Ule usemi usemao kuwa mcheza kwao utunzwa leo ulidhihirika kuwa batili baada ya timu ya Wabongo wa Houston (pichani chini) kuicharaza timu ya TanzAtl (pichani juu) 5-3.

Mbali yakucheza katika uwanja wa nyumbani Atl walijikuta wakiloa bao 3 za haraka haraka zilizopachikwa kimianina mshambuliji hatari Peter B "Mwaikimba".(Pichaniakishangilia goli).

Atl walizinduka na kuanza kuutawala mchezo kuanzi dk ya 30 kipindi cha kwanza hadi mwisho wa mchezo na kufanikiwa kuchomoa bao tatu zilizowekwa kimiani na Kombo, Malik na Liga. Kusema kweli mchezo ulikuwa wa kuvutia na kusisimua.

Jumapili hii timu ya kikapu ya Houston itakwaana na timu ya kikapu ya TanzAtl katika uwanja wa Gwinnet Park.



Habari hizi zimeletwa kwenu na mdau Mark D.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Michu mbona ATL hujatuweka? Tumevaa green leo babu au ulidhani tumechukua timu ya MLS? Noo ndo sisi BABU!!

    ReplyDelete
  2. TanzAtl in (Green and White) and Houston in (white and black)

    ReplyDelete
  3. ooooooh bora wamefungwa hao atl maana wana midomo mirefu sana.

    ReplyDelete
  4. Ningelifurahi sana kama ningepada MAJINA ya wachezaji wote walioko kwenye picha, kuna washikaji nimewafananisha mfano, Wincheslaus Mwesiga na Asumbilwa Rashid. Washikaji, je, ni kweli ni nyie ndo mko kwenye hiyo picha au?

    ReplyDelete
  5. nakuona andrew sanga.

    ReplyDelete
  6. SABAS MNUBI kama kawaida yako ulifanya kweli na kuiwezesha h-town kuwabwaga hao washamba wa a-town...much love from kansas city
    .....mbona haukunipitia twende wote? hamna noma kwani THANKSGIVIN nipo mitaa ya beechnut and westheimer kama kawa

    ReplyDelete
  7. Kwa waliomba majina.
    TanzAtl FC:
    Standing: Hassan, Fredy Mburushi, Imma, Amani, Kombo(Former TZ U-20), Kassim na Said Chambuso.
    Down: Liga Liganga, Mogoha, Hadji Helper, Abou Dimosso, Moses "Moze", Dan na Julius.

    Houston:
    Chini:Denis Mrema, Amasha, Peter Bategeki " Mwaikimba", Jina linatafutwa, Andrew Sanga, Jina linatafutwa.
    Juu: Gunner, Teacher, Dullah, Tibaigana, Andrew na Daktari wa timu.

    ReplyDelete
  8. Hivi tanzatl.org ilifia wapi?Watu wa atl tuelezeni mlikula pesa zetu ama vipi? Ile site ilikuwa powa sana.
    by mbigiri

    ReplyDelete
  9. hivi mpira mlicheza dakika ngapi? Kama sikosei mlicheza kama dakika 60 sio 90, watu wenyewe ni mitambi tu.Hiyo mibaga toka mac d's haiendani na boli washikaji

    ReplyDelete
  10. emmanuel msiba toa e-mail yako hapa tukupige kisindano, duh long time toka mkwawa mshikaji nasikia upo na malise ndonde mpe hi halafu mwambie kinywaji taratibu maana tunasikia jamaa anashinda breweries ya huko.

    ReplyDelete
  11. Picha zaidi za tukio nenda:
    http://tanzatlfc.hi5.com . Thank you!!

    ReplyDelete
  12. hiyo ni difference squad,mwaka huu wamekuja na mganga wao wa kienyeji(kamati ya ufundi) anaitwa mzee wa Europe.

    ReplyDelete
  13. Atl ni MDEBWEDO

    ReplyDelete
  14. Poleni sana atl kwa kufungwa ongeleni houston kwa umoja mliokuwanao.Tunaomba matokeo na picha za basket pia ,kwaani nasikia houston walikuwa wakionyecha kikapu cha hali ya juu wakiongoza na muuwaji wa soko na mchezaji bora wa kikapu miaka ya 90,s peter bategeki.sijui kama kuna hukweli manake nasikia houston walikuwa wamependeza na jezi na atl waligoma kuvaa jezi za pinki zilizofadhiliwa na houston.

    ReplyDelete
  15. Mambo ya tanzatl website yalikuwa magumu maana kila hosting company ametufukuza kwa ajili ya kuelemea server zao. I guess itajaribiwa kwa mara ya mwisho tena 2008, maana shughuli nyingi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...