Mzee michou naomba kuna baadhi ya mambo tuweze kuyabadilisha na tuondoe unazi wetu wa miaka 100 iliyopita, hivi sasa hiyi mijizungu yote ipo pamoja na wanaelewana ile mbaya na wanasaidiana, sisi bado tupo na unazi hata kwa ndugu wa tumbo moja sometimes unaleta upinzani munakuwa hamuelewani.
Napenda tu kujulisha kuwa hivi sasa sisi tunaingia ktk hali ya kujikomboa kiuchumi na kimaendeleo, karibuni tu miaka kidogo inayofata East africa Comunity itakuwa na hela moja, kwa hiyo sisi hivi sasa ni wamoja kama vile nchi za ulaya na marekani, United Kingdom tuondoe ule Utanzania na Ukenya, tunatakiwa baadhi ya mambo tuyafurahie.
Muda mfupi tu uliopita wanariadha wetu wa East African Comunity wa kiume wamenyakua nafasi zote tatu za kwanza kwenye mashindano ya Dunia, na vile vile wakike amechukua ubingwa wa Dunia. Hili naomba tujivunie sana kama tunataka maendeleo kama muungano wa hiyi mizungu huku Ulaya, kama tutakuwa na muungano na kuona wale ni wakenya na sisi ni watanzania maisha hatutoshinda, naomba hivi sasa tufungue macho na viongozi wa Riadha wakae pamoja na wenzetu wa muungano wa kenya ambao wanatisha dunia nzima ili tufanye mazoezi na wanariadha wao kwa pamoja kama kuuweka muungano wetu kujitangaza zaidi Duniani.
Michezo mingine tunaweza tukachelewa kujitangaza duniani kuliko mchezo huu wa Kufukuza upepo, tuna akina nyambui na bayi kibao Bongo wanahitaji kupata uzoefu wa makocha wa muungano wetu ambao kila leo wanatoa vifaa vya kutisha katk kufukuza upepo duniani.
mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Ujumbe umefika kaka. Nadhani wadau tutashikia bango sana suala hili. Big up

    ReplyDelete
  2. yaani mdau huyu kaongea weeeeeeee na wala sijamuelewa anabwabwaja nini. Muungano wa kenya na tz ulaya, wazungu, what????

    ReplyDelete
  3. HATUTAKI EAST AFRICAN COMMUNITY YA HELA MOJA UPO HAPO

    ReplyDelete
  4. Mdau, lugha unayotumia "hii mijizungu huku ulaya" si nzuri. Kama mzungu akisema "hii miafrika huku Afrika" sijui nini kingemtokea - angeitwa "fascist", mbaguzi etc..Wazo lako sio baya lakini tumia lugha nzuri kwani hata hiyo "mijizungu" unaonaowasema, wengine wao, wanajua kiswahili na wanaipenda Afrika labda kuliko wewe "mwaAfrika". Una hasira na nini mdau??

    ReplyDelete
  5. Saafi sana TIDO MHANDO endeleza TUT KWA KASI HII,hii kasi ndiyo inayopa MOAT PRESSURE.Mnafikiri mchezo kuajiri mtu proffessional anaejua anachokifanya?Tatizo la MOAT mmezoea CHEAP LABOUR NDIYO MAANA HAMPATI WATU WA MAANA LIPENI MISHAHARA MIZURI MTAPATA WATU WAZURI AMBAO WATAKUA WABUNIFU MTAPATA MATANGAZO SIYO KUKIMBILIA KULALAMIKA OHOOO SISI TUNALIPA KODI HATUTAKIWI KUSHINDANA NA TUT,NANI KASEMA!JUZI MNALEATEWA MUSWADA AMBAO UNAWATAKA KUAJIRI WATU WENYE DIGRII MNAKATAA KWA SABABU MMEZOEA VYA KUNYONGA SASA MATAKULA JEURI YENU,BADILIKENI

    ReplyDelete
  6. kabla hujaongelea umoja acha kuwa predjudes na pia jifunze kucommunicate na watu vizuri. Sikuelewa unaongea nini and it was short but very boring story

    ReplyDelete
  7. wajinga kama hawa wanatuchanganya tu ndani ya blog.

    unawezaje kusema wanariadha wetu wa E.Africa ??????????

    wewe unaugonjwa gani wa akili hata useme wanawakilisha Rwanda na Burundi ?

    ReplyDelete
  8. nyie wote mnaosema hamjaelewa, what part of the story dont u understand? sasa kama mnashindwa kuelewa kilichoandikwa hapo juu, i wonder how some of u perform in school, college,university.
    yeah East African Community lazima tuwe naushirikiano na acheni fikra potofu.
    from, im only saying

    ReplyDelete
  9. FIKRA MBOVU UNAZO WEWE . JAMAA WAMEBEBA BENDERA YA NCHI YAO KENYA .

    WANATANGAZAJE UGANDA ??????

    UNAWEZAJE KUDAI USHINDI WA NYAMBUI ULITANGAZA BERUNDI ??

    ReplyDelete
  10. wote unaogea kitu kimoja isipokuwa jinsi ya kuelezia ndio mnapishana, kwa suala ya hapo juu mimi binafsi ninapiga kwa sababu nyingi moja kwa sisi ya watanzania (bara na zenji) tuyamalize mambo yetu ili yote yawe wazi ndio tuingia kwenye muungano wa east african maana tutafanya mambo bidaa kujua viongozi wote hawa wafanya kwa masiliyai yao, kwanza kenya (waluo na wakikuyu), burundi (wahutu na watusi),rwanda (wahutu na watusi)na uganda wanao matatizo yao na pia wabongo . tuwalize haya matatiz o maana mwalimu J Nyerer alisema kuwa dini, ukabila ndio adui mkubwa wa maendeleo ya n chini kwa kabda hatujapiga hatua mbele kwanza tutizame wapi tulipo na matatizo yetu na wapi tunakwenda ukiwa na matatizo yetu na je tukiungana nao pia matatizo yao , tutayaiga au ndio watatuiga mfano mliona hivi karibu kwa kipindi kifupi ujambzai wa mabenki kwa kutumia silaha vitu ka hivyo vipo kenya kama kawaida kwetu sisi ndio kazi imeanza kwa kuua ndio kitu cha kawaida kama vita vya wahutu na watusi , sisi tumezoea kutukana, matusi na kashifa lakini silaha nooooo sasa je tutafika...

    pia kuhusu swala la michezo baraza au body ya michezo wanatakiwa wajiuzulu maana wengi wao wapo kwenye uongozi kwa muda mrefu na wameona matatizo lakini wapo kimya ,wanariadha miaka hii wanafanya vibaya na tuwasaidia namna gani au hawataki kubadilika na muda au wanaiba tu au wafanye utafute ni kwa nini matokeo ni mabaya, pia viongozi kwenye body ya riadha pia nao waachia ngazi maana wengi wao walikuwa wanariadha kwa muda mrefu na wanajua matatizo lakini hawafanyi kitu chochote na hii pia kwasababu hawataki wanariadha wapya wafanikiw maana wakishinda gold medali wapata mikataba ya kushiriki michezo duniani na watapata dola nyingi kwa hiyo vongozi wanaona ni vizuri kuua vipaji vyao... pia tunaomba r
    rais wetu hatizame pia michezo yote sio mpira tu.....muona na msema kweli

    ReplyDelete
  11. Acha kuita watu mijizubgu wewe wakikuita mijiafrica utajisikiaje?

    Huo umoja utauweza kama unaroho ya kubagua?

    Wakiokuambia hapo juu hawakukosea.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...