nahodha wa muda mrefu wa taifa staaz mecky mexime leo ametangaza kujikuzulu kuchezea timu ya taifa pamoja na kuuvua unahodha wa timu hiyo aliokuwa anaushikilia kwa miaka 5 mfululizo. amesema uamuzi huo ni wake mwenyewe na wala hajashinikizwa na mtu ama kitu, na kwamba sasa anajikita kuitumikia timu yake ya mtibwa sugar.
tff wamekubali mexime kujiuzuru na kuupongeza uamuzi wake huo kuwa ni wa busara. kocha wa taifa marcio maximo ameeleza kushtushwa na hatua hiyo ila amesema anauheshimu uamuzi huo na kwamba kwake yeye mchezaji huyo atabaki kuwa mfano wa kuigwa kwa umakini wake kama mchezaji awapo ndani ama nje ya uwanja.
tff imesema inamtafutia mexime mchezo wa kimataifa wa kumuaga rasmi katika tarehe itayotangazwa baadae.

sh

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Maxime, watu kama wewe katika jamii ya watanzania ni wachache sana. Ambao inafika muda wanasoma ALAMA ZA NYAKATI na kukubali kwamba INATOSHA, niwapishe wengine. Si kwa wanamichezo, wanasiasa wala wasomi. Katika hili tuna cha kujifunza kutokana na uamuzi wako. I real salute you Brother! Sipendi kwenda mpirani, ila nitakuwepo siku tutakapokuaga, UMEONYESHA UNAZIJUA ALAMA ZA NYAKATI. Waosha vinywa .... - O'C, Sinza.

    ReplyDelete
  2. pamoja na kuthamini mchango wake lazima tukubali kwamba mecky maxime kwisha kazi na kupumzika was long overdue.mechi ya msumbiji kwa kweli alikuwa uchochoro na clearance zake poor,hata kupanda na kushuka hawezi tena.tutake tusitake watanzania lazima tutafute beki tatu wa uhakika,lazima,hatuna njia. tumtafute mohamed chuma mpya,kajole mpya.

    ReplyDelete
  3. wadau wa neshno timu naomba tujiulize,hivi inakuwaje timu ya taifa inakuwa na vijana wengi wa mtibwa hata kanma sio wazuri sana?isije kuwa hii ni fitna ya bayser mkurugenzi wa mtibwa na bosi wa tiefef kutaka vijana wake wapate ulaji na uzoefu?

    ReplyDelete
  4. Kijana umejitahidi sana kuliongoza hilo squad la taifa, ni muda muafaka kuwaachia wengine wajaribu. Congrats Mecky. A.Mdee UK

    ReplyDelete
  5. Hivi ni kweli haya niliyoyasoma kuhusu uwamuzi wa kijana huyu tena mchezaji? Nilitegemea maamuzi kama haya kufanywa na mawaziri walioshindwa kazi katika wizara zao na kutokuwa makini katika mikataba na wawekezaji. Nilitegemea pia maamuzi kama haya yafikiwe na wakurugenzi wanaohusika ktk kuidhinisha mishahara hewa.Nilitegemea viongozi wa michezo kujiuzulu, hasa wale wasiopenda uwazi katika mgawanyo wa mapato timu zao zinapocheza.Nilitegemea wagombea wa CCM waliojitangaza kutumwa na Rais kugombea kama sehemu ya kampen zao wangejiuzulu kabla ya uchaguzi! Lakini ajabu kijana mdogo, wala siyo msomi wa kutisha, ameweza kufikia uwamuzi ghali kama huu! Mwache Mungu aitwe Mungu. Huenda huu ndiyo mwanzo wa mwelekeo mpya wa Tanzania, na kwamba huenda kijana huyu akashangaa hata yeye pale vitabu vya karne hii vitakavyomuenzi kama mwasisi wa dhana ya kujiuzulu katika uongozi kwa manufaa ya Nchi na watu wake. MUNGU AKUPE HERI KATIKA MAISHA YAKO,NA HAKIKA HUTAJILAUMU MAANA KILA BARAKA YA MUNGU IKO NAWE.MWAMINI MUNGU DOGO.

    ReplyDelete
  6. Saafi sana! Naona Mexime amepull a David Beckham. This shows a maturity of Tanzanian football.

    Big ups! And, yeah, a testimonial match would be nice for him.

    ReplyDelete
  7. Maxime HONGERA SANA!
    umeonyesha kitendo ambacho kilifanywa na mzee Mwinyi miaka ileeee! kama kwenye siasa tumeshindwa bora kwenye michezo tupate watu kama wewe. kijana umeonyesha uzalendo na ukomavu katika jamii.
    mifano hii ingetakiwa kuigwa na kina kalamagi na wenzao. congrats Maxime and God bless you.

    ReplyDelete
  8. Ndugu yetu Maxime, asante kwa kulitimikia taifa lako kwa bidii na utiifu, na pia kujua kuwapishe wenzio ili waendeleze msukumo pale ulipokomea.

    Im sure tutakuhitaji katika masuala ya ukocha au uongozi wa mpira, wewe kusanya vyeti vinavyotakiwa kazi hizo lazima utapewa. Good luck for the future.

    ReplyDelete
  9. Unbelievable!

    Hivi kumbe inawezekana eh?!

    Haya na nyie viongozi(majina kapuni), wengine hapo mmekaa madarakani weee, mwabadili tu sijui niite nyadhifa ama wizara!, mpaka Wizara zinaisha mwaundiwa Wizara mpya basi tu kulindana (recycle). Tokeeni muwapishe na wengine.

    Wengine tangu nakua nawasikia tu, Waziri wizara fulani, mpaka leo ninafanya kazi Mupo tu, jamani hata hamzeeki mkastaafu? hamuishi kuapa mahakamani ooh, umri wangu ulikosewa, kujipunguzia umri muendelee kukaa madarakani, waangalie!

    Igeni mfano huu. Kijana wa watu kaona mbali.Hajawa mbinafsi na mwenye tamaa.

    Kaka maxime, hongera sana kaka. Ni wachache sana wenye moyo kama wako, hasa kwa Bongo duh, Baba nimekukubali.

    ReplyDelete
  10. Nigeria honours under-17 players

    Nigeria president Umaru Yar'Adua has rewarded players of the country's under-17 team with a three-bedroom house each for winning the World Cup.

    The Golden Eaglets won their third under-17 world title last Sunday after beating Spain 3-0 on penalties in South Korea
    The players were also decorated with the Member of the Order of the Niger, one of Nigeria's highest honours.

    Team officials received the Member of the Order of the Federal Republic medal, another important award in the country.

    "It's just a mark of appreciation from the good people of Nigeria," Yar'Adua said during a state reception in the country's capital Abuja on Saturday.

    "Words cannot express the gratitude of the Nigerian people but we are grateful for your achievement and success."

    Unlike previous presidential gifts, the certificate of occupancy and necessary documents to the houses in Abuja were instantly given out to the team.

    The award to the Golden Eaglets is the fourth given to a football team by the democratic government since the country returned to civilian rule in 1999.

    Nigeria's under-20 team the Flying Eagles received monetary gifts for winning the African Youth Championship in 2005.

    The Super Falcons, the country's female national team, were also given cash rewards for their annexing of the African Women's Championship title in 2004 and 2006.

    Enyimba, the first Nigerian club to win the African Champions League in 2004, were also rewarded.

    ReplyDelete
  11. Maxime umekuwa mfano mzuri kwa taifa letu, hasa kwa wakati huu ambao timu ya taifa ikiwa na masilahi kwa wachezaji lakini kwa busara zako umeamua kustaafu na kuachia wenzako kwa kweli nimekuvulia kofia. nidhamu na bidii yako inatakiwa iigwe. na kama alivyo sema jamaa hapo juu unejiendeleza na kutafuta shule ya ukocha popote duniani ili uweze kuendelea kutumikia taifa lako
    nakutakia heri na mafanikio mungu akutangulie

    ReplyDelete
  12. NASIKIA WADAU WANASEMA ANARUDI KWAO MSUMBIJI BAADA YA KUKAMIRISHA USHUSHUSHU VIZURI

    ReplyDelete
  13. Eh, alikuwa shushushu tena! Na kumbe ni m-mozambikyu! Ohoooo

    ReplyDelete
  14. UMEFANYA KITENDO CHA KISHUJAA SANA NA CHENYE HESHIMA KUBWA, MUNGU AMEKUONA NA UTAPATA THAWABU YAKO HAPA DUNIA NA MBINGUNI. WEWE NI MWAMBA NA SIMBA WA VITA, NI MTUMISHI MWENYE UNYENYEKEVU WA KWELI, you are the 'MAN'

    ReplyDelete
  15. alikuwa anipeleleza taifa stars ili waifunge vizuri, si unajua hatuchunguzi uraia, basi tena.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...