACHUNGUZI TUNAWATAKIA AFYA NJEMA NA NGUVU NYINGI TUNAHITAJI MAJIBU YA KWELI.

    ReplyDelete
  43. AnonymousJuly 13, 2007

    Bwana wacha watu wale kwa zamu. Kha! nyie WA-TZ ni wabaya sana kiongozi akistaafu hana kitu na heshima yake inashuka.

    Wabunge mmeyataka wenyewe msijidai saa tengenezeni sera madhubuti za kuwajali wafanyakazi wenu wa serikali na taasisi kubwa pindi wanapoacha kazi. Rushwa, Wizi haviishi ngo' ndo maana awamu iliyopita waliamu baada ya makusanyo ya kodi kuwa mazuri na IMF kutupongeza wagawane nyumba za serikali kama watakavyo. NA BADO labda Malaika Mkuu aje kutawala tutaendelea hivi hivi bwana achana na maisha ya full AC kuanzia nyumbani, garini hadi ofisini. MIAKA ikisogea ukiona unafika 50 MMH changamka bwana mtu asikudanganye. Kula usawa wa kamba ila kumbuka watoto na wajukuu wanaokuja.

    ReplyDelete
  44. AnonymousJuly 13, 2007

    Tumekuwa wajinga kwa kipindi kirefu, tangu enzi za ujima lakini sasa tuna uwezo wa kujua jema na baya tutauana kwa mtindo huu.
    Viongozi wa kiafrika hatuko fair bado tuna udictator wa miaka ya 62, umeshakutwa na kashfa kwa nini usijiuzulu bado unaendelea kung'ang'ania madaraka?

    ReplyDelete
  45. Balali apasua bomu

    *Asema Watanzania wa leo hawana uzalendo
    *Awashangaa kuruhusu raslimali yao kupotea
    *Asisitiza hawezi kujiuzulu kwa tuhuma tete


    Na Joseph Lugendo (Alhamis Julai 12, 2007),www.majira.co.tz

    GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Daudi Balali, amesema Watanzania ni wanyonge kifikra na wamekosa uzalendo wa nchi yao, ndiyo maana wameruhusu baadhi ya watu kufanya ubadhirifu.

    Akijibu maswali ya waandishi wa habari aliokutana nao ofisini kwake Dar es Salaam jana kuhusu hali ya uchumi na tuhuma za ulaji fedha zinazoelekezwa kwa BoT, Bw. Balali alisema ubadhirifu huo ni moja ya matatizo yanayojitokeza dhidi ya hali ya uchumi wa nchi.

    Alisema tuhuma zote dhidi ya BoT na yeye binafsi si za kweli na kwamba zimeathiri mtazamo wa watu wengi kwa kiwango ambacho hakutarajia.

    "Taarifa iliyotolewa kwenye intaneti ni uongo mtupu tena haina jina halisi la mwandishi," alisema Bw. Balali kwenye mkutano huo ambao ajenda kuu ilikuwa hali ya uchumi nchini.

    "Inaonekana kuna watu wanagombana au wanagombea kitu, na mwandishi wa taarifa hiyo anaonekana si mzalendo na mchoyo," alisisitiza Bw. Balali.

    Kuhusu uzalendo wa Watanzania kwa nchi yao, Bw. Balali alitoa mfano wa kwenye sekta ya madini na kuongeza kwamba watu wamekuwa wabadhirifu kiasi cha kuonekana kwamba hawaipendi nchi yao.

    "Hatulindi mali zetu na ukienda kwenye madini utakuta watu wamejichimbia," alisema Bw. Balali. Sababu nyingine alizoambatanisha na kukosa uzalendo kiasi cha kushusha uchumi wa nchi ni kutopenda kufanya kazi.

    Alipotakiwa na waandishi kutoa tamko kuhusu maoni ya baadhi ya wananchi wakiwamo baadhi ya wabunge kumtaka ajiuzulu ili kupisha uchunguzi wa upotevu wa fedha kwenye akaunti ya madeni ya nje, Bw. Balali alisema hawezi kujiuzulu kutokana na tuhuma ambazo hazina ukweli.

    "Tuhuma tu hazitoshi lazima kuwe na substance (maelezo ya uhakika) ya ukweli ndani yake, la sivyo watu watakuwa wanatuhumiwa tu ili waache kazi," alisema Bw. Balali

    Aliwataka wafanyabiashara kufuata mfano wa Serikali kubadili tabia na mifumo ili kuendana na hali ya sasa.

    "Wafanyabiashara lazima wafanye structural adjustment (mageuzi muundo) kama Serikali," alisema Bw. Balali na kuongeza kwamba kama walizoea kukopa na kutorudisha, tabia hiyo haiwezekani wakati huu.

    Alisema benki hazitajali kufahamiana mfanyabiashara na Gavana au Waziri, badala yake mfanyabiashara akikopa akashindwa kulipa, atafuatwa huko aliko na benki hizo.

    Alipoombwa kutaja gharama halisi za ujenzi wa majengo pacha ya ghorofa ambayo yamehusishwa na ubadhirifu uliofanyika BoT, Bw. Balali alisema ujenzi bado unaendelea, hivyo hawezi kutoa gharama halisi mpaka utakapokamilika.

    "Kama mnataka gharama zilizokwishatumika mpaka hapo majengo yalipofikia zipo kwenye accounts (hesabu) za BoT ambazo zinatolewa mara kwa mara kwa umma," alisema Bw. Balali na kuongeza, kwamba kelele kuhusu ubadhirifu kwenye ujenzi wa majengo hayo zilianza siku nyingi, tangu mwaka 1984.

    "Jengo hili (Jengo la zamani linalotumika sasa hivi) lilipokamilika mwaka 1984 tuhuma kama hizo zilikuwapo," alifafanua Bw. Balali na kuongeza kwamba wakati huo Gavana alikuwa marehemu Charles Nyirabu.

    "Misingi ya majengo haya (pacha) iliwekwa na Gavana marehemu Gilman Rutihinda," alisema Bw. Balali na kuongeza, kwamba misingi hiyo ilikaa kwa miaka 10 bila kuendelezwa.

    Alisema Gavana aliyemrithi Dkt. Idrisa Rashidi, alijaribu kuendeleza misingi hiyo, kelele za ubadhirifu zikazuka na kusababisha kusitishwa kwa uendelezwaji huo.

    "Mwaka 2000 kuna gazeti lililoitwa Democrats lilianzishwa kwa ajili ya ujenzi wa majengo haya," alisema Bw. Balali na kuongeza kwamba kuliundwa tume maalumu ya kuchunguza ubadhirifu huo.

    "Rais aliagiza CID (Idara ya Upelelezi), Intelligence (Usalama wa Taifa) na PCB (Taasisi ya Kuzuia Rushwa), zilifanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo na kubaini kuwa zilikuwa za uongo, ndipo mimi nikaruhusiwa kuendelea na ujenzi," alibainisha Bw. Balali na kuongeza kwamba ujenzi huo unafanyika kwa sababu BoT imekuwa ikikodi majengo mbalimbali kwa ajili ya kuweka karibu asilimia 40 ya wafanyakazi wake.

    Kuhusu tuhuma za kuwapo kwa kampuni ambayo baadhi ya wafanyakazi wa BoT wanadaiwa kuwa na hisa ndani yake ambayo imesajiliwa nchini Uswisi na inamiliki hisa kwenye benki iliyosajiliwa na BoT hivi karibuni ya Bank M, Bw. Balali aliwataka waandishi kuwa na taarifa za uhakika kuhusu madai yoyote yanayofikishwa kwao na watakapokuwa na uthibitisho wa majina ya wahusika, wampelekee.

    Alipoulizwa kama ameathirika kisaikolojia au kwa namna moja au nyingine na tuhuma hizo, Bw. Balali alisema anafanya kazi kwa moyo mweupe kama kawaida.

    "Niko comfortable (nimetulia) kabisa na moyo wangu ni mweupe na ninafanya kazi nzuri kama kawaida," alisema Bw. Balali na kuongeza kuwa amefurahi kutekelezwa kwa maombi yake kwa Rais ya kupewa wasaidizi ili aboreshe kazi yake ikiwamo ya kuwa karibu na waandishi kwa ufafanuzi wa mambo mbalimbali ya uchumi.

    Wasaidizi walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni ambao ni aliyekuwa Mshauri Mwandamizi wa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Profesa Benno Ndullu, aliyekuwa Mkurugenzi wa usimamizi wa Shughuli za Benki BoT, Bw. Lila Mkila na aliyekuwa Naibu Gavana, Bw. Juma Reli.



    Kuhusu tuhuma za Gavana huyo kuwa na uraia wa Marekani na kulipwa mshahara kwa dola za Marekani badala ya shilingi ya Tanzania, alisema yeye ni raia wa Tanzania wa muda mrefu na kwamba analipwa mshahara wake kwa sarafu ya Tanzania.

    Kuhusu hali ya uchumi, Bw. Balali alisema madini ya dhahabu yanayoongoza kwenye bidhaa na huduma zinazouzwa nje ya nchi, yamesaidia kuhimili vishindo vya matatizo ya uchumi yaliyotokea mwaka jana.

    Alisema ingawa watu wanaona kuwa Tanzania inapata asilimia tatu tu ya mrabaha, ukweli halisi ni kwamba kuna zaidi ya asilimia hiyo ambayo haijawekwa kwenye mahesabu juu ya thamani halisi ya kinachobaki Tanzania.

    "Ukiangalia kwenye makato ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi na kinachoingia au kubakia ndani ya nchi (Balance of Payment) utaona kwenye dhahabu kuna zaidi ya mrabaha unaobaki nchini," alisema Bw. Balali.

    Alisema asilimia 25 hadi 30 ya gharama za kuchimba dhahabu hiyo inatumika kwenye uagizaji wa mafuta ya petroli kwa ajili ya uendeshaji mitambo ya umeme.

    "Kama Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) lingekuwa linapeleka umeme mpaka kwenye machimbo ya dhahabu, fedha zinazopelekwa kwenye nchi zinazozalisha mafuta zingebaki nchini," alisema Bw. Balali.

    Alibainisha, kwamba Serikali inafanya mipango ya kubadilisha mitambo ya kuzalishia umeme inayotumia petroli na kuweka inayotumia gesi, ili kuepuka upotevu wa fedha zinazonunulia petroli.

    Aidha, Bw. Balali alisema asilimia 90 mpaka 100 ya thamani inayoongezwa kwenye dhahabu kabla ya kuuzwa, hufanyikia Italia, ambako kunatengenezwa mapambo kama pete, hereni, mikufu na mengineyo ya dhahabu.

    "Kama tunataka kubakiwa na thamani kubwa ya dhahabu yetu lazima tupige hatua ya kuanza kutengeneza mapambo hayo nchini ili tuuze dhahabu na ongezeko la thamani juu yake," alisema Bw. Balali

    Kuhusu mfumuko wa bei, Bw. Balali alisema Tanzania imepiga hatua kubwa kushusha mfumuko huo kutoka asilimia 35 iliyokuwapo Januari 1995 mpaka asilimia 9.1 mwaka 1999.

    "Kuna wakati tulifikia asilimia nne ya mfumuko wa bei, kupanda kwa bei ya mafuta ya petroli na ukame, vikasababisha kuongezeka kwa kiwango cha mfumuko huo kilichofikia asilimia 7.7," alisema Bw. Balali.

    Kwa mujibu wa Bw. Balali, chakula ndicho kinachochangia sehemu kubwa ya upandaji wa mfumuko wa bei, kwa kuwa kinachukua asilimia 55.9 ya matumizi ya wananchi.

    Alisema mafuta ya petroli yanashika nafasi ya pili ya matumizi ya asilimia nane ya wananchi kwa kusababisha upandaji wa mfumuko wa bei kutokana na umuhimu wake kwenye kazi za kila siku za maisha ya mwanadamu.

    Bw. Balali alifafanua, kwamba Mei mwaka huu, mfumuko wa bei ulifikia asilimia tano na kwamba kama bei ya mafuta na hali ya chakula itakuwa nzuri, utapungua zaidi.

    Hata hivyo, alisema bei ya mafuta imefika dola 75 kwa pipa, aliyoitaja kuwa ni ya juu kwa sasa na kwamba imetokana na ongezeko la uagizaji mafuta ya petroli unaofanywa na nchi zinazoagiza mafuta hayo kwa wingi ikiwamo Marekani.

    Alifafanua, kwamba haitarajiwi bei hizo kupanda zaidi ya hapo, kwa kuwa nchi zinazoagiza mafuta hupunguza kiwango cha uagizaji ifikapo Septemba, kwa kuwa wakati huo ni wa baridi ambapo wananchi wengi hawapendi kutumia usafiri wa magari.

    Kuhusu ongezeko la kodi kwenye Bajeti na tishio la ongezeko la mfumuko wa bei, Bw. Balali alisema wafanyabiashara wengi wana tabia ya kupenda kuongeza bei wanapopata mwanya.

    Alifafanua, kwamba hiyo ni tabia ya uchumi wa kikabaila na kwamba tabia hiyo hudhibitiwa na sheria kama inavyotekelezwa hivi sasa, kwa kudhibiti upandishaji holela wa bei ya mafuta.

    Aidha, aliisifia Bajeti hiyo kuwa inalenga kutekeleza miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, nishati na umwagiliaji katika maeneo mbalimbali ya nchi, miradi ambayo itachangia malengo ya kukuza uchumi kwa muda mrefu.

    Kuhusu uchumi kuwa na mzunguko mkubwa wa fedha za kigeni hasa dola ya Marekani, Bw. Balali alifafanua kwamba hilo limetokana na matatizo ya uchumi yaliyoikumba nchi miaka ya 1980.

    Alisema fedha za nchi zenye matatizo ya uchumi, hukosa imani kwa watumiaji na badala yake fedha ya kigeni hutawala kwenye mauzo na manunuzi ya bidhaa na huduma.

    Alitoa mfano wa Korea Kusini ambayo iliwahi kuwa na matatizo hayo, lakini ikafanikiwa kuondoa mzunguko huo polepole.

    "Sasa hivi hali si mbaya, kwa kuwa kama huna dola ya Marekani wafanyabiashara wanakubali ufanye manunuzi kwa fedha ya Tanzania," alisema Bw. Balali na kuongeza, kwamba hiyo ni hatua nzuri ya kuelekea kuondoa fedha hizo kwenye uchumi.

    Kuhusu kushuka kwa thamani ya shilingi, alisema Tanzania imeondoa mfumo wa kudhibiti kiwango cha ubadilishanaji wa shilingi ya Tanzania na fedha nyingine za kigeni, tangu kuanzishwa kwa uchumi unaofuata nguvu za soko huria.

    Alisema shilingi ya Tanzania kama ilivyo bidhaa nyingine yoyote, inapata thamani kulingana na hali ya nguvu za soko za mahitaji na upatikanaji wa fedha za kigeni.

    "Kama fedha za kigeni zikiwa chache kuliko mahitaji kwenye soko la fedha hizo, shilingi itashuka na kama fedha za kigeni zikiwa nyingi kuliko mahitaji yake, shilingi itapanda," alifafanua Bw. Balali.

    ReplyDelete
  46. AnonymousJuly 13, 2007

    Hivi nyie watu mnaopiga kelele kuhusu ujenzi wa twin towers mna utaalamu wowote kuhusiana na gharama za ujenzi au mnaropoka tu kuunga mkono tuhuma zilizoanzishwa na mtu ambaye uenda nae hajui anachokisema. Swala la kulinganisha gharama za ujenzi Tanzania na New York/London, mmelifanyia uchunguzi kweli au? Jaribuni kuwahusisha wataalamu wa ujenzi ndani na nje ya nchi kisha mtetee mnachokisema mkiwa na ushahidi. Kwa kweli nasikitika sana kuona watanzania wenzangu na hasa wale walio nje ya nchi kwa jinsi wanavyochangia hoja bila mpangilio. Kuwa nje ya nchi ni moja ya fursa ya kutanua upeo wako katika mambo mbalimbali kwa kulinganisha vitu vinavyofanyika nje ya TZ na jinsi tunavyovifanya ndani ya TZ. Wewe uliyeko London (au mtu yeyote) jaribu kuwasiliana na wakandarasi maarufu duniani kwa kutumia mtandao kama unataka kuelimika, nikisema mimi mnaweza msiniamini pia.
    Jamani angalau tushukuru kuona kazi iliyofanya na hela ya nchi, the towers are one of spectacular landmarks nchini, na hiyo pekee inatuinua katika uso wa dunia.

    Orodha ya baadhi ya makampuni maarufu ya ukandarasi na consultancy duniani hii hapa

    ABERTHAW CONSTRUCTION (sio maarufu)
    simu +1 978-654-4500
    estimating@aberthawcc.com

    Laing O'Rourke
    http://www.laingorourke.com/

    SKANSKA
    http://www.skanska.com/

    ARUP
    http://www.arup.com

    Jacobs Engineering Group Inc
    http://www.jacobs.com/

    Scott Wilson
    http://www.scottwilson.com

    Atkins
    http://www.atkinsglobal.com

    Nawatakia watanzania wote maisha mema na yenye amani siku zote.

    ReplyDelete
  47. AnonymousJuly 13, 2007

    Watanzania tumelala na hatuko serious na maisha , mimi jinsi hawa wakubwa wanavyojenga hoja zao inachekesha . Naona Balali anatumia principle za Mahita , mnakumbuka kipindi kile majambazi yalipomshinda akakimbilia kusema ni CUF na huyu bwana anakimbilia kusema ni watu ambao sio wazalendo ndio wanaofanya hivyo !

    Hivi kweli inaingia akilini kwa gharama za kujenga jengo hapo dar kuzidi gharama za kujenga jengo kama hilo New York? Jamani tuamke na waandishi wa habari wafanye kazi ya uandishi.

    ReplyDelete
  48. AnonymousJuly 13, 2007

    Michuzi wewe uliuliza swali gani ?

    ReplyDelete
  49. AnonymousJuly 13, 2007

    Duh... Bravo Br Michuzi kwani kwa kupitia humu tunayajua mengi...
    Niwaombe Vyombo vyote mlivyopigwa STOP kuingia katika P.conference ya Mh Baalaa Hili mjipange mumfuate popote alipo mumhoji...pamoja hayo ya BOT....aliwaogopea nini??? mkimwacha hata siye tutawaogopa....kalagabaho....

    ReplyDelete
  50. AnonymousJuly 13, 2007

    Kwani haya mambo ya kasi mpya na ari mpya yanawahusu baadhi ya watu na wengine no? Mbona wengine wakipewa shutuma imedeately wanaondolewa kwenye post zao kupisha uchunguzi iweje gavana aseme hawezi kujiuzulu kwa uzushi? Balozi Italy alirudishwa Tz speedspeed hata investigation kufanyika, mwingine anaambiwa no need he can keep his post. Can we say we have a fare system or something fishy is going on in our so cald peaceful country? God bless Tanzanians.

    ReplyDelete
  51. AnonymousJuly 13, 2007

    Anon wa 1:14:00PM ya tarehe 13 July 2007. Tunashukuru kwa research yako kwa kutuletea mtundiko wa makampuni mbali mbali ya ujenzi. Pamoja na kuwa umetundika hayo makampuni, labda kwa vile wewe ni engineer haujasema kama wanaopiga kelele wanasema uongo au ukweli kuhusu gharama za Twin. Mimi nimeenda kwenye site moja ya SKANSKA na kukuta wana project moja katika mji wa Helsinki la square 10,000 na square moja ni Euro 3,160(approximately USD 4,300). Ya Twin tumeambiwa ni USD zaidi ya 8,000. Kwa maana hiyo Twin imekuwa inflated at least mara 2. Naomba ulete hoja sio kutuelekeza kwenye site. Hatuwezi kufumba macho kuhusu gharama eti kwa vile Twin in landmark ya Tanzania. Huo ni ulimbukeni wa kununua kitu kwa bei kubwa eti kwa vile ni landmark. Kwani kama ingejengwa kwa gharama reasonable ikapendeza kama ilivyo isingekuwa landmark.

    ReplyDelete
  52. AnonymousJuly 13, 2007

    Jamani nani atakuwa mjinga kiasi gani aende pale na akonfesi kuwa yeye ni jizi. Hiyo hakuna. Hawa watu sio wa kuwachekea. Bongo tumezidi kuleana leana. Hivi tuangalie nchi km Bangladesh kulikokuwa kunaongoza kwa rushwa..sasa hivi wala rushwa wote wametupwa jela...huyu ni kumtia hatiani mara moja huyu. Halafu mbona sura yake km ya wale watu wa GODSI MASTI BI CREZE!!!

    ReplyDelete
  53. AnonymousJuly 14, 2007

    Lisemwalo lipo,........ huyu Gavana asitudanganye kala pesa zetu, mwizi hawezijisema.

    ReplyDelete
  54. AnonymousJuly 14, 2007

    Eti mtu ambae ni Jambazi anaweza kuitisha mkutano na kusema yeye ni Jambazi?? Nyinyi mlitegemea Balali ataitisha mkutano kukubali kuwa ameiba kwenye deals zote hizo. Jambazi anaweza kukamatwa na kithibitisho mikononi lakini akagoma na kusema hajaiba.

    Inabidi uchunguzi ufanywe na huyu mtu awe implicated. Lakini kama ninavyoijua Bongo, hii issue ndio imeshafungwa hiyo na watu walioiba wanaendelea kutanua

    ReplyDelete
  55. AnonymousJuly 14, 2007

    ndugu zaidi Balali wala asiwaumize kichwa,yuko kibra tayari huyo.subirini taarifa ya wachunguzi(ni watasha wametoka marekani) ikamilike halafu mtasikia mziki wake.just be patient and trust in Jakaya.
    ps: in fact mi ningekuwa Balali ningesaga chupa ninywe kuliko hicho kiama kinachokuja.

    ReplyDelete
  56. AnonymousJuly 14, 2007

    Ngurumu alisema kweli, Watanzania tu wavivu wa kufikri, tunaibiwa huku tgukilambishwa maneno matamu nakuridhika. wakati wa tuhuma za nbc ilibainika mkurugezi mmoja wabenki hiyo alikuwa mwenyekiti wa mfuko jimboni kwa mheshimiwa waziri kihenge wakati huo, wtz tulikaa kimya na kuchekelea, mradi wa mchuhuma na liganga haianzi kwa sababu tu waheshimiwa wanataka kumpa jitu! itpl mpaka leo inatumaliza tuko kimya, richmond ndo hiyo ikatungwa barua hakuna anayehoji, bot bala li katumia udhaifu ule ule wa watz anajua yameishia baada ya press conference, hawezi kujibu hoja kwa sababu si wa kwanza na kumbukeni ni yuko kwenye kihenge mnajua ana madhambi mangapi ya wakubwa wake! anajua hawawezi kumuwajibisha kwani nao wamoo...ndo tz hiyo heri yenu mnaobeba mabox ulaya huku inauma na kutia kinyaaa utadhani wote tu mazezeta

    ReplyDelete
  57. AnonymousJuly 14, 2007

    kuitisha press conference siyo lazima uwe msafi hata kama siyo msafi ukiwa nazo wee itisha tu tuone.

    ReplyDelete
  58. AnonymousJuly 16, 2007

    kuna haja ya polisi/usalama wa taifa kukanusha/kuhakiki hoja mbali mbali zinazotolewa Bungeni au vyombo vya habari kupitia Press- conference na inapotokea mwandishi au Mbunge anakuja na hoja zenye lengo la kutoa Uchochezi achukuliwe hatua!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...