Majuzi nilitembele katika viunga vya mji wa Bagamoyo kwa ajili ya kwenda kujionea mwenyewe matukio mbalimbali yaliyojiri kwenye tamasha la 26 la Utamaduni wa Mtanzania.
Katika pitapita zangu nilikutana na Supa staa wavipindi vya maigizo vya Haki Elimu maarufu kama Kayumba. Kijana huyu amefanikiwa kujizolea sifaa na umaarufu nchini kote kutokana na jinsi alivyoweza kuigiza kama mwanafunzi kutoka katika familia maskini ambaye anakumbana na matatizo mbalimbali katika jitihada za kupata elimu.
Hassan Saidi Mwemanda aka Kayumba (pichani shoto akiwa na mwandishi wa makala haya) alinieleza kuwa ni kweli ametoka katika famiali maskini na alifeli darasa la saba, hivyo aliamua kujikita katika sanaa kwani wazazi wake hawakuwa na uwezo wa kumsomesha katika shule ya kulipia.
Kwa bahati nzuri mmoja wa wawakilishi kutoka katika chama cha wasomi Waislamu bwana Hashim Saiboko ameamua kujitolea kudhamini masomo ya kijanahuyu na kwa sasa Kayumba anasoma katika shule ya sekondari ya Sotele iliyopo Mkuranga.
Kijana huyu mcheshi na asiye na makuu ukilinganisha na umaarufu wake alinieleza kuwa yeye anapenda sanaa na amepania kuisomea hadi kufikiangazi ya elimu ya juu. Aliongeza kwa kusema kuwa hivi sasa yeye ni msaniikatika kikundi cha Shada chenye makazi yake mjini Bagamoyo na yeye anchezasarakasi, kuimba pamoja na kupiga ngoma.
Baadhi ya wadau wameonyesha kushangazwa imekuaje msanii huyu asaidiwekusomeshwa na mtu binafsi badala ya taasisi ya Haki Elimu ambayo kwa kiasikikubwa imefanikiwa kufikisha ujumbe wake kwa kumtumia msanii huyu pamoja nawenzake: Jitihada zinafanyika ili kuweza kuwasiliana na uongozi wa taasisihiyo ili kuweza kupata picha halisi.
Kwa wasiofahamu, Kayumba ni msanii anayecheza nafasi ya mwanafunzi kutoka katika ukoo wa kimasikini anayepambana na hali ngumu ya maisha pamoja na masomo kwa wakati mmoja katika tangazo lililojipatia umaaarufu sana nchini lililotayarishwa na taasisi ya Haki Elimu.
Habari kutoka CHUZI NEWS



Jamani Haki Elimu huyu kijana pamoja na kwapandisha kwenye chati namna hii toka bondeni ambako serikali ya awamu ya nne chini ya BWM akishirikiana na kiongozi asiye kuwa na vision kuwaponda mh saaaaaana Joe Mungai, leo mnamwacha kijana huyu namna hii kweli?mpaka anajitokeza mtu baki tena ambaye igizo la Kayumba halijamsaidioa lolote!Jitahidini jamani saidieni huyu kijana ni huko kwetu lakini ingelikuwa huku majuu huyu kijana angelikuwa na haki ya kuwadai na angelitajirika na hayo matangazo yake/yenu.
ReplyDeleteWito msaaidieni huyu kijana ndugu zangu wa Haki Elimu huko nyumbani.Na huku majuu nimeplan kuorganise tumsaidie ni kupitia watu kama hawa akina Kayumba hata akina Eddie Muppy,Willy Smith nk wanapatikana!
Hakika hap haki Elimu ilipasa mtoe mchango wowote katika kumsaidia mtoto huyu ana pata HAKI ya ELIMU.
ReplyDeleteKwa jinsi ninavyofahamu ilo shirika lenu hamuwezi kunishawiwishi kama hamna uwezo wa kumsaidia.
Naamini hata zile posho za masemina kibao mnazofanya mkiamua za mwezi mmoja tu mnaweza kubadili maisha yake.
HAPANA HEBU KARIBUNI HAPA KWENYE BLOGU YETU MTUPE UFAFANUZI.
Kaka michu hii habari isiishie hapa fuatailia tujue mwisho wake.Ukiona wewe wamekupoza na mlungura basi ...mpasie mtu mwingine azame tu mpaka tujue kulikoni.
JADILI.....TUANDIKIE ..ngeee ngeee ..haki ....elimu.
Mimi ndio nimejadili nimewaandikieni
Hawa Haki Elimu hawafanyi haki kama wanavyojitangaza ni wezi kabisa yaani wanmtumia mtu, tena Mtoto, kujitangaza halafu wanamwacha hivi hivi, Kayumba anapaswa kusomeshwa na hao Haki Elimu.
ReplyDeleteLol, hawa haki elimu ni wezi wakubwa sana, wamemtumikisha mtot wa watu Kayumba maskini kuwapandisha chat sasa badala ya kumsaidia wanamuacha hivyo hivyo??? lol, huu ni uonevu na ukiukwaji wa sheria na haki, jamani watanzania hii siyo haki kabisa!! Michuzi naomba email address ya director wa haki elimu!! shenzi hawa hawana aibu hata chembe!!
ReplyDelete