shaka ssali akiteta na george kanuth njogopa (kati) na promota wa muziki wa injili mh. msama
shaka ssali akiwa na wadau wa habari wa bongo majuzi. kushoto ni george kanuth njogopa wa clouds 88.4 fm ambaye ndiye aliyetuletea habari hiyo hapo chini
Mwanahabari mkongwe ambaye bara la Afrika inajivunia kwa sasa Shaka Ssali, amekuwa nchini Tanzania kwa siku kadhaa ambapo pia aliweza kufanya mahojiano ya moja kwa moja live na Rais Jakaya Kikwete.
Shaka ambaye pamoja na kuwa mhariri mkuu wa Sauti ya Amerika kwa Afrika, lakini pia ni mwendeshaji wa kipindi maarufu cha tv cha Straight Talk Africa ni mtu mwenye haiba machoni pa wengi ukiachilia mbali hali ya ucheshi unaotawaliwa na mizaha ya hapa na pale.
Hata hivyo nguli huyo wa habari ambaye ni mzaliwa wa Uganda na baadaye kujielimisha nchini Marekani, siyo tu ni mwenye mizaha, lakini daima huonekana kuwa makini na pia ni mjuzi wa kuchagua maneno ya kuongea.
Wakati wa mahojiano yake na Rais Kikwete ambayo yalirushwa moja kwa moja kutoka makao makuu Mjini Dodoma, Shaka licha ya kuendesha mahojiano yaliyoonekana kubeba sura ya kirafiki lakini alitupa maswali yenye mtego kwa rais Kikwete ambaye naye alionekana kujibu kwa uangalifu mkubwa bila shaka alitambua kuwa ulimwengu mzima ulikuwa ukifuatilia. Kikwete wakati mwingine alilazimika kufikiri sana na kisha alitoa jibu. na wakati fulani Kikwete alikuwa mwepesi kurekebisha kitu.

Madhalani wakati wa ufunguzi wa kipindi hicho cha Straight Talk Afrika, Shaka alitereza ulimi baada ya kusema mahojiano hayo yanaruka moja kwa moja kutoka Dodoma, nchini Tanzania, Rais alimkata kauli kwa kuingia haraka na akasema siyo Tanzania bali ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mahojiano hayo yalifanyika kwa lugha ya kiingereza.
Shaka ambaye pia alihojiwa na vituo mbalimbali vya televisheni hapa nyumbani ikiwa pamoja na kituo cha redio Clouds FM katika kipindi chake Jicho Letu Wiki Hii ambacho ni maarufu sana kwa habari za ulimwengu na uchambuzi ni msomi wa hali ya juu kwenye masuala ya mawasilino katika kiwango cha falsafa ya juu P.hD.
Akiwa nchini aliweza kukirimiwa vyema na ubalozi wa Marekani ambao pia uliweza kuratiba mambo yake mbalimbali na hata ukaweza kuandaa tafrji fupi ambayo iliyajumuisha watu wachache waliaalikwa maalumu.
Katika mahojiano aliyofanya na Clouds FM, ambayo yalifanyika kwa lugha ya kiingereza na kisha kutafsiriwa papo hapo kwa lugha ya Kiswahili na Mwamoyo Hamza ambaye pia ni mwanahabari machachari wa Sauti ya Amerika, Shaka alijieleza vyema historia ya maisha yake na hata ndoto zake kwa siku za usoni. Mwamoyo Hamza alikuwa nchini kwa mapumziko mafupi.
Wakati wa mahojiano hayo, Shaka alieleza Clouds FM, kwamba alizawaliwa nchini Uganda na kupata elimu za awali nchini humo. Baadaye alilazimika kuikimbia Uganda baada ya kulazimishwa kuingia jeshini na kiongozi wa wakati ule Idd Amin Dada. Alitimkia nchini Marekani ambako baadaye alijiunga na Chuo Kikuu cha California, kabla ya baadaye kuajiliwa na Sauti ya America. Hadi sasa anasema kwamba ameshahoji marais wa Afrika zaidi ya 15.
Anakumbuka jambo moka kuwa ilimchukua zaidi ya miaka 4 kuweza kupata mahojiano na rais wa zamani wa Kenya Daniel arap Moi. “ Lakini jambo la kushangaza nilipofanikiwa tu kumhoji akawa rafiki yangu mkubwa na nikamoji tena zaidi ya mara tano. Hata wakati anaondoka madarakani alinikaribisha nyumbani kwake na akanialika pia kwenye shule yake moja nikatoa mhadhara” anasema Shaka
Miongoni mwa maswali mengi aliyoulizwa na kujibu, ni pamoja na hili ambapo mwendeshaji wa kipindi cha Jicho Letu Wiki Hii alimuuliza Shaka kuwa, Where do you see your self after ten years to come,,, ambako shaka hakukawia kutoa jibu. I see my self coming back to Africa, akaulizwa tena doing what, akajibu kwa madaha , doing what I like to do, akimaanisha kwamba ataendelea na fani yake hii ya habari.
Katika hilo alisema kuwa angependa kuungana na wanahabari wengine wa Afrika kuhakikisha kwamba bara hili linapata msukumo mpya kwani kwa muda mrefu bara hili limekuwa halitendewi haki na vyombo vya habari vya magharibi.
Shaka ambaye ni mrefu kwa kimo na hupenda kuzungumza kiingereza kinachoweza kueleweka na kila mtu mwenye ufahamu wa lugha hii, alihitimisha mahojiano kwa neno la mzaha lakini lenye tahadhari kubwa ambapo alisema “If you what the history to favor your self, either your write your self or commission some one”. Bila shaka hapo alilenga kusisitiza matarajio yake ya kurudi Afrika na kuunganisha nguvu kwa ajili ya kubadili picha mbaya inayopachikwa na vyombo vya huko ng’ambo.

Mahujiano ya Shaka na Rais yanapatikana kwenye link hiyo hapo chini:
ReplyDeletehttp://www.voanews.com/english/Afric...TalkAfrica.cfm
Naona hiyo link hapo juu inagoma ila ukitaka kuona mahojiano click link hii then under the latest show click window media play umuone rais wetu
ReplyDeletehttp://www.voanews.com/english/Africa/StraightTalkAfrica.cfm
Sipati picha hivyo vingereza vibovu vilivyojiri hapo CLOUDS FM maana kila sentensi ya kiingereza hapo juu ni mbovu. Hata movie ya Bongo land II wewe subiri ukikuta mahali kuna kiingereza hata cha lazima ni kibovu. Watanzania tumieni Kiswahili au tafuteni watu mahiri kwa kiingereza muwalipe vizuri. Viingereza vibovu vinakinaisha!!!
ReplyDeleteEbwana Huyu Jamaa Nami Namkubali Sana Hasa Hawapo Kwenye Kipindi Chake!....Shaka Stei beta endi noti bita!
ReplyDeleteIzz Wa
Habari nzuri Kaka Michuzi. Lakini huyu George Njogopa ambaye naamini ni msomi wa habari mwenye upana wa mawazo juu yazo, kwa nini anakuwa anachapia namna hii? Kipindi chake kingeweza kuwa moja ya vipindi bora saana kama asingekuwa ana"dongoa" na nilidhani ni kwa sababu anakuwa "live". Sasa soma hiyo nukuhu aliyoweka hapo chini ktk aya ya mwisho ambayo kwa hakika haieleweki.
ReplyDeleteSijajua kulikoni, lakini nadhani anastahili kujiangalia ama kujitafakari mara kadhaa kabla hajayaweka hewani. Hata ku-edit hiyo aya ambayo nina hakika aliisoma (ama alitakiwa kuisoma na kuihariri kabla hajaituma kwako) kunamshinda? Come On George, you know better than that. Apart from that, just keep up informing mankind
Jamani Tatizo si Huyu njogopa tu, ingawa angetafuta mtu aisome habari kabla hajaituma ili pawe na marekebisho.
ReplyDeleteKiingereza ni tatizo sana nchini mwetu, kuanzia UDSM Graduates, Wakurugenzi, Mawaziri, Wabunge. Yote hii ni kwa sababu Primary Schools zilikuwa/bado zinafundisha kwa Kiswahili, Secondary schools za government zilikuwa/bado ni za kiingereza but mwalimu anafundisha na kuongea Kiswahili, so hili ni tatizo la kizazi kilichopita, tuangalie kizazi kijacho 15 to 20 years to come, na sisi tutakuwa kama Wenzetu Waganda na Wakenya, tutaongea kiingereza safi
NJOGOPA ANAJITAHIDI SANA KAMA KIJANA MWENZETU SEMA TU ANGEMPA MTU A- EDIT HATA MTOTO ANGEONA HIVI VIJIKOSA, KEEP IT UP G.
ReplyDeleteSHAKA WEWE SANA TU DO U KNOW SWAHILI?I MEAN YOU ARE VERY GUD TRAIN THESE BROTHERS WAWE KAMA WEWE KAKA, HASWA G NA SHAFII DAUDA KWA SPOTI