Mabwana,
Assalamu Alaykum wa Rahmatullah.
Katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan nitapendakukuleteeni viungo (links) vya mtandao (internet).Baadhi ya Viungo hivi ni vikuukuu na vingine ni vipya.Viungo vyote hivi ni kazi ya Marehemu Sheikh AliMuhsin Al Barwani. Ifuatayo ni hivi viungo pamoja namaelezo kidigo kuhusu kila kiungo:•
Qur’ani Tukufu ni tafsiri ya Qur’ani kwa Kiswahili. Inapatikana kwenye kiungo cha www.quranitukufu.net. Hii ni tarjuma ya “Al Muntakhab” ilio fanywa Misri naBaraza Kuu La Mambo ya Kiislamu kwa kushirikiana naAl-Azhar. Hii tarjuma ya Kiswahili nayo imepasishwa naChuo Kikuu cha Al-Azhar. Kwenye kiungo hiki utapatapia Fahrasa nzuri kabisa ya maneno mbalimbali yaliomokatika Qur’ani.•
Sikiliza Qur’ani Tukufu kwa Kiswahili, inapatikanakwenye kiungo hiki: www.sikiliza.quranitukufu.net .Hapa utapata kusikiliza Qur’ani kwa Kiarabu, maanayake na maelezo kwa Kiswahili. Utapata baadhi ya Surandogondogo za Juzuu Amma.•
Jifunze Kusoma Kiarabu Kwa Wiki Tatu bila ya mwalimu. Kwenye kiungo hiki www.jifunzekiarabu.quranitukufu.net unaweza kujifunzakusoma Kiarabu bila ya mwalimu. Huu mpango wakujifunza kusoma na kuandika Kiarabu umepangwa kwakuwakusudia wasemaji Kiswahili.•
Wacha Biblia Ihukumu, ni kitabu kilichotungwa naSheikh Ali Muhsin Al Barwani ili kuwajuilisha Waislamu na Wakristo mafunzo ya Biblia. Kiungo ni:www.biblia.quranitukufu.net
Uswatun Hasana ni utenzi (mashairi) ya maisha yaMtume SAW. Utenzi huu una beti zaidi ya 1300.Utangulizi wa utenzi huu umeandikwa na marehemu SheikhAbdalla Saleh Al-Farsi.www.uswatunhasana.quranitukufu.net
Mwenyezi Mungu akulipeni kila la kheri, Amin.
Muhamed Ali Muhsin

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako: