Jumla ya maofisa wajuu wa serikali 100 (baadhi yao pichani), watanufaika na mafunzo ya usimamizi wa mikataba yanayogharimiwa na serikali ya Ubelgiji na Jumuiya ya Madola kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Rasilimali Watu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dr. Feisal Issa, wakati akifunga Mafunzo ya Usimamizi wa Mikataba, yaliyofadhiliwa na serikali ya Ubelgiji kwa watendaji wakuu wa wizara, wakala na idara za serikali, katika hoteli ya Paradise mjini Bagamoyo mwishoni mwa wiki.

Dr. Feisal amesema, mafunzo hayo ya maofisa 100 wa serikali, yataendeshwa kwa awamu 4 ambapo awamu ya kwanza naya pili inayohusisha jumla ya maofisa 40, imegharimiwa na serikali ya Ubelgiji kupitia Ubalozi wake hapa nchini kupitia Shirika la Mendeleo la Ubelgiji (BTC) .
Dr. Feisal amesema, maofisa wengine 60, watapata mafunzo hayo kupitia udhaminiwa wa Jumuiya ya Madola chini ya Shirika lake la Maendeleo la CDC na kufanya idadi ya maofisa watakaofadika na mafunzo hayo kufikia 100.
Dr. Feisal amesema, mafunzo hayo yamekuja katika wakati muafaka ambapo serikali ya Tanzania imejivua majukumu ya uendeshaji wa huduma 40 na kuzikabidhi kwa sekta binafsi na tayari huduma nyingine 95 zimesha ainishwa na zote hizi zinahitaji usimamizi makini wa mikataba yake ya uendeshaji ili zoezi hili liweze kuleta tija inayokusudiwa.
Pia Dr. Feisal amezitaka wizara, wakala na idara za serikali zinazojitegemea kuainisha mahitaji yao ya mafunzo mapema kwa kadri ya mahitaji ya makundi husika ili ziweze kupangiwa bajeti za mafunzo na sio kusubiri tuu fursa za mafunzo za serikali kuu ili kila wirara, wakala na idara inayojitegemea iwajee uwezo watumishi wake kwa kadri ya mahitaji yao.
Dr Feisal, alitoa shukrani kwa serikali ya Ubelgiji kwa kufadhili mafunzo hayo na pia kuwashukuru wawezeshaji wa Taasisi ya Mafunzo ya nchi za Kusini mwa Afrika (ESAMI) walioendesha mafunzo hayo.
Serikali ya Ubelgiji kupitia Shirika la Mendeleo la Ubelgiji (BTC) ni moja ya nchi wafadhili wakubwa katika udhamini wa kozi za shahada za pili na shahada za uzamili ambapo katika mwaka huu wa fedha, umeongeza nafasi kwa watanzania toka nafasi 80 kwa mwaka mpaka nafasi 120.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Wafundisheni tu, lakini wanavyopokea mlungulu, yaani wanyonge tunazidi kuumia.

    ReplyDelete
  2. Sio kitu cha kujivunia kwani tatizo letu sio wataalam tuna wataalam wa kutosha tatizo letu ni rushwa na rushwa kuanzi ngazi za juu hao wataalam wanapokea maelekezo toka juu.Hao wafadhili wangetoa kozi ya urais,uwaziri mkuu, uwaziri,ukuu wa mikoa n.k.Msaada huu kwetu ni funzo kweni wameamua kutoa msaada baada ya kuona nchi yetu kwa muda mrefu tunasahini mikataba isiyo na kichwa wala miguu hatua hii ya wadhamini nachukulia kama kumuunga mkono SHUJAA ZITTO.Na ninapendekeza ya kua topic mkataba wa buzwagi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...