
wadau mlio ughaibuni kwa taarifa yenu kwa sasa hapa bongo kuna kipindi cha luninga kinachotamba kuliko vyote kwenye eatv kiitwacho 'ze comedy' kinachorushwa kila siku ya alhamisi jioni na kurudiwa jumapili. kuna wabunifu wamekaa na kuja na uigizaji wa kutangaza taarifa ya habari kwa namna ya kuchekesha sana kiasi wengi huwaga wanawahi nyumbani siku hiyo kujionea vioja kwa lisaa lizima. stelingi ni huyu masanja mkandamizaji ambaye pamoja na mwenzie joti mdebwedo hurusha nyuuzi kwa namna isiyo mfano kiasi hata nahau za 'kandamiza' na 'mdebwedo' zimeshika nafasi kila kona. aidha, mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni - hawa jamaa wamewini...
jamaa wamewini, si mchezo. Lakini mwandishi mbona unaandika huku unanung`unika ? ... kwa nini unamwita Masanja eti mnyonge ? kanyongwa na nani ??
ReplyDeletekitu muhimu ni kuhakikisha umeme wa uhakika, ikiwezekana televisheni za vijiji ili watu wengi zaidi waweze kufaidi uhondo huu.
Jamaa wako juuuuuuu!
ReplyDeleteHasa viongozi na wasanii uchwara wanawakandamiza ile mbayaaa. Safi sana lakini siku moja utasikia kauli kutoka kwa wale jamaa kule Dodoma "Hawa comedy wafungiwe wanapotosha jamii" si mnakumbuka haki elimu?
ReplyDeleteAhaaa,
ReplyDeletebasi hiyo nadhani ni poa sana. Ni kama kipindi huku USA cha saturday night live cha jumamosi usiku, huwa kuna taarifa ya habari moja hivi ya kuchekesha sana. Mimi huwa siikosi,
Labda wangeongezea na kuwaakti baadhi wanasiasa na watu maarufu, hawa wa huku huwa wanaakti prez bush na dik cheney basi ni vichekesho vitupu, kondoleza raisi ndo kabisaaaa, wanampatia mpaka mwanya,
Keep up good stuff Bongo,
grace.
Joti alivyo-pose utadhani Marehemu Tupac Shakur....
ReplyDeleteKaka Michuzi hawa Jamaa wanajitahidi sana kukosoa Jamii. Mi at least mpaka sasa so far nawafagilia sana.
ReplyDeleteKama kwenye show ya wiki iliyopita ile Stori ya WANAOJIDAI MASTAR kwenda kwenye misiba ya watu maarufu kwa lengo la KUJIBIISHOLISHA na "kusafisha nyota" ile ni kweli kabisa.
Kuna WASHAMBA fulani ambao huwa kweli wanapendaga kufanya hivyo kwenye misiba. Sijui upungufu wa elimu! Mheeh!
Eee bwana naomba unifikishie ombi langu kwao kwamba wiki hii WARUDIE TENA ile stori ya WANAOJIBIISHOLOLOLISHA kwenye misiba ili TUKOMESHE kabisa tabia hiyo mbovu!
Big up!
Ila sasa tatizo la Mastaa wa Bongo wakishaanza kupanda chati si unawajua Kaka Michuzi? Wataanza KUPOMBEKA kwa sanaaa, na MABIBI kwa wingiii!
Noma hiyo jamani wWasanii wetu. Ninyi msiwe hivyo
dada Grace (wa july 11,11:32:00),hawa jamaa wa ze comedy si mchezo. juzi wamemuonyesha Kikwete kahonga sh 25,000.-kapewa kitanda na nesi hospital,baada ya muda kaingia kibopa anatembeza mkwanja kiroho mbaya akamwambia nesi'kamati hii minoti toa hiyo taka taka hapo kitandani nilale mimi',kumbe kitandani kalala Kikwete amejifunika,kumfunua tu ili amtoe mkuku,lo! balaaa ni mwenye nchi!you can imagine. ukiona wanavyomuigiza Lowassa utacheka mbavu ziume.hawa jamaa majiniasi.
ReplyDeletehao ndo macelebrity wa bongo kiukweli maana kila kona watayopita watu wanawashangaa kiukweli ukweli..
ReplyDeleteThe are true Tanzanian talent...
ReplyDeletemie nilikuwa najiuliza hii blog yako inabeef na ze comed nini mbona ulikuwa ujawarusha mda wote huo lkn nimefurahi sana yani hawa jamaa uspime kabisa ktk fani ya vichekesho kwa sasa yani wanatisha ile baraa
ReplyDeletePerez hao vijana especially mpoki na mwenzake nadhani wanajiheshimu manake wameshakuwa kwenye umaarufu kwa muda mwingi sana sasa... so nategemea wataendeleza kujiheshimu kule kule. Lakini kama usemavyo kama chati inapanda kwa spindi inaweza walewesha psychologically alafu ikazua mambo mengine!
ReplyDeleteMichuzi tutafutie basi some video clips na sisi tufaidi manake kila mtu akitoka bongo ni kipimabaridi kipimabaridi sasa naachwa hoi tuu.
MICHUZI UMECHELEWA NA ZE COMEDY. TUMESHAONA VIMBWANGA VYAO SIKU NYINGI KATIKA TOVUTI NYINGINE. WALICHOANZISHA WENZIO HUJIFANYA HUKIANDIKI VIPI HIKI CHA ZE KOMEDY AU KWA SABABU NI MAARUFU SANA TENA SIYO KUPITIA KWENYE BLOG YAKO? UNAPENDA SANA MDEBWEDO WEWE...UTAKULA UROJO. SHAURI YAKO.
ReplyDeleteMBONA MICHUZI HUJAWEKA PICHA YA 'LOWASSA'??
ReplyDeletemichuzi fanya basi siku moja tuwekee hao wakandamizaji tusikie. asante.
ReplyDeletehehehe hawa jamaa jamani wanaburudisha sana! Mie ule muondoka wa joti tu hoi babake!! na msemo wake wa kudadadeki!! hehehehe very funny yakhe!! masanja yeye huwa anakandamiza kibara tu high speed!! hehehe!! i like that! mambo ya kubonyeza kizenji! Mdebwedo!! hehehe hawa jamaa ni mwisho wallahi yaani ukiwa na kisirani basi ikifika alhamisi jioni chaisha!!
ReplyDeletehehehe hawa jamaa jamani wanaburudisha sana! Mie ule muondoka wa joti tu hoi babake!! na msemo wake wa kudadadeki!! hehehehe very funny yakhe!! masanja yeye huwa anakandamiza kibara tu high speed!! hehehe!! i like that! mambo ya kubonyeza kizenji! Mdebwedo!! hehehe hawa jamaa ni mwisho wallahi yaani ukiwa na kisirani basi ikifika alhamisi jioni chaisha!!
ReplyDelete