
Malalamiko ya baadhi ya watalii nchini
Wengi mtakubali kwamba nchi yetu Tanzania inasifika sana katika sector yautalii.
Kama wiki mbili zilizopita nilipata bahati ya kusafiri na watalii wapatao 50 na katika kuzungumza nilijaribu kuwauliza ni mambo gani ambayo wameona bado tunahitaji kufanyia kazi au ni yapi yamewashangaza kwa ubaya……kwani kama ni sifa za nchi na raia wake tumezisikia na tunaendeleakuzisikia.
Yaliyowashangaza na kuwaudhi yalitajwa kuwa ni kama ifuatavyo
- Vyoo vichafu sana kuanzia vile vilivyo kwenye restaurants na vile vile hata vyoo vya kulipia navyo viliwashangaza kwani mtu unalipa ili uweze pata huduma bora na safi lakini haikuwa hivyo kwa vyoo vingi vya kulipia
- Wengine walilalamikia kutozwa bei isiyo halali na wabeba mizigo mfanoulitolewa kwa wabeba mizigo wa pale feri Dar es salaam . Jamaa alibeba mzigowa mtu mpaka kwenye boat na kudai 30,000 shilingi
- Wengi wameshangazwa sana na tofauti za bei za boat kutoka Dar – Zanz naZanzibar – Dar ambapo wageni hupaswa kulipa na dola na hivi bei ikiwatofauti na wenyeji.
Kwa hapa waliniuliza iweje ndege au mabasi yasiwe na bei ya mwenyeji na mgeni ? kwa kweli sikuwa na jibu
Wadau naombeni mchangie mada na kama kuna njia yoyote ya kupeleka haya kwawahusika ili yafanyiwe kazi ingekuwa vizuri pia.
Asanteni
mdau Irene James
mdau Irene James
tatizo letu watanzania tunaangalia mbele kwa kutumia taa za baiskeli, unaona hapa tu na si pale. hatuangalii uko mbeleni itakuwaje au utaratibu wa kuwekeza kwa siku za usoni.
ReplyDeleteNakuwabaliana na haya malalamiko mimi mwenyewe nimeingia vyoo vya kulipia nikashangaa sana kwa kweli..na isitoshe hata kwenye restaurants watu hawajui customer service kabisa yaani mtu unakula hata hujamaliza vizuri sahani iskachukuliawa..na hiyo ya bei tofauti ya boat kwa wenyeji na wageni kwa kweli sijui sababu ni nini haswa ila nadhani ni muhimu sana kwa tour operators kufanya kazi kwa ukaribu na pia kuchukua malalamiko ya wageni kwa vyombo husika sababu sector ya utalii ni tegemezi kwa wengi wa raia na serikali kwa ujumla
ReplyDeletemimi hata mchango sina nimechoshwa sana na matatizo ya kila corner ya nchi yetu ushauri wangu mimi kama raia halisi wa Tanzania nchi hibinafsishwe na kila mtanzania agaiwe chake sawa kwa sawa
ReplyDeletemzawa
Mfano pale ferry kuelekea kigamboni.Bado kuna mateja wabeba mizigo na tena wanajipumzisha pembeni ya kituo cha polisi kwenye ule mti naamini bado upo.
ReplyDeleteDawa ni kuwa na wabeba mizigo wenye uniform kama pale ubungo walau itaanza kupunguza usumbufu hasa kwa watalii wa ndani na nje waendao kwenye fuko mbalimbali huko kigamboni.
Ila hali ilivyo hivi sasa ni bora hata huyo aliyelipishwa elfu 30,mimi nilishuhudia msela akimsaidia mzungu mzigo na kulala nao mbele ilikuwa tafrani ingawa alidakwa.
Ene wei tutafika tu ni hayo tu
1.wale wabeba mzigo pale bandarini waondolewe upande wa watalii wafanyie locals tuu,kwanza wanalazimisha pili hawajui kwamba mtu anaouwezo wakubeba mzigo wake mwenyewe.katoka nao nyumbani kwake ulaya leo ashindwe bandarini tza.
ReplyDelete2.tourist routes ziwe organized and separated tokea airport mpaka destinations kwahilo taifa litavuna zaidi dola za watalii.wale watalii "vishuka"masikini au back packers wakabidhiwie registered agencies ndogondogo za wajasilimali au "papasi" ambazo zitatake care na kuwaguide wageni.
3.wizara husika zote za bara na visiwani zilazimike kutoa huduma ya tourist info vituo vya information kwa watalii kwaajili ya ramani,vyoo bora,chakula mzuri bei halali na translations.
this ma 5cent on the issue
mdau wa chelsea pale hlki
Kuweka bei tofauti ni ubaguzi tu.Na ubaguzi huu uko hadi kwao hao wazungu iwe Marekani au Ulaya.
ReplyDeleteUnakuta mfano kwenye Vyuo Vikuu vya mataifa yao raia wa nchi zao wanalipa ada kidogo mno ukilinganisha na wanafunzi wageni toka nchi maskini kama Tanzania kwenye Chuo hicho hicho.
Hawana huruma hao wazungu kwenye ada za vyuo vyao.Mgeni hata kama umetoka kijijini kwenda kusoma vyuo vyao utalipa ada kubwa kuliko anayolipa mtoto wa bilionea Bill Gate kama mnasoma naye chuo kimoja.
Mimi naona hao wapagazi kuwalipisha gharama ya tofauti na wanayowalipisha wazawa ni sawa kabisa tena nawapongeza.Mbona kwao tunalipa bei juu kwenye vyuo vyao kuliko wenyeji wa nchi zao na wao hawatutetei wala kutuhurumia
koloboi@yahoo.com
kweli Aliko mzee wa Suomi nakubaliana na wewe.
ReplyDeleteHaiingii akili eti mtu atoke na mzigo ulaya ashindwe kubeba kutoka kwenye teksi kuingia nao kwenye boat.
Na wazo la tourist Centers ni muhimu sana hasa maeneo kama bandarini,airport,kwenye vituo vikubwa vya mabasi kama vile ubungo.
Nilitembea mwaka huu vyoo vya pale kwenye lile soko la samaki la ferry.
Jamani inatia uchungu kweli utafikiri hakuna waliopewa kufanya tenda za usafi pale.
Vyoo vichafu hadi kichefu chefu.Pili kuna baadhi ya vifaa mule vimeharibika hata kufanyamatengeneza hakuna.Wanasubiri usipo ziba ufa ili wajenge ukuta.
ENE WEI TUTAFIKA TU.
Bwana Michuzi,
ReplyDeleteNakubaliana sana na malalamiko hayo. Kwa upande wa kutunza vyoo, nasikitika kusema kwamba, Watanzania wengi wanaochukua tenda za hivyo vyoo vya kulipia hawana asili ya usafi hivyo kazi hawaijui kabisa.
Kero yangu kubwa ni tofauti za bei kwa kuangalia rangi hili sio kwenye nauli za Boti tu!! (ingawa ni kero kubwa) Mimi nipo hapa A-Tauni, tatizo hilo lipo hata kwa Taxi drivers, na wakati mwingine hata ukifuatana na Mzungu bei inabadilika kweli huu ni ulimbukeni wa hali ya juu!! Eti inaitwa (Mzungu Price)
Pia kwenye vitu vya utamaduni, bei ni kubwa sana sasa hatuelewi ni kwanini mali ya hapa kwetu inakuwa kubwa kuliko vinavyotoka nje! Hii inasababisha sana hata wananchi kuthamini vitu vya nje kuliko vya hapa kwetu.
Tatizo la boti nashauri Wizara na Sumatra waingilie kati ni aibu sana, nadhani ndio maana wanatukomesha kwenye MIKATABA HAWA JAMAA!!!!
i agree na yote yanayolalamikiwa na watali pamoja na most of comments from wadau...these are chronic problem areas...inasikitisha sana...kazi kubwa sana yahitajika kusafisha zogo hili...it will be like organising HILLBROW in johannesburg back to shape...it can be done...
ReplyDeleteAsante sana!! Nyie mnashangaa bei tu! Kuna kero nyingine huku Kilimanjaro na Arusha hasa kipindi hiki wanaita HIGH SEASON hawa wenzetu wa Kampuni za Utalii. Wakiona Mzungu tu!! Wanakimbizana nao hata kilomita 10 ili mradi wamshawishi apande Mt. Kilimanjaro au kwenda mbuga za wanyama na kampuni zao.
ReplyDeleteSasa ngoja uwakute wakimwaga sera zao haangalii huyu mgeni amechoka,au anahitaji muda wa kutafakari mambo yake.
Wao ni kumwaga sera zao tu na kuwabana bana ovyo ovyo, mara nyingine wakisimama kununua vitu madukani au sokoni wanawasubiri mlangoni wakati mwingine wanadiriki kubonyeza muuza duka apandishe bei ili baadae afuate cha juu!!
Yaani kwa kifupi wanawanyima raha kwa kiasi kikubwa na kwa bahati mbaya kuna wengine wezi.
Sasa huu umachinga wa hivi unatia aibu sana. Ni vizuri wafungue website au watengeneze vipeperushi, business card ili wawapatie wakipenda watafika bei.
BARUA YA WAZI KWA MKURUGENZI MKUU WA SUMATRA.
ReplyDeleteMzee wewe ndo mwenye dhamana na usalama wa wasafiri nchi hii.iweje bei za daladala upange lakini za boti dar/zanzibar usipange?iweje uruhusu abiria waibiwe mchana mchana?toa amri bei ya kwenda zenj iwe moja tena kwa madafu.tunajiharibia sifa kwa tamaa za watu wachache,la hawataki hiyo bei wanyang'anye leseni,mtu mzima hatishiwi nyau bwana.
Kwa kweli kazi inahitajika
ReplyDeleteSikubaliana kabisa na huyo annoy wa August 30 saa 2:36: 00 kuna tofauti huwezilinganisha garama ya usafiri na kitu kama elimu na kumbuka yoyote aendayesoma nje ya nchi yake huwa analipa kama International student……au ulitaka na garama ya basin a train etc wakuchaji pia kama mgeni????maana ndo Tanzania inavyofanya.
Ni sawa kabisa pale ambapo kuzuru mbuga za wanyama wageni wanalipishwa bei tofauti na sisi wenyeji lakini jamani mpaka usafiri???? Mimi sioni maana yake zaidi ya tamaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Bado tuna safari ndefu sana
Mimi naona ni sawa kabisa walipuliwe na bei tofauti hata ingewezekana kila mahali.Leo hii ukienda ubalozi wa uingereza uliopo Tanzania, kwa mtu anayetaka kuishi UK zaidi ya 6 month, inabidi ukapimwe TB/typhod sijui na vidudu gani-na hii sio hospitali yoyote ile ya taifa au ya Tanzania, ni kwa muhindi fulani ambaye nadhani anakula nao au ana uraia wa kwao,bei ni pound nyingi kadhaa.Ukichanganya na mifano mingi kama ya vyuo nje etc,naona lazima kama serikali imeshindwa kuwakamua ,wacha mateja waisaidie serikali....jamani sasa mmnataka mtanzaniaakienda Ngorongoro au Serengeti alipe bei moja na mtalii?Upumbavu gani huo??
ReplyDeleteYes ,Koloboi Umesema ukweli.
ReplyDeleteLabda na mimi nipigilie msumari. sasa hawa wazungu wanataka kuundwe tume ya bei itakayosimamia bei?
Wao wenyewe si ndio wanaosisitiza biashara huria? Kama biashara ni huria mtu yuko huru kubeba mzigo wa Mswahili kwa kumcharge shilingi mia moja na kumdai laki moja Mzungu kwa mzigo wa kiwango hicho hicho cha uzito na umbali kama wa mzigo wa mswahili.
Waambieni hao wazungu kuwa hiyo ndiyo raha ya biashara huria waliyotushinikiza tuitekeleze katika mipango ya kurekebisha uchumi.
Waambieni siku hizi tunajua kuangalia nani anazo hela nyingi na nani hana katika kuamua bei gani tum-charge kama wao wanavyofanya kule nchini kwao kwenye Market Segmentation.
Kuhusu kulipa nauli dola wanapoenda au kurudi Zanzibar kutoka Tanzania Bara waambieni kuwa hizi ni nchi mbili tofauti hivyo unapotoka nchi moja kwenda nyingine lazima ulipe dola!
ReplyDeleteWakikuuliza maswali zaidi waambie wanaingilia mambo ya ndani ya nchi wakukome!
Naungana na wenzangu hapo juu, ni kweli hakuna huruma huku kwao wanatulipisha ada kibao hata daladala walipe nauli kubwa wao si walijipangia bei za vyuo kubwa sasa iweje sisi watuingilie? walipe mahala popote pale. Soko huria, hawana huruma hao wakiwa kwao.
ReplyDeleteSikubaliana kabisa na hawa wanaosema eti ada ya vyuo wanalipishwa sioni haki ya nyie kujustifie kwamba haya maswala ni sawa….wakija nchini wanalipa kuzuru sehemu kama mbuga za wanyama kwa kama dola karibu 200 kuingia tu wakati sisi wenyeji ni kiasi kidogo sana , sawa ni haki lakini jamani mpaka usafiri? mnataka na nyie wawalipishe bei tofauti ya kupanda mabasi , train etc mkiwa kwao?
ReplyDeleteKingine ni kwamba walau kwao kuna standard zinazoeleweka kwetu kila mtu anakwambia chake na anaweka charge anayoitaka yeye..wapi na wapi
Tatizo ninaloliona waongoza watalii wengine hawajui kuongoza watalii kama watalii.
ReplyDeleteUtakuta mtalii anauliza wapi anaweza kula chakula bei rahisi mwongozaji watalii utakuta anampeleka kwa mama nitilie.Matokeo yake ndiyo hayo unakuta anaenda kula halafu anaanza kulalamika kuwa hoteli Tanzania mbaya zina huduma mbaya, hazina vyoo vizuri n.k Wazungu wengine Walivyo wajinga wanafikiri kwa mama nitilie alikopelekwa ni hoteli ya hadhi ya juu nchini wanakokula mawaziri! Ndiyo maana nay eye kapelekwa.
Waongoza watalii iweni wajanja.Akisema nipeleke penye bei rahisi nikale chakula mwambie ni mbali mno halafu siyo salama mpeleke na kasha mpeleke hoteli ya kitalii..Usikubali kumpeleka vichochoroni.Hata akipaona kama mnatembea akitaka kwenda mwambie si salama sana.Hakikisha wakati wote unampeleka sehemu za kitalii tu ziwe hoteli n.k huko hawezi lalama kama hawa waliomlalamikia Irene atakutana na wahudumu wazoefu pia ataacha pesa zaidii hapa nchini akipelekwa hoteli kubwa kuliko akila kwa mama Nitilie.
Kazi kwenu waongoza watalii msikubali jina la hoteli za nchi lichafuke kwa sababu ya nyie kuwapeleka vichochoroni kula hata akitaka kujisaidia tafuta hoteli ya kitalii jirani mlazimishe hata anunue soda hapo ili ajisaidie usimpeleke vyoo vya jiji.Iweni wajanja waongoza watalii.
Koloboi@yahoo.com
the guys bugging watalii znz wanaitwa papasi...ni kweli they are a sore...kuhusu nauli,kutoka kwa ndege huko makwao, a return tkt is cheaper if it originates from there than if it originates from here...sisi huku pay more...package tours, one week in znz mahoteli kule east coast kulala tu, kula unajitegemea including a return air tkt costs 1000USD...ni kweli some wanashangaa these relatively or rather comparatively small hic ups wanazopata huku but sisi tukienda kule tunaumia zaidi...you have to have been majuu to appreciate that generally wenzetu wakija huku ni mteremko flani hivi...ni jinsi nionavyo.
ReplyDeleteInabidi tubadilike na tuelewe kua chooni si sehemu inayostahili kuwa chafu
ReplyDeletendugu zangu wabongo tuulizeni sisi tulioko majuu..wazungu tunawaabudu sana wanapokuwa kwetu njooni kwao muwaone hawana huruma na sisi hata chembe..baadhi ya huduma zao zina bei za uzawa na za wageni..hata wasiposema lakini wana fix kujitosheleza wao ni ubaguzi mtupu..wachajiwe zaidi afterall wana hela za kutosha hawafeel hizo gharama ..
ReplyDeleteNdugu zangu hao watu msiwape special teatment kama kwao mbinguni uongo hakuna lolote kwao pia kuchafu nenda vyoo vya treni harufu mbaya ajabu.. mijini vilelevile . tabia za binadamu zinalingane wasijifanye malaika, viloba vya uchafu vimezagaa mitaani..bro michu nitakutumia picha wadau waone.
Duuh wadau bora niyamaze ninausongo nao sana hawana maana hao wanafiki wakija huko "jambo" "jambo" huku wanakupita hata kama unauwawa...
Ungewaambia kuwa kuna bei tofauti kwa vile wenyeji wanalipa tax. Hivyo kwa vile wao hawaishi hapo basi ni lazima walipe hiyo kodi. Wasikusumbue kwa maswali hata huku tuliko ni pesa tu wanajua. Hivyo they get what they pay.
ReplyDeleteWamezoea mambo ya kutreatiwa kama king kwa vijisenti tu. hata huku wanasumbua sana. Walalamishi sana once they pay for something they fill they own you. Makazini tunakofanya kazi wakijua wewe ni mtaifa basi watataka sababu ya kumuita boss wako ili walalamike tu...wamezidi
ndio maana yule mtoto wa teen usa walivyokuzwa na mind zao kaulizwa swali la ujinga wao anatupia "america should help education more in south africa and iraq" pumbavu sana wana sterio type sana hawa hata ukifanya kitu vizuri kwa vile wewe ni mweusi watatafuta sababu....
msiwanyenyekee kama Mungu ni binadamu kama watu wengine
MICHUZI UNAKUMBUKA WEWE MWENYEWE KUNA KIPINDI ULISHATOA PICHA YA UFUKWE WA POSTA YA ZAMANI AMBAO SERIKALI IMEPIGA SENYENGE,MI NI MMOJA WA WATU NILIOKWAMBIA WATANZANIA HATUSTAARABIKA,SASA KAMA CHOO CHA KULIPIA NI KICHAFU SASA HIVYO AMBAVYO SIYO VYA KULIPIA VIKOJE?BONGO KAZI IPO TENA SANA.
ReplyDeletewe anonymous wa august30,9;56pm sijui uko kwa wazungu wa wapi ?kuhusu usafi jamaa wako fresh ndiyo maana huwezi kusikia kipindu pindu wala malaria,na inzi kuona ni adimu ,toa credit panapostahili,masuala ya ubaguzi hayo yanaeleweka.
ReplyDeleteMimi nikiwa mmoja wa viongozi wa wabeba mizigo nasema hao wazungu ni waongo wakubwa.
ReplyDeleteBei tunapotoza huwa tunaangalia uwezo wa mtu tu na mzigo wake,na maeleweno.
Kwa mfano hata mtanzania tukikuona una suti na afya nzuri bei itakuwa tofauti na mtanzania mwingine ambaye ukimtazama tu unamjua ni maskini.
Na wazungu nao kuwabebea mizigo huwa tunawaangalia.Kuna wengine unakuta ana mzigo lakini unamwona ni maskini na unamwona kachoka na nakula kipande cha mhogo cha Shilingi 50 na mkononi ana maji ya viroba ya kunywa ya Shilingi 50 huyu bei yake tunamdai ya Chini.Sababu unajua ukimdai hela nyingi hana uwezo wa kulipa.
Hivyo si kweli kuwa tuna bei maalumu ya wazungu tu waongo wakubwa hao wazungu wenu.
Pia kuhusu hilo la kumlipisha Mzungu Shilingi Elfu 30 kwa mzigo sina cha kujibu kwa sasa sababu mwandishi wa haya madai hajaandika huo mzigo ukikuwa ni mzigo gani na wenye uzito gani.Na ulishushwa wapi kama ni eneo la Bandari au nje ya Bandari na ulibebwa kwa umbali gani na wabebaji wangapi.Maana bei ya kubeba mzigo inategemea vitu vingi si suala tu la uzungu au uswahili tu.
Hao wazungu waliolalamika wasije kuwa ni wale maskini wachovu ambao huja nchini na dola 50 halafu wanataka watalii mwezi mzima kwa kuwapunja waswahili kwa kutaka kila kitu kiwe dezo.
Watalii wengine ambao ni wazungu ni wabaguzi na waonezi hasa wakikutana na mbeba mizigo ambaye hajui kiingereza huwa wanataka kumwonea na kutomlipa kabisa.Unaweza beba mzigo akatoa hata Shilingi 50 ya chenji alizobakiza akakupa au akasema thank you tu akaingia zake melini bila kukulipa.
Mimi naona hayo malalamiko yote yaliyoandikwa yanatoka kwa watalii malofa ambao wanakula vichochoroni,wanalala Guest za Vichochoroni,na wanakula vihoteli vya vichochoroni.
Ulofa wao usitusumbue mpaka tutoe tamko na kuwalaani watanzania wenzetu.
Kuna wazungu wengine wanaokuja ni malofa sijawahi kuona hata huelewi nani aliwaruhusu kuingia nchini kama watalii.Ni dhiki tupu.
Manun`guniko hayo juu naona yanatoka kwa watalii malofa.Wale wanaofikia sehemu za watalii hawewezi kuwa na maning`uniko kama hayo.Hayo ni manung`uniko ya watalii wanaofikia sehemu zisizo za kitalii ziwe hoteli au vyoo.
Mwisho bei mara nyingi tunawatajia kabla ya kuwabebea mizigo na wanakubali sasa wanalamika nini?
wasilete ujinga hao,kama hawana hela warudi kwao,kwenye nchi zao washenzi kweli,mbona wao wanavitu kama hivyo vya tofauti ya bei,ya mwenyeji na mgeni.
ReplyDeletekwa mfano kuhusu elimu,hapa Ireland mgeni analipa hela nyingi kuliko mwenyeji,kwa mfano,mgeni atalipa ada euro alfu 8,mwenyeji analipa alfu mbili.
kwahiyo poa tu,acha tubaniane.
MANYUNYU
Sawa wasipelekwe kwa mama Ntilie au sehemu za vichochoro lakini pia ukumbuke wengi wanatamani kuonja chakula cha waswahili na kadhalika sasa hata hizo restaurants ambazo zina vyakula hivyo nazo pia vyoo vyake ni vya kishenzi�customer service mbovu�. Sio lazima uwe maskini utake kwenda kula kwenye restaurants zenye local food kumbuka five stars hotel nyingi ambazo utakuta vyoo safi, customer service nzuri vingi vya vyakula wanavyouza ni western kwa hiyo watalii huwa hawavimind wanataka local�..
ReplyDeleteHivi wewe unayesema Hotel za kitalii hawapiki local food ulishawahi kuingia kwenye hizo hoteli au huwa unapita hizo Hotel ukiwa kwenye gari lako used uliloagiza kwenye majalala ya magari Japan au Dubai?
ReplyDeleteHoteli za Kitalii Tanzania Ukitaka Local Food unapikiwa bila Tatizo lolote si lazima ule chakula kilichoandikwa kwenye menu.
Tutajie hoteli moja tu hapa Tanzania ya kitalii uijuayo wewe ambayo ilishawahi kukataa kumpikia mtu chakula Local Food alipotaka apikiwe.
Usidhalilishe Hoteli zetu za Kitalii Tanzania Zube wewe.
Ukiona chakula unachokitaka hakipo kwenye Menu waambie unataka nini watakupikia ni pesa yako tu.
Watalii wengi wanakimbia gharama.Malofa tu.Utakuta wengine wakifika siku ya kwanza wanayowasili wanafikia hoteli za kitalii na kesho yake wanahamia vichochoroni kutokana na ulofa wao lakini si kwa sababu hoteli za kitalii zimeshindwa kuwahudumia na kuwapa hivyo vyakula wavitakavyo.
Uelewe kuwa wapishi wa hayo mahotel hadi 5 star ni watanzania.Ukitaka hata Kande waweza pika.
Ukome kudhalilisha 5 Star hotel zetu na hao watalii wako malofa.
Kama wanataka vitu vya kiswahili hawataki western basi wawe tayari pia kuingia vyoo vya kiswahili.
ReplyDeleteHuwezi kwenda Uswahilini kutafuta chakula cha kiswahili halafu ukute choo cha kizungu ambacho chaweza kukuchambisha automatically kwa remote Control?.Hao wazungu wako vipi Michuzi.Ala!
Ukienda uswahilini,ujue utakutana na chakula cha kiswahili,choo cha kiswahili na huduma (customer care)za kiswahili na siyo kizungu hivyo siyo haki kupiga kelele kwani walikulazimisha kwenda huko uswahilini.
Waambieni hao wazungu wenu wakitaka kwenda uswahilini wawe tayari kukutana na uswahili kwenye kila kitu na wasipige yowe wala kunung`unika wakitoka huko uswahilini.
Kuhusu malalamiko ya uchafu na ubovu wa vyoo vya umma huko nakubaliana navyo pamoja na kwamba hata vyoo vya uwanja wa ndege mfano Ukerewe na vya stesheni nk ni vichafu hivyo hivyo!Kwa maBuruda nako loo!! usiseme vyoo vichafuu stesheni,garden,supermarket nk kuta zimechorwa ovyo ovyo huko vyooni.
ReplyDeleteKuhusu kulipishwa usafiri na kubebewa mizigo tofauti na sisi,hayo WASISEME kitu kabisaa!
Niko huku nje miaka kadhaa sasa na hayo yakulipia huduma fulani fulani kiwango tofauti na wazawa huku tunafanyiwa sana.Pamoja na kwamba tunalipa kodi kama wao na zaidi yao(kwa vile wanatupa kazi)!!
Kwa hivyo waje kwetu, walipie huduma tena sana tu; maana hela wanazo.Halafu sio wao wanao semasema kuwa sisi ni maskini sana?Sasa hizo dola kumi zinawashinda nini kumpa msakini anaye wahudumia?Wao hawana huruma nasi hata kidogo,amini haya.Wanalalamika kwa vile wanataka, kama kawaida yao, kutunyonya mpaka washindwe wao.Tusiyaruhusu haya kabisaaa!
Kama alivyoshauri anonymous hapo juu waambie kuwa wazalendo wanalipa kodi hata kabla ya kuzaliwa.
Itabidi tukutumie picha za uchafu wao huku,hii haina maana kwamba sisi turidhike,lah.
Ni vyema hao watalii watoe kwanza boriti kwenye macho yao...