twanga wakipepeta jijini london wikiendi ilopita. ijumaa ijayo watakuwa rotterdam kuvunja jungu kwenye ukumbi wa party centrum de hooiberg, mtaa wa galvanistraat namba 34 rotterdam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Tujulishe Mpakanjia anaendelaje hali yake. Maana mara tusikie ameenda Kigamboni na John Komba kumuomba msamaha YULE BABA MKWE WAKE WA KIARABU.

    ReplyDelete
  2. Mkataba wa Buzwagi ulisainiwa nje haraka ili kukwepa gharama

    Habari Zinazoshabihiana
    • Udurusu mikataba ya madini wakamilika 15.08.2007 [Soma]
    • Suala la rada danadana tupu 08.02.2007 [Soma]
    • Kikwete asifia mradi wa Buzwagi 24.08.2007 [Soma]

    *Barrick yasema majadiliano yalichukua muda mrefu
    *Yasema kisheria mkataba unaweza kusainiwa popote
    *Yaeleza jinsi uchumi wa nchi utakavyokua kwa kasi

    Na Said Mwishehe

    KAMPUNI ya uchimbaji Madini ya Barrick Gold Tanzania imesema mkataba wa mgodi wa Buzwagi uliharakishwa kusainiwa Uingereza ili kuepuka upandaji gharama za uendeshaji.

    Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Barrick Gold Tanzania, Bw. Deo Mwanyika, kutokana na majadiliano juu ya kusainiwa kwa mkataba huo kuchukua muda mrefu, Barrick iliiomba Wizara ya Nishati na Madini kuharakisha uamuzi wake kwa vile ucheleweshwaji wa utiwaji saini ulikuwa ukiuathiri vibaya.

    "Tuliona ni vema tukaharakisha utiaji saini wa mkataba huo baada ya kuona kwamba kama tutachelewa kuna hatari za kuathirika kwa mradi wenyewe kutokana na kupanda kwa gharama za vifaa kila kukicha. Kwa mfano kati ya Juni mwaka jana na Januari mwaka huu, gharama za mradi ziliongezeka kwa kiasi cha dola milioni 20 za Marekani," alisema.

    Kwa upande wa Barrick alisema kulikuwa na ulazima wa kuharakishwa utiaji saini huo kabla ya mwisho wa mwaka huu, ili makao makuu ya kampuni hiyo yaweze kuweka mgodi wa Buzwagi katika mpango wa makadirio ya mwaka.

    Bw. Mwanyika alisema kutokana majadiliano yaliyofikiwa kati yao na Wizara ya Nishati na Madini, waliarifiwa kuwa mkataba wa Buzwagi ungekuwa umesainiwa ifikapo Februari 16 mwaka huu.

    "Barrick tuliambiwa kwamba vibali vyote kutoka vyombo husika vya Serikali vilikuwa vimepatikana. Kutokana na hali hiyo waliendelea kukamilisha taratibu za kusaini mkataba Februari 16 mwaka huu ikiwa ni pamoja na kuandaa maofisa wake walioidhinishwa kusaini mkataba huo na nyaraka zinazoendana na mamlaka hizo," alisema Bw. Mwanyika.

    Hata hivyo, alisema kwa bahati mbaya, ilipofika Februari 15 mwaka huu, wakaambiwa kwamba mkataba huo usingeweza kusainiwa kutokana na Waziri wa Nishati na Madini kuwa katika ziara ya Rais Jakaya Kikwete katika nchi za Ulaya.

    "Kutokana na kuona kwamba kuna hatari ya kutosaini mkataba huo wakati muda unazidi kwenda, uongozi wa Barrick uliwasiliana na Wizara na kupendekeza kwamba isingekuwa vema kuahirisha utiaji saini mkataba huo, kwa vile taratibu zote za maandalizi zilishakamilika," alisema Bw. Mwanyika.

    Alisema baada ya kutoa ombi hilo, ndipo walipoarifiwa na Wizara kwamba Bw. Karamagi angepatikana London, hivyo ujumbe wa Barrick uliondoka Tanzania na kwenda Uingereza ambapo mkataba ulisainiwa Februari 17 mwaka huu katika Hoteli ya Churchil ambapo mbali na maofisa wengine wa Wizara ya Nishati kuwapo, pia Balozi wa Tanzania nchini London, Bibi Mwanaidi Maajar naye alikuwapo.

    "Ni kweli tulisaini hotelini na hilo si kosa, kwani mkataba unaweza kusainiwa mahala popote pale, ilimradi uzingatie sheria na taratibu. Kuhusu nani alichukua mhuri na nyara nyingine za Serikali, hadi Uingereza hatujui, ila inawezekana ni maofisa waliokuwa Tanzania ambao tulikuwa tukijadiliana nao juu ya suala hilo nchini na baadhi yao tulikuwa nao wakati wa utiaji saini, hivyo inawezekana ndio waliokwenda na nyaraka hizo za Serikali," alisema.

    Hata hivyo alisema Barrick haina ofisi wala kampuni Uingereza na wao pia walikuwa wageni ambao walikwenda huko kwa jukumu la kuhakikisha mkataba unasainiwa kama ilivyokuwa imepangwa na kukubalina na Serikali. Lakini ni vema mambo mengine muwaulize maofisa wa Wizara ya Nishati na Madini," alisema.

    Akieleza zaidi juu ya mgodi wa Buzwagi, Bw. Mwanyika alisema pamoja na kusaini mkataba, bado kwa sasa mgodi huo hauna faida kutokana na kwamba hauna dhahabu ya kutosha, ambayo inalingana na gharama zitakazotumika kujenga mgodi huo.

    Alisema mradi wa machimbo ya Buzwagi ni mgodi mdogo unaohitaji uwekezaji mkubwa wa dola milioni 400.

    "Mradi wa Buzwagi ni mdogo, kwa sababu pamoja na kutumia dola milioni 400 ili kuuchimba, utazalisha wakia milioni 2.4 ikilinganishwa na mgodi wa Bulyanhulu ambao ulitumia dola milioni 280 kutoa wakia milioni 10 za dhahabu," alisema Bw. Mwanyika.

    Alisema kutokana na kukosekana kwa dhahabu ya kutosha katika mgodi huo, hakuna kampuni ya uchimbaji duniani ambayo ingekubali kusaini mkataba wa uchimbaji madini ambao utaleta faida ya sh. bilioni 800 kutokana na makato ya kodi mbalimbali kwa kipindi cha miaka 10.

    Alisema mbali na Serikali kupata kiasi hicho cha fedha, pia wanakijiji wa Mwima ambao ndio wako katika eneo la mgodi wa Buzwagi, wamelipwa fidia sh. milioni 78 mbali na sh. milioni 60 zitakazokuwa zikitolewa kila mwaka kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya wana kijiji.

    Vilevile wakati wa ujenzi wa mgodi huo, uchumi wa Tanzania utaongezeka, kwani wakati wa ujenzi kiasi cha sh. bilioni 450 zitapatikana na wakati wa uzalishaji, sh. trilioni 1.3 zitapatikana katika kipindi chote.

    "Kusainiwa kwa mgodi wa Buzwagi, nchi itapiga hatua kiuchumi, kwani wananchi watafaidika na mgodi huo kutokana na ajira zitakazopatikana, lakini pia ni kuhakikisha maendeleo ya wananchi yanaboreshwa hasa walioko eneo husika," alisema Bw. Mwanyika.

    Alisema ajira mpya zaidi ya 900 zitatokana na uwekezaji huo katika kipindi cyha ujenzi na kuingiza jumla ya sh. bilioni 75 kama mishahara.

    "Vile vile kutakuwapo na ajira nyingine 700 zitakazoingiza jumla ya sh. bilioni 130 wakati wa uendeshaji wa mgodi," alisema Bw. Mwanyika.

    Mgodi wa Buzwagi umeingia katika duru za habari baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe, kuwasilisha hoja bungeni akidai kuwa kitendo cha kusaini mkataba wa mgodi huo nje ya nchi kilikuwa na dosari.

    Bw. Kabwe kutokana na hoja yake, alitaka iundwe Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mazingira ya mkataba huo akidai kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Karamagi, alikuwa amelidanganya Bunge. Hata hivyo mambo yalimgeuka na kujikuta akisimamishwa kazi hadi Januari mwakani

    ReplyDelete
  3. Anon hapo juu Mpakanjia awe kaenda kigamboni au la ina kuhusu nini? ni maisha yake binafsi.
    Mnachekwa na mataifa mengine maana kutwa kushupalia yasiyo ya maana wakati wengine wanatafuta maisha wake kwa waume umbea mtupu, aibu sana mijitu mizima kuchunguza eti fulani kafanyaje? nie watanzania mataishia kutafutiana fitina, umbea, unafiki, wajinga sana.

    ReplyDelete
  4. si lolote wala si chochote hao ni extra muzika wa tanzania
    wanajitahidi sana kuwa wacongo
    bure kabisa!

    ReplyDelete
  5. Bloody attention seekers ! Why on earth a put the note above under Twanga pepeta for Crying out loud ?
    On a serious note nani anajua kama Twanga wanapiga Milton Keynes weekend hii ?
    Nilikwenda kwenye website yao na mara ya mwisho kuwa uptodated was October 06 for goodness sake !
    Kalagabaho

    ReplyDelete
  6. Watanzania hongera kwa kuanza kusajili kampuni za miziki promotions nje ya nje ya kupromote watanzania.

    Anzeni kusajili pia makampuni ya kuuza na kununua bidhaa za tanzania.

    Pia sajilini dini za watanzania huko kama wazungu na waarabu na wahindi walivyokuja kusajili za kwao huku.Na wekeni viongozi wa kidini kama Papa,Mitume N.K wa kitanzania.Mtume wa Allah wa kwanza mtanzania napendekeza awe huyo Mugongomugongo.

    ReplyDelete
  7. Jamani hayo mabuti. Watu wa UK hebu mkawaonyeshe wapi wanunue viatu vya Summer au UK summer sasa hivi? i cant imagine wanavyo sweat humo ndani

    ReplyDelete
  8. Bw. Deo Mwanyika atuambie pia kampuni hiyo inatarajia kuvuna pesa kiasi gani, watakuwa wametumia pesa ngapi katika uwekezaji siyo kueleza tu Tanzania na kijiji husika kitapata kiasi gani ili tuone kama inalipa au la!

    ReplyDelete
  9. we Anony 12:00 usitake kuwaziba watu kinywa wacha wateme cheche zao hata mimi nimepata tetesi kuwa yule muheshimiwa mbunge swahiba wake MEDI kaonekaba maeneo ya ferry anaelekea Kigamboni.
    Jamani tuambieni ukweli kwani wakienda kumuomba msamaa kuna tatizo gani si ndio uungwana.

    ReplyDelete
  10. Kwa kweli kuna mijanadume kama mibint i,kazi yao umbea tu mara leo flani kamtia mimba flani, mara mpakanjia kaenda kuomba radhi kwa mkwewe,ili mradi haitafuti mambo ya maana yakadiscuss kudiscuss mambo yaliyokuwa hayajengi tu,pumbaffff

    ReplyDelete
  11. KAKA MICHU VIP ETI MEDI ANAENDELEAJE?NAMUOMBEA UZIMA APONE MAPEMA.TUJULISHE AU FAMILIA PAMOJA NA YEYE AMEWACHIMBA BITI KUONGELEA HALI YAKE?MAANA SIONI UKILOPOKA CHOCHOTE TANGU SIKU ULIPOWEKA HIYO NYUZI

    ReplyDelete
  12. mambo ya deo mwanyika,barrick,karamagi,zitto, mh. six etc yaacheni hivyo hivyo ndugu zangu.atakayezidi kuchonga shauri yake akishushwa mshipa.we are talking about big money halafu nyie eti uzalendo,uzalendo ndo nini? kama nyie mmeshindwa kukaa mkao wa kula pandeni mlima eldonyo lengai mkayeyuke huko.

    ReplyDelete
  13. Kweli TZ bendi ni Nginde na Msondo tu

    ReplyDelete
  14. We anon august 28,2007 4:47 PM na mwenzako pale juu acheni ushamba na ulimbukeni.Sisi watu wenye akili zetu tutahoji hadi tujue hali ya medi na kama kaenda kigamboni pia tujue.Kwani huko kigamboni alivyoenda alichomoa drip aliliokuwa nalo au Komba alimshikia njiani na kuondoka likining'inia?kuhoji lazima.Kama wewe unasema ni wanaume kama mabinti ni kivyako na shida zako za kuinga maudhui ya Lady JD.Kwani mwanao akipigwa mimba na wadau wa hapa kijijini hutohoji???kama emeishiwa Shiiiiiiiii!!!!!
    Majita

    ReplyDelete
  15. NAKUPA SHAVU MAJITA!
    HUYO ANONY 28,2007 4:47PM NDIO WALE WALE WANAO OGOPA KUULIZA BEI YA SAMAKI WAKIOFIA BEI.

    KAMA NOMA NA IWE NOMA TU KAKA MCHUZI TUAMBIE KULIKONI KWANI KUNA UBAYA GANI?NASISITIZA HATA KAMA WALIENDA KIGAMBONI NI JAMBO LA BUSARA TU KUOMBA MSAMAHA.
    MICHU MPIGIE SIMU YULE MH.
    ANAYEONGOZA KWA KUIMBA ACHILIA MBALI AJAWAI HATA MARA MOJA HAJAWAHI KULA TUZO YA KILI

    ReplyDelete
  16. we annoy wa 12.00pm we siyo mtanzania? mpaka useme "watanzania mmezidi kwa umbeya na fitina" Tunataka kujua hali ya Mpkanjia ndiyo maana tumeuliza, wewe kama hutaki kujua kaa kimya, lakini siyo uzuie wenzako wasiulize. Kwanza unatuzuia wewe ukiwa kama nani? Kila mtu ana uhuru wa kuchangia mawazo na kuongea chchote ili mradi havunji sheria. Hatujamtukana mtu hapa bwana umesikia?! PEACE& LOVE!!!

    ReplyDelete
  17. Mmmh! Twanga mmezidisha haya ma boot huku ukerewe yanavaliwa summer labda mngekuja kuanzia november tungewaelewa...mmmh mmepania sana ..next mime ulizeni wenyeji jinsi ya kuvaa.
    Jamani Internet na Choki wako wapi? nasikia wana SOOOO! hawaingii ukerewe wadau mwalijua hilo?

    ReplyDelete
  18. hao annoy wa 12.00pm na wa 04.45pm wamenishangaza, wao ndiyo wale wa 19th kweusi!!! Kwani kuuliza ni matusi? kwanza hamjaulizwa nyie so kama hamkuwa na jibu mngenyamaza tu mana hayawahusu. Ambao wanajua taarifa hizo watachangia tutajua hali ya Mpakanjia. Huyo aliyesema sijui wanaume kama binti, Yeye ndiyo mwanaume kama binti na kama ni mwanamke basi mumewe au bwanake ndiyo mwanaume kama binti tena dikteta wa mawazo!!!

    ReplyDelete
  19. Wadau maada ya mpaka njia si mahala pake mwacheni kidogo apumzike..

    Nauliza CHOKI na INTERNET wako wapi? Eti walinyimwa VIZA?basi wawatoe kwenye matangazo wanatuchanganya.

    ReplyDelete
  20. Lilly internet alikuwa Milton Keynes kasugua vyoo vya wazungu na kuuza kiuno haikulipa , mbaya akazidisha siku kibao kurudi bongo kapigwa wino mwekundu 'NO UKEREWE'

    Kaka Choki sina zaidi ila yasemekana kuna mama anamlea Milton utamu ukamponza kazidisha siku wazungu wakamiga BARN.

    mdau anejua zaidi tupe nyuuuuzzzz

    ReplyDelete
  21. Bro Michuzi, seems like you are very selective in posting comments. Why is it you are avoiding to publish the fact that Ali Choki was not amongst the Twanga Pepeta delegetion. Come on .... we hidding something? Well if not then lets get to the point: Why tell people that we will be seeing the "Full Band" not mentioning "Without it's lead vocal and bang leader". Cheers, Mlonga Mbeka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...