
kikosi cha dc
Timu ya wabongo waishio Atlanta tarehe 7 mwezi huuwaliiadabisha timu ngumu ya H-town 3-1. Ushindi huoulikuja baada ya malumbano ya siku nyingi kati yamahasimu hao wawili.
Habari kutoka mwandishi Marcaliyekuwepo uwanjani zinasema kuwa mpambano huoulichelewa kuanza kwa takribani saa zima baada ndegemaalumu ya kukodi iliyowabeba washindi kuchelewakufika kutokana na mvua nyingi zinazoendelea katikaukanda huu.
Hadi half time Houston walikuwa wakiongozakwa bao moja bila lililolalamikiwa na vijana wa ATLkwa takriban dk 5. Mfungaji akiwa mshambuliaji waomrefu Peter B. "Mwaikimba". Kipindi cha pili timu zotezilifanya mabadiliko na alikuwa midfilder maridadi LIGA aliyepachika bao mbili za haraka haraka.
Msumari wa mwisho kwenye jeneza la H-Town uliwekwa na kijanamachachari sana Magoha nakufanya idadi ya mabao kuwa3-1 hadi mwisho wa mpambano huo. Pichani chini ni timu zote mbili.
wakati huo huo timu ya vijana wakibongo waishio Washington DC na maeneo ya karibu wamefanikiwa kuifunga timu ngumu yaTANZATL katika uwanja wao wa nyumbani jijini ATLANTA.
Hadi tunakwenda mitamboni DC 4 ATL 3.
Shukrani ziwaendee kampuni mdhamini ya ShakaEntertainment iliyodhamini mpambano huo.
Wachezaji wa ATL walevi tuu. Angalia magoa kitambi hicho... Mtavunja miguu iwe mwisho wa dream zenu, maana insuarance and New Immigration code change the whole spectrum
ReplyDeletehahahahaaaa !!!!!!!!
ReplyDeleteRudini Bongo mjenge nchi yenu!
ReplyDeleteMmezidi kutuyeyusha kwa majidai yenu uchwara!
Tujenge nchi kwa kuanzi wapi? wakati mambo ni yale yale? Na kwa wale wanaodhani kila aliye ughaibuni ni mbeba box endeleeni kujua hivyo hivyo
ReplyDeleteKwako wewe Msemakweli, wewe si ujenge tu, kwani lazima tuje wote? Nchi itajengwa na wachache, si kila mtu. Sasa nenda kwa muda wako. Kubwabwaja ovyoo tu...
ReplyDeleteWanaotaka kujenga nchi si hao wanauwawa?? Au hauoni we kinyozi? We jenga tu nchi hiyo na ukijifanya unajua watu watakutuliza. Mnataka turudi mtumalize? Punda nyie!!
ReplyDeleteunajuwa malezi na adabu ndio mtu anajuwa maisha kuishi nje si lazima box hatakama unapiga box nimaisha yako si kwamba ukipiga box unaenda motoni, je wazaramo kijana walikufukuza urudi kwenu mikoani? kuwa na akili ndio utaelewa dunia ni ya wote na si ya mtu mmoja kama wanavyojuwa wazungu mungu kasema ishi patapokufaa kama wazee wako walivyokaa dar wakati kwao mikoani. wacha binadamu aishi, zamani watu walisema muone issa michuzi mpiga picha hanalolote ona sasa yuko wapi anaishi vizuri kwa kupiga picha ukiwa na roho nzuri mungu naye anazidi kukupa wepesi. liverpool uwaaaaa. au sio michuzi jibu basi
ReplyDeletewatu wanaodai mrudi bongo, hawana akili. Unemployment level hapa ipo juu sana, tunashukuru baadhi wakipata ajira nje ya nchi, iwe USA au Swaziland .
ReplyDeleteHuyo anayejiita Msemakweli kawapa ushauri wa bure. Nyie sasa mwamjia juu kama moto wa kifuu, kulikoni? Kwani kuwashauri mrudi nyumbani tusaidiane kuijenga bongo kakosea? Sasa longolongo yote mnayotoa inatoka wapi? Kama hamtaki kurudi si basi?
ReplyDeletejamani mimi naona wote mko njee ya point hapa tugejadili kuhusu mechi ya mpira kati ya ATL na HOUSTON...mahali pa mtu kuhishi nafikiri ni uamuzi wake binafsi kama ni bongo ,USA au mahali popote ni mpango wako mwenyewe nafikiri huyo anaetaka watu warudi ni wivu wake binasfsi...ila kwa kifupi HONGERA ATL kwa ushindi wenu we need to see more postive things like that...KEEP UP HOMMIES
ReplyDeleteJamani mmeleta picha wenyewe michu kapost wananchi wamechangia!!sasa mnarudi na makashifa kibao mara turudi mikoani,mara sio wote wabeba mabox,mara hata kubeba box sio dhambi sasa tuwaelewe nini???mlitaka tujue mpo kwa joji kichaka na mnaweza kukodi ndege(kitu ambacho ni cheap anyways)mbona sisi tunakodi mabasi dar arusha na hatusemi wala kujibandika kwa michuzi????mmezoea maisha bogo kwa mtu anayeingia kwenye blog sio magumu hivyo tatizo mnakumbuka maisha yenu ya manzese!!! wengine tumesoma huko mliko tukitokea mkoani(nakumbuka dar nilikaa 3days)sikuwa na maneno kama nyie mliosota kwanza na kuiona ulaya na amerika kwenye video mkatamani kwenda ndo maana mnamambo ya kishamba shamba.Michu najua utaibania tu bana tuuuuuuu
ReplyDeletenani arudi wewe?nchi gani ya kurudi hiyo infrastuctures ziko dhulf-hal si manzese au masaki kote sawa tuu.
ReplyDeleteNyumbani ni nyumbani hata kama kukiwa kubaya kiasi gani, naamini kila mtu anataka kwenda Ulaya or USA lakini just a matter of time, yote ni maisha tu, popote pale unapopata kazi ndo nyumbani kwako ila unabaki kukumbuka ulipotoka, naamini vijana wanakumbuka walikotoka. kashfa na matusi ya nini jamani. sisi wenyewe tuko huku huku Ulaya tukipiga shule ila tunajua ipo siku tutarudi nyumbani ila si kwa kulazimishwa na mtu hata kama 'UNGA ROBO NA MSOSI WA KUBAHATISHA'. rusha hiyo michu... niione leoleo bado ya moto
ReplyDeletenyumbani ni nyumbani hata kama unga ni robo, mnalinga huko kwenu!!!!!!!
ReplyDeletehapo kazi kweli kweli pale mtu anapojidai akiwa akiwa nyumbani kwa jirani yake.......;
ReplyDeletemimi narudi kwenye point ...je hiyo ni ligi gani au walioshinda wanaenda kucheza na nani? na mshindi atapata zawadi gani? Tungeomba fact zote.
ReplyDeleteand now back to the ongoing topic..wewe anony wa 9:46am speak for yourself ...if you could you would .....umeanza vizuri umemaliza vibaya.....kurent ndege au basi it is not a big deal na haikua point hapa...point ni kuonyesha hali ya hela zilivyokua mbaya sasa (global warming) na delays za airport kama umeishi huku before and after 911 utaelewa. Otherwise elimu sio kupanga vitabu kichwani tu .....unaweza kupata elimu yote iliyopo ulimwenguni na bado usielimike. kama alivyosema Martin Luther King, Jr. Knowledge is a process of piling up facts; wisdom lies in their simplification.
To suggest is to create- to describe is to destroy.
ReplyDeleteHuo mwenye low mind amesuggest na yule wengine wote wenye low mind nadescribe.
Get life people haya malumbano ya rudi nyumbani, sirudi when will it be over? Kila mtu ana huru kuishi mahali anapenda kama ni foreign country or not.
Mbona picha za people having funny here from TZ nobody talks about it? But picha from any other country watu hawapumui.
It is just the way of living...Naweza kuwa na magari, majumba,mashamba and in your house you have plasma tvs, underground cooler, movie thieter, indoor garden, indoor pool or jacuzzi. Everything top of the line ukafill you are so damn rich but mtu mwingine anakua na the same things but it is just the way of living to them.
So get your life streight acha maneno marefu
Kwa anon6:50 EAT. Hakuna zawadi kubwa ila thumuni ni kutafuta wachezaji bora watakaounda timu ambayo itafanya ziara ya Tanzania mapema mwakani kwa mechi kadhaa za kirafiki na timu za Yanga na Simba, KMKM nk. pamoja na Taifa Stars ikiwezekana. Mipango iko mbioni na ikikamilika wote mtataarifiwa.
ReplyDeleteKuhusu swalaa la kurudi nadahani achenikuua watu kwanza ndio tutarudi! Msikunje.
mie nakubaliana na aliyesema mungu ndio anakupa uwezo wapi uishi walio dar hawakufukuza mtu arudi mikoani, naaliyesema mrudi pengine kweli hakusema kwa ubaya ila ukweli ni hapa tumeambiwa kuhusu mpira nchi yoyote ishi kwa duniani si kwayoyote ni kwa mungu hatujafa bila kuumbika tuwache majungu tu comment kilichotakiwa jamani makwetu ni peponi motoni mungu atunusuru basi amin michuzi uwe unasema mada ni ya mpira tu comment ila kumbe wanja letu la taifa linatisha mie nilijuwa huko viwanja vya kapeti hahahaha lazima tuchekeshe jamani mnaonaje huo uwanja labda waliofungwa walifungwa majani makubwa michuzi piga tena uwanja picha.
ReplyDeleteHata mie nakubaliana na wanaosema dunia ni ya mwenyezimungu na nyumbani ni nyumbani kwa hiyo haina haja watu kugombana mpira oyeee, hii imenikumbusha mlevu mmoja alikuja ubalozini wa Uk kule tz akasema nyie mnakesha hapa toka asubuhi mtarudi tu ngoja kupigwe mabomu mtarudi wenyewe kwenu ukitizama ni kweli ila yote maisha michuzi hii picha iweke tena juu juu watu waanze upya kuhusu mpira,jezi,kiwanja,na wachezaji je kipa hapo kavaa glavzi au kama enzi zako michuzi kifuwa wazi na huna glovu za kudakia hahaha. jamani mnaonaje au walivaa DH siku weka picha ya kiatu cha DH na MARADONA
ReplyDeleteAnnon wa 12:47/53,inabidi urudi shule hauleweki kabisa na hicho ni kiswahili, je kiingereza si ndio shida kabisa.Duuh kazi kweli kweli.
ReplyDeletekula negative 5 kwa lugha mbofu mbofu.