Home
Unlabelled
wagagagigikoko
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
kaka Michu, nimefurahia sana hivi vitabu......je, vinapatika bado madukani? safi sana.....
ReplyDeleteBw. Issa Michuzi, nimefurahi sana kuona hiko kitabu cha bulucheka nakuomba kama utaweza kutupa link kitabu naweza kukipata wapi, Miaka kama 15 toka nisome hiko kitabu ni vizuri kama tutakuwa tunasomesha wenetu, mie kusoma nilikuwa sijui mpaka nilivyofundishwa na hicho kitabu fanya kweli kuhusu link ya kitabu.
ReplyDeleteDu Bwana misupu umeikumbusha mbali sana kitabu hiko kina stori za MAKALI HODARI ....
ReplyDeleteDuh Michuzi kweli leo umenivunja mbavu, yaani ni miaka zaidi ya 20 nimesema vitabu hivyo, kusema ukweli sikumbuki hata kuna nini humo ndani, duh PINOKYO ahaha...ila nakumbuka bulicheka alikuwa fara kweli, ila to be honest sikubuki vizuri......hii ndo blog babake,
ReplyDeleteKaka Michuzi hivyo vitabu mi vinanikumbusha mbali sana hasa pale Mfalme Huihui alipokasirika alipoona Bulicheka ameingia mjini kwake, bila ruhusa yake na kujenga nyumba kwa kutumia meza kwenye minazi minne iliyokaa skwea.
ReplyDeleteHuihui alivyokenua domo lake na kujishika mikono kiunoni iliyokaa kama Upinde. Tehe teh tee! We acha tu!
Vinapatikana bukshop gani hivyo?
Michu, hebu tuace masihara....TUNAOMBA KAMA ATAJITOKEZA MDAU KUFUFUA VITABU HIVI KWA AJILI YA WANETU.....halafu pia kile kitabu cha ALF-LELA-U-LELA.....jamani hebu fikirieni wanetu wakiwa wanasoma na kujijengea mazingira ya kupenda kusoma vitabu...usomaji vitabu unapanua sana ubongo wa mtoto.
ReplyDeleteMichuzi,
ReplyDeleteNi aibu sana kuwa watanzania wengi hawapendi kusoma. Mimi nadhani hata watoto wetu wamekosa hamasa ya kusoma kwa vile hakuna vitabu kama hivyo tulivyosoma sisi, maana kila wakati mtu ulikuwa unataka uende shule ili ukasome hadithi za Bulicheka na Elizabeta!
Ilikuwa inapendeza kwa kweli, maana pamoja na mimi kuzizoma hizo hadithi miaka ya 72 na 73 bado nakumbuka kwa mbali zilivyokuwa zinasisimua!
Haluu Bro Michu! Yaani umenikumbusha mbaaali kweli! Mwaka wa Arobaini na Sabaa!! Nilikuwa napenda sana kuvisoma hivi vitabu vya Bulicheka na Paulo Mchafu! Yaani ilikuwa mtu you are actually looking forward kuvisoma, na wakati unavisoma unakuwa veeere excited, na unajenga kabisa picha kichwani, yaani kama unawaona vile walivyokuwa wanafanya. Duh, imenikumbusha pia enzi za Mama na Mwana.
ReplyDeleteAisee kwa kweli tujulishe vyapatikana wapi.
BULICHEKA NA MKEWE ELIZA ELIZA...ISSA MIMI NITANUNUA HIVYO VITABU KAMA UTAWEKA LINKI HUMUNDANI.
ReplyDeleteSi utani Umetukumbusha mbali na vitabu hivi!
ReplyDeletewewe muidini una lazi. Samahani sikutukani bali nakusifia. Kumpata bulicheka na demu wake elizabeti, wakati wakimtoa mfalume huihuihui, hii kiboko. Tunataka mavintuz kama haya babaake.
ReplyDeleteKaka michuzi hivi vilikuwa vitabu vya maana sana. Kuna kitabu pia kiliitwa HEKAYA ZA ABUNUWASI. Kama kuna mdau anafahamu ni wapi vitabu hivi vinapatikana naomaba tafadhali anielekeze niende nikanunue. Kama haviuzwi nitalipia nipige photocopy au hata kunakili kwa mikono. Ninachotaka tu ni maandish yake.Jamani tusiwe wachoyo wa elimu. Kama kuna mdau anayeweza kuni-assist tafadhali nijulishe kupitia 0754711028. Iam very serious about this.Thanks in advance!
ReplyDeletehehehehehe Bulicheka na Elisabeta, nilishasaha jina la huyu mama, hata story sikumbuki vizuri tena. Kama wadau walaivyopendekeza hapo juu, ingekuwa jambo la busara kama tutavipata tena. Looh! Si mchezo!
ReplyDeleteNahitaji vitabu vifuavyo:
ReplyDeleteBULICHEKA
MASHIMO YA MFALME SULEMANI
ALFU LELA ULELA
MALIMWENGU
HADITHI ZA ESOPO
TAFADHALI NIPO TAYARI KUNUNUA
CALL ME OR SMS AT 0713 650 469
Duh, yaani kitabu cha someni bila shida cha Bulicheka, Lizabeta na Wagagagigikoko nilisoma miaka ya 80... Itabidi nikitafute tena nikumbushie zile stories.
ReplyDeleteMichuzi hakujibu hata comment 1, ana hasira gani Michuzi?
ReplyDeleteMsimsahau Kalumekenge asietaka kwenda shule; Hanahela; pia Msimsahau shairi la mgeni siku ya kwanza.
ReplyDelete0678 683 278 anauza hivi vitabu, yuko pale Ubungo UBT
ReplyDeleteJamani pia navihitaji vitabu hivyo lkn sioni mjumbe aliyejibiwa hata mmoja tafadhali tusaidieni tujue namna yakuvipata. Mawasiliano yangu 0758050374
ReplyDelete